Maswali ya Biblia Yona



S: Kwenye Yona 1, tunajua kitu gani kuhusu Nabii Yona?

J: Nabii Yona ametajwa pia kwenye 2 Fal 14:25. Yona alitokea Gath-heferi, mji uliokuwa karibu sana na Nazareti ya Galilaya. Kulikuwa na miaka miwili ambayo Waashuru hawakupigana (karibu mwaka 758-757 KK), na inadhaniwa kuwa Nabii Yona alitokea wakati huo. Kwenye 2 Fal 14:25, Yona anazungumzwa kutokea wakati huo, karibu na wakati wa utawala wa wafalme wa Ashuru Ashur-dan III (karibu mwaka 772-754 KK) na Ashur-nirari V (karibu mwaka 754-746 KK).

S: Kwenye Kitabu cha Yona, tunaweza kujifunza mambo gani?

J: Kitabu cha Yona kinafundisha kwa wakati mmoja mambo yasiyopungua matatu. Kwa urahisi kabisa, mambo hayo ni:
1.
Mungu anataka utiifu kamili, siyo utiifu nusu nusu. Hakuna mtu yeyote, hata nabii wa kweli, mwenye ruhusa ya kutokuendelea katika utiifu.
2.
Unaweza kumkimbia Mungu, lakini huwezi kujificha toka kwake. Mapenzi ya Mungu hayazuiliwi kamwe.
3.
Mungu anawapenda waliopotea, hata walio waovu. Sisi nasi tunapaswa tuwapende.

S: Kwa nini Kitabu cha Yona kimo kwenye Biblia?

J: Yona ni kitabu chenye kuvutia sana ambacho kina mada zisizopungua tatu zilizowekwa pamoja.
Rehema za kwa watu wote:
Mungu hakuwapenda Wayahudi tu. Aliwapenda watu wa mataifa na hata walio waovu.
Utiifu:
Nabii Yona hakuwa mtiifu kwenye eneo moja tu, lakini Mungu anataka utiifu mkamilifu. Kama unafikiri kutokutii kunafaa, hakikisha kuwa unaweza kukabiliana na matokeo yake.
Upendo wetu:
Hatupaswi kutafuta maarifa ya Mungu, na utakatifu wake tu, bali pia moyo wake. Maisha yetu yanatakiwa yajawe na upendo wa Mungu kwanza, kisha upendo wa watu wengine, hata walio waovu kama watu wa Ninawi.

S: Kwenye Kitabu cha Yona kuna mambo gani yanayofanana na Zaburi?

J: Inaonekana Nabii Yona alizifahamu Zaburi sana. Yafuatayo ni mambo yanayofanana.

Yona

Zaburi
 

Yon 2:2a

Zab 3:4; 120:1
 

Yon 2:2b

Zab 18:4-5; 30:3
 

Yon 2:3a

Zab 88:6-7
 

Yon 2:3b

Zab 42:7
 

Yon 2:4a

Zab 31:22
 

Yon 2:4b

Zab 5:7
 

Yon 2:5a

Zab 69:1-2
 

Yon 2:6b

Zab 49:15; 56:13; 103:4
 

Yon 2:7a

Zab 107:5; 142:3
 

Yon 2:8a

Zab 31:6a

"washikao yasiyofaa"

Yon 2:9a

Zab 50:14; 69:30; 107:22
 

Yon 2:9c

Zab 3:8; 37:39
 


S: Kwenye Yona 1, je kitabu hiki kinasimulia habari za kubuni kwani kina mambo ya kindoto?

J: Hapana. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo watu wengine wameyaona, pamoja na majibu yake.
Kumezwa na samaki mkubwa:
Ingawa huyu anaweza kuwa samaki aliyeumbwa kimiujiza, hakuna sababu ya kufanya lazima iwe hivyo. Kumekuwa na matukio mengine mengi ya watu kuliwa na samaki wakubwa (wanaoitwa ‘Jewfish’), kutapikwa, na kuishi hata kuweza kusimulia. Tazama majadiliano kwenye Yon 1:17 kwa maelezo zaidi kuhusu jambo hili.
Kwenda Tarshishi:
Tarshishi (Tartessus) Hispania kulianzishwa na Wafoenike karibu karne ya tisa au kumi KK, kwa hiyo hakuna shida ya kujaribu kwenda Tarshishi, kwani kuliisha kuwepo karne moja au mbili kabla ya Yona.
Dhoruba kubwa:
Upande wa masharki wa Bahari ya Mediterania huwa na dhoruba kubwa na za kushtukiza. Dhoruba nyingine unayoweza kusoma imeandikwa kwenye Mdo 27:13-38.
Kuwepo kwa mji wa Ninawi:
Kwa mujibu wa wataalamu wa elimukale, mji wa Ninawi ulikuwepo kuanzia mwaka 5000 KK. Ninawi imetajwa kwenye maandishi ya kale yenye umbo la kabari ya Mfalme Gudea (karibu mwaka 2200 KK) na Hammurapi (karibu mwaka 1700 KK). Kwa hiyo, inatarajiwa kuwa Ninawi ilifahamika kiasi kikubwa tu hata ikaweza kutajwa kwenye Mwa 10:11.
Ukubwa wa Ninawi:
Ninawi ulikuwa mji mkubwa hata kabla ya wakati wa Yona, kwa hiyo hakuna shida hapa. Mji wa Kala haukufikia hata nusu ya ukubwa wa Ninawi, na ulikuwa na watu 69,574 mwaka 879 KK.
Mfalme wa Ninawi
: Ninawi haukuwa mji mkuu wa Ashuru hadi Mfalme Senakeribu (mwaka 705-681 KK), muda mfupi tu baada ya huduma ya Yona. Hata hivyo, Asur-bani-pal II (mwaka 884/883-859 KK) na Shalmanesa III (mwaka 859-824 KK) walikuwa baadhi ya wafalme walioishi Ninawi kwa muda. Mji wa Ninawi ulikuwa ni moja ya makazi ya kifalme kuanzia mwaka 1100 KK na kuendelea.
Mfalme wa Ninawi dhidi ya Ashuru:
Himaya iliitwa Ashuru, siyo Ninawi, lakini lilikuwa jambo la kawaida kumuita mfalme wa taifa kama mfalme wa mahali mfalme alipoishi. Kwa mfano, Ahabu aliitwa mfalme wa Samaria (siyo Israeli) kwenye 1 Fal 21:2, Ahazia pia aliitwa mfalme wa Samaria (siyo Israeli) kwenye 2 Fal 1:3), na Ben-Hadadi anaitwa mfalme wa Shamu, mtawala wa Dameski (siyo Aramu/Shamu) kwenye 1 Fal 15:18; 2 Nya 16:2.
Mtango unaokua kwa haraka:
Ni kweli kuwa huu unaweza kuwa mmea wa kimiujiza. Kwa kawaida mmea wenye kukua kwa haraka zaidi ni mwanzi, unaoweza kukua hadi sm 91 (inchi 36) kwa siku.
Upepo wa mashariki:
Hakuna kitu cha ajabu kuhusiana na upepo wa mashariki kutokea juu milimani.
Kama Walter Kaiser alivyohitimisha kwenye Hard Sayings of the Bible, uk.332-333, "Hivyo, vipingamizi vya Kitabu cha Yona vinaishia kwenye jambo hili: kuna miujiza mingi sana!"

S: Kwenye Yon 1:2, je Mungu alisema kitu gani hasa alitaka Yona akikemee katika kuhubiri kwake? Unadhani kuna sababu gani mbili za agizo hili?

J: Biblia inasema ilikuwa ni kwa sababu ya uovu wa Ninawi ambao ulimfikia Mungu. Kuna njia tatu za kuangalia jambo hili:
1) Kuna watu ambao wangeweza kusikia mahubiri ya Yona na kutubu na kuendelea kumfuata Mungu baada ya hapo.
2) Watu wengine wa Ninawi wangesikia kabisa kuwa Mungu hakufurahishwa na uovu wao, na wawe na sababu zaidi ya kuhukumiwa kwa sababu walikuwa wameonywa.
3) Watu wengine wasiokuwa Waashuru wangesikia na kuona kuwa kuangamizwa kwa Waashuru wenye nguvu mno kulikuwa ni kazi ya Mungu.

Kwa ujumla, Mungu anapowaonya watu ni vema watubu. Lakini ni jambo bay asana endapo mtu atasikia onyo hilo lakini asilitii. Tazama Yeremia 42, hasa mistari ya 19-22 kwa maelezo zaidi kuhusu dhana hii.

S: Kwenye Yon 1:3, je Yona alikimbilia Tarshishi ipi?

J: Kuna miji mitatu iliyokuwa inaitwa Tarshishi, ambayo inatoa sehemu tatu ambazo nabii aliweza kuwa alikimbilia:
Sehemu ambayo haielekei kuwa yenyewe: Tarshishi (Tarso) iliyo Asia Ndogo:
Huu ni mji mkubwa kiasi wenye bandari uliokuwa karibu kilomita 16 (maili 10) kutoka Bahari ya Mediterania. Mtume Paulo alitokea hapo karne kadhaa zilizofuata. Haielekei kuwa Yona alielekea upande wa kusini kupanda meli kuelekea kwenye mji huu ulio mbali na bahari, wakati angeweza kutembea tu kwenda huko.
Sehemu ambayo inaelekea kuwa yenyewe: Tarshishi (Tartessus) iliyo Hispania:
Sehemu hii ina uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa ndipo mahali alipotaka kukimbilia. Mji wa Tarshishi, ambao umetajwa kwenye Herodotus 4:152, inaelekea kuwa ulikuwa magharibi mwa Gibraltar, mji uliokuwa Hispania au Ureno ya sasa. Ulikuwa ni mji ulioendelea zaidi upande wa magharibi wa wakati ule, mbali ya maendeleo ya Olmec huko Mexico. Mji wa Tarshishi ulianzishwa na Wafoenike kwenye karne ya tisa KK. Dhahabu, fedha, na shaba vilivyochimbwa hapo viliufanya mji huu kuwa moja ya kanda tajiri zaidi za Mediterania ya sasa. Mji huu ulikuwa umbali mkubwa zaidi ambao Yona angeweza kuufikia.
Sehemu ambayo haielekei kuwa yenyewe: Tarshishi iliyo Sardinia:
Neno la Kifoenike ‘Tarshishi’ linatokana na neno la Kiakadia lenye kumaanisha "kuyeyuka" au "kuyeyushwa kwa madini." Kwenye karne ya tisa, Wafoenike waliuteka mji uliokuwa maarufu kwa kuyeyusha madini wa Sardia ambao pia uliitwa Tarshishi. Tunajua jambo hili kwa sababu ya maandishi yaliyo kwenye jiwe la Nora. Hata hivyo, mbali ya jina hili, hakuna sababu nyingine ya kuuhusisha mji huu na Nabii Yona. Haukuwa maarufu kama Tarshishi ya Hispania, ingawa mji huu unaelekea kuwa ndiko kulikotokea madini ya fedha ya Mfalme Sulemani miaka ya baadaye.

S: Kwenye Yon 1:1-3, haijasema kuwa Yona alitamka neno "hapana" kwa Mungu. Inawezekanaje mtu kukaidi bila kutumia maneno?

J: Si lazima kusema neno lolote; mtu anaweza kufanya vitendo ambavyo viko kinyume na mambo ambayo Mungu anayapenda, na kuendelea kuyafanya. Haijalishi kama ukaidi ulitoa sauti kubwa au ulikuwa kimya kabisa, bado ni ukaidi.

S: Kwenye Yon 1:3, Nabii Yona aliukuta "mlango uliokuwa umefunguliwa" kwa namna ya meli ambayo angeweza kuipanda na kuondoka nayo. Lakini ni nani aliyempa Yona mlango huo ulio wazi? Tunapoukuta mlango ulio wazi, tunawezaje kujua endao ni Mungu au Shetani aliyetupa?

J: Kama ambavyo shetani alimpa Yesu "mlango ulio wazi" kwa namna ya njia rahisi ya kuwa mtawala wa ulimwengu, Shetani anaweza akatutengenezea milango iliyo wazi ili tujaribu kukimbia kumtii Mungu. Unapoona mlango ulio wazi si lazima uingie. Kwanza angalia Maandiko kisha muulize Mungu endapo hilo ndilo jambo analotaka ulifanye.

S: Kwenye Yon 1:3, kwa nini Yona alijaribu kumkimbia Mungu?

J: Maandiko hayasemi, lakini tunaweza kukisia. Yona alimwamini Mungu, alipenda kumwabudu na mumtumikia Mungu, na bila shaka alipenda kumtii Mungu kwa jumla. Hata hivyo, Yona hakutaka kumtii Mungu katika eneo hili; Yona anatuonyesha kwa muda mfupi tu sababu ya kufanya hivyo kwenye Yon 4:2.
Yona hakuwa na shida ya kuamini nguvu, ufahamu, au upendo wa Mungu. Badala yake Yona hakuwapenda Waashuru waliokuwa wakatili, lakini Mungu aliwapenda. Yona hakuipenda tabia hiyo ya Mungu, kuwa aliwapenda watu wakatili na watenda maovu. Kitu cha ajabu ni kuwa haiwezekani kumtetea Yona kwa kusema kuwa hakufahamu mambo yote yaliyohusika, au kwamba hakumjua Mungu kiasi cha kutosha.
Badala yake, Yona alichagua kuuchukia ukatili wa Waashuru, na kutoklizingatia jambo alilolifahamu fika kuwa Mungu aliwapenda. Leo hii, endapo kuna kitu kuhusu Mungu ambacho hukutaki, ni jambo zuri kuwa wazi kuhusu udhaifu wako huo. Hata hivyo, kumbuka kuwa ni wewe unayetakiwa kubadilika, na kuwa watu wote walio mbinguni watabadilika, na hakuna manufaa kukimbia hatma ya utakaso wako.

S: Kwenye Yon 1:3, 10, kwa nini Yona alikwendaYafa (iliyo karibu na miji ya sasa ya Jafneh na Tel Aviv)? Ni kitu gani kilichomtatiza kuifanya sababu iwe siri yake?

J: Ingawa kulikuwa na bandari nyingi za Kifoenike kwenye nchi ya sasa ya Lebanoni na pwani ya Shamu (Syria), hapakuwa na sehemu yeyote iliyofaa kuwa bandari ya Yafa, hadi Warumi walipoijenga bandari isiyokuwa ya asili ya Kaisaria karne kadhaa baadaye. Yona asingehitaji kufanya safari ndefu ya ardhini kwenda Yafa, lakini ilikuwa ndio bandari ya karibu zaidi kuelekea sehemu ambayo angeenda kupanda meli.

S: Kwenye Yon 1:3-10, Yona huenda alifahamu kuwa endapo angeenda umbali wa kutosha upande tofauti na kule alikoagizwa aende, lingekuwa jambo lenye kufaa kwa Mungu kumtumia mtu mwingine, badala ya yeye. Je tumewahi kufikiri namna hiyo?

J: Ni jambo rahisi sana kufikiri kuwa Mungu ana njia za kutenda mambo na vipingamizi sawa kabisa na sisi. Lakini Isa 55:8-11 inasema kuwa mawazo ya Mungu na njia zake si kama vyetu. Maneno yake yatafanikisha kitu ambacho alikusudia kukifanya.

S: Kwenye Yon 1:3-10, watu wachache sana kwenye nyakati za Agano la Kale walikuwa na Roho wa Mungu hata kuweza kutoa unabii, lakini kwa vile Yona alitoa unabii, aliwezaje kutokutii na kufanya kinyume na maagizo ya Mungu?

J: Muulize Balaamu. Endapo Mungu amekupa karama iwayo yote, jukumu lako la kuzitii amri za Mungu halipungui. Haja yako ya kuwa mwangalifu, kujichunguza mwenyewe kuona kuwa ungali unatembea na Bwana, haijaondoshwa kwako kama ambavyo haikuondoshwa kwa Mtume Paulo na watu aliowaandikia kwenye 2 Kor 13:5-6.

S: Kwenye Yon 1:3-10, je siku hizi tunayachukulia mapenzi ya Mungu kuwa kama mlo wenye vyakula anuwai, na tunachagua vile vinavyotuvutia?

J: ‘Smorgasbord’ ni sehemu ya kuuzia chakula ambayo walaji hujihudumia wenyewe yenye aina nyingi sana za vyakula zaidi ya mtu yeyote anavyoweza kula. Hivyo mtu huchukua kiasi kidogo cha kitu anachokitaka, na huacha kitu asichokitaka. Je unapenda kitindamlo zaidi, nyama zaidi, tunda kipenzi chako zaidi, uchaguzi ni wako. Lakini kumtumikia Mungu vizuri zaidi ni kama kuwa jeshini, ambako unakula kila kitu unachopewa.
Nyakati zingine watu wanataka kumtumikia Mungu "kwa njia zao wenyewe." Kwa nini usimtumikie kwa njia yake mwenyewe? Njia za Mungu za kumtumikia hazifanani kwa watu wote, kwa sababu tuna karama tofauti. Lakini jambo linalofanana kwa watu wote katika kumtumikia Mungu ni utiifu wa mambo anayoyataka, siyo mambo tunayoyataka. Wakati mwingine tunataka kuwa na huduma za zenye kupendeza Mungu, lakini vipaumbele vyetu maishani haviwi sawa na vipaumbele vya Mungu. Mwombe Mungu akuonyeshe vipaumbele vyake kwa maisha yako, na ujitoe kuvifuata kuliko vipaumbele vyako wewe mwenyewe.

S: Kwenye Yon 1:5, lengo kuu la safari hii ya majini lilikuwa ni lipi? Kwa nini walitupa shehena baharini?

J: Meli kubwa zilikuwa zinasafirisha abiria wachache, lakini lengo kuu la safari za haraka za meli kwenye Bahari ya Mediterania lilikuwa kusafirisha mizigo. Walipokuwa wanatupa vitu vilivyokuwa viende kuuzwa mahali meli ilikokwenda, walikuwa wanatupa lengo kuu la safari yenyewe. Jambo hili lilikuwa bay asana kifedha kwa mmiliki wa meli. Kutupa shehena kuliifanya meli iwe nyepesi, jambo ambalo lingeifanya ielee juu zaidi kwenye maji, na kuipa meli kina zaidi cha usalama endapo ingeanza kujawa na maji. Pia kungepunguza kwa kiasi kidogo uwezekano wa kugongwa na miamba ya kwenye maji.

S: Kwenye Yon 1:4-7, kwa kuwa Mungu hataki tufuate imani ya kishirikina ya kutegemea bahati, kwa nini kupiga kura kulikuwa kwenye manufaa kwa mabaharia hawa? Je kupiga kura ni kitu kizuri kwa ujumla?

J: Kupiga kura si lazima kuwe njia nzuri ya kujua jambo. Kwa ujumla, wakati watu wasioamini wanapofanya kitu kwenye Biblia, hata Mungu hubariki juhudu zao [zinazoweza kuwa] potofu, jambo hilo halimaanishi kuwa kitendo hicho kinakubalika kwa waamini.
Kwenye Biblia, waamini mara nyingine wanapiga kura pia. Kwa mfano, mitume walipiga kura, na imerekodiwa, bila kuungwa mkono au kupingwa kwenye Mdo 1:24-26.

S: Kwenye Yon 1:6, Nabii huyu alikuwaje amelala hapa?

J: Inaelekea kuwa Yona hakujali sana kuwa kinyume na mapenzi ya Mungu. Yona alikuwa amelala fofofo kwa njia zisizopungua tatu.
Kimwili:
Ama Yona alikuwa amechoka kimwili hata akalala wakati wa dhoruba kali, ama Mungu alimpa usingizi mzito ili apumzike, kwa sababu huu ungekuwa ndio usingizi mzuri zaidi ambao angekuwa nao katika kipindi kile.
Kiroho:
Yona alikuwa muumini ambaye ambaye mapenzi yake yanapingana kabisa na Mungu. Efe 5:14 pia inazungumzia kuhusu waumini kutokulala kiroho.
Kiakili:
Endapo Mungu anakuagiza moja kwa moja kufanya kitu, mtoto yeyote anayemfuata Mungu anajua kuwa Mungu anaweza kukuzuia endapo humtii. Huenda Yona alifikiri kuwa Mungu atampuuzia tu endapo "atakwenda mbali ya upeo" wa Ninawi.

S: Kwenye Yon 1:6, je nahodha alimchukia Mungu wa Kweli, kwani anaonyesha kuwa hamwamini Mungu Pekee na wa Kweli, kwa nini alimtaka Yona amwombe Mungu wake (Yona) ? Je kuna watu leo hii wenye fikra za aina hii?

J: Imani za watu wengi ‘hazifuati mfumo mmoja.’ Nahodha huyu alifikiri kuwa halingeweza kuwa jambo baya, na lingeweza kusaidia. Watu wengine hawamkatai Mungu moja kwa moja, lakini badala yake wanataka kumweka Mungu pekee wa Kweli pamoja na miungu yao mingine. Wakristo wengi wa awali waliuawa, si kwa sababu ya kumwabudu Mungu, lakini kwa sababu ya kukataa kumwabudu mtu mwingine yeyote zaidi ya Mungu.

S: Kwenye Yon 1:7, jambo hili linafananaje na mamajusi kwenye Mat 2:1-3?

J: Mungu anaweza kutumia njia yeyote ili watu wasiomwamini waweza kupata habari. Kwa mfano, mamajusi walipoongozwa na nyota, jambo hili halimaanishi kuwa Wakristo wawe wanaangalia nyota kumtafuta Masihi.
Mungu hakusema kuwa analazimika kutumia njia nzuri tu kuwaleta watu kwake. Mara nyingine Mungu hutumia njia za uovu, kama vile jeshi la Babeli (Hab 1:6, 13). Mungu anaweza kutumia magonjwa, watu waovu, na hata dhambi zisizokuwa za makusudi (kama ilivyokuwa kwa mamajusi) kuwaleta watu kwake.
Cha kushangaza zaidi ni kwamba amewahi kutumia dhambi za kudhamiria za waumini kuwaokoa waumini wenyewe. Unaweza kusoma kuhusu jambo hili kwenye habari ya Yusufu na kaka zake kwenye Mwanzo 37 na 50, hasa Mwa 50:20. Ukweli ni kwamba Mungu anaweza kuyafanya mambo yote kuwa mema (Rum 8:28) na kwa ajili ya makusudi yake (Efe 1:11).
Kwa kuhitiisha,
kama jinsi Mungu alivyotumia kutekwa kwa Yusufu kwa makusudi yake hakuhalalishi utekaji watu, kutumiwa kwa unajimu kutimiza malengo ya Mungu hakuuhalalishi unajimu.

S: Kwenye Yon 1:7, je maneno "kazi yako ni kazi gani" yanamaanisha nini?

J: Huenda yakamaanisha "unajfanya nini (kama shughuli ya kujipatia riziki)", au inaweza kumaanisha "unafanya kitu gani (kwenye meli hii)."

S: Kwenye Yon 1:8-10, kwa nini waliogopa Yona aliposema kuwa anamwabudu Mungu aliyeziumba bahari nan chi kavu? Wao hawakuwa wanamwabudu Mungu pekee wa kweli.

J: Hawakumwamini Mungu pekee wa kweli, lakini pia hawakumkana. Wapagani walikuwa na desturi ya kuikubali miungu mipya, na endapo kulikuwa na hoja kuwa aliiumba bahari, basi Mungu huyu ndiye anayepaswa kutambuliwa mwenye umuhimu kwenye mazingira haya. Watu wengine wanafanana na hivi siku hizi. Hawamkubali Mungu pekee wa kweli, lakini pia hawamkani. Wanapenda kuwa kati kwa kati.

S: Kwenye Yon 1:11-15, je watu hawa walifanya sawa kumtupa Yona baharini, jambo ambalo lilionekana kuwa ni kifo cha hakika?

J: Kwa kawaida hawakufanya sawa. Lakini walikuwa wanakabiliwa na hatari, na Yona aliwaambia wafanye hivyo, walifanya kile ambacho walidhani wanatakiwa kufanya.

S: Kwenye Yon 1:16, je mabaharia hawa walifanyika waumini wa Mungu wa kweli?

J: Maandiko hayasemi moja kwa moja. Huenda:
a) waliongoka na kuanza kumwabudu Mungu pekee wa kweli,
b) walimheshimu tu Mungu wa kweli, na walijitoa dhabihu kwake, huku wakiendelea kutoa dhabihu kwa sanamu.

S: Kwenye Yon 1:16, ni kwa namna gani kutokutii kwa Yona kuliwafanya mabaharia wamwabudu Mungu wa kweli?

J: Mara nyingine Mungu hufanya mambo ya ajabu kwa njia zisizokuwa za kawaida. Mungu hawezi kutumia vitu vizuri tu kufanya mambo yawe mazuri, lakini Rum 8:28 inasema kuwa Mungu hufanya mambo yote kuwa mema kwa watu wanaomwamini. Efe 1:11 hata inaenda mbele zaidi na kusema kuwa Mungu hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yale. Hata mambo ambayo Mungu hakuyapenda, ana nguvu za kuyafanya kama sehemu ya mapenzi yake.

S: Kwenye Yon 1:16-17, kunatokea nini wakati mtu au taifa linalimcha Mungu, wanapoacha kufanya mambo ambayo Mungu anayataka?

J: Matokea yanaweza kuwa tofauti. Mungu anaweza kuchagua kutenda kitu ili kumwonyesha mtu huyo umuhimu wa matendo yake kwa Bwana. Au Mungu anaweza kufanya kitu ambacho hakifurahishi, na kuwakaripia watu hao ili waweze kumrudia. Au Mungu anaweza akaamua kuachana nao, na kutowatumia tena, kama kifaa kisichokuwa na faida. Au Mungu anaweza kufanya mambo yote hayo hapo juu kwa mfuatano, kutegemeana na itikio letu.

S: Kwenye Yon 1:17-2:1, kwa unafikiri Mungu huwa anafanya mambo ambayo hayana ufanisi wakati mwingine?

J: Mungu haitaji kuharakisha; anao muda wa kutosha hapa duniani. Mungu haitaji kukusanya nguvu; ana nguvu zote. Mungu haitaji kujua undani zaidi wa jambo lolote lile; tayari anajua kila kitu. Mungu anapendezwa na njia (mchakato) wa mambo, na si matokeo tu.

S: Kwenye Yon 1:17-2:1, je samaki mkubwa alikuwa ndio jibu la maombi ya Nabii Yona?

J: Hapana, kwa sababu Yona alikwisha kuwa ndani ya samaki alipokuwa anaanza kusali, kwa mujibu wa Yon 2:1.

S: Kwenye Yon 1:17 na Mat 12:40, samaki huyu aliwezaje kuwa nyangumi kwani ni nyangumi mwenye meno na kichwa kikubwa tu aliye na koo kubwa liwezalo kummeza mtu mzima, na nyangumi wa aina hii hawapatikani kwenye Bahari ya Mediterania?

J: Kuna mambo manne yanayowezekana hapa:
1.
Samaki wakubwa wanaotumika kwa michezo na chakula wenye kupatikana kwenye maji ya joto ya mwambao (wanaoitwa ‘Jewfish’) ni aina mbalimbali za sangara wakubwa. Wengi wao waliweza kufikia karibu kilo 227 hadi 318 (paundi 500 hadi 700) na urefu wa karibu mita 2 hadi 4 (futi 7 hadi 12).
2.
Nyangumi papa (Rhineodon typicus) wamewahi kumeza binadamu ambao baadaye walikutwa wakiwa wazima kwenye matumbo yao.
3.
Nyangumi wenye meno, vichwa vikubwa na koo pana wanaweza kumeza vitu vizima vizima. Mmoja wao alimmeza papa mwenye urefu wa karibu mita 5 (futi 15). Jambo hili liliandikwa na Frank T. Bullen, kwenye Cruise of the Cachalot Round the World after Sperm Whales (mwaka 1898).
Mwaka 1771, Marshall Jenkin alimezwa na nyangumi mwenye meno na kichwa kikubwa pamoja na koo pana. James Bartley pia alimezwa na nyangumi mwenye meno na kichwa kikubwa pamoja na koo pana mwaka 1891. Toleo la Oktoba 1928 la Princeton Theological Review linaonyesha kuwa baadhi ya maelezo ya simulizi ya Bartley hayako sahihi, lakini ushahidi wa kukosekana kwa usahihi wa baadhi ya maelezo haumaanishi kuwa tukio zima si kweli.
Ingawa nyangumi wenye meno, vichwa vikubwa na koo pana hawapatikani kwenye Bahari ya Mediterania, wanaweza kuogelea umbali mrefu, na Mungu angeweza kumfanya mmoja wapo aogelee hadi Mediterania. Kanusho la Asimov la kuwepo kwa nyangumi wenye meno, vichwa vikubwa na koo pana kwenye Bahari ya Mediterania kunahitaji kudhania kuwa hakuna Mungu anayefanya mambo yatokee.
4.
Alikuwa ni samaki wa pekee, aliyetayarishwa maalumu na Mungu kwa lengo hili. Hata hivyo, huenda jambo hili halikuwa la lazima, kuna aina nyingine tatu za samaki ambao si kuwa wanaweza kummeza binadamu aliye hai lakini pia wamewahi kufanya hivyo.
Kuna masimulizi mengine ya watu waliomezwa wakiwa hai na samaki mkubwa na wameishi kusimulia mikasa hiyo. Mmoja wa watu hawa ni mtu aliyekuwa anasafiri majini kutokea pwani ya New England kwenye miaka ya 1800. Simulizi ya karibuni zaidi ilichapishwa kwenye Dallas Morning News miaka ya 1970 kuhusu mkasa uliotokea kwenye Ghuba ya Mexico.

S: Kwenye Yona 2, jambo hili lililompata Nabii Yona linawezaje kufananishwa na agizo la Mtume Paulo la kumtoa kwa shetani muumini mzinifu kwenye 1 Kor 5:4-5?

J: Paulo aliagiza kumtoa kwa shetani muumini mzinifu kama njia ya kumuadhibu. Shetani anaweza kudhaniwa kuwa mtumishi aliyelazimishwa wa Mwenyezi Mungu hapa. Jambo hili halitamfurahisha muumini mzinifu, lakini linaweza kumshitua ilia take kutubu.
Kuadhibiwa na Mungu kunaweza kuwa kama kwenda kuvua samaki wakati wewe mwenyewe ni mnyoo. Maandiko hayasemi endapo Yona alipenda kwenda kuvua samaki tena baada ya mkasa huu.

S: Kwenye Yona 2, unawezaje kumweleza muumini au mtu asiye muumini aliye mwovu na mzinifu umuhimu wa kumtii Mungu?

J: Mwalimu mkubwa wa Biblia Chuck Swindoll alisema kuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanasumbuliwa na zinaa aliowapa ushauri nasaha, wengi wao walikuwa wakiangalia tu furaha ya wakati wa kufanya tendo. Unaweza kuwaambia waangalie matokeo ya vitendo vyao kwa wakati huu kwa watu wanaowazunguka, wale wanaojua na wale wataoweza kufahamu baadaye. Waambie wafikirie wakati ujao, na jinsi watakavyojibu mbele za Mungu. Waambie wafikirie thawabu zao mbinguni, au jinsi watakavyopoteza thawabu zao. Je kukosa thawabu milele mbinguni ni kitu chenye thamani ndogo kuliko furaha ya dhambi ya muda mfupi, inayofuatiwa na hatia? Lakini kama hawayajali mambo haya yote, huenda hawapaswi kujali thawabu za mbinguni. Badala yake wanatakiwa kujali kuepuka moto wa milele kwenye ziwa la moto katika mauti ya pili. Endapo hawajali mambo haya ya milele, basi labda hawajawahi kuwa na wokovu wa milele.

S: Kwenye Yona 2, kuna faida gani kubwa unapokuwa umelala chali chini? Je kuna wakati wowote katika maisha yako ulipokuwa umelala chali na Mungu aliutumia?

J: Faida moja ni kuwa huwi na mahali pengine pa kuangalia. Wakati mwingine Mungu anawalaza watu chali ndipo wanamwangalia.

S: Kwenye Yon 2:1, je Yoona alikufa kweli?

J: Hapana hakufa. Baadhi ya Wakristo kama J. Vernon McGee, wanasema kuwa mstari huu unaonyesha kuwa Yona alikufa kweli ndani ya yule samaki, na Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. R.A. Torrey kwenye Difficulties in the Bible, uk.115-116, pia anafikiri kuna uwezekano kuwa Yona aliruhusiwa kufa.
Lakini Yona hakufa, kwa sababu kama angekuwa amekufa, basi alikwenda wapi? Ikiwa Yona alikwenda paradiso walikoenda wenye haki, angekuwa na furaha, na asingependa kuondoka. Ikiwa kwa sababu yeyote ile alikwenda kifungoni walikoenda waovu, basi maji ya baridi yasingekuwa kitu cha kusumbuka nacho. Maneno "katika tumbo la kuzimu" ni sitiari ya kishairi ya kufukiwa baharini. Yona alitambua kuwa samaki huyu anakwenda kuwa jeneza lake halisi kama Mungu hatamuokoa. NIV Study Bible, uk.1367 inatoa maoni haya.
Vyovyote ilivyokuwa,
Wakristo wote wanakubaliana kuwa endapo Mungu alipenda angeweza kumfanya Yona awe hai ndani ya yule samaki, au Mungu angeweza kumwacha Yona afe na kisha kumfufua ndani ya yule samaki.

S: Kwenye Yon 2:2-9, Yona angewezaje kuomba kwa lugha ya ushawishi namna hiyo baada ya tukio hili lenye kutia kiwewe?

J: Yona alikuwa na muda mwingi sana, bila vitu vya nje vyenye kuvurugu usikivu wake, hivyo angeweza kufikiria njia zake na kufanya maombi. Yona angeweza "kuyanakishi maombi yake." Hata hivyo, maombi ya Yona yanaweza kuwa itikio lililonakishiwa na ombi "toka moyoni mwake", itikio la kihisia lililotokana na mkasa wa kumezwa na samaki.

S: Kwenye Yon 2:4, 6, 7-8, je Yona alikuwa na tabia gani yenye kudumu? Tunawezaje kujenga tabia hiyo?

J: Pamoja na fikra mbaya alizokuwa nayo Yona za kutokutii na kutokuwa na upendo, Yona alikuwa na imani kubwa kuwa Mungu angemuokoa na kuwa angeweza kuliona hekalu tena, japo kule mbinguni. Ingawa maisha ya Yona yalikuwa yanadhoofika, alikuwa na matumaini kuwa ataliona hekalu la Mungu tena.

S: Kwenye Yon 2:6, ni kwa jinsi gani dunia ilimfunga Yona?

J: Fikiria hatari aliyokuwa nayo Yona, akijua kuwa alikuwa chini kabisa kwenye kilindi cha bahari. Alikuwa na aina ya klaustrofobia (woga aupatao mtu awapo shimoni) ya kiwango cha juu sana. Lugha ya kishairi ya Yona kwenye 2:5-6 inasema kuwa alikuwa chini kuliko mizizi ya milima mirefu zaidi baharini.
Leo hii, kama utajisikia mnyonge zaidi, kumbuka kuwa kuna manufaa ya kushushwa na kulala chali: ni rahisi zaidi kuangalia juu. Nabii ambaye alikuwa anajua mambo mengi zaidi alikosa utiifu kwa kiasi kikubwa sana na akakimbia. Yona aliadhibiwa sana, lakini muda ulipita, naye akarejeshwa na kutumiwa tena na Mungu.

S: Kwenye Yon 2:8, je watu wanaojihusisha na sanamu vipi na rehema zao wenyewe? Vipi kuhusu nadharia kuwa Mungu aliishaamua kabla?

J: Kuamua kabla ni neno lililo kwenye Biblia (Rum 8:29; Efe 1:11) lakini HALIMAANISHI kuwa Mungu anastahili kulaumiwa kwa mtu atakayekosa kwenda mbinguni. Watu walio jehanamu hawawezi kusema kwa ukweli kuwa "Mungu amenilazimisha", "ni makosa ya Mungu", au "Mungu hakunipa nafasi." Kitu pekee wanachoweza kusema ni kuwa yalikuwa makosa yao wenyewe, na hata kama hawakujua vitu vyote ambavyo wangeweza kuvijua, waliukataa ukweli waliopewa.

S: Kwenye Yon 2:8, ni kwa njia zipi sanamu haziwi na thamani?

J: Hazina thamani kimwili, kiroho, na kwa kuambukiza.
Kimwili, sanamu hazina thamani; hata kama mti ungechomwa tu, ungefanya jambo la maana kuliko sanamu inavyofanya.
Kiroho, ziko mbali sana na Mungu.
Sanamu pia hazima thamani kwa namna ya uambukizi. Watu wanaoziabudu na kuziamini hukosa thamini pia kiroho.

S: Kwenye Yon 2:9-10, unadhani Mungu alikuwa anangojea kitu kwa uvumilivu hapa? Unadhani Mungu anangojea kitu maishani mwako?

J: Mungu hajafanya kitu chochote chenye kuonyesha kuwa angefanya jambo lolote "endapo" Yona angefanya kitu. Wakati Yona ameonyesha huzuni kwa sababu ya kuwa kwenye tumbo la samaki mkubwa, Mungu alimsikia. Wakati Yona "amerejesha kiapo chake" na kumweleza Mungu kuwa atafanya jambo analotakiwa kulifanya, kitu kinachofuatia ambacho Maandiko yanatuambia ni kuwa Yona alikuwa nchi kavu nje ya samaki.

S: Kwenye Yona 3-4, kwa nini Mungu alimfanya Yona atoe unabii kuwa watu wa Ninawi wataangamia na kisha walisamehewa?

J: Tabia ya Mungu haibadiliki, na hatima ya mapenzi ya Mungu haibadilika. Hata hivyo, mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa kwa mtu au watu yanabadilika watu wanapotubu na kubadilika, kama Yer 18:1-11 inavyoonyesha.
Kuna mifano mingine mingi ya jambo hili kwenye Biblia ikiwemo Mwa 20:3-7, 2 Fal 20:1-6, na hata utabiri kuwa mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa kwao yatabadilika kwenye Kum 28:68.
Kumbukumbu la kihistoria ni kuwa inaelekea swali hili lilijibiwa karibu mwaka 207 BK na Tertullian kwenye Against Marcion kitabu cha 2 sura ya 23, uk.315.
Tazama maelezo ya Mwa 20:3-6; Kut 33:5-6; Kum 20:17; Yer 15:6; Yon 3:10 na 4:1-2 kwa habari zaidi.

S: Kwenye Yona 3-4, kwa nini watu wa Ninawi walitubu?

J: Kwenye masimulizi ya siku hizi ya watu walionusurika baada ya kumezwa na samaki wakubwa wanaotumika kwa michezo na chakula wenye kupatikana kwenye maji ya joto ya mwambao (wanaoitwa ‘Jewfish’), ngozi zao zilionekana kama zimetolewa rangi. Bila shaka Nabii Yona alionekana tofauti alipokwenda Ninawi.
Zaidi ya hapo, Mungu anaweza kuwa alitumia vitu vingine zaidi kabla ya kufika kwa Yona karibu mwaka 758-757 KK.
Pigo la Ninawi mwaka 765 KK.
Jeshi lililokuwa na nguvu zaidi lilidhoofika kabla ya pigo.
Kupatwa kwa jua tarehe 6/15/763 KK.
Watu wa zamani waliogopa sana kupatwa kwa jua, na Waashuru pamoja na watu wengine waliona jua likipatwa mwaka 763 KK.
Pigo lingine Ashuru mwaka 759 KK.
Hili lilitokea karibu mwaka mmoja au miwili kabla ya kuja kwa Yona.

S: Kwenye Yon 3:1-2, Yona hakutii na alimwangusha Mungu kwa kiasi ambacho Mungu alikiona kuwa ni kikubwa. Inawezekanaje mtu aliyekosa kumtii Mungu kwa kiasi kikubwa kama hicho amtumikie tena, hasa kwa kuwaambia watu kuwa wanatakiwa kutubu na kumgeukia Mungu?

J: Nguvu ya ujumbe haikuwemo kwenye utiifu wa Yona, au kitu chochote kilichomhusu Yona. Nguvu ya ujumbe ilikuwa kwa Mungu. Yona hakuweza kufanya kitu chochote kuhusu kutokutii kwake kwa zamani ambako aliishatubu. Wakati huu ulikuwa wa kuinika na kuendelea mbele, mara hii kwa kufuata maelekezo ya Mungu siyo yake mwenyewe.
Yona alijua kuhusu kutubu, na aliweza kuwaambia watu wengine namna ya kufanya hivyo, bila kupata magumu kama aliyoyapata Yona.

S: Kwenye Yon 3:1, je Yona alikuwa na haja ya kuagizwa na Mungu tena?

J: Kwa ujumla ndiyo, kwani tunapaswa kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Mungu na kumwomba atuonyesha endapo tunaenenda katika njia isiyo bora zaidi. Tunaweza tusiwe tunaenda kwenye njia mbaya, lakin pia tunaweza kuwa hatuendi kwenye njia ambayo Mungu anataka tuende.
Hata hivyo, habari ya Yona inaleta mjadala kwani Mungu anaelekea kuongea kwa njia sahihi. Inawezekana kuwa baada mtumishi wa Mungu kama Yona kuasi, mtumishi huyo atahitaji kuhakikishiwa na Mungu kabla ya kuendelea na huduma aliyopewa kabla ya kuasi. Mungu alito uthibitisho huo.

S: Kwenye Yon 3:2, je Yona alinyimwa raha kuwa hakuwa na ujumbe aliotakiwa kuutoa? Nasi je tunapaswa kukosa raha endapo Mungu anatuita kwenye huduma na mambo hayaendi kama yanavyotarajiwa?

J: Sivyo kabisa. Inaonekana kuwa Mungu alipenda Yona aongee na watu wa Ninawi zaidi ya Yona alivyotaka kuongea nao. Mungu aliyemfikisha Yona mahali hapa, aliyewapenda sana watu wa Ninawi hata akamtuma samaki mkubwa kuliko kumwacha Yona atokomee, asingeshindwa kumpa Yona maneno ya kusema, wakati yalipotakiwa.

S: Kwenye Yon 3:3 na 4:11, ilikuwaje Ninawi uwe mji mkubwa ukiwa na watu 200,000?

J: Mji wa Kala ulikuwa chini ya nusu ya Ninawi, na mwaka 879 KK ulikuwa na wakazi 69,574. (Takwimu hizi zinatokana na maandishi ya Asurnasirpal II (mwaka 883-859 KK, ambapo aliwaalika kwenye sikukuu watu 69,574 wa Nimrodi.
Siku tatu hazimaanishi kutembea kwenye eneo wazi, lakini muda wa kufika sehemu mbalimbali za mji. Mji wenye kipenyo cha kilomita 26 (maili 16) utakuwa na mzingo wa karibu kilomita 80 (maili 50), na unaweza kuwa na watu karibu 600,000.

S: Kwenye Yon 3:3-4, unadhani Yona alijiona kuwa salama wakati anatembea kwenye mji huu uliojaa mauaji?

J: Yona anaweza kuwa alijona kuwa salama zaidi miongoni mwa watu wa Ninawi waliokuwa waovu, waliofurahia kutesa wengine, akiwa kwenye mapenzi ya Mungu, kuliko kuwa peke yake wakati amekasirikiwa na Mungu. Kwa hiyo Yona anaweza kuwa alijiona kuwa salama zaidi kwenda Ninawi, huenda hakuwa na furaha pia. Kwa jinsi hiyohiyo, sisi nasi, na thawabu zetu za mbinguni, tu salama zaidi tukipitia sehemu zisizokuwa salama, tunapotii mapenzi ya Mungu, kuliko kujifanya kuwa salama kwa kujaribu kumkimbia Mungu. Natumaini kuwa tunaweza kutafakari somo hili kwa haraka zaidi kuliko alivyofanya Yona.

S: Kwenye Yon 3:5, ni jambo gani lenye kufurahisha kuhusu jina la Mungu hapa?

J: Hadi kufikia Yon 3:4, jina pekee la Mungu lililotumika ni BWANA (Yahweh), isipokuwa kwa mabaharia waliotumia jina elohim walipokuwa wanaongelea miungu kwa jumla. Kuanzia Yon 3:5, jina Elohim linatumika kwa ajili ya Mungu wa kweli.

S: Kwenye Yon 3:5, 6, 8, nguo za magunia ni nini?

J: Nguo za magunia zilikuwa ngumu na hazikufurahisha sana kuzivaa. Watu walizivaa kama ishara ya majuto na toba.

S: Kwenye Yon 3:6, kwa nini mfalme anaitwa Mfalme wa Ninawi?

J: Alikuwa mfalme wa Ashuru, si Ninawi. Tunaweza kukisia sababu mbili:
Mtazamo wa Yona:
Yona alikwenda Ninawi, makazi ya mfalme wa Ashuru. Bila kujali nchi ambazo Ashuru iliziteka, ambazo zilikuwa zinapinga utawala wake, alikuwa mfalme wa Ninawi.
Watu ambao Yona aliwaandikia kitabu hiki:
Kwa sababu alikuwa mfalme wa Ashuru, alikuwa mfalme wa miji ya Ashuru. Ilikuwa ni rahisi na sahihi kumwita mfalme wa mahali alipokwenda Yona.
Halikuwa jambo geni kumwita mfalme kwa jina la mji wake mkuu. Kwenye 1 Fal 21:1, Ahabu mfalme wa Israeli, anaitwa mfalme wa Samaria. Vivyo hivyo, Ahazia, mfalme wa Israeli, pia anaitwa mfalme wa 2 Fal 1:2, na Ben-Hadadi Mfalme wa Aramu anaitwa mfalme wa Dameski kwenye 2 Nya 24:23.

S: Kwenye Yon 3:6, je hatua yakwanza kabisa ya kutubu ni ipi hapa?

J: Kama ishara ya unyenyekevu mbele ya Mungu, mfalme aliinuka toka kwenye kiti chake cha enzi. Hatua ya kwanza ni kuinuka toka kwenye kiti cha enzi, kukiri kuwa sisi si mabwana wa maisha yetu na wala hatutaki kuwa hivyo, na badala yake tutafanya mambo ambayo Mungu anataka, na kuacha kufanya mambo ambayo Mungu hataki tufanye.

S: Kwenye Yon 3:7, kwa nini amri ilitolewa na mfalme na watu wenye nyadhifa kubwa, na kwa nini watu wenye nyadhifa kubwa walifunga?

J: Ashuru ilikuwa ni nchi ya kijeshi, na watu wake wenye nyadhifa walikuwa makamanda wa kijeshi. Endapo mfalme alikosa kuungwa mkono na makamanda wa kijeshi aliuawa baada ya muda mfupi tu. Watu wenye nyadhifa walipenda kuepusha pigo kwa sababu endapo ingesikika kuwa wengi wa viongozi wakuu wa jeshi wameuawa na askari wengi na wagonjwa, jambo hilo lingeweza kusababisha watu wengi walipenda kulipi kisasi kwa Ashuru kuinuka dhidi yake. Watu wa Urartu, pamoja na Manai na Madai waliungana kupanua mipaka yao hadi kufikia umbali usiozidi karibu kilomita 161 (maili 100) kutoka mji wa Ninawi, kati ya mwaka 782 na 745 KK.

S: Kwenye Yon 3:7, unafanyaje ili kuwafanya watu wengine watubu?

J: Jambo hili lilikuwa rahisi kwa mfalme wa Ashuru, angeweza kutoa tangazo, likifuatiwa na adhabu kwa mtu yeyote ambaye hangetii. Mambo hayawi hivyo kwetu leo hii. Lakini pamoja na hilo, mfalme aliinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, na kutoa mfano kwa kufunga na kuvaa nguo za magunia. Leo hii tunaweza kuwaambia watu kuwa wanahitaji kutubu, kutoa mfano, na kuwatia moyo watubu.

S: Kwenye Yon 3:7, tunawezaje kutoa picha ya kuvaa nguo za magunia leo hii?

J: Tunaweza kuvaa majuto, na bangili nyeusi, au kujinyima kitu ambacho kwa kawaida ni sawa kukifanya, kama ishara ya kujuta kwetu kwa ajili ya mtu au watu. Mungu na watu wengine wanasikia mawasiliano yetu, na tunawasiliana si kwa maneno tu.

S: Kwenye Yon 3:7, kwa nini Waashuru waliwashirikisha hata wanyama kuonyeshatoba?

J: Ingawa wanyama hawangeweza kujua mambo yaliyokuwa yanaendelea, jambo hili lilikuwa ni juhudi ambayo Waashuru waliifikiria ya kuonyesha kujuta kwao na kumfurahisha Mungu. Kihistoria, walikwisha kuwa na mapigo mawili, na Waashuru ambao walikuwa na Himani za kishirikina waliliona jua likipatwa. Huu si wakati pekee watu wa ukanda ule walipojuta pamoja na wanyama. Mwana historia Herodotus kwenye Histories kitabu cha 9 sura ya 24, uk.292-293 anaelezea jinsi Waajemi walivyonyoa nywele za vichwa vyao na kukata manyoya ya kwenye shingo za farasi na punda wao baada ya Masistius, kamanda wa kikosi cha farasi, kufa katika mapigano dhidi ya Wagiriki.

S: Kwenye Yon 3:8, je Mungu alisikiliza maombi ya watu hawa wasioamini? Je walikuwa wanaomba ili kupata wokovu?

J: Ingawa hatujui vitu walivyoomba, tunajua kuwa walimwomba Mungu ayapishiliye mbali nao maafa yaliyokuwa yaliyokuwa karibu kuwafikia.

S: Kwenye Yon 3:9, je walikuwa na uhakika gani kuwa toba yao ingeweza kusaidia kwa namna yeyote kuhusiana na matokeo yao ya baadaye?

J: Watu wa Ninawi hawakuwa na uhakika wowote, walitumaini tu. Walijua kuwa Mungu alichukizwa nao kwa sababu ya uovu wa ukatili wao, na walijua kuwa Mungu alitaka waache na kutubu. Leo hii tuna uhakika mkubwa zaidi. Mungu atatuokoa tunapotubu na kuja kwake. Hata hivyo, wakati mwingine tunaweza kupata madhara ya dhambi zetu katika maisha haya.

S: Kwenye Yon 3:9, je ni vema kuwaambia watu wasioamini kuhusu hasira kubwa sana ya Mungu?

J: Ndiyo, katika tuko hili kulisaidia kuwafanya watubu.

S: Kwenye Yon 3:10, kwa nini Mungu alimfanya Yona atoe unabii kuwa watu wa Ninawi wataangamia na kisha walisamehewa?

J: Tabia ya Mungu haibadiliki, na hatima ya mapenzi ya Mungu haibadilika. Hata hivyo, mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa kwa mtu au watu yanabadilika watu wanapotubu na kubadilika, kama Yer 18:1-11 inavyoonyesha.
Kuna mifano mingine mingi ya jambo hili kwenye Biblia ikiwemo Mwa 20:3-7, 2 Fal 20:1-6, na hata utabiri kuwa mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa kwao yatabadilika kwenye Kum 28:68.

S: Kwenye Yon 3:10, kwa nini watu wa Ninawi walitubu?

J: Katika masimulizi za miaka ya karibuni ya watu walionusurika baada ya kumezwa na samaki wakubwa wanaotumika kwa michezo na chakula wenye kupatikana kwenye maji ya joto ya mwambao (wanaoitwa ‘Jewfish’) ngozi zao zilionekana kupauka sana. Bila shaka Nabii Yona alionekana tofauti alipokwenda Ninawi.
Mungu anaweza kuwa alitumia vitu vingine zaidi kabla ya kufika kwa Yona karibu mwaka 758-757 KK.
Pigo la Ninawi mwaka 765 KK.
Jeshi lililokuwa na nguvu zaidi lilidhoofika kabla ya pigo.
Kupatwa kwa jua tarehe 6/15/763 KK.
Watu wa zamani waliogopa sana kupatwa kwa jua, na Waashuru pamoja na watu wengine waliona jua likipatwa mwaka 763 KK.
Pigo lingine Ashuru mwaka 759 KK.
Hili lilitokea karibu mwaka mmoja au miwili kabla ya kuja kwa Yona.

S: Kwenye Yon 3:10, je Mungu alighairi vipi uovu ambao alisema kuwa angeufanya?

J: Kuna mambo mawili ya kuyazingatia katika kujibu swali hili:
1.
Neno "uovu" kwa Kiebrania lina maana mbili: uovu wa mwenendo, na ubaya na uchungu wa kimwili.
2.
Ingawa Mungu habadilishi mawazo yake (Hes 23:19 na 1 Sam 15:24), mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa kwa watu yanabadilika watu wanapobadilisha fikra zao. Tazama maewlezo ya Yona 3-4 kwa mifano zaidi kuhusu jambo hili.
Waislamu hawapaswi kushangazwa kuwa neno "uovu" linaweza kumaanisha ubaya, na si tu uovu wa mwenendo. Neno hili linatumika hivi katika maandiko yao, kwenye Bukhari Hadith juzuu ya 3 kitabu cha 29 sura ya 7 no.56, uk.35.

S: Kwenye Yon 3:10b, kwa nini Mungu aliwarehemu watu waovu namna hii, na kwa nini hakumrehemu Yona?

J: Ingawa Mungu aliwaumba, na kuwatunza, kama anavyofanya kwa watu wote, hizi si sababu za msingi. Sababu ya msingi ni kuwa Mungu anawapenda watu wote aliowaumba, anajishughulisha kwa ajili yao, na anawarehemu, kwa mujibu wa Zab 145:13b,17.

S: Kwenye Yon 3:10b, mioyo yetu inawezaje kubadilishwa inapokuwa haiendani na moyo wa Mungu?

J: Roho Mtakatifu anaweza kufanya kazi katika mioyo yetu na kuibadilisha; hata hivyo, kama waumini nasi tuna wajibu wa kuwa wepesi kubadilika na kumwitikia Mungu.

S: Kwenye Yon 4:1-2, ni kwa nini hasa Yon alikasirika kiasi hiki kuwa watu wa Ninawi wamesamehewa? Je ilikuwa ni kwa sababu maneno yake hayakutimia, au kwa sababu alitaka kuona watu wa Ninawi wanaangamizwa?

J: Inaweza kuwa ni kwa sababu ya mambo hayo yote. Wazo kuwa maneno yake ya unabii yatatimia lilikuwa la muhimu zaidi kwake kuliko maisha ya watu wa Ninawi. Kwa upande mwingine, kwa vile alifahamu jinsi watu wa Ninawi walivyokuwa wakatili na wapenda vita, na huenda kwa vile alijua kuwa wakati wowote ule wangeweza kuivamia Israeli, hakupenda kuona wanasamehewa.

S: Kwenye Yon 4:1-2, bila kujali sababu ya Yona kukasirika, je Yona alijali zaidi kuona maneno aliyosema yanatimia kuliko maisha ya watu wa Ninawi. Kuna mifano yeyote kwenye Biblia au leo hii ambapo tunajali zaidi maneno yetu kuliko watu?

J: Jeftha alikosea kwa kujali zaidi kutimiza ahadi aliyoitoa bila kufikiri sana kuliko maisha ya binti yake mwenyewe. Herode alijali zaidi kutimiza ahadi yake kwa Salome kuliko maisha ya Yohana Mbatizaji.

S: Kwenye Yon 4:1-2, je kuna nyakati ambazo manabii wa kweli hutoa unabii usiokuwa wa kweli?

J: Hapana. Kwenye Yon 3:4-10, Yona alitoa unabii kuwa mji wa Ninawi utaangamizwa katika siku arobaini zijazo kwa sababu ya uovu wao. Watu walipotubu kwa ujumla wao wote, Mungu hakuwaletea uovu ule aliosema angewaletea. Mawazo ya watu yanapobadilika, mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa kwa watu wahusika hubadilika.
Kuangamizwa kwao kulikokuwa kumetabiriwa kulitokana na kutokutubu kwao uovu wao. Jambo hili linaonekana kuwa lilitegemea kutokutubu kwao. Walipoamua kutubu, Mungu hakuona haja ya kuiangamiza Ashuru wakati ule. Vivyo hivyo, Mungu anapotoa unabii wa kuangamiza, tunaweza kujifunza kuwa hukumu inaweza kuahirishwa au hata kuondelewa kabisa endapo watu watatubu. Kanuni hii, ya kuruhusu toba tunapkuwa tumekabiliwa na hukumu, imeelezwa kwenye Yer 18:7-8.

S: Kwenye Yon 4:1-2, kwa nini Yona alikosea kuwachukiwa Waashuru, kwani Daudi pia alisema aliwachukia watu waliomchukia Mungu kwenye Zab 139:21-22?

J: Kuna mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili:
1.
Waashuru hawakuwa na chuki kubwa dhidi ya Mungu wa kweli; walimfahamu kwa kiasi kidogo tu. Kwenye Yon 4:11, Mungu anawaelezea watu wa Ninawi kuwa watu wasiojua mkono wao wa kulia na wa kushoto, au kwa maneno mengine, wanafahamu kwa kiasi kidogo tu mema na mabaya.
2.
Kuna dhana nzuri ya kujifunza kuhusu ktafsiri Biblia. Zaburi ni mkusanyiko wa maombi na nyimbo zilizohifadhiwa na Mungu ili ziwe mifano kwetu. Ingawa mambo yote anayosema Mungu kwenye Zaburi (na sehemu nyingine za Biblia) ni kweli, si kila kitu watu (bila kumtaja shetani) wanachokisema kwenye Biblia ni kweli. Badala yake, Biblia imerekodi kwa uaminifu mambo waliyosema. Kwa mfano, endapo Ahabu alisema "1 + 1 = 3", na Biblia ikasema kuwa "Ahabu alisema 1 + 1 = 3", Biblia itakuwa imesema ukweli na imerekodi kwa usahihi maneno aliyosema Ahabu ambayo siyo sahihi.
3.
Zaburi 139 inaongelea kuwachukia maadui wa Mungu, na Agano Jipya linatuagiza kuwapenda watu wengine. (Kumbuka, Sauli wa Tarso aliwahi kuwa adui wa Mungu). Hivyo, Daudi aliomba ombi ambalo halikuwa mapenzi makamilifu ya Mungu. Kama ilivyoonyeshwa kwenye Agano Jipya, tunapaswa kuwapenda hata maadui wa Mungu.
4.
Kuna somo la kujifunza kutoka kwenye sala hii iliyo kwenye Zaburi. Usiogope kuomba vyovyote unavyoona unataka kumwomba Mungu. Mungu atatubadilisha mioyo yetu. Hata kwenye mstari wa mwisho wa Zaburi 139, Daudi alimwomba Mungu "uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, ukaniongoze katika njia ya milele."

S: Kwenye Yon 4:1-2, kwa kuwa Yona alikuwa na fikra mbaya, kwa nini hakuwa sahihi kufanya kazi sehemu nyingine badala ya kuhudumu akiwa na fikra mbaya?

J: Kwenye habari hii ya Yona, tatizo ni kuwa alihitaji kubadili fikra zake. Mungu alimtaka Yona abadilishe fikra zake, lakini Mungu alimwamuru kwenda, licha ya fikra alizokuwa nazo. Wakati mwingine fikra ngumu za watu zinaweza kulainka wanapoamua kumtii Mungu bila kujali hisia zao.
Kwenye Fil 1:15-18, Paulo anaongelea watu wanaohubiri injili [ya kweli] kwa husuda, fitina, au bila kuwa na moyo wa dhati. Ingawa watu hawa walipingana naye, Paulo alimsigu Mungu kwa ajili ya kuhubiri kwao, kwa sababu walikuwa wanahubiri injili ya kweli, hata kama kwa lengo baya.

S: Kwenye Yon 4:3, 8-9, 1 Sam 16:30, na 1 Fal 19:4, je waumini wanapaswa kumwomba Mungu achukue maisha yao?

J: Biblia haijibu swali hili moja kwa moja, lakini inatoa mifano mizuri na mibaya.
1.
Hakuna muumini mtiifu kwenye Biblia aliyejua. Sauli hakuwa mtiifu kwenye 1 Sam 16:30. Ahithofeli hakuwa muumini mtiifu kwani alimsaliti Daudi kwenye 2 Sam 17:1-23.
2.
Samsoni alimwomba Mungu achukue maisha yake kwenye Amu 16:30, hata hivyo, ingawa Samsoni alikuwa na lengo la kutaka kujiua hakufanya kitu kingine chochote cha kumfanya atoe uhai wake.
3.
Elia alikuwa amechoka sana hata akamwomba Mungu achukue maisha yake kwenye 1 Fal 19:4. Yona alichukizwa sana na Mungu hata akamwomba amuue. Hata hivyo, kati ya hawa wawili hakuna ambaye ombi lake lilikubaliwa na Mungu.

S: Kwenye Yon 4:1, 4, 9b ni kwa nini Yona alipatwa na kutunza hasira dhidi ya mambo ambayo Mungu aliyafanya?

J: Yona hakuptwa na hasira kwa muda mfupi tu; alijiona kuwa ana haki ya kutunza hasira yake. Kama Efe 4:26 inavyoonyesha, hatuna haki ya kutunza hasira.

S: Kwenye Yon 1:1, 4, 9, ni wakati gani (kama upo) tunapokuwa na haki ya kuwa na hasira kwa ajili ya mambo ambayo Mung u ameyafanya? Inamaanisha nini tunapokasirika kwa ajili mambo ambayo Mungu amefanya?

J: Yona hakuwa na haki kama sisi tu ya kukasirika kwa ajili ya namna watu wengine wanavyochagua kutumia hela zao. Mwisho wa yote hasira yetu ni kuwa Mungu hatendi kama mshiriki mwenzetu kwenye timu, yaani hachezi kwenye timu yetu kama ambavyo tungependa acheze. Tunasahau kuwa Mungu si hayuko kwenye timu yetu, na Mungu hayuko upande wetu. Tunapaswa kuwa kwenye timu ya Mungu, na upande wa Mungu.

S: Kwenye Yon 4:1 ,4, 9 kunatokea nini tunapomkasirikia Mungu? (Unaweza kufikiri tena kuhusu Ayubu).

J: Mungu anaweza kuiondoa. Endelea kuongea naye, na mwombe aubadilishe moyo wako ili uende sawa na wake. Mungu anaweza kuchukua dhambi zetu nyingine pia.

S: Kwenye Yon 4:2, watu wengi huwa wanamkasirikia Mungu kwa sababu wanakuwa na mtazamo usiokuwa sahihi kuhusu Mungu. Je jambo ndilo lililokuwa kwa Yona hapa?

J: Hapana. Yona alikuwa na mtazamo sahihi kuhusu nguvu za Mungu, na kuwa Mungu huwa anapenda kuschilia hasira na kutokuwaadhibu watu. Yona hakuwa anawapenda watu wa Ninawi, ambao Mungu aliwaumba.

S: Kwenye Yon 4:3, ni kwa jinsi gani Yona anasema kuwa ana hasira kiasi cha kufa sawa na Elia alivyosema kwenye 1 Fal 19:4?

J: Hapana. Kwenye vifungu vyote hivi viwili wahusika walikuwa wanamtumikia Mungu kwa uaminifu, na walijiona wako peke yao. Hata hivyo, Elia alikuwa amechoka, na majonzi (siyo hasira) kwa sababu Yezebeli alikwa anamtafuta, na alikuwa hatarini. Yona alikuwa na hasira kwa sababu watu wa Ninawi hawakuadhibiwa, na Mungu hakufurahishwa na Yona.

S: Kwenye Yon 4:5-6, kwa nini Yona alitaka kupata jua, ikiwa alijenga kibanda?

J: Biblia inasema kuwa alijenga kibanda upande wa mashariki wa mji, hivyo huenda alipenda kupata jua la mchana.

S: Kwenye Yon 4:6, kwa nini Yona alifurahishwa na mtango uliokua kimiujiza?

J: Ni kweli alifurahi kuwa ungempa kivuli. Lakini zaidi ya hilo, inaelekea ulikuwa ni ishara kuwa Mungu alimjali sana, alipendelewa na Mungu, na Mungu angetimiza maneno yake. Mtu anapokupa zawadi nzuri ndogo, unafurahia umuhimu wa zawadi, lakini kwa kawaida unafurahia zaidi kuwa mtu huyu alikufikiria kwa namna ya pekee ili akupe zawadi. Licha ya mambo yote aliyopitia, Yona aliweza kufurahia ishara hii kuwa alithibitishwa na kuwa alikwa kwenye mapenzi ya Mungu sasa.

S: Kwenye Yon 4:7, baada ya mambo yote aliyoyapitia Yona, kwa nini Mungu alitoa buu dogo liule mtango? Je Mungu hupenda kuharibu vitu, au kuviondoa, kwa sababu tu vinatufanya tufurahi?

J: Inafana na kama mtu akikupa zawadi nzuri, na baada ya kuwa nayo kwa saa moja au zaidi, aje kuiharibu kwa makusudi kabisa machoni pako mwenyewe. Fikra za Yona na hasira iliyokuwa inapanda polepole vilionekana wazi, na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Yona hakuwa vuguvugu tena.

S: Kwenye Yon 4:8, tunafahamu kitu gani kuhusu upepo wa mashariki kwenye sehemu hii ya ulimwengu?

J: Upepo mkali na wa moto wa mashariki huko Palestina na Mesopotamia unaitwa ‘siroko’ (sirocco). Unaweza ukaongeza joto kutoka selisiasi -9 hadi -6 (farenhaiti 16 hadi 22). Upepo huu ni mkavu sana, wenye kukausha ngozi na mimea. Siroko inapokuja watu hukimbilia kwenye sehemu wanakoweza kujikinga. Siroko ilimjia Yona, lakini hatujui endapo ilimdhuru Yona au la.

S: Kwenye Yon 4:8-9, ni kwa nini Yona alidhani kuwa ana haki ya kukasirika kwa ajili ya buu?

J: Inawezekana Yona alidhani kuwa alimvumilia sana Mungu kwenye tumbo la samaki, na amefanya mambo mengi sana kwa ajili ya Mungu, hivyo Mungu aliwiwa kulitunza buu alilokuwa amelitoa. Inawezekana kuwa Yona alisahau kuwa Mungu anahitaji zaidi utii kuliko sadaka. Mungu hadaiwi kitu chochote kile na sisi. Tunao wajibu wa kumtumikia na kumpendezesha Mungu, na si kwamba Mungu afanye hivyo kwetu.

S: Kwenye Yon 4:10-11, lengo kuu la Mungu halikuwa buu wala hasira ya Yona kuhusiana na buu? Je ni jambo gano ambalo Mungu alikusudia kuwasilisha kwa Yona kuhusiana na buu?

J: Yona angeweza kupata vifaa na kujitengenezea kivuli chake mwenyewe. Buu lilisaidia tu kuonyesha kitu kilichokuwemo kweny moyo wa Yona.
Kimsingi, Mungu alikuwa anamwita Yona mnafiki. Yona alilijali sana buu ingawa hakulitunza wala kulihudumia. Lakini Yona alifanywa kujua kuwa Mungu aliwajali watu wa Ninawi aliowaumba.

S: Kwenye Yon 4:11, buu ni tofauti na sanamu. Aina hii ya buu ni kitu kizuri ambacho Mungu anatupa, kisha mara baada ya kukizoea Mungu anakichukua ili kutufundisha jambo fulani. Je kuna mifano yoyote ya buu kwenye maisha yako au ya watu wengine unaowajua?

J: Inaweza kuwa ni shuleni, kazini, au kwenye fursa za biashara. Kwa mtu aliye bado kuoa au kuolewa inaweza kuwa ni urafiki au uchumba.

S: Kwenye Yon 4:8-11, hata kama Mungu ndiye wa muhimu zaidi maishani mwako, je kuna vitu vingine vilivyo vya muhimu kwako kuliko watu wengine na wokovu wao?

J: Wakati mwingine watu wanaweza kuruhusu mambo wanayofanya ili kupitisha muda (hobbies), burudani, familia, au hata kanisa na kazi ya Mungu kuwa muhimu kwao kuliko Mungu.

S: Kwenye Yon 4:11, kama Mungu ndiye wa kwanza, lakini unapenda vitu vingine mbali ya watu, je unaweza kuwa bado sahihi katika upendo wako kwa Mungu? (Tazama 1 Yoh 3:17; 4:12, 20-21).

J: Hapana. Kwenye 1 Yoh 3:17; 4:12, 20-21 tunaona kuwa hatuwezi kumpenda Mungu kweli ikiwa hatuwapendi watu wengine. Yohana anatuambia kuwa upendo umefunganishwa na utiifu kwa Mungu, na Mungu anatuamuru kuwapenda watu wengine. Tunawiwa kuitii amri hii bila kujali kama tunajisikia kufanya hivyo au la.

S: Kwenye Yon 4:5, kwa nini nabii huyu alikwenda upande wa mashariki wa Ninawi na kukaa chini?

J: Mto Khosr ulikuwa upande wa magharibi wa mji wa Ninawi. Kuna uwezekano mkubwa kuwa jeshi yenye kuivamia Ninawi lingejia upande wa mashariki, na Yona angekuwa mtu wa kwanza kuliona kama angekaa upande huo. Huenda Yona alikuwa na "imani ya kutosha" kuona kuangamizwa kwa Ninawi. Hata hivyo, kazi za Mungu hazitegemei imani yetu, bali mapenzi yake.

S: Kwenye Yon 4:6, je huu ulikuwa mmea wa aina gani?

J: Maandiko hayasemi endapo ulikuwa mmea wa kawaida ulioota kimiujiza, au spishi ya mmea ambayo haikuwepo duniani. Inawezekana kuwa ulikuwa ni mmbarika unaoweza kukua hata kufikia urefu wa mti.

S: Kwenye Yon 4:8, kwa nini Mungu alileta upepo wa mashariki ili kumuudhi Yona?

J: Yona alikuwa amekaa upande wa mashariki wa mji ili kuona baa litakalokuja kuiangamiza Ninawi. Mungu alilituma ‘baa’, lakini si kwa lengo la kuiangamiza Ninawi, lakini kumsumbua Yona. Jambo hili linaonekana kuwa adhabu yenye kufaa sana kwa muumini ambaye fikra zake zinamuudhi Mungu.

S: Kwenye Yon 4:10, idadi ya watu walioishi Ninawi ililinganaje na miji mingine ya wakati ule?

J: Ninawi ulikuwa ni mji mkubwa sana kwa wakati wake. Samaria ilkuwa na watu karibu 30,000, na Samaria ilikuwa kubwa kuliko Yerusalemu. Lakini idadi kubwa ya watu walioishi Ninawi iliufanya mji huu usiweze kujitosheleza kwa njia ya kilimo tu. Mji huu ulitegemea sana ushindi wa kivita na kodi.

S: Kwenye Yon 4:11, kwa nini Mungu aliitaja mifugo wakati alipokuwa anaongea na Yona?

J: Watu wengi wenye upendo wa aina yoyote ile wana desturi ya kuwa na huruma kwa wanyama, ingawa wanyama hawajui jambo sahihi au ovu. Watu (wakiwemo wa Ninawi), ni muhimu zaidi kuliko wanyama. Watu wa Ninawi hawakufahamu njia za Mungu kama ambavyo wanyama hawakufahamu. Kwa kuwa Mungu anavijali viumbe vyake, je hakupaswa kuwajali watu wa Ninawi pia?

S: Kwenye Yon 4:11, je Yona alibadilisha fikra zake na kuwapenda Waashuri?

J: Jambo hili linaweza kwenda upande wowote ule. Habari hii haitupi picha kamili, na huenda ni kwa makusudi kabisa. Hata hivyo, mtu aliyeandika kitabu hiki alikuwa na nia iliyofanana na ya Mungu kuhusiana na jambo hili. Kwa kuwa kuna uwezekano kuwa ama Yona mwenyewe aliandika kitabu hiki, au alitoa imra kwa mwandishi wake, huenda Yona alipata somo lake siku ya siku.

S: Kwenye Yona, je kuna ushahidi wowote zaidi ya ule wa Biblia kuwa Waashuri walitubu?

J: Huenda ikawa hivyo. Jeshi la Waashuri lilipigana kila mwaka, isipokuwa inashangaza kuwa kulikuwa na miaka miwili, karibu na 758-757 KK, ambapo inaelekea kuwa hawakupigana kabisa. Ingawa haiwezekani kuthibitisha kuwa Nabii Yona alikuja mwaka wowote kati ya hiyo miwili, alikuwa karibu na muda huo, na mahubiri ya Yona yanaelezea vizuri sababu ya taifa zima ambalo watu wake wote walikuwa askari walichagua kutokupigana miaka hiyo miwili. Kipindi hiki kilikuwa ama wakati wa utawala wa Ashur-dan III (karibu mwaka 772-754 KK) au vinginevyo wakata wa mtawala aliyekuja baada yake Ashur-nirari V (karibu mwaka 754-647 KK).
Baadaye Waashuri walirudi kwenye njia zao za zamani, na waliangamizwa mwaka 612 KK, kama Nah 2:1-3:9 na Zef 2:13-15 zilivyotabiri.

S: Kwenye Kitabu cha Yona, Nabii Yona alizikwa wapi?

J: Hatujui. Lakini kuna mapokeo kuwa Yona alizikwa kaskazini magharibi mwa Irak, karibu na mji wa Ninawi. Waislamu walijenga msikiti juu ya kaburi lake, na Waislamu wa madhehebu ya Suni pamoja na ISIS waliubomoa tarehe 25 Julai, 2014.

S: Kwenye Yona, je jambo hili ni kinyume cha dhana ya kale kuwa Mungu anataka kuwaangamiza watu wasiokuwa Wayahudi kama vile Waamaleki?

J: Hapana. Kuna mambo matatu ambayo yanafaa kuzingatiwa katika kujibu swali hili.
Waashuri
hawakuwa maadui wa watu wa Mungu. Kinyume chake, Waamaleki walijaribu kupigana na ???? na waliwaua waliobaki nyuma.
Manabii wa baadaye,
akiwamo Yona, hawakupinga kuuawa kwa Wakanaani na Waamaleki.
Mungu alisema kupitia kwa Musa
kuwa watu wasiokuwa Wakanaani, wakiwemo wale walioishi mbali, walikuwa na uwezo wa kurafikiana na kufanya makubaliano ya Waisraeli.
Hivyo, Asimov
alizungumza kuhusu ‘dhana iliyogeuzwa’ inayodaiwa kuwepo, wakati ukweli ni kwamba kuna muafaka kati ya maana halisi na maandishi ya Musa na Yona.

S: Kwenye Kitabu cha Yona, ni maswali gani makubwa tunayoweza kujiuliza sisi wenyewe na kumuuliza Yona, baada ya kusoma kitabu hiki?

J: Tambua kuwa huwezi kukomaa kiasi cha kuacha kulinda imani yako. Kuna maswali makubwa manne ambayo tungeweza kujiuliza kuhusu Yona. Lakini tunapojiuliza kuhusu Yona, tunaweza pia kuyauliza kuhusu sisi wenyewe.
Je Nabii Yona anaweza kwenda mbali sana na mapenzi ya Mungu hata Mungu amsahau?
Je Nabii Yona anaweza kuzama chini sana hata Mungu amwache?
Je Nabii Yona alikuwa amechelewa sana kumtumikia Mungu tena?
Je moyo wa Nabii Yona unaweza kuwahurumia watu waliopotea?

S: Kwenye Kitabu cha Yona, ni hati gani za kale zaidi ambazo bado zipo sasa?

J: Hati za Kukunja kutoka Bahari ya Chumvi (Dead Sea scrolls): (zilizoandikwa karibu karne ya 1 KK). Kuna nakala tatu za Kitabu cha Yona miongoni mwa Hati kutoka Bahari ya Chumvi, zinazoitwa 4Q76 (=4QXIIa), 4Q81 (=4QXIIf) AND 4Q82 (=4QXIIg).
4Q76
ina Yon 1:1-5, 7-10, 15-16; 2:1, 7; 3:2.
4Q81
ina Yon 1:6-8, 10-16.
4Q82
ina Yon 1:1-9; 2:3-10; 3:1-3; 4:5-11.
Hata hivyo, Dead Sea Scrolls Translated uk.478 inataja hati za kukunja za manabii wadogo zenye vitabu vya Hosea na Nahumu, lakini hazina vitabu vya Amosi na Yona.
Nahal Hever
ni pango karibu na Engedi, ambalo lina kipande cha hati cha manabii kumi na mbili kwa Kigiriki (8 Hev XIIgr). Inadhaniwa kuwa kipande hiki kiliandikwa kati ya mwaka 50 KK na 50 BK. Kilifichwa wakati wa maasi ya Barkuba dhidi ya Waroma. Kipande hiki ni marekebisho ya toleo la Kigiriki la Agano la Kale, yaliyofanywa Uyahudi, na kinafanana sana na toleo la Kimasoretiki. Kipande hiki kina Yona 1:14-16; 2:1-7; 3:2-5, 7-10; 4:1-2, 5.
Hati ya kukunja ijulikanayo kama wadi Murabb'at (Mur XII) iliandikwa karibu mwaka 132 BK. Ina Yon 1:1-16; 2:1-11; 3:1-10 to 4:1-11.
Kwa jumla, mistari ifuatayo ya Yona imo kwenye Hati kutoka Bahari ya Chumvi, Nahal Hever, na wadi Murabb’at: 1:1-16; 2:1-10; 3:1-10; 4:1-11. Mistari yote imo kwenye kazi hizi isipokuwa Yon 1:17.
Hati za Biblia ya Kikristo,
zilizoandikwa karibu mwaka 350 BK, zinalo Agano la Kale, kikiwemo Kitbu cha Yona. Mbili kati ya hizi ni Vaticanus (mwaka 325-350 BK) na Sinaiticus (mwaka 340-350 BK) pia zina kitabu kizima cha Yona. Kinaanzia ukurasa huo huo ambao Kitabu cha Obadia kinaisha. Pia kinaishia kwenye ukurasa huo huo ambao Kitabu cha Nahumu kinaanza.
Alexandrinus
(karibu mwaka 450 BK), ambamo vitabu vya manabii wadogo kumi na mbili vilikuwa kabla ya Isaya. Kitabu cha Yona kipo chote kwenye Vaticanus na Alexandrinus.

S: Ni mwandishi gani wa kale aliyeongelea Kitabu cha Yona?

J: Watu walioandika kabla ya baraza la kanisa la Nikea (Pre-Nicene writers) walioongelea au kudokezea Kitabu cha Yona ni:
Kitabu cha kubuniwa cha dini ya Kiyahudi (apokrifa) Ecclesiasticus 49:10 (kabla ya mwaka 190 KK) kinaonyesha kuwa Yona kilikuwa moja ya vitabu vya mababa kumi na mbili (the Book of the Twelve).
Clement wa Roma
(mwaka 96-98 BK) "Yona alitangaza kuangamizwa kwa watu wa Ninawi; lakini baada ya kutubu dhambi zao walirehemiwa na Mungu na kupata wokovu, ingawa hawakuwa sehemu ya (agano la) Mungu" (1 Clement [juzuu ya 1] sura ya 7, uk.7).
Justin Martyr
(karibu mwaka 138-165 BK)
Irenaeus wa Lyons
(mwaka 182-188 BK) alinukuu Yon 1:9 na 2:2 kama maneno ya Nabii Yona (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 20.2, uk.450).
Clement wa Alexandria
alisema, "Na Yona mwenyewe nabii, anadokeza jambo hili hili anaposema: ‘Na nahodha akamwendea na akamwambia,
Una nini, ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako ili atuokoe, hata tusiangamie" (The Stromata [mwaka 193-202 BK] kitabu cha 5 sura ya 141, uk.474-475).
Tertullian
(mwaka 207/208 BK) "Kwenye Kitabu cha Yona kuna kielelezo cha tendo la huruma yake, aliyoionyesha kwa watu wa Ninawi waliokuwa wanasali" (Yona 3:9) [Five Books Against Marcion kitabu cha 5 sura ya 11, uk.452].
Tertullian (mwaka 198-220 BK) "Je hii ndio ilikuwa sababu ya Yona kutokufikiri kuwa toba ilikuwa muhimu kwa watu wa Ninawi wasiomwamini Mungu wa Israeli, alipobadili msimamo kwenye jukumu lake la kuhubiri? Au je alihofu kuwa Mungu angemwondolea sifa njema ya mahubiri yake kwa kujua rehema za Mungu ambayo ingetolewa baadaye hata kwa wageni?" (On Modesty sura ya 10, uk.84).
Origen
(mwaka 225-254 BK) anamtaja Yona kwenye Against Celsus kitabu cha 7 sura ya 57 juzuu ya 4, uk.634.
Adamantius
(karibu mwaka 300 BK) alisema "Maji yalimpokea Yona kwenye kilindi chake kwa siku tatu mchana na usiku, kisha yalimrejesha akiwa na hali nzuri kabisa" (Dialogue on the True Faith Sehemu ya 5, uk. 172 [Adamantius anaongea].
Methodius
wa Olympus na Patara (karibu mwaka 260-312 BK).

Baada ya baraza la kanisa la Nikea (mwaka 325 BK):

Athanasius wa Alexandria
(mwaka 367 BK) (Alidokeza kwa kuwa anaongelea manabii wadogo kumi na mbili) "Hivyo basi, kuhusu Agano la Kale, kuna jumla ya vitabu ishirini na mbili; . . . kisha Manabii, vitabu kumi na mbili vikiwa vimeandikwa kama kitabu kimoja . . ." (Athanasius Easter Letter 39 sura ya 4, uk.552).
Cyril wa Jerusalem
(karibu mwaka 349-386 BK) ananukuu Yon 2:2, 6, 8 kama maneno ya Yona kwenye Mhadhara 14.20, uk.99.
John Chrysostom
(aliyekufa mwaka 407 BK) anamtaja Nabii Yona kwenye juzuu la 9 (Concerning the Statues Hotuba ya 20.21, uk.480).
Sulpitius Severus
(mwaka 363-420 BK) anamwongelea Yona kama Yona kwenye History kitabu cha 1 sura ya 48, uk.94.
Augustine wa Hippo
(mwaka 338-430 BK) anamtaja Nabii Yona kwenye City of God kitabu cha 18 sura ya 44, uk.387.
Miongoni mwa vitabu vya uasi na visivyokuwa vya kweli

Tatian (alikufa mwaka 170 BK) kwenye Diatessaron sehemu ya 16, uk.68 ananukuu Mat 12:41 na Luk 11:24 kuhusu Yona.
Theodore wa Mopsuestia
(mwaka 392-423.429 BK) alinukuu Yon 3:4 (Commentary on Jonah sura ya 1, uk.193).
Baada ya baraza la kanisa la Nikea palikuwa na waandishi wengine pia waliomwongelea Yona.

S: Kwenye Yona, kuna tofauti gani za kutafsiri kati ya toleo la Kiebrania (Masoretiki) na la Kigiriki (Septuajinti)?

J: Zifuatazo ni tofauti chache za kutafsiri kutoka kwenye sura ya 3, ya kwanza ikiwa kwenye toleo la Kiebrania na ya pili kwenye tafsiri ya Kigiriki ya Septuajinti.
Yon 1:9
"Mimi ni Mwebrania" (Masoretiki) dhidi ya "Mimi ni mtumishi wa Bwana" (Septuajinti, Theodore wa Mopsuestia kwenye Commentary on Jonah sura ya 1, uk.197).
Yon 2:4
"Lakini nitatazama tena" (Masoretiki) dhidi ya "Nitatazamaje" (Septuajinti).
Yon 3:2
"Habari nitakayokuamuru" (Masoretiki) dhidi ya "kwa mujibu wa habari ya awali niliyokuambia" (Septuajinti).
Yon 3:3
"Mji mkubwa wa Mungu" (Masoretiki) dhidi ya "mji mkubwa mno" (Septuajinti).
Yon 3:4
"Siku 40" (Masoretiki) dhidi ya "siku 3" (Septuajinti, Theodore wa Mopsuestia kwenye Commentary on Jonah sura ya 1, uk.193).
Yon 3:6
"Ikamfikia mfalme" (Masoretiki) dhidi ya "ikawagusa hata wafalme" (Septuajinti).
Yon 3:6
"Akaondoka katika kiti chake cha enzi" (Masoretiki) dhidi ya "akaondoka kutoka mbali na kiti chake cha enzi" (Septuajinti).
Yon 3:6
"joho" (Masoretiki) dhidi ya "vazi" (Septuajinti).
Yon 3:7
"Akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake" (Masoretiki) dhidi ya "na habari ilitangazwa, na iliamriwa Ninawi na mfalme na wakuu wake" (Septuajinti).
Yon 3:7
"Wanadamu, wala mnyama, wala makundi ya wanyama, wala wanyama wafugwao" (Masoretiki) dhidi ya "wanadamu, wala mifugo, wala ngo’mbe, wala kondoo" (Septuajinti).
Yon 3:8
"Mwanadamu na manyama" (Masoretiki) dhidi ya "wanadamu na wanyama wanaofugwa" (Septuajinti).
Yon 3:8
"Na wakageuke" (Masoretiki) dhidi ya "na waligeuka kila mmoja"
Yon 3:10
"Njia yao mbaya" (Masoretiki) dhidi ya "njia mbaya" (Septuajinti).
Yon 3:10
"Aliwahurumia" (Masoretiki) dhidi ya "alighairi" (Septuajinti).
Yon 4:1
"Lakini jambo hili lilimchukiza Yon asana, naye akakasirika" (Masoretiki) dhidi ya "lakini Yona alikasirika sana, na kufadhaika" (Septuajinti).