Maswali ya Biblia toka Waraka wa Yuda

 

S: Kwenye Yuda 1, je Yuda ni nani?

J: Yuda ni ndugu (kaka) wa Yakobo. Kulikuwa na kina Yakobo wengi, lakini inawezekana Yakobo huyu hapa na Yuda walikuwa kaka za Yesu. Uwezekano mwingine ni Yuda (sie Iskarioti) mmoja wa mitume, na Yuda aliyekuwa kiongozi wa kanisa la Yerusalem aliyetumwa pamoja na Paulo, Barnaba, na Sila kwenye Matendo 15:22.

 

S: Kwenye Yuda 1, kuna mambao gani yanaofanana na kitabu cha 2 Petro na yapi yanayotofautiana?

J: Mambo yanayofanana:

1. Mtumwa wa Yesu Kristo (2 Pet 1:1 na Yuda 1)

2. Wokovu wetu sisi sote (2 Pet 1 na Yuda 3)

3. Marafiki (mara tatu kwenye 2 Petro) na (mara moja kwenye Yuda)

4. Matumizi ya neno la Kigiriki lisilo la kawaida, despotes (2 Pet 2:1 na Yuda 4)

5. Matukano yafanywayo na viumbe wa kimbinguni (2 Pet 2:10 na Yuda 8)

6. Sodoma na Gomora (2 Pet 2:6-9 na Yuda 7)

7. Hukumu ijayo itakayofanywa na Yesu (2 Pet 3:7, 10, 12-14 na Yuda 13-15, 21)

8. Miisho inayofanana ya "sasa na hata milele. Amina" (2 Pet 3:18 na Yuda 25)

Mambo yanayotofautiana:

1. Panapokuwa na kufanana, 2 Petro kwa kawaida hutoa ufafanuzi zaidi, isipokuwa kuhusu viumbe wa kimbinguni

2. Kujitambulisha kama "Mtume" (2 Pet 1:1) dhidi ya "kaka wa Yakobo" (Yuda 1)

3. Neema na amani kupitia ufahamu (2 Pet 1:2) dhidi ya rehema, amani na upendo (Yuda 2)

4. Urefu: 2 Petro ni ndefu mara mbili ya Yuda (maneno 937 dhidi ya 459 kwenye Kigiriki)

5. Mada za ziada: kwa mfano, 2 Pet 1:3-21 haina ulinganisho, kutajwa kwa Paulo

6. Yuda inatumia lugha nyingi sana za picha

7. Waraka wa 2 Petro una mifano ya ziada ya Nuhu na mbwa

8. Nukuu mbili toka kwenye vitabu vya kubuniwa vya dini ya Kiyahudi vijulikanavyo kama apokrifa (apocryphal) kwenye Waraka wa Yuda

9. Kushindania imani kwenye Waraka wa Yuda dhidi ya kuepuka uharibifu kwenye 2 Petro

    Yuda 7, 13 inasistiza umilele wakati 2 Pet 3:3-8, 12 inasistiza muda

11. Wakati Waraka wa Yuda ni mfupi sana, 2 Petro umeandikwa katika njia inayolinda watu dhidi ya kuamini "mafundisho makali ya Calvin." Mifano ni pamoja na: "Bwana . . . [hupenda] wote wafikilie toba" (2 Pet 3:9), "wakimkana hata Bwana aliyewanunua" (2 Pet 2:1), na wale wanaoukimbia uharibifu wa ulimwengu na wanategwa tena (2 Pet 2:19-22)

Muhtasari: Kufanana na kutofautiana kunaweza kuelezwa kwa kutumia watu wawili wenye mitindo tofauti, ambao huenda waliongea kila mmoja kwa mwenzake, na waliandika wakati mmoja kuhusu matatizo yanayofanana, huku Petro akiandika barua yenye kina zaidi.

 

S: Bart Ehrman mwenye kushuku anaandika, "Ni vigumu kuamini kuwa nyaraka hizi mbili [Yakobo na Yuda] zingeweza kuandikwa na wakulima wa Kiaramu wa daraja la chini kutoka Galilaya (ambao kaka yao maarufu sana [Yesu] hafahamiki kuwa aliweza kuandika, achilia mbali kutunga maandiko yoyote magumu kwa Kigiriki)." Jesus, Interrupted uk.134-135.

Sehemu nyingine Ehrman anaandika, "Tunazo habari kuhusu maana halisi ya kuwa mkulima wa daraja la chini kwenye maeneo ya vijijini ya Palestina ya karne ya kwanza. Kitu kimoja ambacho ilimaanisha ni kwamba mtu wa aina hiyo alikuwa hajui kabisa kusoma na kuandika. Yesu mwenyewe alikuwa na upekee mkubwa kwani kuna ushahidi kuwa aliweza kusoma (Luka 4:16-20), lakini hakuna kitu chochote cha kuonyesha kuwa aliweza kuandika . . . Je ni watu wangapi walijua kusoma? Kutokujua kusoma na kuandika kulienea sana kwenye Himaya yote ya Rumi. Katika nyakati nzuri zaidi, asilima 10 tu ya watu wangeweza kuwa wanajua kusoma na kuandika. Na asilimia 10 hiyo ilikuwa ni watu wa tabaka la matajiri . . . Hakuna kitu kwenye injili au Matendo ya Mitume chenye kuonyesha kuwa wafuasi wa Yesu walijua kusoma, achilia mbali kuandika. Kwa kweli kuna maelezo kwenye Matendo ya Mitume ambapo Petro na Yohana wanatajwa kuwa ‘watu wasio na elimu' (Mdo 4:13) – neno la zamani la kutokujua kusoma na kuandika." (Jesus, Interrupted uk.105-106). Pia kwenye Lost Christianities uk.203.

J: Ehrman anasema hivi kwa sababu haamini kuwa watu wa Galilaya wangeweza kuongea Kigiriki. Jambo hili halizingatii kuwa kulikuwa na Kigiriki kwenye sarafu zao na walizungukwa pande tatu na mikoa yenye kuzungumza Kigiriki. Kuna angalau sababu nne zenye kuonyesha kuwa Ehrman hayuko sahihi:

1. Ukaribu wa Kapernaumu na Foinike: Nazareti, alikokulia Yesu, ilikuwa karibu maili 15 (km 24.1) kutoka Foinike kufuata uelekeo mmoja, na karibu maili 20 (km 32.2) kutoka Kapernaumu, ambako watu wengi wenye kuongea Kigiriki na Kilatini waliishi. Galilaya ilipakana upande wa magharibi, kaskazini, na mashariki na mikoa inayoongea Kigiriki. Mashariki mwa Galilaya ilikwa "Dekapoli", neno la Kigiriki lenye kumaanisha miji kumi. Mgerasi aliyekuwa na mapepo aliishi kwenye eneo hili. Nguruwe walifugwa (kwa hiyo waliliwa pia) na watu waliokuwa wanazungumza Kigiriki walioishi hapo. Yesu alihubiri hapo alipovuka Bahari ya Galilaya. Kwa hakika atakuwa alizungumza Kigiriki alipowahubiria.

2. Sarafu za Galilaya: Maelezo yafuatayo yametolewa kwenye Greco-Roman Culture and the Galilee of Jesus kitabu kilichoandikwa na Mark A. Chancey, Cambridge University Press, 2005. Anasema kuwa kwa kuangalia kwenye sarafu za Galilaya, "maandishi yalikuwa yanaandikwa kwenye Kigiriki, ingawa sarafu chache ambazo zimepatikana Palestina zina maandshi ya Kiebrania." (uk.168) ... "Kitu kingine kilichotofautisha sarafu za Kihasmonia ni matumizi yake kidogo ya Kigiriki. Herufi na momogramu za Kigiriki, ambazo maana zake hazieleweki vizuri, zinapatikana kwenye sarafu za Hyrcanus I. Hata hivyo, nyingi za fedha zake zinatumia mwandiko wa hati ya mkono wa Kiebrania uliotumika kabla ya utawala wake" (uk.169) ... "angalau sarafu moja ya Agrippa II ilitengenezwa Galilaya, kama inavyoonyeshwa na neno ‘Tiberias' lililozungushiwa taji ya Kigiriki kweye upande wake wa pili. Sura ya tawi la mtende na maandishi . . . [ya Kigiriki] ‘Mfalme Agrippa, Ushindi wa Mfalme unapatikana kwa kungalia kwa makini" (uk.183).

3. Kiwango cha kujua kusoma na kuandika katika Himaya ya Rumi si muhimu hapa: Ehrman anasahau kuwa asilimia ya watu kwenye Himaya ya Rumi (Hispania, Uingereza, Ujermani, nk.) ambao walikuwa hawajui kusoma na kuandika si ya muhimu; ni asilimia ya watu walioelimika miongoni mwa Wayahudi walioko Uyahudi na Galilaya iliyo muhimu. Wayahudi walikuwa na viwango vya juu sana vya elimu kuliko wengi wa watu wengine katika Himaya ya Rumi. Kwa vile baraza la kidini la Kiyahudi liliwashutumu Petro na Yohana kwa kutokuwa na elimu haimaanishi kuwa walikuwa hivyo.

4. Kiwango cha kujua kusoma na kuandika Palestina: Kama wazo la ziada, huko Beir Allah kwenye bonde la Mto Yordani, wataalamu wa mambo ya kale wamegundua mazoezi ya kuandika ya mtoto wa shule mvulana yanayomwelezea Balaam mwana wa Beor mara tatu. Maandishi haya yalifahamika kuwa yaliandikwa miaka ya 800/760 KK na vipima vya umri vyenye kutafuta kiasi cha Kaboni.

 

S: Kwenye Yuda 3, je Yuda aliandika waraka mwingine kuhusu wokovu wa waumini wote?

J: Hakuna ushahidi wenye kuunga mkono au kupinga kuwa Yuda aliandika waraka wa pili. Kama alifanya hivyo, Mungu hakutakiwa kuhakikisha kuwa unahifadhiwa; Mungu angeweza kuhifadhi waraka wowote aliopenda kuuhifadhi.

Isitoshe, msemo hapa haudokezi hata kidogo kuwa Yuda alitakiwa kuandika waraka wa pili. Badala yake unamaanisha tu kuwa Yuda alipendelea kuandika juu ya ukubwa wa wokovu wa waumini wote, na Yuda alisikitika kuwa kulikuwa na haja ya waraka kama huu.

Kama wazo la ziada, tunapokosoa (kwa usahihi na uhalali) waumini wengine kama Yuda alivyofanya, tunapaswa kufuata mfano wa Yuda na kufanya hivyo kwa shauku na masikitiko kwamba hali iliyopo inahitaji karipio.

 

S: Kwenye Yuda 4-10, iliwezekanaje watu waliokuwa waasherati, wafuatao mambo ya mwili yasiyo ya asili, wenye kuupotosha mwili, wenye kufanya karamu za kilevi pamoja, na wenye kufuata tamaa mbaya, walivamie kundi kwa kushtukiza?

J: Watu wanaweza kufanya mambo sirini. Yuda hasemi kuwa walifanya mambo yoyote kati ya haya wakati wa makusanyiko ya ibada. Badala yake, walifanya mambo ambayo hayakufahamika na ushirika, au pengine waliwaambia baadhi ya watu kwenye ushirika ili kuwapotosha, na bado walivumiliwa.

 

S: Kwenye Yuda 6, malaika waliofungwa ni kina nani ambao Yuda anawaongelea?

J: Hawa ni malaika walioasi ambao wapo kifungoni kwa sasa. Kuna maoni matatu tofauti.

1. Baadhi wamefungwa na baadhi wako huru: Kwa sasa baadhi ya mapepo yamefungwa na mengine yako huru na yanafanya uovu duniani. Hata mapepo yaliyo huru yaliyokabiliana na Yesu yalikuwa yanogopa kuwa yangeweza kutupwa kuzimu.

2. Wote wamefungwa kiasi: Mtazamo tofauti ni kuwa mapepo yote yamefungwa kwa sasa, lakini japo yamefungwa yanaweza kuwaathiri watu. Kama Bible Difficulties and Seeming Contradictions (uk.225-226) inavyosema, "Mtu anaweza kufungwa maisha jela lakini akapewa upendeleo wa kutembea eneo la gereza au hata nje kwa masharti na mipaka kadhaa." Tazama Christian Theology iliyoandikwa na Millard J. Erickson uk.447-448 kwa maelezo zaidi kuhusu jambo hili.

3. Mchanganyiko wa maoni haya mawili: Maoni yangu ni mchanganyiko wa maoni mawili hapo juu. Mapepo tofauti yanaweza kuwa na mipaka tofauti na viwango tofauti vya uhuru. Yuda anasema wazi kabisa kuwa mipaka ya baadhi ya mapepo imeongezwa. Hata hivyo, hakuna pepo linaloweza kwenda kinyume cha amri za Yesu.

 

S: Kwenye Yuda 6, je malaika waliofungwa ni Wanefili wa Mwanzo 6 waliooa mabinti wa wanadamu?

J: Watu wengi hawaafikiani na wazo hili.

Ndiyo. Kitabu cha apokrifa cha dini ya Kiyahudi, 1 Enoch, kwenye "vitabu" vyake vitano vya kwanza na vya mapema zaidi kinasema malaika waliofungwa walikuwa ni wale wa Mwanzo 6. Baadhi ya wakristo wa awali wanakiheshimu sana kitabu cha 1 Enoch.

Hapana. Hawa wanaweza kuwa ni mapepo wanaoasi kwa jumla.

Kwa vyovyote itakavyokuwa, msemo huu unawaongelea malaika walioanguka kwa ujumla, na hausemi chochote kuhusu Shetani akimjaribu Hawa, kama dini isiyo ya kweli ya Unification church ya Mch. Moon inavyoamini.

 

S: Kutoka Yuda 6-7, je tunaweza "kusema kuwa malaika walianguka kama matokeo ya tendo ovu la tamaa isiyo ya asili" kama vile mwasi, Mch. Moon, alivyofundisha kwenye toleo la tano (1977) la Divine Principle uk.71-72?

J: Hapana. Yuda 5-7 inatoa mifano mitatu: Waisraeli walitoka Misri (mstari 5), malaika walioiacha nyumba yao wenyewe (mstari 6), na Sodoma na Gomora (mstari 7). Yuda haongelei kuhusu Anguko la mwanadamu.

 

S: Kwenye Yuda 9, ni lini malaika mkuu Mikaeli alipobishana na Shetani kuhusiana na mwili wa Musa?

J: Maandiko hayasemi, na jambo hili halijaelezwa sehemu yoyote ile nyingine kwenye Maandiko. Yuda anaongelea tukio hili ili kuonyesha jambo lingine, kwa jinsi hiyo Yuda anaonekana kufahamu kuwa wasomaji wake waliishawahi kusikia jambo hili. Tukio hili lilielezwa kwenye kitabu cha apokrifa cha Assumption of Moses, ambacho pia kinaitwa Testament of Moses. Tunayo sehemu kubwa ya Assumption of Moses, isipokuwa mwishoni, ambamo mnaaminika kuwa kuwa na mstari huu.

 

S: Kwenye Yuda 14, je ni Henoko yupi huyu?

J: Huyu si Henoko aliyekuwa mtoto wa Kaini kwenye Mwanzo 4:17. Huyu alikuwa Henoko, mzao wa Sethi aliyekuwa wa saba kutoka kwa Adam kwenye Mwanzo 5:21-24. Huyu ni Henoko yuleyule aliyetembea na Mungu kisha Mungu akamchukua mbinguni. Henoko wa kwenye Mwanzo 4:17, na mtoto wa Kaini na aliyekuwa wa tatu kutoka kwa Adam, ni Henoko tofauti.

 

S: Kwenye Yuda 14, kwa kuwa Henoko alikuwa wa saba kutoka kwa Adam, je jambo hili halithibitshi kuwa hapakuwa na mapengo katika orodha ya uzao kati ya Adam na Henoko?

J: Hapana. Jambo hili linaweza kumaanisha tu kuwa Henoko ametajwa kama mtu wa saba kutoka kwa Adam kwenye orodha ya Mwanzo.

 

S: Kwenye Yuda 14, kwa nini Yuda alinikuu toka kwenye kitabu cha apokrifa kilichoadikwa kwa kutumia jina la bandia la mtunzi cha 1 Enoch kama kweli?

J: Mstari huu ni wa kweli, ingawa kuna makosa kwenye sehemu nyingine za 1 Enoch. Mambo manne:

1. Hakuna uhakika kuwa Yuda alinukuu kitabu cha 1 Enoch. Ingawa maneno ni karibu sawa kabisa, yanaweza kuwa yametoka kwenye chanzo cha pamoja cha waandishi wa 1 Enoch na Yuda. Chanzo hicho kinaweza kuwa kitabu kilichokuwa na uabii huu wa kweli ndani yake, au chanzo cha pamoja kinaweza kuwa Mungu mwenyewe

2. Kitabu cha 1 Enoch kilipata mabadiliko ya mara kwa mara. Ingawa kitabu kiliandikwa kabla ya kipindi cha ukristo, watu wengine wanafikiri kuwa nukuu hii iliongezewa baada ya Waraka wa Yuda kuandikwa, na kabla ya karne ya 15 na mtawa mwanaume aliyepotoka. Itakubidi uchague wewe mwenyewe; ifuatayo ni nukuu ya Hati Toka Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scrolls) 4Q204; angalia mapengo, ". . . idadi kubwa sana ya watakatifu wake . . . wapya kwa . . . zao zote . . . wenye kiburi na waovu . . ." (Nukuu hii imetoka kwenye The Dead Sea Scrolls Translated ya Florentino Garcia Martinez).

3. Kuna uwezekano kuwa Yuda alinukuu kitabu cha 1 Enoch, na jambo hili halina shida. Kitabu cha 1 Enoch kilikuwa na watunzi tofauti wasoiopungua watano, na mstari huu unatoka kwenye sehemu ya kwanza na ya awali zaidi. Kitabu cha 1 Enoch ni mchanganyiko wa ukweli na makosa, na Mungu anaweza kuwa ameruhusu kwa kudhamilia kabisa kuwa Yuda anukuu hapo, ili kwamba unabii huu wa kweli kutoka kwa Mungu uhifadhiwe siyo tu kwenye vyanzo hivi visivyo vya kibiblia bali pia kwenye Biblia.

4. Ingawa kitabu cha 1 Enoch kitakuwa na ukweli mmoja wa Mungu, haimaanishi kuwa kitakuwa sehemu ya Maandiko matakatifu. Kitabu hakitakiwi tu kuwa na neno la Mungu bali pia kinatakiwe kiwe kama vile Mungu anavyotaka kwenye Maandiko matakatifu. Maandiko ya Wesley, Luther na Calvin yana kiasi kikubwa sana cha kweli ya Mungu pia, lakini haimaanishi kuwa hayana makosa yoyote yale, na waandishi hao watatu wangepinga wazo kuwa maandishi yao yachukuliwe kuwa Maandiko matakatifu.

Kitabu cha 1 Enoch kiliheshimika sana. Kuheshimika sana kunamaanisha kuwa kilikuwa na mambo mengi yaliyokuwa ya kweli, lakini haimaanishi kuwa kilivuviwa na Mungu. Naweza kusema Yesu anakuja tena. Jambo hilo ni kweli, lakini kwa kusema hivyo haimaanishi kuwa nimevuviwa na Mungu.

 

S: Kwenye Yuda 14, kwa ufupi, kwa kuwa Yuda [inadaiwa] kupata uvuvio kutoka kwenye kitabu kisichovuviwa cha 1 Enoch 1:9, Wakristo wanawezaje kumkosoa Joseph Smith kwa kupokea uvuvio kutoka kwenye kitabu cha kipagani cha Kimisri, Book of the Dead, wakati Joseph Smith alipoandika kitabu cha Wamomoni, Book of Abraham?

J: Kitabu cha 1 Enoch ni kitabu cha Kiyahudi kisichokuwa sehemu ya Maandiko matakatifu, chenye sehemu/tabia tofauti, na mchanganyiko wa ukweli na makosa. Kwa kuwa nukuu ya Yuda inafanana na mstari wa 1 Enoch, haimaanishi kuwa Enoch hakusema hivi.

Tofauti na hivyo, watu wengi wamethibitisha kuwa hati ambayo Joseph Smith anadai kwa uongo kuwa ndio chanzo cha tafsiri ya kitabu cha Wamomoni, Book of Abraham, ilikuwa ni kitabu cha kipagani chenye kuhusika na ibada ya sanamu.

Kwa muhtasari:

1. Haiwezi kuthibitishwa (au kukanushwa) kuwa Yuda alinukuu mstari huu toka 1 Enoch

2. Hata kama Yuda alitoa maneno haya kutoka kitabu cha 1 Enoch, 1 Enoch ni kitabu chenye sehemu/tabia tofauti, na kinaweza kuwa na sehemu zenye unabii uliovuviwa na Mungu.

3. Kwa utofauti mkubwa kabisa, tafsiri bandia ya Joseph Smith ilitokana na kitabu cha sanamu.

Tazama swali linalofuata kwa jibu kamilifu zaidi.

 

S: Kwenye Yuda 14, kwa kuwa Yuda [inadaiwa] alipata uvuvio kutoka kwenye kitabu kisichovuviwa cha 1 Enoch 1:9, Wakristo wanawezaje kumkosoa Joseph Smith kwa kupokea uvuvio kutoka kwenye kitabu cha kipagani cha Kimisri, Book of the Dead, wakati Joseph Smith alipoandika kitabu cha Wamomoni, Book of Abraham?

J: Angalia swali lililotangulia ili kupata jibu fupi. Kwa jibu kamilifu, zingatia mambo haya yafuatayo.

Utangulizi wa kitabu cha Kiyahudi cha 1 Enoch:

Kitabu cha 1 Enoch kina sehemu/tabia mchanganyiko, sehemu tano zikiwa zimeandikwa nyakati tofauti na waandishi tofauti. Nukuu inayohusu swali hili inatoka kwenye sehemu ya kwanza na ya awali zaidi. Hata hivyo, inawezekana kuwa nukuu hii iliongezwa baadaye. Nakala ya awali zaidi iliyopo inatoka kwenye Hati kutoka Bahari ya Chumvi (Dead Sea scrolls). Lakini, nakala ya awali zaidi yenye nukuu hii iliandikwa karne ya 15 huko Ethiopia. Kitabu hiki kina mambo kadhaa ya kweli ndani yake, lakini pia kina mambo ya kubuniwa, pamoja na mijadala yote ya malaika na mapepo. Kitabu cha 1 Enoch hakijatoweka kabisa katika ulimwengu wa sasa.

Utangulizi wa kitabu cha Kimisri, Book of the Dead:

Kuna uwezekano kuwa kitabu cha Kimisri, Book of the Dead hakikusomwa sana. Badala yake, lengo la kuandikwa kwake lilikuwa ni kukizika pamoja na matajiri ili kiwe kama hirizi yenye kurahisisha kuingia kwao kwenye maisha ya baada ya kifo. Kulikuwa na kutofautiana kwingi sana kwa kitabu kulikolingana na idadi ya nakala zake, kwani kila kila kitabu kilikuwa na jina la marehemu ndani yake. Watu wengi wametafsiri sehemu ambayo inadaiwa kuwa Joseph Smith aliitumia kutafsiri kitabu cha Abraham.

Utangulizi wa kitabu cha Kimomoni, Book of Abraham:

Kwa mujibu wa Joseph Smith, kitabu cha Kimomoni, Book of Abraham, kinadaiwa kuandikwa na Abrahamu kuhusu safari zake alizokuwa Misri. Joseph Smith alidai kuwa kiliandikwa kwenye lugha ileile kama Book of Mormon, na Joseph Smith alikitafsiri kwa msaada wa kiungu. Wamomoni wa jiji la Salt-Lake, Uttah, Marekani (LDS) wana maandiko manne, na moja kati ya hayo ni Pearl of Great Price, ambalo lina The Book of Abraham kama moja ya vitabu vyake. The Book of Abraham 1:21-26 ni maandiko pekee ya Kimomoni yaliyo msingi wa mafundisho yao dhidi ya Waafrika. Kitabu hiki kinasema kuwa Waafrika hawawezi kupewa ukuhani mkuu. Mafundisho haya yalibadilishwa na kanisa la Momon mwaka 1978.

Utangulizi wa madai ya Joseph Smith:

1. Joseph Smith alidai kuwa "alitafsiri" hati kwenye Pearl of Great Price, uk.29.

2. Tatu kati ya nakala nne za asili zina maandishi ya Kimisri sambamba na Kiingereza.

3. Picha tatu zinafanana

4. Jambo dhahiri zaidi, Joseph Smith aliandika kitabu, Egyptian Alphabet and Grammar, ambacho alikusudia kujaribu kuwafundisha watu wengine Kimisri cha uongo.

5. Smith alitafsiri wastani wa zaidi ya maneno 100 kwa hieroglifu moja, wakati ilitakiwa iwe neno moja au mawili kwa hieroglifu moja.

6. Hakuna mtu aliyetambua udanganyifu huu wa Joseph Smith kwa wakati ule, kwa sababu hakukuwa na mtu Marekani kote aliyeweza kusoma maandishi ya zamani ya Kimisri.

Kwa muhtasari: Wamomoni wana tafsiri ya uongo ya kitabu cha kipagani chenye kuhusiana na ibada ya sanamu kama sehemu yao ya maandiko. Ingawa baadhi yao wameona kufanana kwa muktadha wao na kuwemo kwa Yuda 14 kwenye 1 Enoch. Muktadha ni tofauti kabisa kwa sababu

1. Hata kama Yuda alinukuu kutoka kwenye kitabu cha 1 Enoch, si kitabu cha kisiri wala chenye kuhusiana na ibada ya sanamu. Ni kitabu cha Kiyahudi chenye mchanganyiko wa ukweli na makosa.

2. Haiwezi kuthibitishwa endapo Yuda alinukuu kitabu cha 1 Enoch. Vitabu hivi viwili vinaweza kuwa vilitumia chanzo kimoja, au tukio hili liliongezwa kwenye 1 Enoch kabla ya karne ya 15 na mtawa mwanaume aliyepotoka.

 

S: Kwenye Yuda 21, kwa kuwa hatuwezi kupoteza wokovu wetu, ni vipi na kwa nini tunadumisha kumpenda Mungu?

J: Baadhi ya Wakristo wa kweli wanaamini kuwa watu wanaweza kupoteza wokovu. Wengine hawaamini hivyo. Bila kujali maoni juu ya suala hili, wote wanakubali kuwa kama ambavyo mtoto anaweza kufanya vitu ambavyo vinawasikitisha wazazi wake na yeye mwenyewe, tunaweza kufanya vitu ambavyo vinamhuzunisha Mungu. Kama ambavyo mtoto anaweza kupenda kuondoka nyumbani, sisi pia, kama Yona, tunaweza kujaribu kuondoka kwa Mungu.

 

S: Kwenye Yuda 23, tunawaokoaje wengine?

J: Hatuwezi kuchukua nafasi ya msalaba, lakini tunaweza kutoa mchango muhimu katika kuleta ujumbe wa msalaba na kuwaleta watu kwa Kristo. Tazama mjadala kuhusu Kol 1:24 kwa habari zaidi.

 

S: Kwenye kitabu cha Yuda, tunawezaje kujua kuwa kiliandikwa na Yuda?

J: Mwandishi amesema kuwa aliuwa Yuda, na huu ndio ushahidi pekee tulionao, ubaya na uzuri. Kanisa la awali halikuwahi kupinga jambo hili.

 

S: Kwenye Yuda, tunawezaje kujua kuwa Maandiko matakatifu ya leo ni nakala ya kuaminiwa iliyohifadhiwa ya yale yaliyoandikwa mwanzoni?

J: Kuna angalau sababu tatu:

1. Mungu aliahidi kulihifadhi neno lake kwenye Isa 55:10-11; 59:21; 40:6-8; 1 Pet 1:24-25; na Mt 24:35.

2. Ushahidi wa kanisa la awali. Wafuatao ni waandishi walionukuu mistari toka kwenye Waraka wa Yuda. Kati ya mistari 25, waandishi walioandika kabla ya Mkutano wa Nikea walinukuu au kugusia mistari yote isipokuwa mitano (mistari kamili 4 na nusu mistari 2). Hii ni Yuda 2, 18, 20-22a, 23b-25.

Muratorian Canon (karibu mwaka 170 BK) inautaja Waraka wa Yuda

Irenaeus (mwaka 182-188 BK) Yuda 3 "imani waliyokabidhiwa watakatifu" Irenaeus Fragment 36 uk.574. Yuda 3 inatumia "watakatifu" badala ya "sisi", lakini ukiachia neno hili, msemo huu ni ule ule. Msemo huu unapatikana Yuda 3.

Irenaeus (mwaka 182-188 BK) anagusia Yuda 7 akzitaja Sodoma na Gomora za wakati wa Luti kuwa mfano wa hukumu ya haki ya Mungu. Irenaeus Against Heresies kitabu cha 4 sura ya 36.4 uk.516. Wazo la Sodoma na Gomora kuwa kama mfano linapatikana Yuda 7 tu kwenye Biblia.

Clement wa Alexandria (mwaka 193-217/220BK) ananukuu Yuda 5, 6 kama maneno yaliyoandikwa na Yuda. The Instructor kitabu cha 3 sura ya 8 uk.282

Clement wa Alexandria (mwaka 193-202 BK) ananukuu sehemu ya Yuda 19, 22b, 23a. Stromata kitabu cha 6 sura ya 8 uk.495

Clement wa Alexandria (mwaka 193-202 BK) anataja Yuda 8-17 kama maneno yaliyotabiriwa na Yuda. Stromata kitabu cha 3 sura ya 2 uk.383

Clement wa Alexandria (mwaka 193-217.220 BK) ananukuu Yuda 1, 4-14, 19 kama maneno yaliyoandikwa na Yuda kwenye sehemu ya Cassiodorus uk.573

Tertullian (mwaka 198-220 BK) anataja kazi iliyoandikwa na Mtume Yuda kwenye On the Apparel of Women kitabu cha 1 uk.16

Tertullian (mwaka 198-220 BK) anagusia Yuda 23 kwenye On Modesty sura ya 18 uk.94. ". . . ilizuiliwa kwa wenye dhambi, hasa kwa kuwa ‘imechafuliwa na mwili'"

Origen (mwaka 225-254 BK) akijadili vitabu vya kwenye Biblia, ananukuu Yuda 1 kama maneno yaliyoandikwa na Yuda. Origen's Commentary on Matthew kitabu cha 10 sura ya 17 uk.424. Pia ananukuu sehemu ya Yuda 1 kama maneno ya Yuda kwenye maoni yake kuhusu Injili ya Mathayo, kitabu cha 13 sura ya 27 uk.491.

Origen (mwaka 225-254 BK) ananukuu kijuujuu Yuda 8. Origen's Commentary on Matthew kitabu cha 10 sura ya 24 uk.430

Baada ya Mkutano wa Nikea

Athanasius (mwaka 367 BK) haongelei mstari wowote hasa kwenye Yuda, bali anaorodhesha vitabu vya Agano Jipya kwenye Festal Letter 39 uk.552

Hilary wa Poitiers (mwaka 355-367/368 BK)

Ephraem Msiria (mwaka 373 BK)

X Didymus Kipofu (mwaka 398 BK) anataja Yuda 4, 19. Lakini anaukataa Waraka wa Yuda kuwa sehemu ya Maandiko matakatifu.

Mtu wa ufarakano Lucifer wa Cagliari, Sardinia (mwaka 361- karibu 399 BK) anataja Yuda 1, 3, 4, 5, 8, 12

Epiphanius wa Salamis (mwaka 360-403 BK) anautaja Yuda 8

Jerome (mwaka 373-420 BK) anaitaja Yuda 8, 23

Augustine wa Hippo (mwaka 388-430 BK) anaitaja Yuda 1, 19

Cyril wa Alexandria (mwaka 444 BK) anaitaja Yuda 4, 5, 19

3. Ushahidi wa waasi na waandishi wengine

Priscillian (mwaka 385 BK) anaitaja Yuda 8

Pseudo-Hippolytus anazitaja 2 Pet 2:1 na 3:3 kwenye A Discourse on the End of the World sura ya 10 uk.244

4. Maandiko ya awali kabisa yaliyopo ya Yuda yanaonyesha kuwa kuna tofauti ndogo za maandishi, lakini hakuna makosa kwenye mafundisho ya msingi.

p72 Bodmer 7 & 8 Papyrii 1 Pet 1:1-5:14, 2 Pet 1:1-3:18 na Yuda 1-25, karibu mwaka 300 BK

p74 (=Bodmer 17) Matendo ya Mitume 1:2-5, 7-11, 13-15, 18-19, 22-25; 2:2-4; 2:6-3:26; 4:2-6, 8-27; 4:29-27:25; 27:27-28:31; Yakobo 1:1-6, 8-19, 21-23, 25, 27; 2:1-3, 5-15; 18-22, 25-26; 3:1, 5-6, 10-12, 14, 17-18; 4:8, 11-14; 5:1-3, 7-9, 12-14, 19-20; 1 Pet 1:1-2, 7-8, 13, 19-20, 25; 2:6-7, 11-12, 18, 24; 3:4-5; 2 Pet 2:21; 3:4, 11, 16; 1 Yoh 1:1, 6; 2:1-2, 7, 13-14, 18-19, 25-26; 3:1-2, 8, 14, 19-20; 4:1, 6-7, 12, 16-17; 5:3-4, 9-10, 17; 2 Yoh 1, 6-7, 13; 3 Yoh 6, 12; Yuda 3, 7, 12, 18, 24 (karne ya 7)

p78 (=papyrus Oxyrhynchus 2684) karibu mwaka 300 BK. Yuda 4-5, 7-8 The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts uk.602 unaonyesha kuwa maandishi haya si ya kutumainiwa sana. "kwenye mistari minne ina maandishi mawili ya pekee na matatu ambayo yametumika kwa uchache sana sehemu nyingine, yote haya yanapingana na vielelezo vya awali [uk.72]." (imenukuliwa kutoka Grenfell na Hunt Oxyrhynchus Papyrus, 34:4). Kutangulia si kuwa bora zaidi kila wakati.

Vaticanus [B] (mwaka 325-350 BK), Sinaiticus [Si] (mwaka 340-350 BK), na Alexandrinus [A] (karibu mwaka 450 BK) yana waraka wote wa Yuda.

Bohairic Coptic [Boh] karne ya 3/4

Sahidic Coptic [Sah] karne ya 3/4

Ephraemi Rescriptus [C] karne ya 5

Armenian [Arm] kutoka karne ya 5

Georgian [Geo] kutoka karne ya 5

Ethiopic [Eth] kutoka karibu mwaka 500 BK

 

Tazama www.BibleQuery.org/jdeMss.html kwa maelezo zaidi juu ya maandiko ya kale ya waraka wa Yuda.