Maswali ya Biblia, Injili

 

S: Ni mtu gani wa kwanza kuandika kitabu chenye kujibu maswali kuhusu injili?

J: Mtu wa mwanzo kabisa ninaymfahamu ni Eusebius wa Kaisaria (aliyeishi mwaka 313-339/340 BK) aliyeandika vitabu viwili. Cha kwanza kiliitwa Gospel Questions and Solutions Addressed to Stephanus, ambacho pia kiliitwa Questions and Solutions on the Genealogy of our Savior, na cha pili ni Gospel Questions and Solutions Addressed to Marinus. Vitabu hivi viwili vinaitwa kwa pamoja Gospel Questions and Solutions. Eusebius aliandika pia kanusho la ukinzani unaodaiwa kuwepo uliotolewa na Hierocles, mwana falsafa anayefuata nadharia za Plotinus na gavana wa Kiroma wa Bithynia na baadaye Misri aliyewatesa Wakristo sana wakati wa utawala wa Domitian. Kabla ya hapo, waandishi wengi wa kikristo walijibu maswali kwa mtu mmoja mmoja pia.

Tazama Nicene and Post-Nicene Fathers Second Series juzuu ya 1, uk.32, 38-39 kwa maelezo zaidi.

 

S: Je Yesu aliwezaje kuwa wa kabila la Yuda, kwani kabila la mtu hutambuliwa kupitia upande wa baba (Hes 34:14; 1:18-44; Law 24:10)? Kabila la mama halikuhusika katika kutambua kabila la mtoto na kabila halikuweza kurithiwa kupitia kwa baba wa kambo; mali tu ndizo zilizoweza kurithiwa. Kwa kuwa Wakristo wanaamini kuwa Yesu hakuwa na baba mwanadamu, hakuweza kuwa na kabila na hivyo hawezi kuchukuliwa kuwa wa ukoo wa Yuda au Daudi na hivyo kuondolewa sifa ya kuwa Masiha. Tovuti hii hapa chini http://www.jewsforjudaism.org/faq-primary-211/birth-of-jesus-primary-360/59-whos-genealogy-is-given-by-luke inatoa madai haya kuhusiana ukoo wa Yesu: "kudhania kuwa Mariamu alikuwa wa ukoo wa Daudi kunaleta shida kuwa Mariamu hakuweza kumpa Yesu kitu asochokuwa nacho: (1) Undugu kupitia upande wa mama hauhusiki kwenye kupata fursa ya kuirithi enzi ya Daudi ambayo ilipitia kwa wazao wa kiume tu: 'Daudi hataakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha nyumba ya Israeli' (Yer 33:17); (2) Kibilia, haki za kiukoo, yaani ufalme na ukuhani, ilipita kwa wazao wa kiume tu. Habari ya urithi wa mabinti wa Selofehadi (Hesabu sura za 27 na 36) haihusiki hapa kwa kuwa inahusu uruthi wa mali na si haki za kiukoo."
J: Kwanza jibu la sekunde tano, kisha jibu la kina. Kimsingi, ingawa kabila lilitambuliwa kupitia upande wa baba kwa kawaida, makabila ya Kiyahudi yalitambuliwa kupita upande wa mama SIYO baba, kwenye familia ya Yarha (1 Nya 2:34-41), na watoto wa kuhani (Ezr 2:61; Neh 7:63). Je kabila litakosaje kutambuliwa kupitia upande wa mama kwa kiasi kikubwa zaidi kwa mtoto aliyezaliwa na bikira!

Kwa jibu la kina, ni nani aliyesema kuwa kabila au ukoo unapita upande wa baba tu? Hakuna mtu aliyesema hivyo kwenye Biblia. Hes 34:14 haionyeshi kitu chochote kile. Hes 1:18-24 inaonyesha kuwa mtoto wa kiume wa mwanaume wa Mmisri na mwanamke Muisraeli aliitwa Muisraeli. Watu wangeweza kumfikiria kuwa Mmisri au Muisraeli nusu. Law 24:10 (na vifungu vingine vingi) vinaonyesha tu kuwa kwa Waisraeli wa kawaida kabila hupitia upande wa baba. Lakini jambo hili si AGIZO LA MUNGU. Shauri linalohusu wazazi halisi wawili halihusiki na shauri linalohusu mzazi halisi mmoja. Lakini, hata kwenye shauri linalohusu wazazi halisi wawili, kuna mifano kwenye Agano la Kale ya kuchukua ukoo kupitia upande wa mama.

Mifano mitatu ya kuchukua ukoo kupitia upande wa mama.

Kwenye kabila ya yuda, Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, alikuwa na mabinti tu. Hivyo alimwozesha binti yake kwa mtumwa wake wa kiume aliyekuwa Mmsisri, Yarha, na walipata mtoto wa kiume aliyeitwa Attai. Ukoo wa Attai umejumuishwa na Waisraeli wengine kwenye 1 Nya 2:34-41. Watoto wa kiume waliozaliwa nao si tu kwamba walihesabiwa kuwa Waisraeli lakini pia waliorodheshwa kuwa wazao wa Yuda.

Mfano wa pili ni Yairi, mjukuu wa Hezroni wa kabila la Yuda na binti wa Makiri, wa ukoo wa Manase. Kwenye 1 Nya 2:21-23, Yairi alikuwa na miji 23 katika nchi ya Gileadi (kwenye nchi ya Manase). Ingawa babu wa Yairi alikuwa wa ukoo wa Yuda, Yairi aliitwa Mmanase kama alivyokuwa mama yake kwenye Hes 32:41 na Kumb 3:14.

Mfano wa tatu ni Ezr 2:61 na Neh 7:63, ambamo wana wa kuhani aliyemwoa binti wa Barzilai aliitwa wana wa Barzilai.

Mfano mwingine wenye kuonyesha kuwa ukoo haukutambuliwa kupita upande wa baba tu ni ndoa za kaka/mdogo wa mume. Mume anapokufa kabla ya kuwa na watoto, kaka/mdogo wa marehemu alimuoa mjane, na mtoto wa kwanza kuzaliwa atahesabika kuwa mtoto wa mume wa kwanza wa mjane ambaye ni marehemu, hata kama kihalisi si hivyo.

Hata hivyo, swali hili linaonekana kuwa halina tofauti sana. Je DNA ya kibinadamu ya Yesu ilikuwa ni ipi? Ilikuwa ya Kiyahudi kwa 100%. Kulikuwa na makabila 12 ya Kiyahudi (kwa kweli makabila 11 pamoja na nusu makabila 2). Je DNA ya kibinadamu ya Yesu ilitokana na kabila lolote kati ya haya? Ndiyo ilitoka kabila la Yuda kwa 100%. Kama kutokuwa kwake na baba Myahudi kutamfanya asiwe mmoja wa makabila 12, je kabila lake litakuwa ni lipi?

Swali hili linaonekana kama njia amna ya kukwepa swali kubwa zaidi. Kama Yesu alizaliwa na bikira na aliktumwa na Mungu kutufundisha, je uko tayari kumfuata au la? Kama swali lingekuwa kubaki na imani na desturi za Kiyahudi au kumfuata Mungu pekee wa kweli, ungechagua kitu gani? Kama mtu hatachagua kumfuata Mungu pekee wa kweli kwa jinsi yoyote ile, basi swala hapa si DNA ya Yesu bali kutokuwa tayari kumfuata Mungu pekee wa kweli.

Jambo la pili ni kupewa enzi. Muuliza swali alikosea aliposema kuwa Mariamu hakuwa wa ukoo wa Daudi; orodha ya uzao wake iliyo kwenye Luka 2; Rum 1:3; na 2 Tim 2:8 inaonyesha kuwa Yesu (na yeye, Mariamu) walikuwa wazao halisi wa Daudi. Hata hivyo, muuliza swali yuko sahihi anaposema kuwa ukoo wa Mariamu hauhusiki na kupewa enzi. Kwa ajili hii, ilikuwa muhimu kwa Yesu kuwa mtoto aliyeasiliwa na Yusufu, ambaye alikuwa na haki ya kupewa enzi kwa sababu alikuwa mwanaume wa ukoo wa Daudi.

 

S: Kwenye injili, kwa nini kuna haja ya kuwa na mpangilio wa Injili unaofuata matukio?

J: Kupangilia Injili kwa kufuata matukio kungekuwa jambo kubwa kama Mungu angekuwa ametuhifadhia injili moja tu, au kama Mungu mwenyewe angekuwa ametoa mpangilio ulio kamili wa aina hiyo. Badala yake, tuna simulizi nne, ambazo kila mwandishi mwanadamu ameandika mambo ambayo aliamini kuwa ni ya muhimu zaidi katika yale ambayo Mungu alimsaidia kukumbuka. Tazama swali baada ya lifuatalo kujua kwa nini tuna Injili nne.

 

S: Je ni nani waliokuwa waandishi wa kwanza wa mpangilio wa Injili unaofuatisha matukio?

J: Tatian (mwaka 170 BK) ni mtu wa kwanza tunayemjua kutengeneza mpangilio wa Injili unaofuatisha matukio uitwao, Diatesaroni (Diatessaron), yaani "kupitia nne." Andiko hili linathibitisha kuwa kulikuwa na Injili nne tu zilizotambuliwa, na linanakiri kiusahihi neno kwa neno 70% ya aya za Injili. Hata hivyo, Tatian alikuwa Mnostisia wa Kienkrati, na alichugua kuiacha mistari yote inayosistizia uanadamu wa Yesu, kama vile orodha ya ukoo wake. Lakini hata mtu huyu aliyekuwa na msimamo potofu aliweka mistari yote yenye kuonyesha kuwa Yesu ni Mungu.

Ammonius wa Alexandria alitengeneza mpangilio wa Injili unaofuata matukio mwanzoni mwa karne ya tatu. Alitumia Injili ya Mathayo kama msingi, na alionyesha jinsi Injili nyingine zinavyofanana au kutofautiana. Tazama Nicene and Post-Nicene Fathers Second Series juzuu ya 1, uk.38-39.

Juvencus (mwaka 329 BK) aliandika shairi refu la Injili, akizipangilia kwa kufuata matukio kwa kiasi kikubwa.

Eusebius wa Kaisaria (mwaka 313-339/340 BK) alitengeneza mpangilio wa Injili wenye kufuata matukio uliokuwa rahisi kuusoma kwa sababu aliweka safu sambamba. Tazama Nicene and Post-Nicene Fathers Second Series juzuu ya 1, uk.38-39.

Augustine wa Hippo (mwaka 354-430 BK) pia aliandika kazi iliyoitwa Harmony of the Gospels.

 

S: Kwa nini kuna Injili nne?

J: Injili nne zina malengo tofauti na kwa kiasi fulani watu tofauti walioandikiwa.

Mathayo: iliandikwa kwa mara ya kwanza kwenye lugha za Kiebrania (Kiaramu?) kwa mujibu wa Papias. Injili hii inatilia mkazo ufalme wa Mungu, tofauti na Injili ya Yohana inayotilia mkazo jinsi ya kuupata wokovu. Injili ya Mathayo inanukuu nabii nyini za Agano la Kale, na inaonyehsa jinsi ambavyo maisha ya Yesu yanavyofanana na maisha ya Israel kwenye Agano la Kale. Watu wanaichukulia Injili ya Mathayo kuwa kama "simba" kwani inamsistiza Kristo kuwa Mfalme. Irenaeus (mwaka 182-188 BK) kwenye kipande cha 28 cha kazi yake anasema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwa Wayahudi, ikisistizia kuwa Kristo ni wa ukoo wa Daudi.

Marko: Inasistizia matendo ya Kristo. Watu wengi wanaichukulia Injili ya Marko kuwa kama "maksai", yenye kumsistiza Kristo kuwa mtumishi.

Luka: Injili ndefu zaidi, iliandikwa na daktari na mshiriki wa safari za kimisheni za Mtume Paulo. Luka anaonekana kuwa mwanahistoria mkubwa zaidi wa ulimwengu wa kale. Watu wengi wanaichukulia Injili ya Luka kuwa kama "binadamu", ikisistizia uanadamu wa Kristo.

Yohana: Hii inaweza kuwa Injili ya maana zaidi, kwani inasistizia maisha ya Kristo kwa kiasi kidogo lakini maneno na mafundisho yake kwa kiasi kikubwa. Watu wengi wanaichukulia Injili ya Yohana kuwa kama "tai", ikisistizia uungu wa Kristo.

Kwenye Agano la Kale, Masihi anaitwa ". . . Chipukizi . . . mfalme" wa nyumba ya Daudi (Yer 23:5, 6), "mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi" (Zek 3:8), "huyu ndiye . . . Chipukizi" (Zek 6:12), na "chipukizi la Bwana" (Isa 4:2).

Hapakuwa na injili zaidi ambazo Wakristo walizikubali kwa ujumla. Irenaeus, aliyeandika karibu mwaka 182-188 BK, alisema palikuwa na Injili nne (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 11.8, uk.428).

 

S: Ni Injili ipi iliyoandikwa kwanza?

J: Ingawa hatuna uhakika, maoni yenye kufuatwa na Wakristo wengi ni Injili ya Marko, ingawa kuna wanazuoni wenye kuheshimika wanoaamini kuwa ilikuwa ni Injili ya Mathayo au Luka. Kama wazo la ziada, kati ya aya 661 kwenye Injili ya Marko (yenye mwisho mfupi), 600 zinafanana na aya zilizoko kwenye Injili ya Mathayo, 350 kwenye Injili ya Luka, na 31 tu hazipatikani sehemu yeyote ile.

 

S: Je kila Injili imeandikwa kwa kufuata jinsi matukio yanayoripotiwa yalivyotokea?

J: Hapana. Yafuatayo ni maelezo ya vyanzo vinne vyenye kufuata fikra na maadili ya kiasili ya kikristo:

The NIV Study Bible, uk.1437 inasema, "(Mfuatano halisi wa matukio hauelekei kufuatwa hasa kwenye Injili yeyote ile.)"

The New Geneva Study Bible, uk.1504 inasema, "Hata hivyo, Mathayo na Luka hawakumfuata Marko kila mahali kuhusiana na mfuatano wa maukio ya maisha ya Yesu, au mfuatano wa mafundisho yake." Kwenye uk.1698 inasema, "Ingawa kuna changamoto kadhaa katika kuhusanisha maelezo, mambo makuu yanaafikiana kikamilifu."

F.F. Bruce kwenye Hard Sayings of the Bible, uk.454-455 anasema, . . . hakuna mwandishi wa Injili anayedai kutoa mfuatano halisi wa matukio yaliyoripotiwa . . . Lilikuwa jambo muhimu zaidi kwa mwana historia wa zamani zile kutupa maana ya historia kuliko mfuatano halisi wa matukio yanayoripotiwa. Hivyo, Mathayo anayaweka pamoja mahubiri ya Yesu kwenye ‘vitabu' vikubwa vitano kwa kufuata mada . . . Luka anatumia njia nyingine kugawa habari anazoziripoti . . . Katika Injili hizi mbili kuna mipangilio yenye kufuata mada inayotupa mfuatano mzuri kwani inapangilia habari zilizoandikwa ili tuweza kuzielewa. Katika Injili hizi mbili hatufahamishwi mandhari halisi ambayo Yesu alisema mambo haya yote."

Kwenye kanisa la awali, kazi ya Eusebius, Ecclesiastical History 3:39, uk.170-173 inamnukuu Papias, mwanafunzi wa Mtume Yohana, akisema, "Mark, aliyekuwa mkalimani wa Petro, aliandika kwa usahihi mambo yote aliyokumbuka, ama maneno au matendo ya Kristo lakini bila kufuata mtiririko wa jinsi yalivyotukia. Kwa sababu hakuwa amemsikia au ameandamana na Bwana; lakini baada ya hapo, kama nilivyokwisha kusema, aliandamana na Petro, ambaye aliyawasilisha kufuatana na uhitaji uliokuwepo, si kama mtu aliyekuwa anayaandika kama yalivyokuwa yamesemwa na Bwana. Kwa hiyo basi Marko hakufanya kosa alipoandika baadhi ya vitu kwa kadri alivyokumbuka; kwani alishikwa na jambo hili tu - kutokondoa kitu chochote alichosikia, au kuweka maelezo yeyote yasiyokuwa sahihi ndani mwake" (sehemu hii imenukuriwa kutoka The New Bible Dictionary 1962, uk.782).

Waandishi walichukulia kuwa watu watasoma kitabu chote mara kadhaa. Kwa mfano, Yoh 11:2 inasema kuwa Mariamu ndiye mpaka Yesu marhamu. Lakini haikuelezea tukio la Mariamu kumpaka Yesu marhamu mpaka Yoh 12:1-3. Kwenye Mat 10:4 inasema, "Yuda Iskariote, naye ndiye mwenye kumsaliti", na Yuda bado hajamsaliti Yesu.

 

S: Kwa nini Injili za Kisnoptiki (Mathayo, Marko na Luka zenye kuelezea matukio ya maisha na huduma ya Yesu kwa mtazamo unaofanana, tofauti na ule wa Injili ya Yohana) zinafanana kiasi hiki?

J: Kuna maoni manne, na matatu ya kwanza yanaweza kukamilishana.

1. Kufanana kwa malengo: Injili tatu za kwanza zinakwenda sambamba na ziliandikwa kutoa "picha ya jumla" ya maisha ya Kristo. Yohana, iliyoandikwa baadaye, huenda ilichukulia kuwa wasomaji wake walikuwa wanazifahamu Injili nyingine. Injili ya Yohana imeelezwa kuwa iliandikwa ili kuwafanya watu wamwaamini Yesu na kuupata uzima wa milele kupitia kwa jina lake, kama Yoh 20:31-31 inavyosema.

2. Kufanana kwa maneno: Marko alikuwa mshiriki wa safari za kimisheni za Mtume Petro, na Luke alisafirii pamoja na Mtume Paulo. Marko alikuwa Roma kwenye 1 Pet 5:13. Kuna uwezekano kuwa Luka na Marko walikuwa Roma wakati mmoja, na kama mtu mmoja alivyosema, "huenda hawakutumia muda wao wote kuongea kuhusu hali ya hewa." Ingawa hatujui sehemu zote ambazo Mathayo alizitembelea, wenye kutoa maoni haya wanasema kuwa kufanana huku kulitokana na mawasiliano ya mdomo miongoni mwa waandishi.

3. Kiunganishi cha maandishi cha Injili ya Marko: The New Geneva Study Bible, uk.1504, inasema, "Injili hazionyeshi ratiba tu ya shughuli za Yesu. Wala si kazi za siku za leo, vitabu maalamu vyenye kuelezea maisha ya mtu vyenye kufuata njia ambazo hazikufahamika wakati ule."

4. "Q": Maoni ya nne ambayo wanazuoni wengi wasioafiki maoni na mapokeo ya asili ya kanisa, ni kuwa kuna kitabu ambacho kimepotea kwa sasa, wanachokiita "Q" kilichokuwa na mambo yanayopatikana kwa pamoja kwenye Injili za Mathayo na Luka lakini siyo Marko.

 

S: Nimekutana na madai kuwa sijui kuelezea vizuri, na nilitaka kujua endapo utakuwa na maoni yeyote yale!

1) Hatufahamu kuwa hati za maandiko ya kale ambazo nakala zake za awali hazipo ziliandikwa kwenye Kigiriki, kwani hati za zamani zaidi [zinadaiwa] kuwa miaka mia kadhaa BK. Zinawezakuwa zilitafsiriwa kutoka kwenye lugha nyingine, na kusababisha makosa.

2) Inawezekana Yesu hakuwa anaongea Kigiriki. Jambo hili linamaanisha kuwa waandishi (au watafsiri) wa Agano Jipya waliyafafanua maneno yake kwa njia yao wenyewe, na kisha kuyatafsiri (kwa njia ambayo huenda haikuwa sahihi).

Je kuna taarifa zozote za Girikinaizesheni (kuenea/kuenezwa kwa utamaduni na lugha ya Kigiriki ya kale) ya Palestina wakati wa Yesu, ambayo ingeweza kuthibitisha kuwa waandishi wa Agano Jipya waliandika kwa Kigiriki? Kuna uwezekano mkubwa kuwa Yesu aliongea Kiaramu, hivyo unawezaje kuelezea kuwa mambo yaliyoripotiwa hayakuwa na makosa? Kama waandishi waliandika kwa Kiaramu au lugha nyingine, tunawezaje kuthibitisha (au kuonyesha bila shaka yeyote ile) kuwa maneno haya yametafsiriwa na kuenezwa katika karne zote hizi kwa usahihi?

Kama unafahamu vyanzo vyovyote unaweza kunijulisha na itakuwa vema sana. Au kama umeishafikiri kuhusu jambo hili, ningependa kujua mawazo yako. Ninaamini juu ya ukuu wa Mungu na uwezo wake wa kulilinda neno lake, lakini maelezo yeyote ya jinsi alivyofanya hivi yatanisaidia hakika!

J: Inaelekea kuna mambo manne ya msingi hapa:
1. Yesu alitumia lugha gani

2. Ni lugha gani ambayo Injili ziliandikwa

3. Ushahidi wa kuaminika kwa Injili

4. Kurekodiwa kusikokuwa na makosa kwa mafunzo ya Yesu

1. Yesu alitumia lugha gani

Tunafahamu kuwa Yesu alitumia Kiaramu kwa sababu alitamka misemo ya Kiaramu (Mat 5:22, n.k.). Yesu aliposema msalabani, "Eloi, Eloi, lama sabakthani", kuna watu waliodhani alikuwa anamwita Eliya kwa sababu hawakufahamu Kiaramu, ingawa Waroma wote walikuwa wanafahamu Kigiriki na Kilatini. Kwenye eneo ambalo Yesu alikulia, watu wengi walizungumza Kiebrania, Kiaramu na Kigiriki. Kwa mfano, pande jirani za kaskazini na mashariki mwa Bahari ya Galilaya zilikuwa na watu wenye kuzungumza Kigiriki. Ndiyo maana Pilato aliamuru maelezo yawekwe juu ya kichwa cha Yesu yaliyoandikwa katika lugha tatu.
2. Ni lugha gani ambayo Injili ziliandikwa

Kuhusu Injili, tunao ushuhuda wa Papias, mwanafunzi wa Mtume Yohana. Kwa mujibu wa taarifa iliyohifadhiwa na mwana historia Mkristo wa karne ya nne Eusebius, Papias alisema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa katika lugha ya Kiebrania kwa mara ya kwanza kabisa (Kiebrania au Kiaramu). Wakristo wa awali walitumia Kigiriki zaidi, ingawa watu waumini toka kwenye dini ya Kiyahudi walikuwa wanaongea Kiebrania na Kiaramu pia.

3. Ushahidi wa kuaminika kwa Injili

Nimewasikia watu kadhaa wakisema kuwa hati za zamani zaidi za Agano Jipya lote (au karibu na lote) zilizopo ziliandikwa karibu na mwaka 350 BK. Hata hivyo, madai haya si sahihi. Nyingi za aya za Injili zilizopo zilihifadhiwa muda mrefu sana kabla ya hapo. Kwa mfano, hadi mwaka 200 BK. Kuna hati zilizohifadhiwa zenye 71% ya aya za Luka (aya 818 kati ya 1151). Aya hizo ni: Luka 1:58-59; 1:52-2:1; 2:6-7; 3:8-4:2; 4:29-32; 4:34-5:10; 5:30-7:32; 7:35-39,41-43; 7:46-9:2; 9:4-17:15; 17:19-18:18; 22:4-24:53.
Kwa upande wa Injili ya Yohana, hati ya kale ya zamani zaidi ni p52 iliyoandikwa kati ya mwaka 100 na 150 BK. Nyingi ya hati nyingine za kale ziliandikwa hadi kuanzia mwaka 200 BK (p45, p66, p75, p90). Hati hizi pamoja na p52 zina aya 855 kati ya 878 za Injili ya Yohana (97%). Baadhi ya aya hizo ni 1:1-14:30; 15:2-26; 16:2-4, 6-7, 10-33; 17:1-20:20; 20:22, 23, 25-41; 21:1-9, 12, 17.

Usisahau kuwa kanisa la awali lilikuwa na maandiko mengine pia. Maandiko ya zamani zaidi ya kikristo yasiyokuwa sehemu ya Biblia First Clement (kwa Wakorintho) mwaka 96-98 BK, ambayo yananukuu kwa kiasi kikubwa sana Waraka kwa Waebrania pamoja na vitabu vinginge, na Shepherd of Hermas kilichoandikwa karibu mwaka 100 BK. Diatessaron ni mpangilio wa neno kwa neno Injili unaoweka pamoja matukio yanayofanana wa karibu 70% ya aya zote za kwenye Injili uliondikwa na Mnostisia wa kienkrate kabla ya mwaka 170 BK.

4. Kurekodi kusikokuwa na makosa kwa mafunzo ya Yesu

Maandishi ya awali yalikuwa ni ufafanuzi wa mafundisho ya Yesu uliotumia maneno tofauti na yale aliyoyasema. Wakati Yesu alifundisha makutano kwa masaa kadhaa, nasi tunaweza kusoma maneno yake kwenye vifungu vitano tu, ni dhahiri si maelezo ya neno kwa neno ya mambo aliyosema Yesu. Mafundisho ya kikristo kuwa Biblia haina makosa kwenye lugha za asili zilizotumika kuinadika yana sehemu kuu tano:
1. Kwenye hati zake za kale za awali kabisa Biblia haina makosa katika mambo yote inayosema.

2. Tunapaswa kuelewa mandhari, shairi ni shairi, masimulizi ni masimulizi, tunaweza kuelewa sitiari (lugha ya picha yenye kutoa maana ya kitu au kitendo iliyo tofauti na maana halisi) na maelezo ya hotuba, n.k.
3. Mungu alikuwa na uhuru wa kutumia "kalamu zake mwenyewe" kuandika Biblia, na kalamu hizo walikuwa ni watu waliokuwa wanaandika maneno. Hivyo, vitabu tofauti vilivyoandikwa na waandishi tofauti vina mitindo tofauti ya kuandika, na jambo hili halina shida;Kweli ya Mungu inang'ara kupitia vyote hivyo.

4. Ni maana iliyoandikwa bila makosa, si kila neno.

5. Hati za kale za Biblia zilizopo leo zina makosa na kutofautiana, lakini neno la Mungu lilihifadhiwa bila makosa makubwa yenye kuathiri imani, mafundisho na maisha ya kikristo.
Kwa habari zaidi tazama www.BibleQuery.org.ntmss.html.

 

S: Mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anasema, "Tunazo baadhi ya taarifa kuhusiana na maana ya kuwa mkulima wa ngazi ya chini wa Palestina ya karne ya kwanza. Kitu kimojawapo kilichomaanisha ni kuwa kwa kiasi kikubwa hutakuwa unajua kusoma na kuandika. Yesu mwenyewe alikuwa na upekee wa ajabu sana, kwani ni dhahiri kuwa aliweza kusoma (Luk 4:16-20), lakini hakuna kitu chochote chenye kuonyesha kuwa aliweza kuandika . . . Ni watu wangapi walioweza kusoma? Tatizo la kutokuweza kusoma lilienea kwenye himaya nzima ya Roma. Katika kipindi bora zaidi karibu asilimia 10 to ya watu wote walijua kusoma na kuandika. Na asilimia 10 hiyo ilikuwaa ni watu wa tabaka la matajiri . . . Hakuna kitu kwenye Injili au Kitabu cha Matendo chenye kuonyesha kuwa wafuasi wa Yesu walikuwa wanaweza kusoma, achilia mbali kuandika. Kwa kweli kuna habari kwenye Kitabu cha Matendo ambayo Petro na Yohana wanaelezwa kuwa "watu wasio na elimu" (Mdo 4:13) – neno la kale lenye kumaanisha kutokujua kusoma na kuandika." (Jesus, Interrupted, uk.105-106). Maana hii inafanana pia na ya kwenye kitabu cha Ehrman kiitwacho Lost Christianities, uk.203.

J: Asilimia ya watu kwenye Himaya ya Roma (Hispania, Uingereza, Ujerumani, n.k.) ambao hawakuweza kusoma haina umuhimu; ni asilimia ya watu walioelimika miongoni mwa Wayahudi walioishi Uyahudi na Galilaya ndiyo iliyo na umuhimu. Wayahudi walikuwa na kiwango kikubwa cha kujifunza kuliko watu wengine wengi kwenye Himaya ya Roma. Hakuna mtu aliyefikiri kuwa si jambo la kawaida kwa Zakaria, baba yake Yohana Mbatizaji, aliweza kuandika. Kwa kuwa baraza kuu la Wayahudi lilidai kuwa Petro na Yohana hawakuwa na elimu haimaanishi kuwa ndivyo hivyo walivyokuwa, au kwamba hawakuweza kabisa kuandika.

Kumb 6:9 inawaagiza Waisraeli kuandika sheria kwenye miimo ya milango ya nyumba zao na malango yao. Je waandishi wenye kushuku wanafikiri kuwa hakuna Wayahudi waliokuwa watii amri zao wenyewe?

Kama maelezo ya ziada, huko Beir Allah kwenye bonde la Mto Yordani, wataalamu wa mambo ya kale wamekuta mazoezi ya kuandika ya mtoto wa shule yanayomtaja Balaamu mwana wa Beori mara tatu. Muda wa kuandikwa mazoezi haya ulipimwa kwa kutumia kwa kupima kiasi cha kaboni kuwa ni mwaka 800/760 KK.

 

S: Nabii za kimasihi ni kitu gani kwenye Injili?

J: Hizi ni nabii ambazo Mungu alitoa ili kwamba watu wake waweze kuja kumtambua Masihi. Hizi hapa ni nyingi kati ya hizo.

Masihi atakuwa nani?

Kutoka kwenye kabila la Yuda (Mwa 49:10; Mat 1:2; Luk 3:23, 33; Ebr 7:14).

Mzao wa Yese (Isa 11:1; Mat 1:6; Luk 3:23, 32).

Mzao wa Daudi (Yer 23:5; Luk 3:31; Mat 1:1; 9:27; Mak 10:47-48; Yoh 7:42; Mdo 13:22-23; Ufu 22:16). Talmudi nyingi za Kiyahudi zinasema kuwa Masihi atatokea kwenye uzao wa Daudi.

Kuhani kwa mfano wa Melkizedeki (Zab 110:4; Ebr 5:6).

Mwana wa Mungu (Zab 2:7 Mat 3:17; 16:16-17; 27:54; 9:7; Luk 9:35; Yoh 1:34; Mdo 13:33; Ebr 5:5).

Neno la BWANA kwa Bwana wangu (Zab 110:1; Mat 22:43-45; Mak12:36-7; Luk 2:11; 20:42-44. Midrash Tehillim, Commentary on Psalms (mwaka 200-500 BK) linaichukulia Zaburi 110 kuwa yenye kumwongelea Masihi.

Ataitwa ‘Mungu pamoja nasi' (Isa 7:14; Mat 1:23; Luk 7:16; ~John 20:28).

Mtoto ataitwa Mungu mwenye nguvu, Mfalme wa amani, n.k. (Isa 9:6; Yemenite Midrash 349-350 na Pereq Shalom, uk.101).

Uzao wa mwanake utaponda kichwa cha shetani (Mwa 3:15; Targum Pseudo-Jonathan).

Alizaliwa na mwanamwali bikira (utimilifu pacha, Isa 7:14; Mat 1:18, 25; Luk 1:26-35). Mwanamwali bikira kwa mujibu wa Septuajinti (tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale).

Masihi atakuwa wapi?

Atazaliwa Bethlehemu ya Uyahudi (Mik 5:2; Mat 2:1, 5-8; Yoh 7:42; Luk 2:4-7; Targum Isaiah ).

Atahudumu Galilaya (Isa 9:1-2; Mat 4:12-16; Mak 1:14; Luk 4:31; Yoh 4:43).

Ataingia kwenye hekalu la Yerusalemu (Mal 3:1; Mat 21:12; Mak 11:15).

Masihi atakuja lini?

Fimbo ya enzi haitatoka (Mwa 49:10; Luk 3:23, 33; Babylonian and Jerusalem Talmuds, Targum Jonathan, Targum Pseudo-Jonathan, Targum Onkelos, Dead Sea Scroll Commentary, and the Aramaic Targum). Wayahudi walipoteza mamlaka ya kutoa adhabu ya kifo mwaka 11 BK kwa mujibu wa Babylonian Talmud, Sanhedrin sura ya 4.

Israeli ataachwa mikononi mwa aduai hadi wakati wa kuja kwa Masihi (Mik 5:3).

Kabla ya kubomolewa kwa hekalu, yaani mwaka 70 BK (Mal 3:1).

Baada ya kuja mtangulizi wake (Isa 40:3; Mat 3:1-3; 11:10; Luk 1:17; Yoh 1:23).

Atauawa mwaka 32/33 BK (Dan 9:20-27; Neh 2:1-10 mwaka 445/4 KK; Igeret Teiman, Rabbi Moses Abraham Levi in The Messiah of the Targums, Talmuds and Rabbinical Writers).

Je Masihi atafanya nini?

Huduma ya miujiza (Isa 35:5, 6a; Mat 9:6-7, 22, 32-35; 11:4-6; 12:13; Yoh 5:5-9; 9:6-11, n.k.)

Aliyachukua magonjwa yetu (Isa 53:4; Mat 8:17; Mak 2:10-12; Luk 5:13; Yoh 5:5-9).

Atafundisha kwa mifano (Zab 78:2; Mat 13:34).

Ataingia kama mfalme akiwa amepanda punda (Zak 9:9; Mak 11:2-10; Luk 19:35-37; Mat 21:5-9; Yoh 12:15).

Toka kuwa kwazo na kuwa jiwe kuu la pembeni (Zab118:22-23; Isa 8:14-15; 28:16; Mat 21:42; Mak 12:10-11; 1 Pet 2:6-8; Mdo 4:11).

Hataachwa mautini (Zab 16:8-11; 30:3; Mdo 2:31; 13:33; Mak 16:6; Mat 28:6; Luk 24:46

Wivu wa nyumba ya Babab yake (Zab 69:9; Yoh 2:17).

Roho wa Bwana atakaa juu yake (Isa 11:2; Mat 3:16; Mak1:10-11; Luk 4:15-21, 32; Yoh 1:32; Targum Isaiah and the Babylonian Talmud).

Mathayo anaonyesha kuwa maisha ya Yesu yanafanana na ya wana Israeli (Yer 31:15 na Mat 2:18; Hos 11:1 na Mat 2:15; Isa 9:1, 2 na Mat 4:15-16, n.k.)

Itikio la watu

Watamchukia bila sababu (Zab 35:19; 69:4; Isa 49:7; Yoh 15:25).

Baadhi ya watu watapanga kumuangamiza (Zab 38:12; Mak 11:18).

Atasalitiwa na rafiki yake (Zab 41:9; Mat 10:4; 26:48-50; Mak 14:43-44; Luk 22:47-48; Yoh 18:3, 5).

Atakataliwa na watu wake mwenyewe (Zab 53:3-4; 69:8; Yoh 1:11; 7:5; Mat 21:42-44).

Alinyweshwa siki (Zab 69:21; Mat 27:48).

Hata rafiki zake walimwacha (Zab 38:11; Mat 27:55; Mak15:40; Luk 23:49).

Mpige mchungaji na kondoo watatawanyika (Zak 13:7; Mak14:27, 50; Mat 26:31).

Atakataliwa na serikali (Zab 2:1-2; Mdo 4:25-28).

How will the Messiah die?

Aliuzwa kwa vipande 30 vya fedha (Zak 11:12-13; Mat 26:15).

Alitupa, hakuweka kwa uzuri, fedha ndani ya hekalu (Zak 11:13b; Mat 27:5a).

Hela kwa mfinyanzi (Zak 11:13; Mat 27:7).

Alichukuliwa isivyo haki (Isa 53:7-8; Mat 26:60; Mak14:55; Luk 23:4).

Mashahidi wa uongo (Zab 35:11; Mat 26:60).

Alikaa kimya mbele ya washtaki wake (Zab 38:13-14; Isa 53:7; Mat 27:12).

Alimuuliza Mungu kwa nini amemuacha (Zab 22:1; Mat 27:46; Mak 15:34).

Alidhihakiwa (Zab 22:7, 8; Mat 27:31, 39; Mak15:31-32).

Moyo wake uliyeyuka kama nta (Zab 22:14b; Yoh19:34).

Alichomwa kwa ajili yetu (Isa Isa 53:5; Zak 12:10; Mat 27:26; Yoh 19:34).

Watu walimtazama (Zab 22:17; Luk 23:35).

Watu walipigia kura vazi lake (Zab 22:18; Luk 23:34; Yoh 19:23, 24).

Hakuna mfupa uliovunjika (Zab 22:17; 34:20; Yoh 19:33).

Alipigwa na kutemewa mate (Isa 50:6; Mik 5:1; Mat 26:67; Luk 22:63).

Aliuawa pamoja na waovu (Isa 53:12; Mat 27:38; Mak 15:27).

Aliwaombea watesi wake (Isa 53:12b; Luk 23:34).

Alizikwa kwenye kaburi la mtu tajiri (Isa 53:9; Mat 27:57-60).

Alijitwisha dhambi zetu (Isa 53:5, 6, 10-12; Yoh 1:29; 1 Kor 15:3; 1 Yoh 2:2; 4:10).

Yesu alikufa akiwa anasema Zaburi (Zab 31:5; Luk 23:46).

 

S: jina "Bethlehemu" linamaanisha nini kwenye Mat 2:1, 5-8; Luk 2:4-7 na Yoh 7:42?

J: Bethlehemu inamaanisha "nyumba ya mkate."

Bethlehemu ya Uyahudi ni mji wa zamani sana uliokuwepo kabla ya wana Israeli. Mwa 35:19 inasema, "Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrathi, ndiyo Bethlehemu." Mwa 48:7 inasema kama hivyo. Kwa hiyo jina la awali la Bethlehemu ni Efrathi, na ndiyo sababu kwenye Mika 5:2 mji huu unaitwa "Bethlehemu Efrata."

Maandishi ya Amarna, waliyoandikwa na Wakanaani kwa Wamisri muda mfupi baada ya mwaka 1400 KK wakati wa utawala wa Yoshua, yanasema kuwa "Bit-Lahmi" waliwaasi Waapiru (jina la jumla la watu walioishi maeneo yanayoanzia Mesopotamia hadi mpaka na Misri miaka ya 1800 hadi 1100KK).

Pamoja na hayo, kuna mji mwingine pia, ulio kaskazini unaoitwa Bethlehemu, kwenye eneo la Zabuloni (Yos 19:15).

 

S: Mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anadai kuwa, "Hakuna mantiki kwenye Mathayo na Luka kuwa Yesu alikuwepo kabla ya kuzaliwa kwake." (Jesus, Interrupted, uk.75. Pia kwenye Jesus, Interrupted, uk.103)

J: Mik 5:2, ambayo Mathayo anainukuu kwenye 2:6, inasema kuwa mwanzo wa Masihi ni "zamani za kale" kwenye toleo la Kimasoretiki (toleo rasmi la Biblia ya Kiebrania, yaani Agano la Kale), au "kutoka mwanzo, hata kutoka milele" kwenye Septuajinti, yaani tafsiri ya Kifiriki ya Agano la Kale. Kwenye Mathayo, waandishi wameacha baadhi ya sehemu, ikiwemo sehemu inayosema kutoka zamani, lakini rabi yeyote wa Kiyahudi atatambua sehemu iliyobaki ya aya hii.

Kwenye Mat 23:37 na Luk 13:34, Yesu anasema, "Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale walitumwa kwao! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chin ya mabawa yake, lakini hukutaka!" Maneno haya yalisemwa siku chache baada ya kuingia kwa shangwe, wakati Yerusalemu ilipotoka kumpokea Yesu. Hivyo wakati Yesu alipokuwa akifanya kazi yake hapa duniani, kabla ya muda huu, Yerusalemu ilipewa nafasi kukusanywa pamoja chini ya Yesu? Jibu ni hapana. Mathayo na Luka (na Yesu) walikuwa wanafikiria muda ambao Yesu aliishi kabla ya kuzaliwa, wakati manabii ambao Yesu alishiriki kuwatuma Yerusalemu walikuwa wanauawa.

 

S: Mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anasema, "Lakini inastusha kuwa kwenye Injili ya Marko Yesu hajitambulishi kuwa mwenye uungu, kama aliyeishi kabla ya kuja ulimwenguni, kama aliyekuwa sawa na Mungu kwa namna yeyote ile. Kwenye Marko, yeye si Mungu na hasemi kuwa yeye ni Mungu" (Jesus, Interrupted, uk.79)

J: Mak 2:5-12 (pia Mat 9:26 na Luk 5:20-23) inasema kuwaMungu tu ndiye mwenye uwezo wa kusamehe dhambi, lakini Yesu alisamehe dhambi za mtu aliyekuwa amepooza. Yesu aliposhutumiwa kwa kufanya kitu ambacho Mungu tu ndiye anayeweza kukifanya, Yesu hakusema kuwa alikuwa tu anatangaza msamaha wa Mungu wala hakukana mawazo yao (kuwa ni Mungu tu mwenye uwezo wa kusamehe dhambi). Badala yake alisema na kuonyesha kuwa yeye anao uwezo wa kusamehe dhambi.

 

S: Kuhusu Mat 12:30 na Mak 9:40, mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anasema, "Kwenye Mathayo, Yesu anasema, ‘Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu.' Kwenye Marko anasema, ‘Asiye kinyume chetu yu upande wetu.' Je alisema mambo yote haya mawili? Je mambo haya yanawezaje kuwa kweli kwa wakati mmoja? Au kuna uwezekano kuwa mmoja wa waandishi alibadilisha maneno?" Jesus, Interrupted, uk.41.

J: Kwa kweli, siwezi kuelewa ni kwa jinsi gani Ehrman aliyaona maneno haya kuwa yanakinzana. Ni kweli yote yanaweza kuwa kweli. Ni kweli Yesu anaweza kusema mambo ambayo ni tofauti lakini yanakamilishana kwenye madhari tofauti na nyakati tofauti bila kujipinga mwenyewe. Kwenye Mat 12:22-37 (kifungu kinacho endana na Mak 3:20-29), tukio hili lilitokea wakati Yesu aliletewa mtu aliyekuwa amepagawa pepo. Baadaye sana, kwenye mandhari tofauti kabisa, kwenye Mak 9:38-41, Yesu alisema kuhusu mtu mwingine aliyekuwa akikemea pepo. Huenda Ehrman alidhani kuwa ni kukinzana kuwa endapo mtu alipingana na Yesu alipingana na wafuasi wake pia, au kinyume chake. Lakini Yesu alitabiri kuwa wafuasi wake watateswa na kuuawa kwa sababu watesi wao hawamjui Baba yake au Yesu mwenyewe kwenye Yoh 16:3. Yesu alisema kwenye Yoh 15:18-21, "Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia nyinyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake.Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu." Yesu alijifananisha kwa karibu sana na wafuasi wake kwenye Mat 25:34-46 kwenye mfano wa kondoo na mbuzi. Kwenye Yoh 15:1-8, Yesu anasema kuwa tuko ndami yake kama vile matawi yalivyo unganika na mzabibu.

 

S: Kwenye Mat 17:12 na Mak 9:11-13, Yohana Mbatizaji alitimizaje unabii wa Eliya? Je alikuwa ni Eliya aliyezaliwa upya katika mwili wa Yohana?

J: Hapana. Katika ujio wa kwanza wa Yesu, Yohana alikuwa na lengo na makusudio ya Eliya. Kwa kweli, Eliya (si Yohana) mwenyewe alitokea kwa muda mfupi wakati wa kubadilika kwa sura ya Yesu. Watu wengi wanadhani kuwa Eliya atakuwa mmoja wa mashahidi wawili watakaotokea kabla ya baragumu ya saba kupigwa kulingana na Ufu 11:3-12.

Mwandishi wa kwanza anayefahamika kuongelea aya hii ni Justin Martyr (aliyeishi karibu mwaka 138-165 BK), aliyesema kuwa dhana ya mtu kuwa na roho ya mwingine haipo kwa Eliya na Yohana Mbatizaji tu. Mungu aliahidi kuwa Yoshua atakuwa na roho ya Musa (Dialogue with Trypho the Jew sura ya 49, uk.220). Pia Elisha alikuwa na sehemu maradufu ya roho ya Eliya kulingana na 2 Fal 2:9-10.

 

S: Kwenye Luk 13:23, je kuna watu wanaotaka kuingia lakini hawawezi, wanatafuta lakini hawapati, kwenye Yoh 7:34, au wanaotafuta wanapata kama Mat 7:7; 1 Nya 28:9; Isa 55:6; Mdo 10:35 zinavyoonyesha?

J: Ukweli wa mambo ni kuwa, kuna watu wanaomtafuta Mungu HAWAMPATI. Kwenye Jer 29:13, Mungu aliwaahidi Waisraeli waliokuwa uhamishoni Babeli kuwa watamwona endapo watamtafuta kwa moyo wao wote. Hasemi chochote kuhusu watu wasiomtafuta kwa moyo wao wote, au wanaomtafuta kwa sehemu tu, kwa namna watakavyo wao wenyewe, na si kama atakavyo yeye.

 

S: Kwenye Mat 17:12 na Mak 9:11-13, je kwa Yesu kuongea na Musa na Eliya [kwa kiasi fulani] kunaonyesha kuwa tunapaswa kuongea na watu waliokufa, kama baadhi ya Wakatoliki walivyowahi kusema?

J: Hapana. Hakuna mtu aliyeongea na Musa na Eliya kwenye mlima ambapo uso wa Yesu ulibadilika isipokuwa Yesu mwenyewe. Hawakuongea kwa mtu yeyote pia, isipokuwa Yesu na wao kwa wao. Kuabudu kwetu kunatakiwa kuelekee kwa Mungu tu. Wakatoliki wanaafiki lakini wanasema kuwa kama ambavyo tunaweza kuomba msaada na maombi toka kwa Wakristo wengine wanaoishi ulimwenguni, tunaweza pia kuomba mambo hayo toka kwa Wakristo wanaoishi mbinguni. Kwenye 2 Kor 11:3 Biblia inasema hatupaswi kujitoa kwa yeyote yule isipokuwa Kristo. Ingawa kusali kwa mtu si lazima kumaanishe kuwa umejitoa kwao, maombi ya Wakatoliki wengi ni maombi ya kujitoa kwa Mariamu au watakatifu wengine. Hakuna mfano kwenye maandiko matakatifu wa muumini yeyote aliyeomba kwa yeyote isipokuwa Mungu.

 

S: Kwenye Mak 15:25, Yesu alisulubiwa saa tatu, au alikuwa bado mbele ya Pilato saa tatu kulingana na Yoh 19:14.

J: Kwanza nitaelezea kitu ambacho siyo jibu la swali hili.

Ukweli lakini si sehemu ya jibu: Namna ya kuandika namba tatu na sita kwa Kigiriki zilitofautiana kwa nukta moja tu, kwa hiyo kuna wanaodhani kuwa pana makosa ya kunukuru. Hata hivyo, kuna maelezo rahisi zaidi.

Jibu: Majibu yote ni sawa, kwa sababu saa za Wayahudi na Waroma zilitofautiana. Yoh 19:15 inasema kuwa Yesu aliondoka kwa Pilato saa ya sita, ambayo ingekuwa saa 12 asubuhi, kwani siku ya Waroma ilianza saa sita usiku. Mak 15:22, 25 inasema Yesu alisulubiwa saa ya tatu, ambayo ni saa tatu asubuhi kwa sababu siku ya Wayahudi ilianza jua linapochomoza (karibu saa 12 asubuhi), na usiku wao ulianza jua linapoama (karibu saa 12 jioni).

 

S: Kwenye Mat 19:16-30, Mak 10:17-31 na Luk 18:18-30, tunawezaje kuyafanya maelezo haya yafanane?

J: Yanafanana sana mara mtu anapoelewa kuwa waandishi wa Injili walitoa maelezo bila kunukuu maneno yale yale yaliyokuwa yameongelewa. Kwa mfano, Mathayo anasema, "Mwalimu . . . nipate uzima wa milele . . . Aliye mwema ni mmoja", wakati Marko na Luka wanasema, "Mwalimu mwema . . . nipate kuurithi uzima wa milele . . . Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu", na kadhalika.

 

S: Kwenye Mat 19:28 na Luk 22:28-30 mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anadai kwa uongo kuwa Yesu alisema kuwa wanafunzi kumi na wawili watakuwa na viti vya enzi kumi na mbili. Vipi kuhusu mwanafunzi Yuda Iskariote? (Jesus, Interrupted, uk.159)

J: Hapana, hakuna kiti cha enzi kwa ajili ya Yuda. Kwanza kabisa, Luk 22:28-30 haiongelei viti vya enzi kumi na viwili ila makabila kumi na mbili tu. Kwa kweli Mat 19:28 HAISEMI kuwa wanafunzi kumi na mbili watakaa juu ya viti vya enzi kumi na viwili. Badala yake, inasema, ". . . ninyi mnao nifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli." Hivyo inasema kuwa kutakuwa na viti vya enzi kumi na viwili lakini haisemi kuwa wanafunzi watavikalia. Badala yake, Yesu aliahidi jambo hili kwa "ninyi mlionifuata" tu. Yuda hakuendelea kumfuata Yesu na aliiacha nafasi yake kama mwanafunzi baada ya kumsaliti Yesu, kulingana na Mdo 1:20. Kwenye Mat 19:28, Yesu aliwaahidi "ninyi mlionifuata" tu.

 

S: Kwenye Mat 26:14, mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anasema, Yuda alimsaliti Yesu kwa fedha, wakati Luk 22:3 Yuda alimsaliti kwa sababu shetani alimwingia. Kwenye Injili ya Yohana, Yuda anaitwa mwovu, hivyo inaonekana alikuwa na msimu wa uovu (Jesus, Interrupted, uk.45-46)

J: Kama ambavyo hauanzishwi na kitu kimoja tu lakini vitati (hewa, nishati, na cheche), vitendo vingi huwa na vitu kadhaa vyenye kuvisababisha pia. Vitu vingi vinasababishwa na mambo matatu: uwezekano wa kianzilishi kama vile maji nyuma ya bwawa, kisababishi cha karibu kama vile ufa kwenye bwawa, na kisababishi kinachoweza kuepukwa kilichokuwa kimeondolewa kama kusimamisha ukaguzi wa bwawa. Kitu gani kati ya haya matatu kilisababisha bwawa kubomoka? – vyote vitatu vilihusika. Vivyo hivyo Yuda alikwisha kuwa mwizi kabla ya jambo hili, kwa hiyo, alikuwa na mwenendo wa kishetani. Yuda alipewa motisha ya ziada ya kibinafsi ya kupewa hongo na makuhani. Mwishoni, aliiona fursa baada ya karamu ya mwisho. Hivyo basi ni sababu gani hasa ilimfanya Yuda amsaliti Yesu? – Sababu zote tatu zilihusika.

 

S: Kwenye Mat 26:26-28; Mak 14:22 na Luk 22:19, kwa nini mkate na divai si mwili halisi wa Yesu?

J: Tunaweza kuona kuwa Yesu alimaanisha kuwa mkate na divai vilikuwa ishara ya mwili wake kwa sababu mbili.
Kwanza, hakuna kiasi chochote kidogo cha ushahidi kuwa watu walikuwa wanasijudu mkate na divai, iwe kwenye Biblia au kanisa la awali. Hatupaswi kukiabudu kitu chochote au mtu yeyote mbali ya Mungu. Tunamwabudu Yesu lakini kama mkate na divai si Yesu, hatupaswi kuviabudu.
Pili, kama mtu akiichukua sitiara hii kuwa mkate na divai vilikuwa au vilifanyika kuwa Yesu basi ili kudumisha mtazamo huu tungetakiwa kuzichukua sitiara nyingine pia za mwili wa Yesu kuwa Yesu, kama vile kwenye 1 Kor 12:27. Sisi (kanisa) ni mwili wa Kristo. Je unadhani kuwa watu wakuabudu, au kusanyiko unalohudhuria? Kama si lolote kati ya hayo mawili, kwa nini basi humwabudu Mkristo, aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu kuliko mkate na mvinyo, ambavyo havijaumbwa kwa mfano wa Mungu.
Sasa, hatupaswi kuwaabudu Wakristo wakati wowote ule. Lakini je kuwaabudu watu wengine, na kuhalalisha jambo hilo kwa kielelezo cha Kristo, kunaweza kuwa kubaya zaidi ya kuabudu mkate na mvinyo, na kulihalalisha jambo hilo kwa kielelezo cha Kristo?

 

S: Kwenye Mat 26:49-50, kwa nini Yesu alisalitiwa na Yuda kwa njia ya busu, kisha Yesu alitwaliwa, lakini kwenye Yoh 18:2-9 Yesu alisogea mbele na kujitambulisha, bila ya Yuda kumpiga busu?

J: Kutokutoa maele kuhusu busu kwenye Yoh 18:2-9 hakumaanishi kuwa hakuna busu iliyopigwa. Yuda anaweza kuwa alimbusu Yesu, kwa mujibu wa Mat 26:49; kisha askari walirudi nyuma kwenye Yoh 18:2-9, na baadaye walimtwaa Yesu kwenye Mat 26:50. Jambo pekee lililosemwa kuwa lilitokea "mara" lilikuwa ni busu ya Yuda mwanzoni.

 

S: Mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anadai kuwa kwenye Injili ya Marko mashtaka dhidi ya Yesu yalifanyika kwa haraka ambapo Yesu ni kama hakusema kitu chochote, lakini kwenye Injili ya Yohana mashtaka yalifanyika kwa muda mrefu na Yesu aliongea kirefu na washtki wake (Jesus, Interrupted uk.43).

J: Hoja hii ni ya kipumbavu, kwa sababu si Marko wala Yohana anayeeleza bayana maongezi yalikuwa marefu kiasi gani, na Yesu anaweza kuwa alisema vitu vingi kuliko wainjilisti hawa walivyoandika. Mashtaka yaliendeshwa mara mbili siyo moja (kwanza na Wayahahudi, kisha na Waroma). Mwinjilisti Marko ameeleza sentence mbili ambazo Yesu alizisema kwenye mashtaka yaliyoendeshwa na Wayahudi, na sentensi moja kwenye mashtaka yaliyoendeshwa na Waroma. Mwinjilisti Yohana ameeleza sentensi tano ambazo Yesu alizisema kwenye mashtaka yaliyoendeshwa na Waroma. Lakini pia, hakuna injili inayosemaa kuwa imeeleza mambo yote ambayo Yesu aliyasema.

 

S: Kwenye Mat 27:11-14, kwa nini Yesu hajibu hata shtaka moja mbele ya Pilato, kwani Yoh 18:33-37 [inadaiwa] inatueleza kuwa Yesu alijibu mashtaka yote alipokuwa mbele ya Pilato?

J: Hizi nyakati tofauti. Kwenye Mat 27:11-14, wakati makuhani wakuu na wazee walipokuwa naye (mstari wa 12), Yesu hakuwajibu kitu chochote. Yoh 18:28 Wayahudi hawakuingia kwenye jumba la Pilato (Praitorio), hivyo kwenye Yoh 18:29 Pilato (akiambatana na Yesu) alikwenda nje walikokuweko watu. Yoh 18:33 inasema kuwa baada ya Yoh 18:33 inasema kuwa baada ya hapo Pilato aliingia kwenye Praitorio na kumwita Yesu. Kisha kwenye Yoh 18:34-37 Yesu alijibu maswali ya Pilato. Licha ya hilo, si sahihi kusema kuwa Yoh 18:33-37 inasema kuwa Yesu alitoa majibu kwa mashitaka yote; inasema tu kuwa Pilato alisema, "Mimi sioni hatia yo yotr kwake."

 

S: Kwenye Mat 27:14, wakati wa kusikiliza mashtaka mbele ya Pilato, je Yesu hakutoa jibu lolote, au alijibu maswali ya Pilato kwa njia isiyokuwa dhahiri kama Yoh 18:33-37 [inavyodaiwa] kuonyesha?

J: Yoh 18:33-37 HAISEMI kuwa Yesu alijibu maswali yote ya Yesu. Yawezekana Pilato alimuuliza maswali mengi, na Yoh 18:33-38 imeyataja manne tu, ambayo kati yake Yesu aliyajibu matatu. Mat 27:14 inasema kuwa Yesu hakujibu neno lolote wakati makuhani na wazee waliposema kuwa amefanya makosa, na wakati Pilato alipomuuliza swali ambalo halikuelezwa kwenye Yoh 18:33-37. Hivyo Yesu hakujibu swali lolote lililoulizwa na makuhani na wazee, hata baada ya Pilato kumuuliza endapo alisikia mashitaka hayo. Baadaye, Yesu alijibu maswali [yasiyopungua] matatu aliyouliza Pilato.

 

S: Kwenye Mat 28:1-8, nabii zinawezaje kuthibitisha kuwa Yesu alikuwa Mungu, endapo alikuwa mgeni? (Nimesikia jambo hili toka kwa mwanafunzi wa chuo kikuu aliyekuwa anakuwa anashiriki kwenye hadithi za kubuni zihusuzo sayansi za Kimarekani ziitwazo ‘Star Trek' na Kanisa la Sayantolojia, yaani the Church of Scientology)

J: Kama Yesu angekuwa kiumbe wa kubuniwa atokaye kwenye ulimwengu mwingine, angekuwa na akili sana kiasi kufanya nabii zote hizi zitimie. Kwa kweli, ukilinganisha na sisi, angekuwa anajua kila kitu. Yesu pia angekuwa kiumbe mgeni mwenye uwezo wa kufanya miujiza yote aliyofanya, ikiwa pamoja na kufufuka toka katika wafu. Tungeyachukulia mambo haya kuwa yenye uwezo wote. Ili aweze kuwafunza watu mafunzo ambayo Yesu alifundisha, alipaswa kuwa na maadili mazuri, karibu na kuwa mkamilifu. Kwa hiyo kama unafikiri Yesu alikuwa ni nafsi yenye uhai yenye kujua mambo yote, yenye nguvu zote, na kamilifu kimaadili isiyotoka kwenye ulimwengu huu, iliyokuja kutuonyesha kweli, nakubaliana na wewe!

 

S: Kwenye Injili, ni mtu gani mwingine mbali ya Yesu aliyedai kuwa Masihi au Mungu?

J: Watu wafuatao ama wamesema maneno yafuatayo, au watu wengine wamesema maneno yafuatayo kuhusu wao.

... Kristo alirudi mara ya pili

Grigori Rasputin (angalau kuna watu waliosema hivi)

Rev. Jim Jones wa Jonestown (alikufa 11/16/1978)

Rev. Moon wa Kanisa la Wamuni (Unification Church)

Jacob Katzan (1977-)

Guru Maharah Ji wa Divine Light Mission

Wahindu wengi na viongozi wa kiroho wa ‘New Age'

... Masihi wa Kiyahudi aliyekuja mara ya kwanza

Sabbatai Sebi/Zvi Sept. 1666 BK alisilimishwa kwa nguvu

Rabbi Schneerson wa New York (sasa ni marehemu)

Theudas kwenye Mdo 5:36 huenda alidai kuwa yeye ni mtu mkubwa

... Mahdi kwenye madhehebu ya Kishia

Khalifa Mfatimidi wa kwanza ‘Obaidallah/‘Ubaydullah (mwaka 909-933/934 BK)

Imamu al Husayn bin al-Kasim al-‘Iyani (1010-1013 BK) (dhehebu la Husayniiya Zaydite)

Mirza Ghulam Ahmad (mwaka 1879 BK, harakati ya Ahmadiyya)

Baha'ullah (Baha'is) (mwaka 1817-1892)

Husayn ‘Ali Nuri Baha', kaka wa Baha'ullah

Sliman Murshad wa Shamu (mwaka 1900-1949)

Harakati ya Kimahdi ya Sudan

Wengi wengineo

... Masihi wa Kizoroastria, au Saoshyants

... Mungu anayeonekana

Muhammad aliabudiwa kama Mungu anayeonekana na Wahammidiya

‘Ali ni mungu kwa mujibu wa ‘Ulyaniyya/'Alaya'iyya

‘Ali bin Abi Talib na Saliman al-Farisi. Hawakudai kuwa mungu, lakini muda mrefu baada ya kufa kwao baadhi yamadhehebu ya Ki‘alawi yaliwaabudu kama miungu mitatu ya Uislamu.

Bwana Hakim (Mdruze) [mwaka 996-1021 BK]

Mungu amekuwepo kupitia manabii wote kwa mujibu wa dhehebu la Kishia la Rizamiyya/Muslimiyya

 

S: Je kuna mtu mwingine mbali ya Yesu aliyefanya miujiza mingi huko Palestina?

J: Hapana. Hata hivyo, kuna watu wanaodai kuwa Onias mtengeneza circle wa karne ya kwanza KK alifanya muujiza, kwa sababu aliomba mvua inyeshe na ilinyesha. Ifuatayo ni nukuu kutoka Taanith 3.8 kwenye The New Testament Background, uk.170. "Kuna wakati watu walimwambia Onias Circle-Maker, ‘Omba ili mvua inyeshe.' Alijibu, ‘Nendeni nje na kuleta oveni za Pasaka ili zilainishwe [yaani kwa mvua].' Aliomba lakini mvua haikunyesha. Ulifanya nini? Alichora mduara na kusimama ndani yake na alisema mbele za Mungu, ‘Eh Bwana wa ulimwengu watoto wako wamegeuzia nyuso zao kwangu, kwa kuwa mimi na kama mtoto wa nyumbani mwako machoni pako. Naapa kwa jina lako kuu kuwa sitaamka mpaka hapo utakapowaonea huruma watoto wako.' Mvua ilianza kunyesha tone kwa tone. AlisemaH, ‘Hatujaomba kwa ajili ya mvua kama hii, bali mvua itakayojaza matangi ya maji, mashimo, na mapango.' Mvua ilianza kunyesha kwa nguvu sana. Alisema, ‘Sikuomba kwa ajili ya mvua ya namna hii, bali mvua ya wema, baraka, na neema.' Kisha mvua ilinyesha kwa kiasi [na iliendelea] adi Waisraeli walipokwenda kutoka Yerusalem hadi Kilima cha Hekalu kwa sababu ya mvua." Hatimaye mvua ilinyesha sana hata walimwomba kuwa aombe ili iache kunyesha. Josephus pia anaelezea kwa ufupi kuwa Onias aliomba mvua iache kunyesha kwenye Antiquities of the Jews 14.2.1 (au 14 §§22-24).

 

S: Kwenye injili, kuna vianzo gani vya habari kuhusu Yesu mbali ya Biblia vilivyoandikwa kbla ya mwaka 200 BK?

J: Inawezekana mtu kufikiri kuwa maisha ya Yesu na Ukristo havikuelezwa, hata nje ya Biblia. Moja ya malengo ya kutoa nukuu hizi ni kusitisha madai ambayo watu wenye kushuku wanayatoa kuwa Yesu hakuwahi kuishi hapa duniani.

Cornelius Tacitus (aliyeishi karibu mwwaka 55 hadi karibu mwaka 117 BK) alikuwa mwanahistoria wa Kiroma aliyeandika kuhusu matukio ya Roma na Uingereza kuanzia mwaka 15-70 BK. Dharau aliyoionyesha inadhihirisha kuwa hakuwa rafiki wa Ukristo. Kwenye Annals 15:44 aliandika: ". . . Lakini juhudi zote za kibinadamu, zawadi zote za kifahari za Mfalme, na kuiridhisha miungu, havikuondoa imani mbaya kuwa moto mkubwa [wa Roma] ulitokana na amri [ya Mfalme]. Kwa ajili hiyo, ili kujiepusha na taarifa hiyo, Nero alikazia hatia yake na kutoa mateso makubwa zaidi kwa kundi la watu lililochukiwa kwa ajili ya mambo yake yasiyopendeza, ambalo watu wengi waliliita Wakristo. ‘Christus', ambaye jina hili lilitokana naye, alipewa adhabu kubwa zaidi na mmoja wa maliwali wetu, Pontio Pilato, wakati wa utawala wa Tiberius, na ushirikina wenye kusumbua sana, ambao ulidhibitiwa kwa muda, uliibuka tena Uyahudi, mahali ulikoanzia, na hata Roma, ambako mambo yote yenye kuchukiza na kuaibisha kutoka sehemu zote za dunia hufanya makao na kupata ummarufu. Kwa ajili hiyo, kwanza kabisa watu waliobainika kuwa na hatia walikamatwa; kisha, baada ya taarifa zao, umati mkubwa ulionekana kuwa na hatia, si kwa ajili ya kuuunguza mji bali kuwachukia binadamu wengine. Vifo vyao viliandamana na dharau za kila namna. Wakiwa wamefunikwa na ngozi za wanyama, walishambuliwa na mbwa na wakaangamia, au walisublubiwa msalabani, au walihukumiwa kutupwa kwenye moto na kuunguzwa, kutumika kama mwanga wakati wa usiku, wakati mwangaza wa mchana unapokuwa umeondoka . . ."

Tacitus kwenye Histories kitabu cha 5 pia anaongelea undani wa vikosi mbalimbali vya Kiroma, cha 5, 10, 15, 12, na watu wengine kutoka vikosi vya 18 na 3 walivyozimisha maasi Uyahudi na kuuteketza mji wa Yerusalem.

Nukuu za Tacitus zimechukuliwa kutoka kwenye kitabu kiitwacho The Annals and The Histories kilichoandikwa na P. Cornelius Tacitus, Encyclopedia Britannica, Inc. 1952.

Mara Bar-Serapion alikuwa Mshamu wa kawaida aliyemwandikia mwanae, Serapion, barua baada ya mwaka 73 BK. Anamsihi kuiga mwenendo wa watu wenye hekima katika historia ambao walkufa kwa ajili ya mambo waliyoyaamini, kama vile Socrates, Pythagoras, na mfalme mwenye hekima aliyeuawa na Wayahudi. Kazi hii imo kwenye jumba la Makumbusho la Uingereza (British Museum).

Josephus alikuwa mwanazuoni wa Kiyahudi aliyezaliwa mwaka 37/38 BK, aliyeandika mambo mazuri kuhusu Kristo. Kuna vifungu viwili ambavyo anamwongelea Yesu. Kwenye kifungu cha kwanza, Josephus anaongelea maisha na huduma ya Yesu (Antiquities of the Jews 18.3.3, au 18 §§63-64), na kwenye kifungu cha pili anamtaja Yesu kama kaka yake Yakobo (Antiquities of the Jews 20.9.1, or 20 §§200-203). Kuna matoleo mbalimbali ya kifungu cha kwanza, lakini tutaongelea kwa ufupi matoleo ya Kiarabu na Kilatini. Toleo la Kilatini, ambalo limeonyeshwa hapa, na toleo la Kiarabu, ambalo liliandikwa karne ya 10, yanafanana sana isipokuwa toleo la Kiarabu halina sehemu zilizopigiwa mstari.

"Karibu na kipindi hiki, Yesu, mtu mwenye hekima, kama ni sahihi kumuita mtu, kwani alikuwa mtendaji wa mambo ya ajabu, - mwalimu wa watu kama hawa waliopokea kweli kwa furaha. Aliwavuta kwake wengi wa Wayahudi, na wengi wa mataifa. Alikuwa Kristo; na wakati Pilato, kwa mapendekezo ya wakuu wa watu miongoni mwetu, alipomhukumu asulubiwe, watu wale waliompenda tokea mwanzo hawakumuacha, kwani alitokea kwao tena akiwa hai siku ya tatu, kama ambavyo manabii wa Mungu walivyokuwa wametabiri mambo haya na kisha mambo mengine ya maajabu elfu kumi kuhusu yeye; na kabila la Wakristo, walioitwa hivyo kwa jina lake, hawajatoweka leo." (Antiquities of the Jews 18.3.3, iliyoandikwa karibu mwaka 93-94 BK). Kifungu hiki kimetolewa kutoka Josephus: Complete Works. Kregel Publications 1960. Maneno haya ni muunganiko wa tafsiri ya William Whiston (1867) na toleo la lenye kutumika sana lililotolewa na Porter na Coates, Philadelphia, Pennsylvania).

Toleo la Kiarabu ambalo ni fupi kuliko la Kilatini huchukuliwa kuwa sahihi zaidi. Toleo lolote lililo sahihi, huu ni ushuhuda wa kuwa Yesu alikuwepo hapa duniani na kuwa alisulubiwa.

Lucian wa Samosata, (pia alifahamika kama Lucian Mgiriki) mwandishi tashtiti wa karne ya pili, aliyeandika kuhusu Kristo, ". . . mtu aliyesulubiwa Palestina kwa sababu ya kuanzisha mfumo wa kidini ulimwenguni . . . Pia, mto sheria wao wa kwanza aliwashawishi kuwa wote ni ndugu wa kila mmoja wao baada ya kukiuka kwa kukataa miungu ya Kigiriki na kwa kumwabudu mwalimu wa filisofia mwenyewe aliyesulubiwa na kuishi kwa kufuata sheria zake." (The Passing Peregrinus -pia inaitwa The Death of Peregrine 11-13).

Clement wa Roma alikuwa askofu wa Kikristo aliyeliandikia kanisa lililoko Korinto, kimsingi aliwauliza kwa nini hawakuwa wanatii mambo ambayo Paulo aliwaandikia miaka 50 iliyopita. Barua ya Clement iliandikwa mwaka 96-98 BK.

Pliny Mdogo alikuwa liwali wa of Bithynia aliyewaua Wakristo wengi kwa sababu ya imani yao. Alimwandikia Mfalme Trajan mwaka 112 BK na kumuuliza endapo aendelee kuwaua wanaume, wanawake, na watoto kwa ajili ya kutokuiabudu sanamu ya mfalme. Pliny anasema kuhusu Wakristo, "hata hivyo walithibitisha kuwa hatia yao yote ilikuwa kwamba walikuwa na mazoea ya kukutana kwenye siku moja iliyopangea kabla ya jua kuchomoza, baada ya kuimba mistari ya nyimbo kwa kupokezana wakimtukuza Kristo kama Mungu, na kuweka kiapo cha kutokufanya matendo yeyote maovu, bali kujiepusha na ulaghai, uizi, uzinzi, kutokusema uongo, kutokukataa jukumu wanapotakiwa kulitimiza (Epistles 10.96). Pamoja na hayo, Pliny pia anatupa habari kuhusu Waesene.

Papias ni askofu mwingine aliyekuwa mwanafunzi wa Mtume Yohana. Aliandika kazi nyingi sana karibu na miaka 110 hadi 130 BK. Kwa bahati mbaya maandiko yake yamepotea, isipokuwa maelezo mafupi yaliyotolewa na Eusebius wa Kaisaria (aliyeandika karibu mwaka 325 BK). Eusebius anasema kuwa pamoja na mambo mengine, Papias alisema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwenye Kiebrania, Marko alikuwa mkalimani wa Petro, na kwama Papias alifundisha kuhusu kuja kwa Yesu kabla ya kipindi cha kutawala kwake duniani kwa muda wa miaka elfu moja, yaani ‘premillennialism.' (Eusebius alikuwa haamini uwepo wa kipindi hicho, hivyo anaitwa ‘millennialist').

Ignatius alikuwa mwanafunzi wa Mtume Yohana. Aliandika barua kwa makanisa mengi, na alikufa ama mwaka 107 au 116 BK wakati wa utawala wa Mfalme Trajan.

Polycarp askofu wa Smyrna, alikuwa mfiadini Mkristo na mwanafunzi wa Ignatius aliyeongea kuhusu Kristo. Alikufa karibu mwaka c.163 BK.

Irenaeus, askofu wa yon (Ufaransa), alikuwa mwanafunzi wa Polycarp, na mfiadini aliyeishi kutoka mwaka 120/140-202 BK. Aliandika andiko kubwa dhidi ya mafundisho ya uongo ya wakati ule kutoka mwaka 182-188 BK.

Didache (au Mafundisho ya Mitume Watakatifu) kilikuwa ni kitabu cha kiada cha mafundisho ya kanisa ambacho mtunzi wake na tarehe ya kuandikwa havifahamiki, inakisiwa kuwa karibu mwaka 380 BK.

Justin Martyr alikuwa ni mwanafilosofia Mgiriki aliyezaliwa ama mwaka 110 au 114 BK. Alibadili dini na kuwa Mkristo karibu mwaka 138 na kwa mujibu wa kazi yake, First Apology ilikuwa miaka 150 baada ya Kristo kuzaliwa. Kwenye utetezi wake wa kwanza na wa pili, na kazi yake, Dialogue with Trypho the Jew, Justin anaeleza kuwa Yesu ni Mungu. Chronicon Paschale inaeleza kuwa Justin aliuawa kwa sababu ya imani yake mwaka 165 BK.

Suetonius, mwanahistoria wa Kiroma na afisa wa mahakama aliyeandika karibu mwaka 120 BK, anasema kuwa "Wakati Wayahudi walipokuwa wanafanya vurugu zilizotokana na Krestus (Chrestus, ni tahajia nyingine ya Kristus [Christus], yaani Krsto), aliwafukuza Roma (Life of Claudius 25.4).

Theophilus, askofu wa Antiokia alikuwa mwandishi wa kwanza anayefahamika sasa kutumia neno la Kigiriki lenye kumaanisha Utatu (Triad) kwenye To Autolycus kitabu cha 2 sura ya 15, uk.101. Aliandika kati ya mwaka 168 na 181/188 BK.

Clement wa Alexandria, huyu ni tofauti na Clement wa Roma aliyeongelewa hapo awali, ambaye aliishi kutoka mwaka 193-217/220 BK. Aliandika kwa kiasi kikubwa sana ikiwa ni pamoja na wimbo wa Kristo na kazi kubwa iitwayo Miscellanies.

Hippolytus aliandika kutoka mwaka 225-235/6 BK na aliandika Refutation of All Heresies. Hippolytus alikuwa mwanafunzi wa Irenaeus.

Tatian aliishi kutoka mwaka 110-172 BK na aliandika mpangilio wa injili nne unaoweka pamoja matukio yanayofanana wenye karibu 79% ya mistari yote ya kwenye injili. Kwa bahati mbaya, baadaye aliiasi imani na kujiunga na Waenkrate (dhehebu la Kinostisia la karne ya pili waliokuwa wanazuia kuoa au kuolewa, kula nyama na kunywa mvinyo), dhehebu la mafundisho ya uongo la Kinostisia (harakati kizushi ya zama za kanisa la Kikristo la karne ya pili BK iliyokazia kuwa mada ni ovu na kuwa uhuru unapatikana kwa ufahamu).

Talmudi za Kiyahudi zinamwongelea Yesu sehemu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Babylonian Talmud, Tol'doth Yeshu, Barailu, Amoa ‘Ulla', Yeb. IV 3, na Baraita. Tazama pia Tractate Sanhedrin.

Phlegon alikuwa mwandishi wa Kigiriki kutoka Caria na mtumwa wa Mfalme Harian aliyeachwa huru. Aliandika muda mfupi baada ya mwaka 137 BK kuwa kwenye mwaka wa nne wa kipindi cha 202 cha miaka mine baina ya michezo ya Olimpiki [33 BK] kulikuwa na "kupatwa kwa jua kukubwa zaidi" na kwamba "kulitokea giza saa sita mchana [saa 6:00 kamili] hata nyota zilionekana mbinugni. Kulitokea tetemeko kubwa la ardhi huko Bithynia, na vitu vingi vilipidnuliwa huko Nikea" (Case for Christ, uk.111). Nukuu nzima kwa mujibu wa Baker Encyclopedia of Christian Apologetics, uk.384 inasomeka: "Yesu, alipokuwa hai, hakujipa msaada wowote ule, lakini alifufuka baada ya kufa na kuonyesha alama za kuteswa kwake, na kuonyesha jinsi mikono ilivyochomwa nan a misumari" na baadaye "kupatwa kwa jua wakati wa utawala wa Kaisari Tiberius, ambao unaelekea kuwa ndio muda Yesu aliposulubiwa, na tetemeko kubwa lililotokea wakati huo" kwenye Origen Against Celsus kitabu cha 2 sura ya 33, uk.455 kwenye Ante-Nicene Fathers juzuu ya 4, na Julius Africanus Events in Persia sura ya 18, uk.136. Tazama pia Origen Against Celsus kitabu cha 2 sura ya 59, uk.455.

Thales (au Thallus) alikuwa mwanahistoria wa Kipalestina aliyetajwa na Julius Africanus (aliyeandika mwaka 232-245 BK) Julius anaongea kuhusu giza lililotkea wakati wa Kristo, "Giza hili Thallus, kwenye kitabu cha tatu cha historia yake, analiita, kama inavyoonekana kwangu bila sababu, kupatwa kwa jua" (The Ante-Nicene Fathers juzuu ya 6 kipande cha 18, uk.136). Muktadha ni Julius anapoongelea jinsi muda kuanzia amri ya Ahasuero hadi kusulubiwa kwa Kristo, ulivyotimiza Danieli 9.

Mwanahistoria wa Samaria, Thallus, ambaye ni tofauti na mwanahistoria wa Kigiriki, Thales, alikuwa anafahamika sana. Kazi zifuatazo zinamtaja Thallus.

Justin Martyr's Hortatory Address to the Greeks kitabu cha 9, uk.277 inawataja Thallus, Philo, Josephus, na wengineo.

Theophilus to Autolychus sura ya 29, uk.120 anamtaja Thallus, pia kabla ya hapo Berosus ambaye ni mwanahistoria Mkaldayo aliyeongea kwenye uk.121.

Octavius wa Minucius Felix sura ya 22, uk.186

Tertullian's Apology sura ya 19, uk.33 inawataja Thallus na Josephus.

Julius Africanus kipande cha 18, uk.136.

The Shepherd of Hermas ni kazi ya Kikristo ambayo mwandishi wake hafahamiki iliandikwa karibu mwaka 160 BK.

Athenagoras alimwandikia mfalme wa Roma utetezi wa Ukristo karibu mwaka 177 BK.

Aristides wa Athens na Quadratus pia wanafahamika kuandika utetezi wa Ukristo, lakini tuna baadhi tu ya maandiko yao yaliyohifadhiwa.

 

S: Ni toleo lipi lililopo la Josephus linalofanana zaidi na kazi aliyoandika mara ya kwanza kabisa?

J: Huenda ikawa nit oleo fupi. Kwanza tutaonyesha tofauti, kisha ushahidi wa maoni matatu, na mwisho mahitimisho ya wanazuoni mbalimbali.

 

 

Tofauti:

Toleo la Kilatini lina sehemu zilizopigiwa mistari, na toleo la Kiarabu la karne ya kumi halifanyi hivyo.

"Sasa karibu na wakati huu, Yesu, mtu mwenye hekima, kama ni halali kumuita mtu, kwani alikuwa mtenda kazi za ajabu, - mwalimu wa watu walioipokea kweli kwa furaha. Aliwavuta wengi wa Wayahudi na wamataifa. Alikuwa ni Kristo; na Pilato, kwa kushauriwa na wakuu wetu, alimhukumu asulubiwe, wale waliompenda mwanzoni hawakumwacha, kwani alitokea kwao akiwa hai tena siku ya tatu, kama manabii wa Mungu walivyotabiri mambo haya na kisha mambo mengine elfu kumi ya ajabu kuhusu yeye; na kabila la Wakristo, walioitwa hivyo kwa jina lake, hawajatoweka hadi leo hii" (Antiquities of the Jews 18.3.3, iliyoandikwa karibu mwaka 93-94 BK). Nukuu hii imechukuliwa kutoak Josephus: Complete Works, Kregel Publications 1960. Maneno haya ni mchanganyiko wa tafsiri ya William Whiston (1867) na toleo la lenye kutumika sana lililotolewa na Porter and Coates, Philadelphia, Pennsylvania.

Ushahidi wa sehemu zilizopigiwa mistari:

Maandishi haya, yenye sehemu zilizopigiwa mistari, yamenukuliwa kutoka kwenye kazi zifuatazo:

Eusebius, Ecclesiastical History 1.11 (mwaka 324 BK).

Hieronym (Jerome), De Vir. Illustr (mwaka 400 BK)

Isidorus, Pelusiota kitabu cha 4 barua ya 225.

Macarius, Actis Sanctorum kitabu cha 5, uk.149 ap. Fabric. Joseph uk.61 (jina la kitabu halifahamiki)

Cedrenus, Compendium Historia, uk.,196 (karibu mwaka 1060 BK)

Zonaras, Annal litabu cha 1, uk.27 (karibu mwaka 1120 BK)

Gotfridus Viterbiensis, Chronicale, uk.366 e Vers. Rufini (karibu mwaka 1170 BK)

Platina de Vitis, Pontificum (karibu mwaka 1480 BK)

Wafuatao hawakumnukuu Josephus bali walisema kuwa alimwita Yesu kibayana kuwa Kristo.

Sozomen, Ecclesiastical History kitabu cha 1 sura ya 1 (mwaka 370-380/425 BK)

Cassiodorus kwenye historia yenye sehemu tatu Sozomeno (mwaka 510 BK)

Chronicles of Alexandria, uk.514, 526, 527, 584, 586 (mwaka 640 BK)

Johan. Malela Chronicles kitabu cha 10 (karibu mwaka 850 BK)

Photius Codex kitabu cha 48 I Codex 238, Codex 33 (mwaka 860 BK)

Glycus Annal uk.234 (karibu mwaka 1120 BK)

Unaweza kusoma maandishi ya kazi hizi kwenye Josephus: Complete Works, uk.640-643.

Pia, mtindo wa sehemu zilizopigiwa mistari unaelekea kufanana na sehemu iliyobaki.

Ushahidi dhidi ya Sehemu Zilizopigiwa Mistari:

Toleo la Kiarabu halina sehemu hizi, na toleo la Kilatini linazo. Toleo la Kilatini lina maelezo mengi sana kuhusu Kristo hata linaweza kumfanya msomaji ajiulize kuwa kwa nini Josephus hakuwa Mkristo. Jambo la uhakika ni kuwa mwanazuoni Mkristo wa kale Origen anasema kuwa Josephus hakuamini kuwa Yesu alikuwa Masishi kwenye Origen Against Celsus kitabu cha 1 sura ya 47, uk.416; kitabu cha 2 sura ya 13, uk.437. F.F. Bruce anahisi kuwa Josephus anaweza alinaidka maneno haya lakini alikuwa anafanya mzaha. Hata hivyo, hakuna kitu kwenye toleo la Kilatini lenye kuonyesha mzaha wa aina yeyote ile. Kwenye Josephus: Complete Works, kiambatisho kwenye uk.644 kinasema kuwa Josephus anamtaja Yesu kuwa Kristo [Masihi] kwa kuwa tu alikuwa mmoja wa watu ambao walielezwa kuwa Masihi, bila kumaanisha kuwa Josephus mwenyewe aliamini hivyo.

Je Kuna Yeyote Kati ya Hizo Iliyo Sahihi?

Faida: Tertullian hakusema kitu chochote kuhusu Josephus, na Clement wa Alexandria aliandika kuwa Josephus alisema kuhusu miaka kadhaa, lakini si mambo yanayohusiana na Kristo.

Hasara: Vyanzo vingi sana vinalitaja angalau toleo la msingi la Kiarabu hivyo haitakuwa rahisi kuwa vyanzo vyote hivi vitakuwa vimekosea kabisa. Hata vyanzo hivi kama vile Origen vyenye kusema kuwa Josephus hakuamini kuwa Yesu alikuwa Masihi vinamaanish kuwa Origen alisoma kwenye kazi za Josephus ambazo zimentaja Yesu. Nukuu toka kwa Origen (kama ilivyotolewa kwenye kiambatanisho cha tafsiri ya Whiston) kwa sehemu: "kwa sababu Josephus anashuhudia kwenye kitabu cha nane cha Antiquities of the Jews, kuwa Yohana alikuwa ndiye Mbatizaji, na kwamba aliahidi utakaso kwa watu waliokuwa wamebatizwa. Josephus huyo huyo pia, ingawa hakuamini kuwa Yesu alikuwa Kristo, alipokuwa anatafiti juu ya sababu ya kuangushwa kwa Yerusalemu, na kubomolewa kwa hekalu, na alipaswa kusema kuwa njama dhidi ya Yesu zilikuwa ndio chanzo cha ‘taabu zilizowapata watu, kwa sababu walimuua yule Kristo ambaye alitabiriwa na manabii, ambaye, ingawa haikudhamiriwa, na hakuwa mbali na ukweli, anasema kuwa taabu hizi zimewapata Wayahudi kama malipo ya Yakobo Mwenye Haki, ambaye alikuwa mdogo wa Yesu aitwaye Kristo"

Hitimisho - Toleo la Kiarabu ni Sahihi Zaidi

Mwanazuoni wa Agano ipya R. T France anasema hivi kwenye tovuti hii http://www.leaderu.com/truth/1truth21.html.

"Kimsingi, wanazuoni wote wanakubaliana kuwa toleo la Kilatini ni maboresho ya maandishi ya awali, lakini wengi wao wako tayari kuafiki kuwa kwenye maandishi ya awali, maelezo mafupi kuhusu Yesu, wazo hili lilikuwepo, huenda kwa kwa namna iliyo na sifa kidogo kuliko hizi. Maelezo mafupi ya Josephus kuhusu Yesu, aitwaye Masihi kwenye Antiquities 20 §§200 ni ngumu kuielezea bila kuwa na maelezo ya awali kuhusu Yesu, hususani kwa kuwa Josephus haongelei Ukristo mahali kwingine kokote, wala kumuita mtu mwingine yeyote yule jina Kristo (Christos). Toleo la Kiarabu la Testimonium lililo tofauti na ambalo ‘halijajitoa sana' lililoandikwa kwenye nukuu ya karne ya kumi ya Josephus, ingawa haielekei kuwa ndiyo maandishi ya awali, linashuhudia uwepo wa maelezo ya Yesu kwenye kazi za Josephus zilizotumika kwenye maandishi yaliyoboreshwa ya Kikristo. Hata hivyo, kuyapata maneno ambayo Josephus aliyaandika ni jambo la kubuni tu."

Baker Encyclopedia of Christian Apologetics, uk.382 inasema, "Ukweli wa kifungu hiki umetiliwa shaka na wanazuoni wa maeneo yote ya imani kwa sababu inaelekea kutia shaka kuwa Myahudi aliyeishi na kufanya kazi nje ya mandhari ya Kikristo angeweza kusema maneno kama haya kuhusu Yesu . . . Licha ya maoni haya, kuna sababu za kutosha za kuchukua sehemu kubwa ya maandishi haya kuwa kweli . . . Hata bila sehemu ambazo zinaweza kuwa ni nyongeza zilizofanywa na Wakristo, maandishi haya yanatoa ushahidi mkubwa sana wa maisha, kifo, na mvuto wa Yesu.

 

S: Kwa nini orodha ya vizazi vya Yesu kwenye Injili ya Luka inaanzia kwa Adamu, wakati ile ya Mathayo inaishia kwa Abrahamu tu?

J: Maandiko hayasemi hivyo, ila tunaweza kukisia. Mkazo wa Luka ulikuwa kwa Yesu kama Mwana wa Adamu, wakati mkazo wa Mathayo ulikuwa ni Yesu kama Masihi wa Kiyahudi aliyeahidiwa. Orodha ya vizazi ya Luka kupitia kwa Mariamu inathibitisha kuwa Yesu alikuwa mzao halisi wa Daudi (lakini siyo Sulemani). Orodha ya vizazi ya Yusufu ambayo Mathayo anaonyesha kuwa inaanzia kwa Daudi na Sulemani inathibitisha kuwa Yesu, kama mtoto halali wa Yusufu, alikuwa na mamlaka ya ufalme.

 

S: Kwenye Mat 1:1-17, je orodha hii ya vizazi vya Yesu inafananaje na ile ya Luk 3:23-38?

J: Kumbukumbu za kifalme kwa ujumla zilikuwa zinatoa orodha moja ya vizazi, lakini Yesu alikuwa na orodha mbili. Watu wengi wameona tatizo kwenye orodha za vizazi za Mathayo na Luka hasa utofauti wa majina ya watu baada ya Daudi. Lakini natujiulize maswali yetu wenyewe mawili. Yesu angekuwa na mamlaka gani kwenye kiti cha enzi cha Daudi endapo angekuwa mzao wa Daudi? – hakuna, kama angekuwa mzao kwa upande wa mama yake tu. Hii ndio maana ni muhimu kuwa Yesu alikuwa mtoto halali wa Yusufu wa kuasiliwa kwenye Injili ya Mathayo; watu huwa hawapati mamlaka ya ufalme kupitia upande wa mama. Kwa upande mwingine, endapo Mariamu hakuwa wa ukoo wa Daudi, je unabii kuwa Yesu alikuwa mzao wa Daudi kungekuwa na umuhimu gani? Hii ndio sababu orodha halisi ya vizazi kwenye Injili ya Luka ni ya muhimu. Hivyo, ili kuonyesha kuwa Yesu alitimiza jukumu la Masihi, orodha zote mbili za vizazi zilihitajika.

Tatizo ambalo baadhi ya watu wanalo ni kuwa orodha y vizazi ya Luka haisemi bayana kuwa "hii ni ya upande wa Mariamu." Lakini inamaanisha hivyo inaposema, "[Yesu] akidhaniwa kuwa mwana wa Yusufu, wa Eli . . ." Orodha za vizazi za kale kwa ujumla na zile za Kiyahudi bayana hazikuwa za wanawake.

Eli ametajwa kama baba wa Yesu kwa sababu, kama Justin Martyr (karibu mwaka 138-165 BK) alivyoandiaka, "kwa ajili hii kuzaliwa kwake [Yesu] na bikira, ambaye alikuwa, kama nilivyosema, wa ukoo wa Daudi, na Yakobo, na Isaka, na Abraham; au kwa sababu Adamu alikuwa baba wa Yesu mwenyewe na wa watu wote waliorodheshwa kwanza kupitia kwao Mariamu alizaliwa. Kwa kuwa tunajua kwamba mababa wa wanawake ni mababa [yaani mababa wa ukoo] pia wa watoto ambao mabinti zao wamewazaa" (Dialogue with Trypho the Jew ch.100 [ANF] juzuu la 1, uk.249).

Julius Africanus (mwaka 232-245 BK) kwenye barua yake, Letter to Aristides (Ante-Nicene Fathers juzuu ya 6, uk.125-127) pia alitofautisha kati ya orodha ya vizazi ya sheria na asili. Hata hivyo, alisema kuwa orodha moja ilikuwa halisi (ya kimwili) ya Yusufu na nyingine ilikuwa orodha ya asili ya Yusufu. Tazama pia Eusebius' Ecclesiastical History kitabu cha 1 sura ya 7 na kitabu cha 6 sura ya 31.

Mwandishi mwingine Mkristo wa kale aliyeona orodha moja ya vizazi ilikuwa ya Yusufu na nyingine ya Mariamu (ingawa alikuwa amezipindua) alikuwa Clement wa Alexandria kwenye The Stromata (mwaka 193-202 BK) kitabu cha 1 sura ya 21 (ANF sura ya 2, uk.334).

 

S: Kwenye Mat 1:12 na 1 Nya 3:15-17, baba wa was the father of Shealtieli Yekonia, au Neri kwenye Luk 3:27?

J: Palikuwa na watu wengi walioitwa Shealtieli na Zerubabeli.

Kwenye Mat 1:12 orodha inakwenda hivi Yosia (babu)->Yekonia->Shealtieli->Zerubabeli->Abihudi->Eliakimu

Kwenye Luk 3:26-27 orodha inakwenda Melki->Neri->Shealtieli->Zerubabeli->Resa->Yoana->Yuda->Yusufu

Kwenye 1 Nya 3:15-17 orodha ya vizazi inakwenda hivi Yosia ->Yehoyakimu->Yekonia->Shealtieli and Pedaya. Watoto wa Shealtieli hawajatajwa, lakini kwenye kizazi cha kifalme kinachofuata Pedaya anatajwa kuwa mtoto wa Zerubabeli.

Orodha za vizazi za Mariamu na Yusufu zinafanana hadi kwa Daudi, baada ya hapo zinatofautiana. Baada ya hapo, hakuna majina yanayofanana ama ya wazazi au watoto. Huenda Shealtieli and Zerubabeli kwenye Luka walitajwa kwa heshima ya maliwali waliotajwa kwenye 1 Nya 3:15-17 na Mat 1:12. Kumbuka pia kuwa Luk 3:26-27 inawataja Yuda na Yusufu, lakini hawa walikuwa watu tofauti na Yuda mtoto wa Yakobo, na Yusufu mume wa Mariamu.

 

S: Kwenye Luk 1:26, je kuzaliwa kwa Yesu kulijulishwa kwa Mariamu, au kwa Yusufu kwenye Mat 1:20?

J: Wote. Kulijulishwa kwanza kwa Mariamu, kwani angeshangaa kujiona kuwa mjamzito. Baadaye, malaika alitoa habari hizi kwa Yusufu ili kwamba Yusufu asimwache Mariamu kwa kukosa uaminifu.

 

S: Kwenye injili, taarifa za kuzaliwa kwa Yesu zina mambo gani yanayofanana?

J: Marko na Yohana hawatoi maelezo yeyote kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Yafuatayo ni mambo sita yahusuyo kuzaliwa kwa Yesu yenye kufanana kwenye injili za Mathayo na Luka:

1. Orodha ya vizazi kutoka Abrahamu hadi Daudi (Mat 1:2-6; Luk 3:31-34)

2. Mfalme Herode alikuwa anatawala (Mat 2:1; Luk 1:5)

3. Malaika wa Bwana anawatokea wazazi watarajiwa (Yusufu: Mat 1:20; Mariamu: Luk 1:26-38)

4. Yesu alizaliwa Bethlehemu ya Uyahudi (Mat 2:1; Luk 2:4-7)

5. Yusufu, Mariamu na mtoto Yesu walirudi Nazareti (Mat 2:19-22; Luk 2:39)

6. Yesu alikulia Nazareti (Mat 2:23; Luk 2:40)

Kwa ujumla, injili hizi mbili zinaungana pamoja kwa namna nzuri sana kutoa picha kamili ya maisha ya utoto wa Yesu. Mathayo anaelezea orodha ya vizazi vya Yusufu, mamajusi, na kukimbilia Misri. Luke anaongea kuhusu Gabrieli, Yohana Mbatizaji, orodha ya vizazi vya Mariamu, wachungaji, Simeoni, na Ana. Ingawa hatujui ipi iliandikwa kwanza, Luka anasema kuwa watu wengine wameandika habari za Yesu. Hivyo, Injili ya Luka inawezakuwa iliandikwa baada ya Injili ya Mathayo, na baada ya kusoma Injili ya Mathayo, Luka aliamua kutoa maelezo zaidi ambayo Mathayo hakuwa ameyaandika. Yohana anaweza kuwa aliandika baada yao wote, na inaonekana Yohana hakuwa na kitu chochote cha kuongezea.

 

S: Kwenye injili, je Yesu aliamini kuwa Maandiko hayana makosa (kwenye maandishi yake ya awali)?

J: Jibu hili lilitolewa kwenye tovuti ambayo haipo tena www. wam.umd.edu /~cbernard/Theology/inerrancy.html.

Yesu amekuwa akiyachukua masimulizi ya kijistoria ya Agano la Kale kama rekodi za ukweli halisi. Anataja:

Abeli (Luk 11:51)

Nuhu (Mathayo 24:37-39; Luk 17:26, 27)

Abrahamu (Yohana 8:56)

Tohara (Yohana 7:22; linganisha na Mwa 17:10-12; Law 12:3)

Sodoma na Gomora (Mat 10:15; 11:23,24; Luk 10:12)

Lutu (Luk 17:28-32)

Isaka na Yakobo (Mat 8:11; Luk 13:28)

Mana jangwani (Yoh 6:31, 49, 58)

Nyoka jangwani (Yoh 3:14)

Yesu kama Bwana wa Daudi (Mat 22:43; Mak 12:36; Luk 20:42)

Daudi akila mikate ya wonyesho (Mat 12:1-8; Mak 2:23-28; Luk 6:1-5)

Sulemani (Mat 6:29; 12:42; Luk 11:31; 12:27)

Elisha (Luk 4:27)

Yona (Mat 12:39-41; Luk 11:29, 30, 32)

Zakaria (Luk 11:51)

Kifungu cha mwisho kinaleta dhana ya Yesu ya umoja wa historia kutokea "kuumbwa kwa dunia" hadi "kizazi hiki." Amemwongelea Musa mara kwa mara kama mtoaji sheria (Mat 8:4; 19:8; Mak 1:44; 7:10; 10:5; 12:26; Luk 5:14; 20:37; Yoh 5:46; 7:19). Hutaja mara kwa mara mateso ya manabii wa kweli (Mat 5:12; 13:57; 21:34-36; 23:29-37; Mak 6:4 [linganisha na Luk 4:24; Yoh 4:44]; 12:2-5; Luk 6:23; 11:47-51; 13:34; 20:10-12) na anatoa maoni kuhusu umaarufu wa manabii wa uongo (Luk 6:26). Anathibitisha vifungu muhimu kama Mwanzo 1 na 2 (Mat 19:4,5; Mak 10:6-8).

Kuna watu wanaoweza kupinga kuhusiana na jambo hili na kusema kuwa Yesu alikuwa akitumia mambo ya kubuniwa na hadithi za kimila kuelezea mambo aliyokuwa akifundisha. Wazo hili linawezekana kuwa sahihi katika vifungu vingine lakini halielekei kuwa hivyo hapa. Kwanza, jambo ambalo mtu analipata tokana na kusoma habari za kwenye injili ni kuwa Yesu anachukulia masimulizi ya Agano la Kale kuwa historia halisi. Lengo la kunukuu Maandiko linaonyesha kuwa Yesu aliamini masimulizi haya kuwa yanawasilisha matukio halisi kihistoria. Pili, haionekani kuwa ni maana mojawapo ya kweli kudai kuwa Yesu alikuwa anatumia tu mambo ya kubuniwa yaliyopo kwenye jamii yake kuelezea mafundisho yake kwenye vifungu kama Mat 12:41; 24:37; 11:23,24; 5:12; 4:4.

Tatu, anachukulia kuvuviwa kwa Biblia kuwa ni jambo la kweli. Anatumia misemo "Andiko linasema . . .", na "Mungu anasema . . ." kwa kubadilishana na kwa kufanya hivyo anaonyesha kuwa maandishi ya Agano la Kale ni Neno la Mungu. Akinukuu Mwa 2:24, Yesu alisema, "Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sabaabu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye . . ." Tazama kuwa Mwa 2:24 si nukuu ya moja kwa moja ya maneno ya Mungu kwenye maandishi bali ni ufafanuzi wa mwandishi au msimulizi wa maandishi haya. Yesu anayachukulia maneno ya kifungu hiki cha Maandiko kuwa maneno ya Muumba mwenyewe. Kuvuviwa kwa nakala za awali (autographa) kunaonyesha kuwa Maandiko yalichukuliwa kutokuwa na makosa. Kama Yesu alikuwa sahihi kulichukua Agano la Kale kuwa ni maneno halisi ya Muumba, kulichukulia Agano la Kale kuwa lina makosa ni sawa na kumchukulia Mungu kuwa ana makosa.

Nne, aliamini kidhahiri kabisa mamlaka ya Biblia. Katika malumbano haya na Mafarisayo na Masadukayo, Yesu anayatumia Maandiko kama mamlaka yake ya kutatua malumbano haya. Anayaona Maandiko kuwa neno maneno yenye nguvu zaidi (Yoh 5:39-47; Mat 22:29, 31; Mak 12:24-26, Luk 20:37). Maandko yanaposema, Mungu anasema na suala lenye kuleta malumbano linasuluhishwa.

 

S: Kwenye injili, je mpangilio wa injili nne unaofuatisha matukio ni upi?

J: Ni muhimu kutenganisha kati ya mpangilio halisi na ule unaodhaniwa. Kwa matukio haya 27, tarakimu zinawakilisha matukio ambayo ni lazima yafuate matukio ya namba zilizotangulia. Herufi kama a, b, c zinawakilisha matukio ambayo yangeweza kutokea kwa kufuata mfuatano wowote ule. Kabla ya huduma ya Yesu kuanza, matukio yote kwenye injili yaliandikwa kwa kufuata mfuatano wa kutokea kwao, isipokuwa sehemu zilizopigiwa mistari. Vielelezi vya mahali, muda, na mfuatano uliopo kwenye injili vimeonyeshwa kwa herufi zenye wino mzito.

Kabla ya Huduma ya Yesu Kuanza: Mat 4:1-11; Mak 1:1-13; Luk 1:1-3:18; Luk 3:21-4:13; Yoh 1:1-42

B1a. Hapo mwanzo, Yesu aliishi mbinguni kabla ya kuja hapa duniani (Yoh 1:1-5; Yoh 17:5)

B1b. Orodha ya vizazi vya Mariamu kuanzia Adamu (ina mapengo kadhaa) [Luk 3:23-37]

B1c. Orodha ya vizazi vya Yusufu kuanzia Abrahamu (ina mapengo kadhaa) [Mat 1:1-17]

B2. Yesu akiwa Yerusalemu, wakati wa utawala wa Herode (mwaka 37 KK hadi 4 BK), Malaika Gabrieli anamtembelea Zakaria; Elizabeti mjamzito (Luk 1:1-25)

B3. Katika mwezi wa sita wa ujauzito wa Elizabeti, Malaika Gabriel anamtembelea Mariamu Nazareti, akimwambia kuwa atazaa mwana (Luk 1:26-38)

B4. Mariamu mjamzito, ingawa bado bikira (Mat 1:18-19)

B5. Baada ya Mariamu kuwa mjamzito, Malaika Gabrieli anamtembelea Yusufu (Mat 1:20-25)

B6. Safari ya kwenda Uyahudi, Mariamu amtembelea Elizabeti (Luk 1:39-56)

B7. Yohana Mbatizaji azaliwa (Luk 1:57-80)

B8. Wakati Herode alipokuwa mfalme (mwaka 37-4 KK), Kristo azaliwa Bethlehemu ya Uyahudi (Mat 2:1; Lk 2:1-7)

B9. Makondeni, malaika awaambia wachungaji kwenda kumwona Yesu (Luk 2:8-20)

B10a1. Siku ya nane, Yesu atahiriwa (Luk 2:21)

B10a2. Baada ya Mariamu kutakaswa (baada ya siku 33 kwa mujibu wa Law 12:1-4), kwenye hekalu la Yerusalemu, Yesu awekwa wakfu kwa Bwana (Luk 2:22-38)

B10b. Kwa wale walio kwenye nyumba ya Bethlehemu, Mamajusi kutoka mashariki waenda kumwabudu Yesu (Mat 2:2-12)

B11. Baada ya Mamajusi kuondoka, kukimbilia Misri (Mat 2:13-15)

B12. Kipindi cha miaka miwili, Herode aua watoto wa kiume wa Bethlehemu (Mat 2:16-18)

B13. Baada ya Herode kufa, Yusufu, Mariamu, na Yesu warudi Nazareti (Mat 2:19-22; Luk 2:40a)

B14a. Wakiwa Nazareti ya Galilaya, Yesu anakua (Mat 2:23; Luk 2:40b)

B14b. Kila mwaka wakati wa Pasaka, wazazi wa Yesu wanakwenda Yerusalemu (Luk 2:41)

B15. Akiwa na umri wa miaka 12, Yesu aenda hekaluni Yerusalemu (Luk 2:42-52)

B16. Kwenye jangwa la Uyahudi, Yohana Mbatizaji ahubiri (Mat 3:1-12; Mak 1:1-8; Luk 3:1-18; Yoh 1:6-28)

B17a. Wakati Yesu alipokuwa na miaka kama 30 hivi (huenda ilikuwa mwaka 33-34), anabatizwa kwenye mto wa Yordani (Mat 3:13-17; Mak 1:9-11; Luk 3:21-23)

B17b. Siku iliyofuata [ufafanuzi wa Yohana mtume] Yesu anakwenda kwa Yohana Mbatizaji. Yohana Mbatizaji anashuhudia kuwa Yesu ni Mwana Kondoo wa Mungu (Yoh 1:29-34)

B18a. Kwenye mto wa Yordani, Yesu anamwita Petro, Andrea na mtu mwingine (Yoh 1:35-42)

B18b1. Yesu anaamua kurudi Galilaya siku iliyofuata baada ya Yohana Mbatizaji kuongea (Yoh 1:43a)

B18b2. Yesu anamwita Filipo na and Nathanaeli (Yoh 1:43b-51)

B18c. Siku 40 nyikani, shetani anamjaribu Yesu (Mat 4:1-11; Mak 1:12-13; Luk 4:1-13)

Kwenye orodha hii, tukio moja linafanana kwenye injili zote nne, mawili kwenye injili za kisnoptiki (Mathayo, Marko na Luka), matatu kwenye Mathayo na Luka, matano kwenye Mathayo peke yake, matano kwenye Yohana peke yake, kumi kwenye Luka peke yake, na hakuna tukio lililo kwenye Marko peke yake. Marko peke yake amechangia matukio matatu hapa, na yanafanana na Mathayo na Luka. Ni rahisi kusema kuwa kati ya hawa hakuna aliye shuhudia matukio haya wa awali, walizipata habari hizi kutoka kwenye vyanzo mbalimbali, ingawa Luka ana habari nyingi zaidi kabla ya huduma ya Yesu na Marko ana chache zaidi.

 

S: Je ni kweli kuwa habari za maisha ya Yesu kabla ya huduma yake ya wazi ni "chache"?

J: Hapana, kulinganisha na watu wengine mashuhuri wa kale. Maoni haya hayatokani na utafiti wa kitaalamu usio na upendeleo, lakini wa kutokuamini kwa "wakosoaji wa Kikristo." Kuna mambo matano ya kuzingatia katika jibu la swali hili:

1. Jambo la kukumbuka ni kuwa, wakati wa huduma ya wazi ya Yesu kabla ya kifo chake, tumepewa angalau mambo 176 kuhusu maisha na mafundisho yake.

2. Kabla Yesu hajaanza huduma yake, tunajua angalau mambo 37 kuhusu Yesu.

3. Tumepewa habari zaidi kuhusu Yesu kabla ya maisha yake mbele ya watu, kuliko ambavyo wanahistoria wanavyotueleza kuhusu wafalme mashuhuri wa Babeli, Misri, Umedi, Uajemi, Ugiriki, Makedonia, au Roma ya awali. Kwa maneno mengine, tunafahamu kuhusu Yesu, kabla ya kutokea kwake kwa mara ya kwanza mbele za watu, kuliko tunavyojua kuhusu maisha ya utotoni ya Mbabeli Nebukadreza, Wamisri Akhenaten na Nefertiti, Waamedi Kyaxares na Astyges, Waajemi Koreshi, Dario, na Ahasuero, Wagiriki Agamemnon na Pericles, au maseneta wa Kiroma. Mtu pekee ambaye tunafahamu habari nyingi zaidi kabla ya kufahamika na watu wengi ni Alexander wa Makedonia.

4. Tuna habari chache zaidi kuhusu watu mashuhuri kihistoria kwenye karne ya 18 na 19, kabla hawajawa mashuhuri, kuliko tulivyo na habari za jinsi hizo za Yesu.

5. Kama mtu atasema kuwa habari za Yesu kabla ya huduma yake ya wazi ni chache, angalau kulinganisha na watu wengine, atatakiwa ataje watu mashuhuri wa kale ambao kuna habari nyingi zaidi zilizotolewa kuhusu maisha yao kabla ya kuwa mashuhuri, au vinginevyo aache kusema mambo yasiyo sahihi.

Tazama pia swali linalofuata kuona mambo angalau thelathini tunayoambiwa kuhusu Yesu kabla ya kuanza kwake huduma ya wazi.

 

S: Kwenye Mat 2:13-30, kama Yusufu, Mariamu na Yesu walikimbilia Misri, wangewezaja kurudi Nazareti moja kwa moja kwenye Luk 2:39?

J: Luk 2:39 haisemi kuwa familia ya Yesu ilirudi Nazareti mara moja. Inasema tu kuwa walitimiza matakwa ya sheria [Yerusalemu] kabla ya kurudi Nazareti. Inaweza kusemwa kuwa jambo hili lilitokea mara moja kwa sababu hakuna jambo lingine lililoelezwa. Huenda Luka hakuona haja ya kuelezea safari ya kwenda Misri, au huenda Luka hakuifahamu safari hiyo.

Kwa vyovyote vile, taarifa hii ya Luka haitofautiani na injili nyingine. Swali linalofuata lina maelezo ya mpangilio wa injili nne unaofuata mtiririko wa matukio. Herufi kama a, b, c zinawakilisha matukio ambayo yangeweza kutokea kwa mfuatano huo.

 

S: Kabla ya huduma ya wazi ya Yesu, tunaambiwa kitu gani bayana kuhusu Yesu?

J: Tunaambiwa mambo yasiyopungua 37 kuhusu Yesu kabla ya huduma yake. Habari tulizopewa zinaweza kugawanywa kwenye makundi matatu:

Yesu mwenyewe

1. Mama yake alikuwa Mariamu.

2. Alizaliwa na bikira (Hata kama watu wenye kutia shaka wanalikana jambo hili, wanapaswa kukubali kuwa ilidaiwa kuwa Yesu alizaliwa na bikira).

3. Baba yake kisheria alikuwa Yusufu.

4. Alizaliwa wakati wa utawala wa Herode Mkuu (mwaka 37-4 KK).

5. Alizaliwa Bethlehemu.

6. Alitahiriwa siku ya nane.

7. Alipelekwa hekaluni (kama watoto wengi wa Kiyahudi).

8. Familia ya Yesu ilisafiri kwenda Misri (Mat 2:13-15).

9. Baada ya Herode kufa, familia ya Yesu ilirudi Nazareti ya Galilaya (Mat 2:19-23).

10a. Alizaliwa Nazareti (Luk 2:39-51), mji mdogo uliochukuliwa na wengi kutokuwa muhimu.

10b. Baada ya Yesu kwenda hekaluni, alirudi Nazareti tena (Luk 2:51).

11a. Alipokuwa na miaka 12, Yesu alikwenda hekaluni.

11b. Kila mwaka wazazi wa Yesu walikwenda hekaluni wakati wa sikukuu ya Pasaka (Luk 2:41).

12. Alipokuwa na miaka 12, alikuwa mdadisi na aliyajua Maandiko vizuri sana (Luk 2:41-46).

13. Yesu hakuwa na dhambi hata kidogo (Heb 4:15; 2 Kor 5:21). Hata kama watu wenye kushuku hawatakubaliana na usemi huu, mistari hii pamoja na Luk 2:40 inatufahamisha kwa uchache kuwa "Yesu alikuwa mtoto mzuri."

14. Yesu alizungumza Kiaramu (Mat 5:22, n.k.).

15. Kwa ujumla watu toka Galilaya walizungumza Kigiriki pia.

16. Dini ya Yesu ilikuwa Uyahudi; alikuwa karibu sana na Mafarisayo, aliamini vitabu vyote vya Agano la Kale. Waandishi wa kanisa la kale wanasema kuwa ni Masadukayo waliiamini Torati (vitabu vitano vya kwanza vya Biblia).

17. Yesu alifanya kazi ya ufundi seremala (Mak 6:3).

18. Alipofikisha umri wa karibu miaka 30 alibatizwa na Yohana Mbatizaji (Mat 3:13; Mak 1:9-11).

19. Alikwenda nyikani kabla ya kuanza huduma yake ya wazi (Mat 4:1-11; Mak 1:12-13).

Familia ya Yesu

20. Yusufu alikuwa fundi seremala

21. Mariamu alikuwa mjamzito kabla hajaolewa (Mat 1:18).

22. Yusufu alifikiria kumwacha Mariamu (Mat 1:19).

23. Orodha ya ukoo wa Yusufu, iliyochukuliwa kama kitu kimoja tu (Mat 1:1-16).

24. Orodha ya ukoo wa Mariamu, iliyochukuliwa kama kitu kimoja tu.

25. Alikuwa na wadogo zake wane walioitwa Yakobo, Yusufu, Yuda, na Simeoni (Mat 13:55-56; Mak 6:4; Gal 1:19; Yuda 1, Eusebius' Ecclesiastical History (karibu mwaka 360 BK) 2:23 na 3:20).

26. Though of royal ancestry, Jesus grew up in a common family of a subject people, and probably were poor (Luke 2:23 + Leviticus 12:6-8).

27. Binamu wa Mariamu alikuwa Elizabeti, ambaye alikuwa mzao wa kuhani Haruni (Luk 1:5).

28. Mume wa Elizabeti alikuwa ni kuhani Zakaria, wa zamu ya Abiya (Luk 1:5).

29. Yohana Mbatizaji, mzaliwa wa kwanza/mtoto pekee wa Zakaria na Elizabeti, alikuwa ndugu wa Yesu.

30. Mariamu, Yakobo, na Yuda walikuwa bado wanaishi wakati Yesu anasulubiwa.

Maitikio na matarajio ya watu kwa Yesu

31. Matarajio ya Mariamu kwa mtoto wake.

32. Yesu alifikiriwa kutimiza nabii kuhusu Masihi (Mat 2:6).

33. Kuabudiwa na wachungaji (Luk 2:15-20)

34. Zawadi za wafalme (Mat 2:10-11).

35. Itikio la kushuku na kutoamini la Herode Mkuu.

36. Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji.

37. Ana na Simeoni hekaluni. (Mtu anaweza kusema kuwa haya ni mambo mawili tofauti, lakini nitachukua kuwa ni moja).

Mambo haya si machache kulinganisha na jinsi tunavyojua kuhusu maisha ya watu wengine mashuhuri kabla ya kupata umaarufu wao. Kwa ulinganishi zaidi, angalia swali linalofuata.

 

S: Kwa kuwa tunajua mambo yasiopungua 37 kuhusu maisha ya Yesu kabla ya kuanza kwake huduma ya wazi, kwa kulinganisha na jinsi tunavyojua kuhusu maisha ya watu wengine mashuhuri wasiokuwa viongozi wa kidini kabla ya kufanya mambo yaliyowapa umashuhuri?

J: Kuwa ulinganishi, tunafahamu mambo machache sana kuhusu Pompey, karibu mambo 12 kuhusu Aristotle, na mambo 26 kuhusu Alexander wa Makedonia, kabla ya kufanya kwao mambo yaliyowapa umaarufu.

Pompey

    Pompeius Gnaeus alikukwa jenerali mashuhuri wa Kiroma na mwanasiasa aliyezaliwa Septemba 30, 106 KK. Alikuwa mtoto wa kamanda wa kijeshi

3. Alipokuwa na miaka 17, aligombana na baba yake kwenye vita ya kijamii.

4. Kama Waroma wengi walivyo, huenda aliabudu miungu ya Kiroma.

5. Alizungumza Kilatini, na huenda Kigiriki pia

Bila shaka kuna mambo zaidi, lakini kwa hakika hayazidi 20.

Aristotle mwenyewe

1. Alizaliwa karibu mwaka 384 KK.

2. Alizaliwa Stagira, mji wa Kigiriki ulio pwani ya kaskazini magharibi ya Bahari ya Aegean

3. Alizungumza Kigiriki.

4. Watu wengi walikuwa wanaiamini miungu ya Kigiriki.

5. Baba yake alikuwa Nicomachus, daktari wa chama cha ushirika cha watu wenye matakwa yanayofanana cha "watoto wa Aesculapius."

6. Alifundishwa na Plato kwenye shule ya Athens alipokuwa na umri wa kuanzia miaka 17 hadi 37.

7. Mwaka 342 KK, Aristotle alikuwa mwalimu wa Alexander wa Makedonia kwa miaka 7.

8. Kwenye kaburi lililo karibu na Eretria ya Euboea, kuna fuvu na vitu vingine kadhaa ambavyo vinaweza kuwa vya Aristotle. Alikufa karibu mwaka 322 KK.

Familia ya Aristotle

9. Baba yake alikuwa mganga kwenye makazi ya kifalme ya Amyntas II, baba wa Philip wa Makedonia.

10. Orodha ya vizazi vya baba yake: ya mandahari ya Kigiriki ya Kiionia.

11. Orodha ya vizazi ya mama yake: Kiionia kutoka Chalcis ya Euboea.

Maitikio na matarajio kwa Aristotle

12. Walikuwa na matumaini ya kitaaluma kwake, walimtuma kujifunza kwa Plato kwenye shule ilioko Athens.

Tuna maandiko matano tu ya kazi zake, na lililo la kale zaidi ni la mwaka 1100 BK.

Kutoka India hadi Spain, mtu aliyekuwa maarufu sana kabla ya Yesu alikuwa Alexander wa Makedonia, ambaye mara nyingi alikuwa akiitwa Alexander Mkuu. Hebu tuangalie mambo tunayoyajua kuhusu mwanzo wa maisha yake.

Alexander mwenyewe

1. Baba yake alikuwa Philip II wa Makedonia

2. Mama yake alikuwa Olympias, binti wa mfalme wa Molosia kutoka Epirus.

3. Alizaliwa karibu Oktoba mwaka 356 KK

4. Alizaliwa Pella, mji mkuu wa Makedonia

5. Wakati Alexander ametimiza miaka 14 (mwaka 342 KK), Aristotle alikuwa mwalimu wake kwa miaka 7.

6. Alexander alipenda kusoma mashairi ya Homer.

7. Alexander alizungumza lahaja kadhaa za Kigiriki.

8. Alexander aliiamini miungu ya Kigiriki

9. Alexander alikuwa mpanda farasi mzuri, akiwa na farasi mweupe aliyeitwa Beucephalus.

10. Alipokuwa na umri wa miaka 16, Alexander alizimisha uasi wa makabila ya mlimani wakati baba yake alipokuwa hayupo

11. Alexander aliongoza mapambano yaliyolikishinda ‘Kikundi cha Kutukuzwa' (Sacred Band) huko Chaeronea mwaka 338 KK.

12. Baada ya Philip kumwach Olympias, Alexander aliishi na mama yake Epirus.

Familia ya Alexander

13. Orodha ya ukoo vya Olympias. Alikuwa binti wa Mfalme Neoptolemos wa Epirus, na binti wa kaka wa Arybbas, wote wawili walikuwa watoto wa Mfalme Alketus, mfalme wa Kimolosia wa Epirus.

14. Babaye Alexander, Philip II, alikuwa ni mtoto wa tatu wa Amyntas II wa Makedonia. Hata hivyo, hatuna uhakika wa orodha ya ukoo wake zaidi ya hapo.

15. Baba yake mdogo/mkubwa alikuwa Alexander I, mfalme wa Epirus.

16. Hivyo Alexander alilelewa kama mwana wa mfalme.

17. Tuna sanamu na jeneza vya Philip II wa Makedonia (Greek World uk.174-175).

18. Philip alikuwa mtawala mshikiliaji wa Makedonia mwaka 359 KK, lakini alitwaa mamlak ya ufalme mwaka 356 KK.

19. Philip alimwacha Olympias na kumuoa Kleopatra/Cleopatra, mwanamke mlodi wa Makedonia.

20. Alexander I alimuoa binti wa ndugu yake Kleopatra/Cleopatra, dada wa kambo wa Alexander mwaka 337 au 336 KK.

21. Alexander alikuwa na mtoto aliyekuwa kaka/dada wa kambo wa Philip na Cleopatra, ambaye Alexander alimuua mara baada ya kuwa mfalme.

22. Alexander alikuwa na binamu aliyeitwa Amyntas, ambaye Alexander alimuua mara baada ya kuwa mfalme.

23. Mwaka 336 au 336 KK, Philip II aliuawa kwa kisu cha Kiseltiki (miongoni mwa watu wanaozungumza lugha zilizotumika sehemu kubwa ya Ulaya na Asia) asubuhi ya harusi ya binti wake Kleopatra.

24. Alexander alimtumia mama yake mateka mwaka mwaka 335 KK.

Maitikio na matarajio ya Alexander

25. Philip alimuandaa kama mfalme atakayechukua nafasi yake.

26. Urafiki wa Alexander na Philip uliisha pale Philip alipomwacha mama wa Alexander.

Kazi za watu wengi walioandika kuhusu Alexander zimepotea. Kazi zilizopo leo hii ni pamoja na:

"Didot edition of Arrian" cha Karl Muller

Diodorus kitabu cha 17 (karibu mwaka 20 KK)

Quintus Curtius (karibu mwaka 42 BK)

Plutarch (karibu mwaka 45-125 BK) Life of Alexander

Anabasis and Indica cha Arrian (mwaka 150 BK)

Ufupisho wa History of Trogus cha Justin (karibu mwaka 10 KK?)

Itinerarium Alexandri (mwaka 324-361 BK)

Epitome Rerum Gestarum Alexandri Magni (karne ya 4 au 5)

Kwa maelezo zaidi angalia Encyclopedia Britannica, The Greek World, na National Geographic.

Mwandishi wasifu wa kisasa Mary Renault kwenye Nature of Alexander, uk.30 anasema kuhusu wandishi wasifu wa Alexander, "Historia ya Arrian inaanzia wakati wa kuanza ufalme wake [Alexander's], huenda ikawa ni kwa sababu ya mambo ambayo Ptolemy alifanya, ambayo yanasikitisha, kwani ufahamu wake wa miaka ya awali ungekuwa wa maana sana."

Endapo mtu atapenda kudai kuwa mambo tunayoambiwa kuhusu Yesu kabla ya kunza kea huduma yake ya wazi ni "machache", anapaswa kuwa mkweli na aongeze kuwa anafikiri kuwa mambo ambayo tumeambiwa kuhusu maisha ya watu wengi mashuhuri kwenye Himaya ya Roma kabla ya kuwa kuanza kufanya mambo ambayo yamewapa umashuhuri ni machache kuliko yale ya Yesu.

Pia ninaamini kuwa tunafahamu mambo mengi zaidi kuhusu maisha ya Yesu kabla ya kuanza huduma yake ya wazi kuliko tunavyofahami kuhusu Wayahudi wengine mashuhuri wa wakati ule kama Josephus, Philo (mwaka 20 KK hadi 50 BK), na Bar Kochba. Ninaamini pia kuwa tunafahamu mambo mengi zaidi kuhusu Yesu kabla hajatimiza miaka 30 kuliko tunavyojua kuhusu Musa, Buddha, na Muhammad, ingawa bado sijafanya utafiti wa jambo hili. Tunaweza kuwa tuna mandhari kubwa zaidi ya Julius Caesar na Josephus, lakini sifahamu kuhusu watu wengine wote.

Musa

Yafuatayo ni mambo tunayofahamu kuhusu Musa kabla hajaanza huduma ya wazi.

1. Musa alizaliwa karibu mwaka 1525 KK kaskazini kwa Misri.

2. Ama wazazi wake, au mababu na mabibi zake waliitwa Amram na Jochabed.

3. Alikuwa Mwebrania, watu ambao walikuwa utumwani kwa miaka 320.

4. Alikuwa na dada mkubwa aliyeitwa Miriam.

5. Alikuwa na kaka aliyeitwa Haruni.

6. Musa aliishi kwenye nyumba ya baba yake miezi mitatu ye kwanza (Mdo 7:20).

7. Kama mtoto, Farao alipoamuru kuwa watoto wa kiume wa Kiebrania watupwe kwenye Mto Naili, mama yake alimweka kwenye kikapu.

8. Binti wa Farao alimkuta, na kumtunza kama mtoto wake mwenyewe.

9. Alikulia kwenye jumba la Farao, alifundishwa hekima yote ya Wamisri, na akawa hodari wa maneno na matendo (Mdo 7:21-22), na alipata elimu na mafunzo vya Wamisri.

10. Alilelewa na mama yake mwenyewe.

11. Alijishughulisha na mambo ya Waebrania wakati alipomuua Mmisri aliyekuwa anampiga Mwebrania.

12. Hata alipokuwa na miaka 40 Musa alikuwa na nguvu nyingi tu hata akaweza kumuua Mmisri.

13. Farao alijaribu kumuua Musa.

14. Musa alikimbilia Midiani, ambako aliwaona wanawake waliokuwa wanateka maji kwa ajili ya kuinywesha mifugo yao.

15. Wakati wachungaji wanajaribu kuwafukza, Musa aliwaokoa kutoka kwa wachungaji.

16. Musa alimuoa Sipora.

17. Baba mkwe wa Musa aliitwa Reueli, ambaye pia aliitea Yethro.

18. Musa na Sipora walikuwa na mtoto aliyeitwa Gershomu.

19. Musa alikuwa na miaka karibu 80 alipokiona kichaka kilichokuwa kinawaka moto.

Gautama Buddha

Kwa ajili ya majadiliano, tutachukulia kuwa hadithi za kale ambazo ukweli wake haujathibitishwa kuhusu kijana Buddha kuwa ni kweli.

    Mtoto wa kiume wa mfalme wa Sakyas, tabaka la watu mashujaa kutoka kaskazini mwa Kosala Kuna uwezekano mkubwa zaidi kuwa aliabudu sanamu za Kihindu alipokuwa mtoto mdogo.

3. Alijitenga na jamii endapo alimwona mgonjwa, mzee, na maiti.

4. Aliondoka nyumbani kwake alipokuwa na umri wa miaka 29.

5. Aliutafuta ufahamu wa kiroho kwa muda wa miaka 6, ambao anadai aliupata chini ya mti mtini wenye asili ya India na kusini mashariki mwa Asia, ambao Wabudha wanauchukulia kuwa mtakatifu.

6. Alikufa ama mwaka 544 KK au 483 KK alpokuwa na miaka 80.

 

He wondered if they were from Satan, but his wife convinced him they were from God.

 

S: Kwenye Mat 1:18 na Luk 2:7, je kuzaliwa kwa Yesu na bikira hakuendani na kuwepo kwake kabla ya kuzaliwa, kama Rudolph Bultmann na Wolfgang Pannenberg walivyofikiri?

J: Hapana. Jambo hili lilionekana kutokuendana na wanatheolojia walioasi tu ambao wanamwamini Mungu anayetakiwa kukidhi mipaka waliyomwekea. Kristo alikuwepo kabla ya kuzalia, lakini jambo hili halikumzuia kufanya mambo yafuatayo:

1. Kuchagua kwa muda fulani na kwa hiari kutokutumia baadhi ya sifa zake za asili na kuficha sehemu ya utukufu wake.

2. Kuonekana kama kitu chochote alichotaka, ikiwa pamoja na kuwa binadamu.

3. Kuutwaa utu na kuwa mwanadamu

4. Kuja duniani kwa mara ya kwanza kama mtu mzima, mtoto, mtoto mdogo, au mimba, au namna yeyote aliyotaka.

Kwa kweli, kuwepo kwa Yesu kama Mungu mwenye nguvu kabla ya kuzaliwa kwake hakukumzuia kufanya kitu chochote kile. Vizuizi vyote vya Mungu mwenye nguvu ni vile ambavyo ameviweka mwenyewe. Mungu hawezi kudanganya (Ebr 6:18; Tit 1:2), hawezi kujikana mwenyewe (2 Tim 2:13), na hawezi kujaribiwa na uovu (Yak 1:13).

 

S: Je "tangazo" la kwenye Mat 1:18-21 lilitolewa baada ya Mariamu kuwa mjamzito, au kabla kufuatana na Luk 1: 26-31?

J: Yusufu na Mariamu ni watu wawili tofauti. Malaika aliongea na MARIAMU kabla ya bikira kuwa mjamzito (Luk 1:26-31). Malaika aliongea na YUSUFU baada ya Mariamu kuwa mjamzito na Yusufu kuamua kumwacha (Mat 1:18-21).

 

S: Kwenye Mat 1:18 na Luk 2:7, Waebioni waasi ni watu gani, na waliamini nini?

J: Waebioni walikuwa na maoni duni kuhusu Kristo, waliamini kuwa ametoka kwa Mungu Baba, lakini hakuwa Mungu Mwana. Waliamini kuwa Yesu anaweza kuitwa Mungu kwa namna ya heshima, lakini hakuwa na uungu. Waebioni walidai kuwa mila za Kiyahudi zinapaswa kuendelea kufuatwa. Walikana kuzaliwa kwa Yesu na bikira wakisema kuwa baba yake alikuwa Yusufu (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 21, uk.451), na walikubali tu ufupisho wa Injili ya Mathayo (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 10.7, uk.428).

 

S: Kwenye Mat 2:2, 7, 9 nyota iliyoonekana Bethlehemu Yesu alipozaliwa ilikuwa ni nini?

J: Ingawa Maandiko hayasemi waziwazi, huenda ilikuwa ni utukufu wa Mungu (shekinah glory) kwani "nyota" ilikuwa inawaongoza kwenye kijiji maalumu na hata kwenye nyumba maalumu. Tazama Complete Book of Bible Answers, uk.100 kwa maelezo zaidi.

S: Kwenye Mat 2:2, 7 nani mwingine aliyeitaja nyota hii ya mashariki ambayo Mamajusi waliiona?

J: Waandishi kadhaa wa kale wanaitaja:

Ignatius (karibu mwaka 100-117 BK) Letter to the Ephesians sura ya 19, uk.57.

Justin Martyr (karibu mwaka 138-165 BK) Dialogue with Trypho the Jew sura ya 88, uk.237

Irenaeus (mwaka 182-188 BK) Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 9.2, uk.423.

Tertullian (mwaka 198-220 BK) On Idolatry sura ya 9, uk.65.

Hippolytus (mwaka 222-234/5 BK) Refutation of All Heresies kitabu cha 7 sura ya 15, uk.108

Origen (mwaka 225-249 BK) alichukulia hii kuwa nyota mpya, si moja ya vitu vinavyokuwa angani kwenye Origen Against Celsus kitabu cha 1 sura ya 48, uk.422.

Treatise on Rebaptism (karibu mwaka 250-258 BK) sura ya 8, uk.671.

Petro wa Alexandria (mwaka 306, 285-311 BK) Canonical Epistle sura ya 13, uk.277 inawataja Mamajusi, lakini siyo nyota.

 

S: Kwenye Mat 2:11, inaonekana ni sahihi kuamini kuwa Mamajusi waliokwenda kumwabudu Yesu waliufahamu unabii wa Danieli kuhusu Masihi, waliusoma, na kutambua kuwa kuja kwa Masihi kumekaribia. Unafahamu sehemu yeyote kwenye kazi za Wazoroastria au Waajemi wengine (watu wa Mashariki ya Kati), ambayo inataja unabii wa Danieli kuhusu Masihi?

J: Danieli aliwahi kuishi Uajemi, na alikuwa akiongea na watu wenye hekima na wanajimu wa huko. Mamajusi walikuwa wanatoka kwenye kabila la Zoroastria / makuhani wa Kimidiani, sawa na Walawo walivyokuwa makuhani na wahudumu wa hekalu wa Israeli. Sifahamu kazi yeyote ya Kizoroastria, lakini sina uhakika kuwa watu wengi wanafahamu kwani Waislamu wangeharibu nyingi ya kazi hizo kwa kadri ambayo wangeweza. Wazoroastria hawakuwa na ulinzi mkubwa chini ya utawala wa Waislamu hivyo "watu wa Kitabu", yaani Wakristo, Wayahudi, na Wasabi. Kazi za Kiislamu zimewataja Wasabi mara kwa mara, lakini, kwa kadri ninavyojua, hazijaongelea kuja kwa Wazoroastria.

 

S: Kwenye Mat 2:11, kwa nini Mamajusi waliingia nyumba moja hadi nyingine, kwani Yesu alizaliwa kwenye hori la ng'ombe kwa mujibu wa Luk 2:7?

J: Yesu alizaliwa zizini kwa sababu hapakuwa nafasi kwenye nyumba za kulala wageni. Yusufu Mariamu hawakupenda kukaa kwenye zizi muda wowote isipokuwa tu walilazimika. Walihamia kwenye nyumba mara baada ya Mamajusi kuja.

Nyimbo za Krismas za kimagharibi za sasa kwa ujumla zinawaelezea Mamajusi kana kwamba walikuja usiku uleule aliozaliwa Yesu. Ukweli ni kwamba walikuja baadaa ya muda kupita. Makanisa ya Korthodox yanasherehekea Krismas Desemba 25th, lakini kuja kwa Mamajusi katikati ya mwezi Januari.

 

S: Kwenye Luk 2:22-38, je Yesu alipelekwa hekaluni (Yerusalemu), au Yusufu aliipeleka familia yake Misri baada ya Mamajusi kuja kama Mat 2:13-18 inavyosema?

J: Yote ni sahihi.

1. Yesu alipelekwa hekaluni Yerusalemu siku nane baada ya kuzaliwa. Kisha walirudi Bethlehemu na kuelekea Misri. Mara baada ya Mariamu kuwa tayari, walianza safari.

2. Tofauti na hadithi za Krismas za kimagharibi, Mamajusi hawakuja usiku uleule Mariamu alipokuwa na uchungu. Walikuja majuma kadhaa baadaye. Kama jambo la ziada, Wakristo wa Kiorthodox wa mashariki kwa ujumla huwa hawaoi zawadi siku ya Krismas. Wanatoa zawadi katikati ya mwezi Januari muda ambao wanaamini Mamajusi walikwenda kumwona Yesu.

 

S: Kwenye Mat 3:17, je Mungu alisema "Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu . . .", au "Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu . . ." kama Mak 1:11 inavyosema?

J: Inawezekana kuwa vyovyote kati ya hivyo kwa sababu tatu.

1. Waandishi wa injili wamekuwa wanafafanua maneno wanayoyanukuu.

2. Mungu Baba anaweza kuwa alisema maneno haya Kiebrania au Kiaramu, lakini injili ziliandikwa Kigiriki.

3. Papias, mwanafunzi wa Mtume Yohana, aliandika kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa katika lugha ya Kiebrania (Kiaramu?) hapo awali, na huenda nukuu hiyo hapo juu ilifafanuliwa wakati injili ilipokuwa inatafsiriwa kwenye Kigiriki.

 

S: Kwenye Mat 4:1 na Mak 1:12, je Yesu aliongozwa kwenda nyikani kujaribiwa mara baada ya kubatizwa, au alichukua muda kiasi kama Yoh 1:29, 35, 43 inavyosema na kisha kwenda Kana ya Galilaya kama Yoh 2:1 inavyodokezea?

J: Ingawa Yesu alikwenda Galilaya muda kiasi baada ya majaribu kwisha, Mat 4:11-12; Mak 1:13-14 na Luk 4:13-14 haisemi Yesu alikwenda wapi mara baada ya siku 40 kuisha. Hivyo, kuna mambo mawili tofauti yanayoweza kuwa yalitokea.

Ubatizo kisha siku 40 Galilaya: Inawezekana Yohana alimbatiza Yesu siku iliyoelezewa kwenye Yoh 1:29-34. Kisha Yesu alikaa siku moja zaidi (Yoh 1:35), na siku iliyofuata aliamua kundoka Galilaya (Yoh 1:43).

Harusi ya Kana ilifanyika baadaye sana, ama kwenye siku ya tatu ya juma au siku ya tatu baada ya kufika Galilaya. Isingeweza kuwa siku moja baada ya Yoh 1:43 (ambayo ilikuwa baada ya Yoh 1:35), kwa sababu ingekuwa siku nne, siyo tatu.

Mat 4:1 inasema tu kuwa Yesu alikwenda nyikani baada ya kubaizwa. Mak 1:12 inasema kuwa Yesu alikwenda nyikani "mara", lakini jambo hilo lingeweza kumaanisha siku chache baadaye.

Ubatizo kisha siku 40 kisha alikwenda kwa Yohana: Yohana 1 haisemi siku ambayo Yesu alibatizwa. Yesu angeweza kubatizwa na Yohana siku 40 hivi kabla ya Yoh 1:19. Baada ya majaribu ya Yesu, alirudi kwa Yohana kwenye Yoh 1:29.

 

S: Kwenye Mat 4:1-11, je mfuatano wa majaribu ya Yesu ulikuwa mkate, majivuno, na mamlaka, au ulikuwa mkate, mamlaka, na majivuno kama ilivyo kwenye Luk 4:1-12?

J: Kuna majibu mawili, na yote yanaweza kuwa sahihi.

1. Luka anatumia neno "na", ambalo halimaanisha kuwa anaonyesha mfuatano wa matukio haya.

2. Pia, katika siku arobaini Yesu alijaribiwa, na majaribu haya na mengineyo yawezekana yalitolewa mara kadhaa na kwa mfuatano tofauti.

 

S: Kwenye Mat 4:1-11; Mak 1:13; na Luk 4:1-13, tunwezaje kudhania kuwa "Mungu" anajaribiwa na mwovu, kama Ahmad Deedat anavyosema?

J: Shetani anaweza kujaribu kufanya kitu chochote kile, lakini kwa kuwa shetani alimjaribu Yesu, matendo ya shetani hayamfanyi Yesu awe asiwe Yesu kwa kiasi chochote kile.

Yesu alikuwa Mungu mkamilifu, lakini pia alikuwa mwanadamu mkamilifu. Ikiwa Yesu kama Mungu alitokea kama aina fulani ya zimwi basi asingeweza kujaribiwa. Lakini kwa sababu Yesu alikuwa mwanadamu mkamilifu, na kama kafara ya kuondoa dhambi za wanadamu, alipitia mambo yote ambayo wanadamu wanayapitia.

S: Kwenye Mat 4:1-11 na Luk 4:1-13, majaribu ya shetani kwa Yesu yanafananaje na majaribu ya shetani kwa Hawa kwenye Mwa 3:6?

J: Ingawa hayafanani, shetani hutumia mbinu zinazofanana mara kwa mara, na hii inaweza kuwa ni kwa sababu zinaleta mafanikio kwake.

Hawa aliuona mti uliozuiliwa kuwa

1. Unafaa kwa chakula [hamu ya kula],

2. Unapendeza macho [uzuri, urembo, tamaa ya macho],

3. Unatamanika kwa maarifa [macho yatafunguliwa, na kuwa kama Mungu, kujua mema na mabaya, nguvu kama ya kiungu ya kufuata amri za shetani].

Yesu, ambaye alikuwa anafunga, alijaribiwa na

1. Mawe yafanyike mkate [hamu ya chakula],

2. Kujiangusha kutoka kwenye kinara cha hekalu [kujionyesha],

3. Mamlaka juu ya falme zote za dunia [nguvu kama za kiungu iliyo chini ya mamlaka ya shetani].

1 Yoh 2:16 inataja aina tatu za dhambi duniani, nazo ni tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima.

 

S: Mwanazuoni mwenye kushuku Bart Ehrman ameandika, "Kwenye Mathayo, Yesu alikataa kufanya miujiza ili kuonyesha yeye ni nani; kwenye Yohana, hili ndilo lengo pekee la yeye kufanya miujiza" (Jesus, Interrupted, uk.103). Kwenye Mathayo, kwenye jaribu la pili na mahali pengine, Yesu hakufanya ishara yeyote kuthibitisha asili yake (Jesus, Interrupted, uk.84).

J: Ehrman anafananisha kutokutii maneno ya shetani au Mafarisayo wenye kushuku na kufanya ishara kwa watu wanaotafuta majibu, au msaada. Yesu alisema sababu ya kutokujirusha ilikuwa kwamba mtu yeyote asije akamtia Mungu majaribuni kwenye Mat 4:7. Yesu "hakulazimika" kufanya ishara hata moja kwa mtu yeyote; na hakuwahi kufanya ishara kwa watu wenye kushuku walidhani kuwa analazimika kufanya hivyo. Badala yake, Yesu alifanya sihara kwa hisani kwa watu waliokuwa na imani ili aimarishe imani zao.

 

S: Kwenye Mat 4:12 na Mak 1:14, baada ya majaribu ya Yesu, je Yohana aliwekwa gerezani kabla ya huduma ya Yesu Nazareti na Kapernaumu, au baada aya Yesu kurudi Galilaya kwenye Yoh 1:43?

J: Biblia inasema mambo yafuatayo:

Yoh 1:43 inasema kuwa Yesu aliamua kurudi Galilaya (si kwamba alirudi siku ileile) siku ambayo Yohana Mbatizaji alisema tena kuwa Yesu ni Mwana Kindoo wa Mungu. Yohana Mbatizaji alikuwa bado hajawekwa gerezani.

Mat 4:12 inasema kuwa wakati Yesu aliposikia kuwa Yohana amewekwa gerezani, alirudi Galilaya.

Mak 1:14 inasema kuwa baada ya Yohana kuwekwa gerezani, Yesu alikwenda Galilaya.

Mfuatano wa matukio:

1. Yohana alisema tena kuwa Yesu ni Mwana Kondoo wa Mungu.

2. Siku iliyofuatia Yesu aliamua kuwa (muda wowote ujao) atarudi Galilaya.

3. Ama kabla ya Yesu kuondoka Galilaya, au vinginevyo baada ya kuondoka lakini kabla ya kufika Galilaya, Yohana aliwekwa gerezani.

4. Yesu alikwenda Galilaya.

 

S: Kwenye Mak 1:12-13, je Yesu alikwenda nyikani kwa siku 40 baada ya kubatizwa, au alikwenda Kana kwenye sherehe ya harusi siku ya tatu kama Yoh 2:1 inavyosema?

J: Vyote. "Siku ya tatu" ilikuwa ni siku ya tatu baada ya kurudi Galilaya, siyo siku ya tatu baada ya kubatizwa. Jibu tofauti ni kuwa "siku ya tatu" likuwa siku ya tatu ya juma.

Expositor's Bible Commentary juzuu ya 9, uk.42 inasema kuwa siku ya tatu inaweza kuwa siku ya tatu kuanzia alipoondoka kwa Yohana Mbatizaji. Ingawa Biblia inasema "siku ya tatu" kwenye Yoh 1:29-35,43 inaweza ikawa inamaanisha siku hiyohiyo. Hata hivyo haielekei kuwa hii ndio maana. Maana ingeeleweka zaidi kama usemi "siku pili yake" usingekuwa umetumika mara nyingi.

 

S: Kwenye Luk 3:22 wakati Yesu anabatizwa, je sauti ilipaswa kusema "Wewe ndiwe Mwanagu, leo nimekuzaa", [inadaiwa] kwa mujibu wa Justin Martyr, [inadaiwa] Clement wa Alexandria, [inadaiwa] Augustine, na wengineo, au "Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu, nimependezwa nawe." (Hii ni nusu ya kwanza ya pingamizi ambalo Muislamu mmoja alilileta).

J: Kwanza natuangalie maana ya madai ya Muislamu huyu, pili tutumie kigezo hicho hicho kwenye Uislamu, tatu undani wa tofauti wa maandishi haya, na mwisho tutumie matokeo ya utafiti huu kwenye Ukristo kwa jumla.

A. Maana ya madai ya Muislamu huyu

Hebu tuchukulie kwa muda kuwa Muislamu huyu yuko sahihi kabisa. Mstari huu ulisema kama ambavyo Muislamu huyu anasema. Kwa upande mwingine, hebu fikiri kuwa tunaweza kuwa na uhakika na uhakika na maneno yale tu yaliyokuwa yameandikwa kwenye matoleo yote mawili: "WEWE NDIWE MWANANGU." Hongera: Kama ni kweli kuwa Mungu alisema hivyo, kwa mtu yeyote yule, maneno ya Muislamu huyu yanauthibitisha Uislamu kuwa hauko sahihi na kuonyesha kuwa Kurani inasema uongo kuhusu Mungu. Kurani inasema si sahihi kusema kuwa Mungu ni Baba, au kuwa Mungu ana watoto (Sura 2:116; 4:171; 5:116,117; 6:100, n.k.). Kama ni kweli kuwa Mungu alimwita Yesu "Mwana wangu", basi Kurani inasema uongo kuhusu Mungu. (Nachukulia kuwa Muislamu anayeuliza swali hili ni Muislamu wa kweli, ingawa naweza nisiwe sahihi kwa kufikiri hivi).

B. Tumia kigeso hicho hicho kwenye Uislamu

Tofauti hii ya maandishi haibadilishi mafundisho yeyote ya Kikristo, kwani maneno haya yote yako kwenye sehemu nyingine pia za Biblia. Dhana ya Biblia kutokuwa na makosa inamaanisha kuwa Biblia haikuwa na makosa yeyote kwenye hati ya awali kabisa yenye maandiko, tofauti za maandiko ziliingia, lakini hakuna ambazo zinazobadilisha mambo ya msingi ya imani au matendo. Tofauti na hilo, Waislamu wengi wanaamini kuwa Kurani ya leo ni nakala hasa ya Kurani ya awali ya duniani, iliyokuwa ni nakala halisi ya mbao za mbinguni (Sura 85:20-22). Hata hivyo, Kurani imethibitishwa kuwa imefanyiwa mabadiliko pia. Watu wanaoongea Kigiriki wasiokuwa Waisraeli walikuwa kilomita 48 (maili 30) kutokea hapo.

a) Sahih Muslim 2:2286, uk.500, 501 inaitaja sura ya Kurani iliyopotea. Ina nukuu kubwa ya sura hii, na kwa uhakika, haipo kwenye Kurani ya leo.

b) Toleo mojawapo la kale la Kurani (‘Ubai) ambalo lilinusurika na kusanifisha kwa ‘Uthman halikuwa na sura za kwanza na mwisho. (Si kwamba zilichanwa bali hazikuwahi kuwepo). Kwa sasa, toleo hili lipo kwenye makumbusho ya Al-Azhar Kairo Misri.

c) Abu Yunus mtumwa wa ‘Aisha aliyeachwa huru alimwaandikia ‘Aisha nakala ya Kurani. Ilikuwa tofauti kidogo kwenye Sura 2:208. "Abu Yunus, mtumwa wa ‘A'isha aliyeachwa huru alisema: ‘A'isha (Mungu awe naye) alimiamuru nimwandikie nakala ya Kurani na kusema: Utakapofika mstari huu: ‘Linda maombi na ombi la katikati' (2:28) nifahamishe; hivyo nilipoufikia mstari huo, nilimfahamisha na akaniambia niandike namna hii: Linda maombi na maombi ya katikati na maombi ya mchana, na simama kwa utiifu wa kweli mbele ya Mungu. ‘A'isha (Mungu awe naye) alisema: Hivi ndivyo nilivyosikia kutoka kwa Mjumbe wa Mungu (amani na baraka za Mungu ziwe juu yake)" Sunan Nasa'i juzuu ya 1 na.475, uk.340.

d) "Kisha Mungu alitufunulia mstari uliokuwa miongoni mwa ile iliyokuwa imefutwa baadaye" (Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 27 na.416, uk.288).

"Alisimulia Anas bin Malik: . . . Ilifunuliwa kuhusu watu waliouawa Bi'r-Ma'una aya ya Kurani tuliyozoea kuinukuu, lakini ilifutwa baadaye. Aya ilikuwa: ‘Wafahamishe watu wetu kuwa tumekutana na Bwana wetu. Amefurahishwa nasi na ametufurahisha sisi pia'" (Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 sura ya 19 na.69, uk.53. Tazama pia History of al-Tabari juzuu ya 7, uk.156).

Kazi nyingine zenye kuelezea aya zilizoondolewa ni: Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 sura ya 9 na.57, uk.45; Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 sura ya 184 na.299, uk.191; Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 27, uk.416, 288, na Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 sura ya 27 na.421, uk.293 zote zinarudia kitu hicho hicho kuhusu mstari huo.

e) Bukhari Hadiths sehemu ya misemo ya Kurani inayokosekana au imeondolewa ni juzuu ya 4 kitabu cha 51 sura ya 12 na.62, uk.48-49; juzuu ya 4 kitabu cha 51 sura ya19 na.69, uk.53; juzuu ya 6 kitabu cha 61 sura ya 3 na.510, uk.489-480; juzuu ya 6 kitabu cha 61 sura ya 4 na.511, uk.480.

f) Sehemu nyingine chache zenye maandishi tofauti (si voweli moja tu) ni:

Sura 11:46 Abu Dawud juzuu ya 3 maelezo chini ya ukurasa 3383, uk.1116.

Sura 11:46 Abu Dawud juzuu ya 3 maelezo chini ya ukurasa 3383, uk.1116.

Sura 18:76 Abu Dawud juzuu ya 3 maelezo chini ya ukurasa 3384, uk.1116.

Sura 18:86 Abu Dawud juzuu ya 3 maelezo chini ya ukurasa 3385, uk.1116.

Sura 24:35 Abu Dawud juzuu ya 3 maelezo chini ya ukurasa 3387, uk.1116.

Sura 34:23 kwa sababu ya voweli, lakini kwenye sehemu nyingine konsonanti, Abu Dawud juzuu ya 3 maelezo chini ya ukurasa 3392, uk.1117.

Sura 39:59. Hii inanukuu huku ikitumia pronauni ya kike kwenye neno nafsi, wakati maandishi mengine yanayofahamika sana yanatumia pronauni ya kiume, Abu Dawud 3:3979 maelezo chini ya ukurasa 3393, uk.1117.

Sura 89:86 Abu Dawud juzuu ya 3 maelezo chini ya ukurasa 3399, uk.1118.

Sura 89:25-26 Abu Dawud juzuu ya 3 maelezo chini ya ukurasa 3408, uk.1119.

Sura 12:23 Abu Dawud juzuu ya 3 maelezo chini ya ukurasa 3411, uk.1120.

Sura 2:58 Abu Dawud juzuu ya 3 maelezo chini ya ukurasa 3413, uk.1121.

Sura 24:1 (haina au imezidisha "r" Faradnaha (na tuliloamuru) dhidi ya wengi wa farradnaha (tuliloelezea kwa undani), Abu Dawud juzuu ya 3 maelezo chini ya ukurasa 3414, uk.1121.

g) Uhalalishaji wa mabadiliko wakati wa uhai wa Muhammadi: Shetani hurushia vitu kwenye maneno ya nabii kwa mujibu wa Sura 22:52, lakini Mungu huyaondoa. Haya yanaweza kuwa maelezo ya sababu ya vyanzo vinne tofauti vya kihistoria vya Kiislamu vinasema kuwa Sura 53:19-20 mwanzoni ilisema maombezi (msaada) wa sanamu nne za mungu mke zilitakiwa kutumainiwa.

Je Muislamu huyu anayeuliza swali angeweza kuridhika kuhusu Biblia endapo Wakristo wangeharibu ushahidi na kuchoma hati zote za kale zenye maandiko isipokuwa moja toleo moja ambalo wanalipenda? Kwa upande mmoja usingefikiri hivyo, lakini hivyo ndivyo ‘Uthman alivyofanya alipowaamuru watu walete nakala zao za Kurani ili ziharibiwe, na alitoa nakala nyingine. Hata hivyo, Kurani leo hii hazifanani na maandishi ya ‘Uthman's. Kwa mfano, tofauti ya maandishi: Sura 6:160a (6:159a kwenye Yusuf ‘Ali): ". . . madhehebu, mimi si miongoni mwao kwa namna yeyote ile" (wakati wa uhai wa ‘Uthman) dhidi ya ". . . madhehebu, huna sehemu nayo" (al-Tabari juzuu ya 15, uk.181 na maelezo chini ya ukurasa 323).

C. Maelezo ya tofauti ya maandishi

"Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe" (p4 [ya karne ya 3], Sinaiticus, Vaticanus, Alexandrinus, Lekshenare ya Kibezantini, baadhi ya hati zenye maandishi ya kale za Kilatini, Kimisri cha Kisahidi, Kiethiopia, Kijojia [Georgian], na Augustine]. Augustine alikuwa na maandishi ya kwanza kwa muibu wa Aland na wenzake (toleo lililorekebishwa la 4), hivyo Muislamu anayeuliza swali hakuwa sahihi kumweka Augustine kwenye kundi la pili.

"Wewe ndiwe Mwanangu, leo hii nimekuzaa" (Bezae Cantabrigiensis, baadhi ya hati zenye maandishi ya kale za Kilatini, Justin Martyr Dialogue with Trypho sura ya 88, uk.244 [iliyoandikwa karibu mwaka 138-165 BK); Hilary, apokrifa ya Methodius Gospel of Nicodemus [muundo wa Kigiriki kutoka sura ya 2; kazi ya Kiapokrifa Infancy Narrative 54).

"Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa, leo hii nimekuzaa" (Clement wa Alexandria mwaka 193-217/220 BK). Maneno haya yanafanana na maandishi ya pili, isipokuwa kisifa "mpendwa" cha kwenye maandishi ya kwanza. Hivyo, Muislamu mwenye kuuliza swali hakuwa sahihi kumweka Clement wa Alexandria kwenye kundu la pili.

D. Matumizi yake kwenye Ukristo kwa ujumla

Yawezekana Justin alikuwa ananukuu kutoka kwenye kumbukumbu, na hata watu wazuri wanaweza kufanya makosa madogo katiak kukumbuka vitu. Hatuamini kuwa ujumbe wa Mungu ni voweli na konsonati za Bibla, lakini ujumbe wa Biblia, na ujumbe ni ule ule, hata kama utachagua maandishi ya pili, kwani mistari mingine inasema kwamba a) Yesu alipendwa, na b) leo hii nimekuzaa (Zaburi 2). Kitu ambacho kinaweza kuwa kosa la bahati mbaya, kumbukumbu isiyo sahihi, hakimaanishi kuwa ni kughushi, yaani, isipokuwa A'isha mke wa Mtume Muhammadi akiwa na maandishi ya aya ya Kurani yenye maana tofauti inaonyesha kuwa alikuwa anaghushi pia.

 

S: Kwenye Luk 3:22, je tofauti hii ya maandishi inaonyesha kuwa palikuwa na mtu aliyekuwa anaghushi, na mstari wa Biblia ulibadilishwa kuondoa neno kuwa Yesu alifanyika Mwana wa Mungu wakati wa kubatizwa kwake dhidi ya kuzaliwa au kabla ya hapo? (Hii ni nusu ya pili ya pingamizi la Kiislamu).

J: Sivyo hivyo kabisa. Ingawa hatufahamu undani wote, kuna mambo manne yanayowezekana, kila moja ya hayo linatoa jibu lenye kuridhisha.

Maelezo ya aina nyingi: Mungu Baba anaweza kuwa alitoa maelezo ya namna nyingi. Kwa nini Mungu Baba awekewe kikomo cha kumwita Yesu Mwana wake mara moja tu hapa?

Maelezo ya jumla yaliyotolewa mara moja: Mungu Baba anaweza kuwa alisema sentensi moja tu, na ilikuwa kama hii: "Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe; leo hii nimekuzaa." Kila mmoja alinukuu kwa usahihi sehemu ya sentensi hii.

Justin Martyr alikosea katika kukumbuka: Justin Martyr, huenda alikosea wakati akinukuu usemi huu kutoka kwenye kumbukumbu ya kichwani, na waandishi waliofuata waliomsoma Justin Martyr na kazi za waandishi waliowatangulia waliomsoma Justin Martyr, walinakiri makosa yake.

Tofauti ya maandishi ya Biblia: Waandishi wengine waliomtangulia Justin Martyr walinaakiri usemi huu kimakosa, na Justin alifuata kwa usahihi maandishi yaliyo kuwemo kwenye Biblia.

Kwa Waislamu wengi, kama mabadiliko yeyote ya Kurani, hata yale yasiyokuwa ya kitheolojia, yanamaanisha kughushi, basi nakala zote za Kurani leo hii zinatakiwa zichomwe moto kwa sababu zimeghushiwa pia. Kurani ina mabadiliko kutoka toleo la ‘Uthman (Sura 159a (au 160a) ni mfano mmoja tu. Na maandishi ya ‘Uthman yaliyosanifiwa ni tofauti na maandishi ya ‘Ubai, na yote haya hayana sura iliyopotea. Kwa kweli, Kurani inakiri kuwa shetani (japo kwa muda) hutupia kiasi kidogo cha mafundisho yake kwenye maneno ya manabii pia (Sura 22:52). Kama mfano wa jambo hili, fikiria maandishi ya awali ya Sura 53:19-20.

 

S: Kwenye Luk 3:23, Yesu alikuwa na umri gani alipoanza huduma yake?

J: Luk 3:23 inasema "kama miaka thelathini" umri unaoweza kuwa miaka 25 hadi 35. Yesu alizaliwa wakati wa utawala wa Herode Mkuu, aliyekufa mwaka 4 KK, na Yesu alianza huduma yake baada ya Yohana Mbatizaji kuanza ya kwake. Yohana alianza huduma yake mwaka wa 15 wa utawala wa Kaisari Tiberius, ambao ulikuwa mwaka 28 BK. Hivyo, kama tarehe za elimukale ni sahihi kiasi cha kutosha, Yesu alikuwa na umri wa miaka kama 33 hadi 35. Pia, Pontio Pilato alikuwa gavana wa Uyahudi kuanzia mwaka 26 hadi 36/37 BK, hivyo Yesu atakuwa alisulubiwa kabla ya muda huo. Kisio zuri zaidi tulilonalo ni kuwa Yesu alianza huduma yake karibu mwaka 30 BK na yaelekea alikufa April 3, 33 BK.

 

S: Kwenye Mat 4:12-13, Simoni na Andrea waliwezaje kuwa wanafunzi wakati Yesu alikuwa na Yohana Mbatizaji, kwani Yesu aliwaambia wamfuate Galilaya kama inavyoonyesha kwenye Mat 4:18-20, Mak 1:16-20, na Luk 5:1-11?

J: Kwanza, walikuwa "wanafunzi" wakti Yesu alikuwa na Yohana Mbatizaji. Baadaye ndipo walipokuwa wanafunzi maalumu, na kisha wakateuliwa kuwa mitume, huko Galilaya. Kumbuka kuwa Yesu alikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi, baadhi yao walimwacha kwenye Yoh 6:66. Zaidi ya hao, alikuwa na wanafunzi aliokuwa amewachagua, jumla ni 72, kwenye Luk 10:1. Mwishoni, Yesu alikuwa na thenashara, ambao walikuja kuwa mitume, kwenye Mat 6:7 na Yoh 6:67.

 

S: Kwenye Yoh 1:35-37, je Andrea na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu siku moja baada ya kubatizwa kwake, au walingojea siku 40 baada ya Yesu kujaribiwa?

J: -Baada. Yesu alibatizwa na Yohana (Mat 3:13-17; Mak 1:9-11; Luk 3:21-23), alijaribiwa kwa siku 40 (Mat 4:1-11; Mak 1:12-13; Luk 4:1-12) alirudi kwa Yohana (Yoh 1:29-32).

 

S: Je tunaweza kujua mfuatano wa matukio kwenye huduma ya Yesu?

J: Tunaweza kujua mfuatano wa baadhi ya matukio tu. Hata hivyo, watu wengi wanaweza kuchanganyikiwa sana kuhusu mfuatano wa matukio ya kwenye injili kwa sababu ya mambo matatu yanayo chukuliwa kimakosa, ambayo yanahitaji kufafanuliwa.

Si kila tukio lililotokea wakati wa huduma ya Yesu liliandikwa na waandishi wa injili; hata hivyo, waandishi hawa hawajawahi kudai kufanya hivyo. Kwa mfano, Yohana, ambaye awali alikuwa mwanafunzi wa Yohana Mbatizaji, anafahamika kutokuandika kitu chochote kuhusiana na kipindi kuanzia kubatizwa kwa Yesu na yeye kujiunga na Yesu. Yoh 21:25 anasema bayana kuwa Yesu alifanya mambo mengine mengi ambayo hayakuandikwa. Injili ya Yohana iliandikwa baada ya injili nyingine, na Yohana anaelekea kusistizia sehemu ambazo wainjilisti wengine hawakuzitaja.

Marudio: Fikiria Yesu anasafiri kwenda kwenye miji mingi aliyotembelea Galilaya, Uyahudi, na Dekapoli, na asirudie hata amri au mfano mmoja, na aongee kitu tofauti kabisa kwenye kila mji aliotembelea ¾ jambo hili si rahisi kutokea! Yaelekea kuwa Yesu aliongea mifano hii mara nyingi zaidi kuliko ilivyorekodiwa kwenye kila injili, na watu waliongea kuhusu Yesu mara nyingi zaidi ya ilivyo rekodiwa. Hivyo, kwa mfano, ni jambo ambalo halijapatiwa ufumbuzi endapo Hotuba ya Mlimani kwenye Mathayo, na Hotuba ya kwenye eneo tambarare kwenye Luka, yalikuwa matukio mawili tofauti ambamo alirudia baadhi ya mafundisho, au tukio moja, ambalo Yesu aliongea kutoka kwenye sehemu tambarare ya nchi iliyoinuka.

Hayaonyeshi mfuatano wa matukio: Waandishi wa injili hawakuandika matukio yote kwa kufuata mtiririko wa kutokea kwayo, lakini pia hawajawahi kusema kuwa wameyarekodi kwa kufuata mtiririko wa kutokea kwake. Ukweli ni kwamba, Papias, mwanafunzi wa Mtume Yohana, anasema bayana kuwa Marko hakuandika matukio kwa kufuata mpangilio wowote ule.

Katika muda wa jumla wa kila kipindi cha huduma ya Yesu, waandishi wa injili hawajawahi kudai kitu kuwa kuna kitu chochote kilichofuata mpangilio, isipokuwa sehemu zifuatazo, ambazo maneno "baada", "siku iliyofuata", n.k. yametumika. Kwenye maswali kuhusu mpangilio wa injili nne unaofuata mtiririko wa kutokea kwa matukio, tazama maneno yenye wino mzito ambayo yanaonyesha viashiria muda, mfuatano wa matukio, na mahali.

 

S: Kwenye injili, je ni mpangilio upi wa injili nne unaonyesha mfuatano wa matukio ya mwanzo wa huduma ya Yesu?

J: Mwanzo wa huduma unahusisha matukio yaliyotokea hadi kifo cha Yohana Mbatizaji. Kabla ya kutoa mpangilio mwingine wa matukio, ni vema kujifunza jiografia kidogo.

Jiografia: Bahari ya Galilaya, Bahari ya Tiberia, ni ziwa hilohilo la maji baridi. Galilaya iko magharibi mwa Bahari ya Galilaya, na Dekapoli iko kusini mashariki mwa Bahari ya Galilaya. Bethsaida pembeni mwa Bahari ya Galilaya kwenye upande waa kaskazini, na upande wake wa magharibi ni Kapernaumu ukingoni mwa bahari, huku Korazini ikiwa kaskazini mwa Kapernaumu. Magdala iko ukingoni magharibi mwa Bahari ya Galilaya, na Kana iko upande wake wa magharibi. Naini iko upande wa kusini magharibi mwa Bahari ya Galilaya karibu kilomita 16 (maili 10) kutoka ufukoni. Nchi ya Wagerasi au Wagenesareti, au Wagadarene inaweza kuwa inawakilisha sehemu moja au sehemu zilizokuwa zimekaribiana mashariki na kusini mashariki mwa Bahari ya Galilaya. Gerasa ilikuwa kilomita 48 (maili 30) kusini mashariki mwa Bahari ya Galilaya na ardhi yake haikufika baharini. Gadara ilikuwa kilomita 8 (maili 5) kusini mashariki mwa Bahari ya Galilaya na ardhi yake ilifika baharini, kama ilivyothibitishwa na Josephus aliyeeleza jambo hili na sarafu ya Gadara inayoonyesha meli.

Mpangilio: ni muhimu kutofautisha kati ya mambo yanayosemwa kuwa mpangilio na mambo ambayo yamo kwenye mpangilio. Kwani matukio haya 65, tarakumu zinawakilisha matukio ambayo yanatakiwa kufuata namba zilizotanagulia kwenye mpangilio. Harufi kama a, b, c zinawakilisha matukio yanayoweza kuwa yanafuata mpangilio, lakini yangeweza kutokea kwa mfuatano wowote ule. Maneno yaliyoandikwa kwa wino mzito yanaonyesha vielelezi vya muda, mpangilio, na mahali. Aya zilizopigiwa mistari inaonyesha vifungu ambavyo huenda havikupangiliwa kama matukio yalivyotokea kwenye injili.

Huduma yaa mwanzo: Mat 4:12-14:12, Mak 1:14-6:29, Luk 3:19-20; 4:14-9:9, Yoh 1:43-5:47

E1a1. Kana kwenye siku ya tatu (siku ya tatu baada ya kurudi Galilaya, baada ya Yohana kuongea, au siku ya tatu ya juma?), Yesu anayabadili maji kuwa mvinyo. Muujiza wa kwanza kufanyika Galilaya, ingawa muda wake ulikuwa bado kutimia (Yoh 2:1-11).

E1a2a. Wakati wa sherehe ya Pasaka (siku ya 14 ya mwezi wa kwanza) akiwa Yerusalem, Yesu anawafukuza watu wanaobadilisha hela (Yoh 2:12-25).

E1a2b. Yesu anamfundisha Nikodemu kuhusu kuzaliwa upya (Yoh 3:1-21).

E1a3. Katika vijiji vya Uyahudi, Yohana anamshuhudia Yesu (Yoh 3:23-35).

E1a4a. Sikari ya Samaria, njiani kuelekea Galilaya, Yesu anaongea na mwanamke Msamaria (Yoh 4:1-42).

E1b1. Yohana anamkaripia Mfalme Herode (Mat 14:3; Luk 3:19-20).

E1b2a. Baada ya Yesu kusikia kuwa Yohana Mbatizaji amewekwa gerezani, Yesu anarudi Galilaya na anaanza kuhubiri "Ufalme wa Mungu umekaribia" (Mat 4:12-17, Mak 1:14-15; Yoh 4:43-45).

E1b2b. Kutoka Kana Yesu anamponya mtoto wa diwani Kapernaumu kama muujiza wake wa pili (Yoh 4:46-54).

E1b2c1. Galilaya na Nazareti, Yesu anasoma gombo (Luk 4:14-15).

E1b2c2. Yesu anaelezea unabii, na Wayahudi wanajaribuu kumuua (Luk 4:16-31).

E1b2d1. Kando mwa Bahari ya Galilaya, Yesu anawaita Simoni Petro, Andrea (Mat 4:18-20; Mak 1:16-18; Luk 5:1-10).

E1b2d2. Kapernaumu Yesu anafukuza mapepo (Mak 1:21-28; Luk 4:31-37).

E1b2e. Kuitwa kwa Yakobo na Yohana (Mat 4:21-22; Mak 1:19-20; Luk 5:6-11).

E1b2f. Galilaya, Yesu anaponya wagonjwa (Mat 4:23-25; Luk 4:40-44).

E2a. Hotuba ya Mlimani, ikiwa ni pamoja na Sala ya Bwana (Mat 5:1-7:29).

E2b. Jioni, anamponya mama mkwe wa Simoni na watu wengine (Mat 8:14-17; Mak 1:29-34; Luk 4:38-39).

E2c. Yesu anaomba peke yake (Mak 1:35-38; Luk 4:42-44).

E2d. Safari ya kupitia Galilaya (Mak 1:39).

E2e. Anamponya mtu mwenye ukoma ambaye alikuwa msengenyaji (Mat 8:1-4; Mak 1:40-45; Luk 5:12-15).

E2f. Faraghani, mara kwa mara Yesu alijitenga faraghani ili kuomba (Luk 5:16).

E2g1. Kapernaumu Yesu amponya mtu aliyekuwa amepooza (Mak 2:1-12; Luk 5:17-26).

E2g2. Kuitwa kwa Mathayo/Lawi (Mat 9:9-13; Mak 2:13-17; Luk 5:27-32).

E3c1. Galilaya ufukoni mwa bahari, gharama ya kumfuata Yesu (Mat 8:18-22).

E3c2. Nazareti Yesu amponya mtu aliyepooza (Mat 9:1-8).

E3c3. Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wauliza kuhusu kufunga (Mat 9:14-17; Mak 2:18-22; Luk 5:33-39).

E2h1. Kwenye siku moja ya Sabato, Yesu apita kwenye mashamba; atumia tukio la Daudi kujibu shutuma dhidi yake (Mat 12:1-8; Mak 2:23-27; Luk 6:1-11).

E2h2. Kwenye sinagogi, Yesu amponya mtu mwenye mkono uliopooza (Mat 12:9-14; Mak 3:1-6; Luk 6:6-11).

E2h3. Makutano wamfuata Yesu (Mak 3:7-12).

E2i1. Pembeni mwa mlima, Yesu aomba kwa Mungu usiku kucha (Luk 6:12).

E2i2. Yesu anawachagua wanafunzi 12 (Mak 3:13-19; Luk 6:13-16).

E2j1. Hotuba ya sehemu iliyo tambarare (Luk 6:17-49). Kama ni tukio lilelie kama kwenye Injili ya Mathayo, itafaa kuitwa Hotuba kwenye sehemu tambarare ya nchi iliyoinuka.

E2j2. Kapernaumu Yesu anamponywa mtumwa wa akida (Mat 8:5-13; Luk 7:1-10).

E3a. Baada ya muda fulani akiwa Yerusalem kwenye sikukuu [huenda ikawa mwezi wa saba] kwenye kisima Yesu amponya mtu aliyekuwa anaumwa kwa miaka 38 (Yoh Jn 5:1-15).

E3b. Maisha kupitia kwa Yesu (Yoh 5:16-47).

E3c. Akiwa Naini, Yesu amponya mtoto wa mjane (Luk 7:11-17).

E4. Njiai kuelekea nchi ya Wagadarene/Wagerasi, Yesus atuliza dhoruba akiwa ndani ya mtumbwi (Mat 8:23-27; Mak 4:35-41; Luk 8:22-26). Kumbuka kuwa dhoruba huwa nyingi zaidi majira ya majani kupukutika kuliko majira ya baridi kali.

E5a. Genesareti, kuponywa kwa watu wawili waliokuwa wamepagawa pepo; mapepoeyatumwa kwenye nguruwe (Mat 8:28-34).

E5b. Kuponywa kwa Mgerasi [Mgenesari] aliyekuwa amepagwa pepo (Mak 5:1-20; Luk 8:26-39). Kumbuka Gadarene, Genesareti, na Gerasi inaweza kuwa ni sehemu moja.

E6. Kufufuliwa kwa binti wa Jairo, na mama aliyekuwa anatokwa damu (Mat 9:18-26; Mak 5:21-43; Luk 8:40-56).

E7. Alipoendelea Yesu awaponya vipofu wawili wasengenyaji (Mat 9:27-31).

E8. Walipokuwa wanatoka, Yesu amponya mtu aliyepagawa pepo na kipofu. Mafarisayo wanamshutumu Yesu kwa kutoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli. Kifungu hiki hakimwelezi Yesu akijibu shutuma hizo kwa wakati huu (Mat 9:32-34).

E9a. Yesu aenda kwenye miji mingi na vijiji (Mat 9:35-38; Mak 6:6).

E9b. Yesu awatuma thenashala (Mat 10:1-42; Mak 6:7-13; Luk 9:1-9).

E9c. Yesu ahubiri Galilaya (Mat 11:1).

E9d. Yohana Mbatizaji atuma ujumbe kutoka gerezani, na Yesu anatoa mfano wa watoto wanaopiga ngoma sokoni (Mat 11:2-19; Luk 7:18-35).

E9e. Chakulani kwenye nyumba ya Mfarisayo Simoni,mwanamke mwenye dhambi aliyekuwa na chupa ya manukato apaka miguu ya Yesu mafuta. Yesu aongea kuhusu kupenda zaidi na kupenda kidogo (Luk 7:36-50).

E10. Mara Yesu anakwenda mlimani (Mak 6:45-46).

E11. Baadaye Genesareti, Yesu anawaponya wengi (Mak 6:53-56).

E12a. Kukemewa kwa miji y Galilaya (Mat 11:20-24).

E12b. Wakati ule, Yesu alifundisha kuhusu pumziko kwa waliochoka (Mat 11:25-30).

E13. Yesu anaondoka kutoka mahali pale (Mat 12:15-21).

E14. Ndani ya nyumba ambamo kuna umati mkubwa sana wa watu hata inazuia kula, familia ya Yesu inadhani amerukwa akili (Mak 3:20-21).

E15. Yesu anamponya mtu kipofu ambaye pia amepagawa mapepo (Mak 12:22-23).

E16. Yesu anaongea juu ya kuiteka nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kumkufuru Roho Mtakatifu (Mat 12:24-37; Mk 3:22-30).

E17. Mama na ndugu wa Yesu (Mat 12:46-50; Mk 3:31-35; Lk 8:19-21).

E18. Ombi la kwanza la ishara, na unabii wa siku mchana na usiku (Mat 12:38-45).

E19. Galilaya kutoka kwenye mtumbwi, mfano wa mpanzi (Mat 13:1-23; Mk 4:1-20; Lk 8:1-15).

E20. Mfano wa magugu (Mat 13:24-30).

E21. Mfano wa taa kwenye kiango (Mak 4:21-25; Lk 8:16-18).

E22. Mfano wa mbegu inayokua (Mak 4:26-29).

E23. Mfano wa punje ya haradali (Mat 13:31-35; Mk 4:30-34).

E24. Ndani ya nyumba, anaeleza maana ya mfano wa magugu (Mat 13:36-43).

E25. Mifano ya hazina iliyofichwa, lulu na nyavu (Mat 13:44-53).

E26. Yesu anarudi Nazareti; nabii asiyeheshimiwa (Mat 13:53-58; Mk 6:1-6).

E27. Jinsi Yohana Mbatizaji alivyouawa (Mat 14:1-12; Mak 6:14-29; Luk 9:7-9).

Kwenye orodha hii ya matukio 65, matukio yanafanana kwenye injili zote 4, matukio 13 yalifanana kwenye injili zote za Snoptiki, tukio moja linafanana kwenye Mathayo na Luka, matukio 4 yanfanana kwenye Mathayo na Marko, matukio 4 yanafanana kwenye Mathayo na Luka, matukio 4 yanafanana kwenye Marko na Luka, matukio 15 yapo kwenye Mathayo tu, matukio 7 yapo kwenye Marko tu, matukio 7 yapo kwenye Luka tu, na matukio 8 yapo kwenye Yohana tu.

 

S: Kwenye injili, ni mambo gani ya msingi yanayodhaniwa kuhusiana na siku za mwanzo za huduma ya Yesu?

J: Kila kitu huwa kinakuwa na mambo yanayodhaniwa, na kuna mambo niliyoyadhania hapa.

a) Baadhi ya vifungu vya Yohana viliwekwa kwenye kipindi cha katikati, wakati vingeweza kufaa hapa pia.

b) Injili ziliandikwa kwa mfuatano zilio nao kwenye Biblia, isipokuwa sehemu ambazo zimepigwa mistari, ambazo ni zaidi ya 10.

 

S: Kwenye Yoh 1:43-50, je Yesu aliwaita wanafunzi hawa wamfuate wakati huu, au aliwachagua kuwa mitume baadaye kama Mat 4:18-22; Mak 1:14-20, na Luk 5:1-11 zinavyoonyesha?

J: Yote. Yesu aliwaita kumfuata wakati huu, lakini baadaye aliwafanya kuwa thenashala. Inabidi kutofautisha kati ya usaili wao wa kwanza na wito wao wa kudumu. Kwenye Yoh1:39, walikaa na Yesu siku ile moja tu.

Leo Mungu anatuita kwanza kuwa watoto wake. Watu wengi baadaye huitwa kwa ajili ya huduma kubwa, na wengine hupewa huduma kubwa zaidi baadaye.

 

S: Kwenye Mat 4:17; 10:17; Mak 1:15; Luk 8:10; Yoh 3:5, je ufalme wa Mungu na ufalme wa mbinguni vinafanana, au kuna tofauti ndogo kati ya mambo haya mawili?

J: Watu wengi wanayachukulia misemo hii kuwa inafanana; huwezi kushiriki kwenye jambo moja bila kushiriki kwenye lingine. Mathayo anatumia misemo yote, na Marko, Luka, na Yohana wanatumia ufalme wa Mungu tu. Yesu anatumia misemo hii yote kwenye mistari inayokaribiana kwenye Mat 19:23-24. Wayahudi wa wakati ule siyo tu kuwa hawakupenda kutamka jina halisi la Mungu (Yahweh), lakini pia Elohim. Kwa hiyo walitumia majinaa yanayofanana na hayo ha-shem (Jina), maqom (anga), na shamayim (mbingu). Hivyo badala ya kusema "ufalme wa Mungu", baadhi ya Wayahudi waliweza kusema "ufalme wa mbinguni."

Wengine wanaona tofauti ndogo; ufalme wa mbinguni ni mahali ambapo waamini wote wanakwenda wanapokufa, na ufalme wa Mungu ni himaya ambayo tunakuwemo sasa tunapokuwa tumeokolewa.

Bila kujali neno moja moja, tunaweza kukubaliana kuwa wokovu wetu unahusisha maisha ya sasa hapa duniani, na maisha ya baadaye mbinguni (1 Kor13:12; Fil1:21-24) ambayo haitaweza kufikiwa mpaka hapo tutakapofika mbinguni. Kwenye Yoh 3:5, watu wengine wanadhani maji yanamaanisha maji ya uzazi yenye kuizunguka mimba na kutoka tumboni mwa mama mtoto anapozaliwa, lakini wengine wanadhani kuwa yanamaanisha ubatizo. Hayawezi kumaanisha ubatizo, kwani ingekuwa hivyo basi yule mwizi pale msalabani asingeokolewa! Lakini yanaweza kumaanisha kuwa mtu hawi si sehemu inayoonekana ya ufalme wa Mungu hapa duniani mpaka anapokuwa amebatizwa. Wazo linalofanana na hili, makanisa mengi hayapendi watu kushiriki meza ya Bwana hadi hapo wanapokuwa wamebatizwa.

 

S: Kwenye Luk 6:12-49 na Luk 12:3-38, kwa nini maneno haya yanafanana na Hotubaa ya Mlimani kwenye Mat 5:1-7:29?

J: Kuna majibu matatu tofauti.

a. Yesu alitoa mahubiri yanayofanana mara zisizopungua mbili. Watu wote wasingeweza kuyasikia mahubiri yote hayo mara yalipotolewa mara ya kwanza.

b. Huenda yalikuwa ni mahubiri yale yale, na kila mwandishi aliandika ufafanuzi wa kitu alichokikumbuka. "Tambarare" juu ya mlima ni uwanda wa juu au nchi iliyo inuka ikawa ya mlalo kama meza.

c. Luka 6 inasema tu kuwa Yesu alisimama kwenye sehemu tambarare, siyo kwamba makutano walifanya hivyo. Yesu kusimama kwenye sehemu iliyo tambarare ili kuhubiri kwa umati uliokuwa umesimama pembeni mwa mlima kunafanya uwanja duara wa asili wa kufanyia maonyesho.

Vyovyote itakavyokuwa, mafundisho ya Yesu ni ya muhimu wakati wote bila kujali kuwa aliyasema mara ngapi.

 

S: Kwenye Luk 6:17, je Yesu alisimama kwenye sehemu tambarare alipokuwa akiwafundisha, au alikaa kama ambavyo Mat 6:17 inasema?

J: Kuna majibu mawili na yote yanaelekea kuwa kweli.

Mahubiri ya kwenye injili za Mathayo na Luka yanaelekea kuwa matukio tofauti. Isitoshe, hata Yesu aliposimama, baada ya kuongea kwa muda mrefu sana, huenda alihitaji kukaa. Kumbuka mahubiri yanaweza kuchukua masaa kadhaa, na maelezo tuliyonayo kwenye injili za Mathayo na Luka ni muhtasari.

 

S: Kwenye Mat 5:3, je Yesu alisema "maskini wa roho", au maskini tu kama kwenye Luk 6:20?

J: Yesu anaweza kuwa alisema vyote. Wote Mathayo na Luka wanafafanua mafundisho ya Yesu. Mahubiri haya kwenye Mathayo na Luka yanaweza kuwa yanawakilisha matukio mawili tofauti, na Yesu anaweza kuwa aliyasema yote. Kwa upande mwingine, mahubiri haya kwenye injili za Mathayo na Luka yanaweza kuwa yanawakilisha tukio moja. Moja lilikuwa kwenye mlima na lingine kwenye tambarare. Yanaweza kuwa mahubiri yaliyotolewa sehemu moja kwenye uwanda ulioinuka ukawa tambarare, ambayo ni sehemu tambarare juu ya milima.

Vyovyote itakavyokuwa, tunafahamu kuwa Yesu aliongelea watu waliokuwa wahitaji na walitambua kuwa wao ni wahitaji.

 

S: Kwenye Mat 8:5-13; 9:9-13; je Yesu alimponya mtumwa wa akida kabla ya kumwita Mathayo (Lawi), au baada kama Luk 5:27-32; 7:1-10 inavyomaanisha?

J: Inaweza kuwa vyovyote vile, kwani injili hizi zote mbili hazitoi mfuatano, na injili zote nne hazichukuliwa kuwa zinapangilia matukio kufuatana na jinsi yalivyotokea. Hata hivyo, injili hizi mbili zinasema kuwa Mathayo/Lawi aliitwa baada ya kuponywa kwa mtu aliyekuwa amepooza.

 

S: Kwenye Mat 8:5-10, je akida alimwona Yesu moja kwa moja, au hakumwona Yesu balia aliwatuma marafiki zake kwenye Luk Lk 7:6?

J: Kuna majibu mawili yanayowezekana.

1. Akida alimfuata Yesu kupitia marafiki zake, si kwa njia ya kwenda yeye mwenyewe. Mathayo anaacha maelezo haya, na anasema tu kuwa akida alimletea ombi Yesu, bila kusema bayana kuwa alifanya hivyo kupitia kwa marafiki zake. Mathayo anaweza kuwa hakupenda kuweka ukungu kwenye jambo hili kuwa Yesu alikuwa anamsaidia mtu asiyekuwa Myahudi. Vivyo hivyo Pilato alipompiga Yesu viboko kwenye Mat 27:26, Mathao HASEMI kuwa Pilato yeye mwenyewe alimpiga viboko Yesu, bali aliamuru Yesu apigwe viboko.

2. Mara ya kwanza akida alitumia marafiki. Jambo hilo linaweza kuwa llifanyika ili isije ikatahayarisha endapo Yesu angekataa kusikiliza ombi la mtu asiyekuwa Myahudi. Baada ya hapo, akida alikwenda yeye mwenyewe.

 

S: Kwenye Mat 9:18-25, Mak 5:23-43, Luk 7:11-17, 8:41-56, na Yoh 11:1-44, ni watu gani ambao Yesu aliwafufua kutoka mauti wakati wa huduma yake, na ni kwa nini?

J: Miujiza yote hii mitatu ilimletea Mungu utukufu na ilionyesha kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu.

Mtoto wa kiume wa mwanamke mjane kwenye Luk 7:11-17. Huenda mtoto hakurudishwa kwa ajili yake yeye mwenyewe, bali kwa ajili ya mama yake.

Binti wa Jairo kwenye Mat 9:18-25; Mak 5:23.35-43; Luk 8:41-42, 49-56. Kwenye suala hili, msichana alikuwa anakufa, na Yesu alichelewa kwa sababu alikuwa anamhudumia mwanamke mwingine. Mungu anaweza asije mapema mara nyingine, lakini daima hachelewi kufanya kazi yake.

Lazaro kwenye Yoh 11:1-44. Kwa udadisi ingawa Yesu alimpenda sana Lazaro kwenye Yoh 11:3, Yesu alichelewa siku mbili zaidi kwenye Yoh 11:7, wakati Lazaro alipokuwa mgonjwa, hadi alipokufa. Mwanzoni, jambo hili linaweza kuwa limeishtua imani ya Mariamu na Martha, lakini wakati mwingine Mungu anajaribu imani zetu kwa ajili ya utukufu wake, na kuimarisha imani yetu.

 

S: Kwenye Mat 9:18, je binti wa Jairo alikuwa amekufa, au alikuwa anamkaribia kufa kama Mak 5:22 na Luk 8:42?

J: Kwanza Kigiriki kidogo, kisha mambo mawili ambayo huenda si jibu, ndipo jibu linaloelekea kuwa sahihi.

Kigiriki

Kwenye Mat 9:18, maneno ya Kigiriki arti eteleutesen yanamaanisha "sasa hivi amekufa", au "amekufa sasa hivi" lakini siyo "anakufa sasa hivi"

Kwenye Mak 5:22 maneno ya Kigiriki eschatus exei yanamaanisha mwishoni. Tunapata neno la Kiingereza ‘eskatolojia' (eschatology), yaani mafundishao kuhusu siku za mwisho, kutoka kwenye neno la kwanza, eschatus.

Kwenye Luk 8:42 neno la Kigiriki apethnesken linamaanisha "kufa."

Si jibu: hali ya kuzimia ni kama kifo

Kupumua kwa mtu aliye kwenye hali ya kuzimia ni kuchache sana, na ni vigumu kusema mtu aliyekuwa katika hali hii amekufa lini. Hata hivyo, maoni haya hayaelekei kuwa sahihi kwa sababu Jairo aliondoka muda mrefu uliotangulia, na mtu aliyekuwa kwenye hali ya kuzimia angekuwa wa moto kwa namna fulani. Mwisho, kwa kuwa marafiki wa Jairo walimwambia kuwa binti yake amekufa itakuwa ni kinyume na maoni haya.

Jambo hili linaweza lisiwe jibu sahihi: Jairo alisema maneno yote haya matatu

Jairo mwenyewe hakuwa na uhakika endapo binti yake alikuwa hai wakati yeye anaongea na Yesu, au alikufa wakati akiwa njiani kwenda kwa Yesu. Hivyo Jairo anaweza kuwa alisema amekufa, na wakti mwingine alisema alikuwa mwishoni mwa maisha yake, na wakati mwingine tena alisema alikuwa anakufa. Hata hivyo, kwenye injili zote tatu, Jairo alisema maneno haya akimuuliza Yesu, na ingawa anaweza kuwa alirudia ombi lake mara tatu, akitumia maneno tofauti, jibu linalofuata lina uwezekano mkubwa zaidi.

Jibu sahihi: Waandishi wa injili walitoa ufafanuzi wa maneno ya Jairo

Kwenye maeneo mengine katika injili maongezi huwa yanafafanuliwa, si nukuu halisi, na mawazo makuu hupewa mkazo na maelezo mengine yanaachwa. Kwa mfano, wakati watu walikuja siku nzima kusikiliza mafundisho ya Yesu, tunaweza kusoma habari hiyo kwa dakika tano tu, je watu hao walifanya nini muda mwingine wote? Kama Yoh 21:25 inavyosema, "Kuna na mambo mengi aliyofanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa."

Fikiria jambo hili: inachukua sekunde tat utu kusoma maneno ambayo Jairo aliyasema kwenye kifungu chochote kile. Wakati Jairo amekuja, je aliongea na Yesu kwa sekunde tatu tu, kisha akakaa kimya? – kwa kweli hatifikirii hivyo. Lakini jambo hili linamaanisha kuwa kila mwandishi wa injili alichagua kuacha maelezo mengi ya ziada na alitaka kurekodi ujumbe mkuu aliokuwa nao Jairo. Msemo wowote ambao Jairo aliutumia, na huenda alitumia zaidi ya mmoja, binti yake mpendwa alikuwa anapitia mwisho wa maisha yake.

 

S: Kwenye Mat 9:24, Mak 5:39 na Luk 8:52, kwa nini Yesu alisema kuwa binti alikuwa amelala tu?

J: Kwanza jambo ambalo linaweza lisiwe jibu, kisha jibu.

Jambo ambalo huenda si jibu – hali ya kuzimia na ubongo kutoonyesha kufanya kazi

Ingawa kulala hutumika kuelezea kifo, inaweza kuwa ni hali ya kuzimia na ubongo kutoonyesha kufanya kazi. Yesu alisema, "Kijana hakufa, bali amelala tu" kwenye Mak 5:39. Lakini kwenye Mak 5:35 wakati marafiki wa Jairo wanamweleza kuwa asimsumbue Yesu kwa sababu binti yake amekufa, alikuwa amekufa kabisa kwa kadri walivyoweza kutambua.

Jibu:

Yesu alitaka kusistiza kuwa kwake yeye kifo ni sawa na mwili kulala.

 

S: Kwenye Mat 9:22, 29, na 15:8, unaweza kunielezea tofauti kati ya imani inayoponya na imani iokoayo? Kwa mfano, kwenye Mat 9:22, Yesu anasema, "Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya", na kwenye Mat 9:29, Yesu aliwagusa macho yao akisema, "Kwa kadri ya imani yenu mpate", na kwenye Mat 15:28, "Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, ‘Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo.' Akapona binti yake tangu saa ile." Je imani ni kitu asilia? Je imani iliyoonyeshwa kwenye uponyaji uliofanywa na Yesu ilitokana na watu waliokuwa wanaponywa au Mungu kupitia kwa Roho Mtakatifu aliwapa imani inayotakiwa kuleta uponyaji hivyo kwamba Mungu apewe utukufu? Kwenye Efe 2:8, "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu." Hapa naona kuwa imani ni kipawa cha Mungu.

J: Umeuliza swali la kina sana. Jibu fupi ni kuwa kun imani moja tu: imani kwa Mungu. Lakini imani hii inaweza kujionyesha kwenye uponyaji wa mwili, na maisha matakatifu, na imani ambayo inaweza pia ikasongwa au kuchukuliwa.

Kwa jibu refu zaidi, kwanza natuangalie imani kwa ujumla, na kisha maeneo mbalimbali ya imani. Ingawa imani inahusisha kukubali kiakili, Yako 2:19 inaonyesha kuwa imani ni zaidi ya hivyo; imani ni kutumaini. Kuna habari inayofahamika sana kwenye karne ya 19, mtembea kwenye kamba maarufu sana aitwaye Charles Blondin alikuwa akitembea kuvuka Maporomoko ya Niagara kwenye kamba huku akiukuma toroli. Kuna watu waliomwambia kuwa wanaamini kuwa ataweza kufanya hivyo. Alisema kuwa kama kweli wanaamini hivyo, basi wapande kwenye toroli. Imani si kusema tu "Naamini" lakini kuwa tayari kupanda toroli. Je tunamtumaini Mungu hata tukawa tayari kuonekana wajinga endapo Mungu asingejidhihirisha? Imani ni kitu kinachosifiwa, na Waebrania 11 inatoa mifano mingi ya kutokukubali kiakili tu bali pia kuishi kwa imani.
Imani inatakiwa iwe kitu sahihi cha kusimamia; kuamini sanamu kidhati hakutakupeleka kokote kule, au hakutakupeleka mahali pazuri. Endapo mtu anaamini na anafanya mambo mengi mazuri, lakini haamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kuwa alifufuka kutoka kwa wafu, imani yake ni bure kwa mujibu wa 1 Kor 15:1-8. Hawakuponywa kwa sababu ya kuwa na imani katika uponyaji, imani kwao wenyewe, imani kwa baadhi ya watakatifu, au imani kwenye imani; waliponywa kupitia imani kwa Yesu. Inafurahisha kuwa kabla ya kifungu hiki kwenye Mat 9:1-8, Yesu alimponya mtu aliyekuwa amepooza na haisemi kitu kuhusu imani yake, au kitu chochote kile kuhusu yeye mwenyewe. Tunaweza kuona kuwa marafiki wake walikuwa na imani ya kutosha kumbeba na kumpeleka kwa Yesu; na ingawa inawezekana kuwa alikuwa na imani, jambo hili halijaelezwa. Hivyo ingawa hatuwezi kuwa na imani iokoayo kwa ajili ya mtu yeyote isipokuwa sisi wenyewe, imani yetu inaweza kuwa chombo chenye kufaa ambacho Mungu anakitumia kwenye maisha ya watu wengine. Kwa upande mwingine, Yesu aalichagua kutokufanya miujiza mingi Nazareti kwa sababu ya kutokuamini kwao kwenye Mat 13:57-58.
Kwa bahati mbaya imani yetu inaweza isiwe kamili nyakati nyingine na yenye kupungua udhati na mapana.

Imani tu kwa muda: Yuda Iskariote alimwamini Yesu hata akayaacha maisha yake ya awali na kumfuata Yesu, angalau kwa muda. Lakini hata kabla ya kumsaliti Yesu, Yuda alikuwa anaiba hela zilizokuwa kwenye mfuko (Yoh 12:6). Yuda alikuwa anakwenda na wanafunzi wengine kumi na moja kuhubiri (Mat 10:4-16), lakini ingawa imani ya watu wengi ingeweza kukua kwa kusikia miujiza mikubwa, hakuweza (au inaweza kuwa vizuri kusema kuwa hakupenda kufanya hivyo) kuwa na imani kuwa Mungu angeweza kutimiza mahitaji yake kifedha na kwamba hakuhitaji kuiba kutoka kwa Yesu na wanafunzi wengine. Hivyo kwa kuwa na imani kwa muda, ingawa naamini kuwa watu waliookolewa kweli hawawezi "kuacha kuchaguliwa", ninaamini pia maonyo ya kwenye Biblia kuwa baadhi ya watu waliokwisha kupewa nuru, kukionja (lakini haisemi kukimeza) kipawa cha mbinguni, wanaweza kuangukia kwenye maangamizo ya milele (Ebr 6:4-6).

Kukosa udhati na imani: Kuna watu, kama mbegu zilizopandwa kwenye miamba, wanaokuwa na imani kwa muda lakini kisha wanasongwa. Wanaweza kusema kwa uwazi kabisa kuwa hawana imani tena, au wasiwe wazi na wadai kuwa wana imani lakini wakawa wanafiki. Mtu anaweza kuwa na imani ya ukweli iliyochanganyikana na uongo lakini akawa wazi kuhusu jambo hili. Wakati Yesu alipomuuliza baba wa mtoto aliyekuwa amepagawa ikiwa anaamini, alijibu "Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu" (Mak 9:24). Wengine hawana imani ya kweli, bali ni imani isiyokuwa ya kweli, kama Simoni mchawi kwenye Mdo 8:18-22.

Upana wa imani: Watu wengine wanaweza kumwamini Mungu kwa mambo makubwa pale panapokuwa hakuna jinsi nyingine, lakini hawamwamini Mungu kwa mambo madogo. Wengine kama Gideoni wanaweza kuwa na imani kubwa sana kuwa Mungu atawaokoa kwenye vita kwa kutumia askari wachache sana, lakini hawaamini kuwa njia ya Mungu ndiyo bora zaidi badala ya kupata hela kutokana na sanamu, kama Gideoni alivyofanya kwa aibu kwenye Amu 8:24-27. Samsoni naye alifanya namna hiyo.
Siamini kuwa kuna aina mbili za imani: imani iokoayo, na imani iponyayo; kuna imani moja tu (Efe 4:5). Lakini imani hii, kama mbegu kwenye Mat 13:12-23, inaweza kukua (ama kwa kiasi kikubwa au kidogo tu), kujizidisha kwenye maisha ya watu wengine, lakini inaweza pia ikadhoofika na kufa. Kama onyo kwetu, natuiangalie mifano minne ya imani iliyokufa:

Yesu alifundisha kwenye Mat 7:21-23 kuwa kutakuwa na watu watakaohubiri injili (natumaini ni injili ya kweli), na hata kufanya miujiza kwa jina la Yesu, jambo ambalo utakubali kuwa linahitaji imani kubwa. Lakini mwishoni watu hawa watakwenda jehanamu kwa kuwa walikuwa watenda mabaya. Ni muhimu kuwa Yesu hakusema "Nimewasahau" au "Mmepoteza wokovu wenu." Badala yake, Yesu aliwaambia watenda mabaya hawa waliokuwa na imani kubwa, "Sikuwajui ninyi kamwe."

Je mtu anayekwenda jehanamu anaweza kusaidiwa na imani? Ndiyo, japo kwa muda mfupi. Kwenye 2 Pet 2:20-22 Biblia inasema, "kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa. Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, ‘Mbwa amerudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaagaa matopeni.'" Watu hawa hawakuwa wameokolewa, siku zote walikuwa mbwa au nguruwe. Hata hivyo mtu huyo kwa namna fulani "alimjua" Yesu, Bwana na Mwokozi wetu. Ufahamu wao ulitosha kuwainua kutoka kwenye maisha ya dhambi kwenda kwenye maisha matakatifu, lakini kwa kitambo kidogo tu.

Watu wengi wanasaidiwa na Yesu kama wale wenye ukoma tisa walivyosaidiwa kwenye Luk 17:11-19. Yesu aliwaponya watu kumi wenye ukoma, lakini ni Msamaria mmoja tu aliyerudi kumshukuru Yesu. "Yesu akajibu, akanena ‘Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?' Akamwambia, ‘Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.'" Wale wengine tisa walisaidiwa kweli kimwili, na Biblia haisemi kuwa kuponywa kwao kulichukuliwa. Lakini kitu pekee walichokipata ni uponyaji wa kimwili; ni Msamaria tu aliyekwenda kwa Kristo kumtukuza Mungu. Kama nina shida ya kiroho, na ninatakiwa kuchagua ama imani iponyayo au imani iokoayo nitapenda imani iokoayo na iponyayo kiroho kuliko imani iponyayo kimwili tu. Mungu anatupa imani inayoweza kufanya vyote viwili, lakini hakikisha kuwa unasistizia Mtoaji, siyo zawadi tu.

Imani yetu inapaswa iwe thabiti kama Yak 1:12 inavyofundisha ili kuweza kustahimili hata hali ngumu zaidi; lakini imani ya mtu inaweza kuwepo kwa muda tu kisha inakufa. Nadhani tofauti nzima ipo kwenye jambo hili kwamba je imani hii inatunzwa na Mkulima (Yoh 15:1b), na je imani hii imeshikamana na Mzabibu (Yoh 15:1-8). Kuwa na imani, hata imani kubwa, hakudumu isipokuwa tu inaendelea kutunzwa na Mungu. Hivyo, ingawa imani ni muhimu, ni muhimu zaidi kuwa karibu na Mungu. "And now these three remain: faith, hope and love. But the greatest of these if love." (1 Kor 13:13).

Lakini imani iokoayo ina umuhimu gani?

Wokovu ni kipawa cha Mungu; hakitokani na sisi na hatookolewi na imani yetu. Badala yake, tunaokolewa kwa neema ya Mungu, kwa njia ya imani, si kwa matendo kama Efe 2:8-9 inavyosema. Kuna mambo matatu ambayo jozi hii fupi lakini ngumu kuelezeka inasema:

Ni kwa neema. Hatuwezi kuupata wokovu kama malipo ya mambo mazuri tuliyoyafanya, vinginevyo haitakuwa neema.

Ni kwa njia ya imani. Imani ina wajibu tofouti na neema. Imani ni itikio letu kwa kazi ambayo Mungu ameianzisha.

Si kwa matendo. Matendo hayana jukumu lililo sawa na neema, hayafanyi kitu chochote kutufanya tuupate wokovu kama malipo ya kazi nzuri tulizozifanya.

Matendo yana jukumu tofauti na imani; hatuokolewi kwa matendo, bali wa imani.

Kwa ajili hii tunaweza kujiuliza endapo matendo yana nafasi yeyote katika wokovu wetu. Paulo alitarajia swali hili na alilijibu kwenye Efe 2:10. Matendo yana nafasi katika wokovu, lakini si nafasi ambayo baadhi ya watu na wengi wa Wakatoliki wanafundisha. Matendo ni matokeo ya wokovu wetu, si kigezo cha wokovu. Hatuokolewi kwa kutumika, lakini tunaokolewa ili tutumike. Ikiwa mambo haya mawili hayaendi pamoja kwa waumini, itabidi kujiuliza endapo mtu huyu ni muumini kweli kama Yak 2:14-25 inavyosema. Hata hivyo, matendo yana jukumu tofauti.

Lakini kwa kuwa si sahihi kusema kuwa matendo yana jukumu linalifanana na imani katika wokovu wetu, kama baadhi ya Wakatoliki wanavyosema, , si sahihi pia kusema kuwa imani ina wajibu ulio sawa na matendo katika wokovu wetu, kama baadhi ya Wakalvinisti wanavyosema. Ebr 4:2 inasema, "Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halkuchanganyika na imani ndani yao waliosikia."

Je imani hii yenye kustahimili ni kipawa cha Mungu, au wajibu wetu, ni vyote. Mungu hutupa imani kama zawadi, na tunaweza na tunapaswa kuomba tuongezewe imani. Lakini tuna wajibu wa kuamini na wajibu wa kupiga mbio kwa saburi (Ebr 12:1). Tunao wajibu wa kujipima sisi wenyewe na waalimu wetu (2 Kor 13:5-6). Lakini tunaweza kumtumaini Mungu kuwatia watu wote waliookolewa muhuri wa Roho Mtakatifu, ambaye ni "Arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kwa sifa ya utukufu wake" (Efe 1:14). Tazama www.BibleQuery.org kwenye orodha ya vitu iliyoko upande wa kushoto yenye kichwa "Mafundisho", na kisha chini ya kichwa "kuchaguliwa tangu awali" (Predestination) kwa habari zaidi.

 

S: Kwenye Mak 5:35 na Luk 8:49, je Jairo alikuwa ameambiwa kuwa binti yake amekufa?

J: Ingawa inaweza kuwa jambo lolote kati ya haya mawili, la kwanza linaweza kuwa sahihi zaidi.

a) Yawezekana Jairo alifahamu kwa binti yake alikuwa anakaribia kufa wakati (Jairo) alipokuwa anaondoka kwenda kumuona Yesu, na alikuwa alipokuwa anarudi, walimwambia kuwa binti wake amekwisha fariki.

b) Jambo lenye uwezikano mkubwa zaidi, linaweza kuwa Jairo alkwishajua kuwa binti yake amekufa, au yuko mahututi sana karibu sawa na kufa, wakati alipokuwa anaondoka kwenda kumwona Yesu, na alipokuwa anarudi, aliambiwa kuwa, he was told in effect, "Binti yako amekwisha kufa; usimsumbue mwalimu."

Hata hivyo, jinsi yeyote itakavyo kuwa, ujube alioambiwa Jairo ni huu: "Usimsumbue Yesu, kwani hata yeye hatakuwa na kitu cha kufanya kuhisiana na swala hli." Natumaini kuwa hatuna fikra hii, kama Jairo alivyochagua kuwa na imani na kukataa fikra za namna hiyo.

 

S: Kwenye Mat 10:2-5, Mak 3:16-18, Luk 6:13-16, Yoh 1:45-47; 21:2, naMdo 1:13, je orodha ya wanafunzi kumi na mbili ni tofauti, kama Asimov's Guide to the Bible, uk.998 inavyomaanisha?

J: Hapana. Ingawa mpangilio wa majina ni tofauti kwa kiasi, orodha hizi zinafanana kwa kadri tunavyofahamu mambo haya yafuatayo.

Simoni Baryona ni sawa na Petro. Baryona maana yake "bar" (mwana wa) Yona. Simoni ni jina la Kiebrania, na Petro ni jina la Kigiriki.

Mathayo mtoza ushuru = Lawi mwana wa Alfayo mtoza ushuru kwenye Mak 2:13-17. Lawi ni jina la Kiebrania. Mathayo pia ni jina la Kiebrania, ufupisho wa Mathiya. Kama mtoza ushuru Mathayo anaweza kuwa alipenda kuwa na jina lingine pia.

Yakobo, Mwana wa Alfayo ni mtu huyo huyo anayefahamika kama Yakobo mdogo kwenye Mak 15:40. Kwenye lugha ya Kiingereza, jina la Yakobo linaitwa ‘James' ambalo ni jina la Kigiriki lenye kuwasilisha jina la Kiebrania ‘Yakobo.'

Batholomayo (kwenye orodha zote) ni mtu huyo huyo anayefahamika kama Nathanaeli kwenye Yoh 1:45-47; 21:2. Jina la Kiaramu Bartholomayo halikuwa jina lake la kwanza, lakini jina lake la mwisho, kwa kuwa linamaanisha "Bar" (mwana wa) Talmai/Tolmai/Talmar. Nathanaeli pia neno la Kiaramu linalomaanisha "Zawadi ya Mungu."

Thadayo ni jina sawa na Yuda mwana wa Yakobo kwenye Luk 6:16 na Mdo 1:13, sawa na Petro na Simoni kuwa mtu mmoja. Huenda baada ya Yesu kusulubiwa Thadayo hakupenda kuitwa Yuda, kwa sababu ya uwezekano wa kuchanganywa na Yuda Iskariote. Yuda ni jina la Kiebrania. Kuna hati za Kigiriki zinasema Thadayo, na nyingine zinasema "Lebbaeus", na nyingine zinasema "Lebbaeus aliyeitwa, au ambaye jina lake la mwisho ni Thadayo."

Yuda Iskariote halipo kwenye Mdo 1:13 kwa sababu zinazoeleweka kabisa.

Kwa wengine, Andrea, Yajobo mwana wa Zebedayo, Yohana, Filipo, Tomaso, na Simoni Mkananayo, tunaelezwa jina moja tu.

Inawezekana kuamini kuwa Nathanaeli kwenye Yoh 1:43-45; 21:2 hakuwa mtu yule yule sawa na Batholomayo. Jambo hili halimaanishi kuwa Biblia imekosea, ila inamaanisha kuwa Nathanaeli alikuwa mwanafunzi wa Yesu lakini hakuwa miongoni mwa thenashara.

 

S: Kwenye Mat 10:9-10 na Luk 9:3, ilikuwaje wanafunzi hawakutakiwa kuchukua fimbo, kwani walitakiwa kuchukua fimbo tu kwenye Mak 6:8-9?

J: Wakristo wanatoa majibu matatu tofauti, lakini jibu la tatu ndilo linaloelekea kufaa zaidi.

Safari nyingi: Huenda walifanya safari nyingi. Hata hivyo, sababu pekee ya kufikiri ni safari nyingi ni kuwianisha maagizo ya kuchukua fimbo na kutokuchukua fimbo.

Maneno tofauti ya Kigiriki: neno "kuchukua" lililotumika kwenye Mathayo ni tofauti na neno lililotumika kwenye Marko. When Critics Ask, uk.339, inasema wanafunzi waliruhusiwa kuchukua vitu ambavyo tayari walikuwa navyo, lakini si kuchukua vitu vya ziada, au kitu kingine chochote kwa ajili hiyo. Neno la Kigiriki lenye kumaanisha "kuchukua/kupata" kwenye Mat 10:9 linaweza kumaanisha kupata, kama kwenye usemi usinunue au kukusanya vitu hivi. Neno la Kigiriki kwenye Mak 6:8 linamaanisha kumuliki. Changamoto inayoyakabili maoni haya ni kuwa neno la Kigiriki lililotumika kwenye Luk 9:3 ni unyambulisho tofauti wa neno lile lile lililotumika kwenye Mak 6:8.

Kosa la kunakiri: Huenda nakala zilizopo za Marko zimeweka neno "tu" badala ya "msichukuet", kwenye Kigiriki tofauti kati ya maneno "tu" na "us/msi . . ." ni nyongeza ya neno ei. Linaweza kuwa ni kosa la aina tofauti la kunakiri, ambapo Mathayo aliifahamu sana Injili ya Marko, lakini aliifuata Injili ya Luka hapa. Hivyo, kwa maneno mengine, "fimbo tu/isipokuwa fimbo" kwenye Marko, huenda ilitakiwa kuwa "msichukue fimbo" kama kwenye Mathayo na Luka.

 

S: Kwenye Mat 10:9-10, je wanafunzi hawakutakiwa kuchukua viatu/makubadhi, au walitakiwa kuchhukua kama Mak 6:8-9 inavyosema?

J: Neno la Kigiriki kwenye Mathayo linaweza kumaanisha "viatu", ingawa neno la Kigiriki kwenye Marko haliwezi kumaanisha viatu. Neno halisi kwenye Mak 6:9 ni "funga chini ya makubadhi." Luk 9:3 haisemi chochote kuhusu viatu au makubadhi.

Kwa hiyo kwa kuhitimisha, inaelekea wanafunzi wangeweza kuchukua makubadhi, lakini si viatu, jambo ambalo lingekuwa bora zaidi kwa safari ndifu. Maoni haya yanafanana na agizo la kutokuchukua fimbo pia.

 

S: Kwenye Mat 10:22; 24:13; na Mak 13:13, kuvumilia hadi "mwisho" ambako Yesu alikuongelea kunamaanisha nini hasa?

J: Huu ni mwisho wa dhiki kuu.

 

S: Kwenye Mat 11:14 na Yoh 1:21, inakuwaje Yohana Mbatizaji awe ndio Elia anayekuja?

J: Mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

1. Elia mwenyewe alitokea wakati sura ya Yesu ilipobadilika, na Elia huenda akatokea tena kiuhalisi kabla ya kuja kwa Yesu kwa mara ya pili, lakini Yohana Mbatizaji ni mtu tofauti na Elia.

2. Yohana alitimiza jukumu la Elia kwenye Mal 4:5, kwa kuja kwa Yesu kwa mara ya kwanza, lakini Elia mwenyewe atatokea kwenye kuja kwa Yesu kwa mara ya pili.

3. Yesu hakusema kuwa Yohana ni Elia aliyerudi. Badala yake, Yesu alisema Yohana alikuwa ni Elia atakayekuja.

4. Justin Martyr (karibu mwaka138-165 BK) kwenye kitabu chake, Dialogue with Trypho the Jew sura ya 49 anaonyesha kuwa msemo kwamba mtu mmoja "ana roho ya mtu mwingine" ulitumka sehemu nyingine pia kwenye Biblia, wakati Mungu alipochukua roho iliyokuwa juu ya Musa na kuiweka juu ya Yoshua, na wakati Elisha alipopokea sehemu mara mbili ya roho ya Elia. Hakuna mtu aliyeweza kuifahamu mifano hii miwili kuwa ni kufanyika mwili upya au kuwa mtu yule yule, kwa sababu katika mifano hii yote mkuu na mtu wa chini yake waliishi wakati mmoja.

 

S: Kwenye Mat 11:14 na Yoh 1:21, je vifungu hivi vinaunga mkono hoja ya kufanyika mwili upya kwa Eliya?

J: Hapana. Mafundisho haya mapotofu ya kufanyika mwili upya yanasema kuwa mtu anakufa, anauacha mwili wake wa zamani milele, na anaurudi kuwa hai akiwa kwenye mwili mpya. Elia hakuwahi kufa, na (tofauti na Yohana Mbatizaji) alitokea kwa Yesu wakati wa kubadilika kwa sura yake. Elia atarudi akiwa na mwili wake mwenyewe siku za mwisho. Tertullian (mwaka 198-220 BK) alijibu swali hili vizuri sana kwenye Treatise on the Soul sura ya 35, uk.217-218. Anaogezea kuwa "‘roho na nguvu' vilitolewa kwa neema ya Mungu kama zawadi za nje."

 

S: Kwenye injili, nini ni mpangilio wa masimulizi unaofuata mtiririko halisi wa matukio wa kipindi cha kati cha huduma ya Yesu?

J: Kipindi cha kati chenye matukio 24 kinahusisha kulishwa kwa makutano na kinaazia wakati Yohana Mbatizaji alipouawa na Yesu alipoondoka Galilaya hadi wakati akiwa Kaisaria Filipo. Tarakimu zinawakilisha matukio ambayo yanatakiwa kufuata namba zilizotangulia. Herufi kama a, b, c zinawakilisha matukio ambayo yangewea kutokea kwa mtiririko wowote ule. Maandishi yenye wino mzito yanaonyesha viashiria muda, mfuatano, na mahali. Aya zilizopigiwa mstari zinaonyesha vifungu ambavyo havina uwezekano wa kutokufuata mtiririko halisi wa matukio.

Huduma ya kati: Mat 14:13-16:28, Mak 6:30-9:1, Luk 9:11-27, Yoh 6:1-7:9

M1. Kuondoka Galilaya, Yesu na wanafunzi wanaondoka kuelekea Bethsaida (Luk 9:10).

M2a. Makutano wamwona Yesu (Luk 9:11).

M2b. Ufukoni upande wa pili wa Kapernaumu, Yesu anahubiri kwa makutano na kuponya (Mat 14:13-14; Yoh 6:1-4).

M3. Nyikani (siyo Genesareti), Yesu awalisha makutano kwa mara ya kwanza: wanaume 5,000 pamoja na wanawake na watoto, kwa kutumia mikate 5 na samaki 2. Vikapu 12 vya mabaki (Mat 14:15-21; Mak 6:30-44; Luk 9:12-17; Yoh 6:1-14).

M4. Njiani kuelekea Genesareti, kwenye zamu ya nne ya usiku, Yesu na Petro watembea juu ya maji (Mat 14:22-36; Mak 6:45-52).

M5a. Huko Genesareti, Yesu awnaponya watu wengi (Mat 14:34-36; Mak 6:53-56).

M5b. Yesus anajitenga na kwenda mlimani (Yoh 6:15).

M6a1. Njiani kwenda Kapernaumu baada ya kuvuta makasia kadri ya maili tatu au nne, wanafunzi wanamwona Yesu akitembea juu ya maji (Yoh 6:16-24a).

M6a2. Mara mtumbwi unafika (Yoh 6:24b).

M6a3. Ufukoni mwa ziwa Kapernaumu, Yesu ni mkate wa uzima (Yoh 6:25-71).

M6a4. Hadi Sikukuu ya Vibanda Yesu abaki Galilaya (Yoh 7:1-9).

M6b. Mafaridayo wanawalalamikia wanafunzi wa Yesu; safi na najisi (Mat 15:1-20; Mak 7:1-23).

M7. Huko Tiro na Sidoni, Yesu anamponya binti wa mwanamke (Mat 15:21-28; Mak 7:24-30).

M8. Huko Dekapoli Yesu anamponya mtu aliye bubu na kiziwi (Mak 7:31-37).

M9. Huko Galilaya Yesu anaponya na kuwafundisha makutano (Mat 15:29-31; Mak 8:1).

M10. Karibu na Bahari ya Galilaya, Yesu anawalisha makutano wengi kwa mara ya pili: wanaume 4,000 pamoja na wanawake na watoto kuwa kutumia mikate saba na samaki wachache. Vikapu 7 vya masazo (Mat 15:32-38; Mak 8:2-9).

M11. Yesu anakwenda chomboni akielekea Magadani/Dalmanutha (Mat 15:39; Mak 8:10).

M12a. Mafarisayo wahitaji kwa mara ya pili ishara kutoka mbinguni (Mat 16:1-4; Mak 8:11-13).

M12b. Yesu anafundisha kuhusu chachu na matukio mawili ya kulisha watu (Mat 16:5-12; Mak 8:14-21).

M12c. Huko Bethsaida Yesu anamponya kipofu (Mak 8:22-26).

M12d. Karibu na Kaisaria Filipo (palipokuwa na mwamba mkunwa sana), Petro anamkiri Yesu kuwa ndiye Kristo (Mat 16:13-20; Mak 8:27-30; Luk 9:18-20).

M13. Yesu anatabiri kifo chake (Mat 16:21-22; Mak 8:31; Luk 9:21-22).

M14. Yesu anamwambia Petro, "Nenda nyuma yangu, Shetani" (Mat 16:23; Mak 8:32-33).

M15. Gharama ya kumfuata Yesu (Mat 16:24-28; Mak 8:34-9:1; Luk 9:23-27).

 

S: Kwenye injili, kulikuwa na dhana zipi zinazohusiana na mpangilio wa masimulizi unaofuata mtiririko halisi wa matukio ya kwenye kipindi cha kati cha huduma ya Yesu?

J: Zifuatazo ni dhana ambazo nilizoea kuzitoa kuhusiana na mfuatano wa matukio.

a) Injili zinafuata mtiririko halisi wa matukio kwenye kipindi cha kati cha huduma ya Yesu. Ingawa kuna baadhi ya mambo ambayo hayafuati mtiririko huo, hakuna sababu ya kudhania hivyo.

b) Vifungu kadhaa kwenye Luka, ambavyo nimeviweka kwenye kipindi cha baadaye cha huduma ya Yesu, vinaweza kuingia hapa.

 

S: Kwenye Mat 12:30, Bart Ehrman anauliza, "Kuna maneno ya Yesu yaliyotafsiriwa kwa njia zinazofanana lakini pia zinatofautiana. Moja wa mifano ninayoipenda sana ya aina hii ni jozi ya maneno haya ni yale yanayohusiana na Mat 12:30 na Mak 9:40. Kwenye Mathayo, Yesu alisema, ‘Mtu asiye pamoja name yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya.' Kwenye Marko, alisema, ‘Asiye kinyume chetu, yu upande wetu.' Je Yesu alisema maneno haya kwa namna zote hizi mbili? Je kuna uwezekano wowote kuwa alimaanisha vitu vyote hivi? Je maneno haya yanaweza kuwa sahihi yote kw wakati mmoja? Au kuna uwezekano kuwa mmoja wa waandishi wa injili alibadilisha maneno?" (Jesus, Interrupted, uk.41).

J: Kwa uwazi kabisa, nashindwa kuelewa kabisa jinsi ambavyo Ehrman anavyoyachukulia maneno haya kwenye injili hizi mbili yanapingana. Kwenye Mat 12:22-37 (inayofanana na Mak 3:20-29), tukio hili linatokea wakati Yesu alipopelekewa mtu aliyekuwa amepagawa mapepo. Baadaye sana, tukio la tofauti kabisa, kwenye Mak 9:38-41, Yesu anaambiwa kuhusu mtu mwingine aliyekuwa akitoa mapepo. Ni kweli alikuwa na uwezo wa kuongea mambo tofauti kwenye siku tofauti. Ehrman anaweza kuwa akifikiri kuwa ni jambo kinzani endapo mtu atakuwa anapingana na Yesu anaweza pia kuwa anapingana na wafuasi wake, au kinyume chake. Lakini alitabiri kuwa wafuasi wake watateswa na kuuawa kwa sababu watesi wao hawamjui Baba au Yesu, kwenye Yoh 16:3. Yesu alisema kwenye Yoh 15:18-21, "Hapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngelikuwa wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu,kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu." Yesu alijifananisha kwa karibu sana na wafuasi wake kwenye Mat 25:34-46 kwenye mfano wa kondoo na mbuzi. Kwenye Yoh 15:1-8 Yesu sisi tu ndani yake kama vile matawi yalivyoungana na mzabibu.

 

S: Kwenye Mak 9:40, maneno haya "Asiye kinyume chetu, yu upande wetu", na "Msimkataze" kwenye Luk 9:50 yanafananaje na Luk 11:23, "Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu?"

J: Kuna majibu mawili tofauti.

Makosa ya wenye kunakiri: Karibu maandishi yote ya Kigiriki yaliyoandikwa kabla ya karne ya nane, kwenye Luk 11:23 yanasomeka "kinyume chenu . . . pamoja nanyi" badala ya "kinyume chetu . . . pamoja nasi." Hata hivyo hakuna sababu ya maneno haya kufanana kwani yalitolewa kwenye nyakati tofauti.

Aina tofauti za watu: Mtajwa kwenye Mak 9:40 na Luk 9:50 alikuwa ni mtu si kwamba alikuwa anataka kutoa mapepo kwa kutumia jina la Yesu, bali pia alikuwa anayatoa. Kinyume chake, katika wakati tofauti kwenye Luk 11:23, Yesu aliwakemea watu waliokuwa wanasema Yesu anatoa mapepo kwa kutumia nguvu za Beelzebuli.

Hata hivyo, mtu aliyekuwa anatoa mapepo kwa jina ka Yesu alikuwa pamoja na Yesu, kwa sababu alimwamini Yesu, ingawa alikuwa mahali tofauti. Leo hii, ni rahisi kufikiri kuwa mtu ni tofauti kwa sababu yuko sehemu tofauti, kanisa tofauti, au ana utamaduni tofauti na anafanya vitu kwa njia tofauti. Hata hivyo, kama mtu huyu ni ndugu au dada wa kweli katika Bwana basi yuko pamojaa na Yesu. Pia, usisahau kuwa watu kutoka utamaduni wetu wenyewe, huenda toka kwenye makanisa yetu wenyewe, wanaoyakataa mambo ya msingi ya Ukristo, wako kinyume cha Kristo, hata kama tutakuwa tunawahurumia itawahurumia.

 

S: Kwenye Mat 14:15-21; Mak 6:30-44; Luk 9:12-17, na Yoh 6:1-14, je Yesu aliwalisha wato 5,000, au 4,000 kama Mat 15:32-38 na Mak 8:2-9 zinavyosema?

J: Wote.

Wanaume 5,000 pamoja na wanawake na watoto (Mat 14:21) walikuwa Wayahudi (Yoh 6:14-15) waliowahi kuwa na Yesu siku moja (Yoh 6:35) na walikaa kwenye majani. Mikate mitano na samaki wawili vilitumika (Mat 14:17). Masazo yalijaa vikapu 12 (Mat 14:20).

Wanaume 4,000 pamoja na wanawake na watoto (Mat 15:38) huenda walikuwa watu wa mataifa, ambao walikuwa na Yesu kwa muda wa siku tatu (Mak 8:2) na walikaa mahali palipokuwa hapana. Mikate 7 na samaki wachache vilitumika (8:5,7). Masazo yalijaza vikapu 7 (Mak 8:8).

Wote wametajwa kwenye Mat 16:7-11, na Mak 6:52. Yesu angeweza kuwahudumia Wayahudi, na watu wa mataifa pia.

Ikiwa tutakazia kulishwa kwa Wayahudi 5,000 kwenye Yoh 6:14-35, au kulishwa kwa watu 4,000 wa mataifa, au wote kama Mat 15:38; 16:7-11 na Mak 6:52, 8:2-8 zinavyosema, tunapaswa kuchagua ama kuamini ama kutokuamini kuwa Yesu wa kwenye injili atatulisha pia milele.

 

S: Kwenye Mat 14:15-21; Mak 6:30-44; Luk 9:12-17, na Yoh 6:1-14, je palikuwa na wanaume tu wakati muujiza wa kulishwa watu 5,000 kwa kutumia mikate mitano na samaki wawili kutoka Mak. 6:44 na Yoh 6:10?

J: Hapana. Hawakuwa wanaume tu. Neno la Kigiriki lililotumika ni andres (andros, umoja) ni lile lile lililotumika kwenye Mak 6:44; Luk 9:14, na Mat 14:21, na kimsingi linamaanisha "mwanaume." Lakini Mat 14:19-21 inasema walikuwa karibu watu 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.

Kwa hiyo, kwenye umati huu wa watu mchanganyiko kuna mambo mawili ambayo yaliza kuwa yametokea:

a) Kulikuwa na karibu idadi sawa ya wanaume na wanawake, na walikaa kwa kufuata familia zao.

b) Kulikuwa na wanaume wengi zaidi kuliko wanawake na watoto. Kumbuka, tofauti na muujiza wa kulishwa kwa watu 4,000, muujiza huu ulitokea kwenye upande wa mashariki wa Bahari ya Galilaya uliokuwa unakaliwa na watu wa mataifa, na Wagiriki hawakuwa wanawathamini sana wanawake. Hivyo inawesekana wengi wa wanawake walibaki nyumbani.

 

S: Kwenye Luk 9:52-53, je Wasamaria walimkataa Kristo na hawakumpokea, au umati mkubwa wa Wasamaria ulikutana na Yesu kwenye Yoh 4:39-40?

J: Mambo yote mawili ni ya kweli kwa njia tatu tofauti.

a) Matukio haya mawili yalitokea nyakati tofauti kwenye huduma ya Yesu. Kukubalika kwake kulitokea mwanzoni mwa huduma, na kukataliwa kulitokea baadaye, walipojua kuwa Yesu alikuwa anaelekea Yerusalemu.

b) Matukio haya yalitokea mahali tofauti, wakati kundi moja la watu, mfano kundi la Waafrika likikubali kitu fulani haimaanishi kuwa kila Mwafrika aliye mahali kokote kule atakukubali kwa namna hiyo hiyo.

c) Lakini, hata miongoni mwa Wayahudi, wako waliomfuata Yesu kwa muda kisha wakaondoka. Yoh 6:66 inasema kuwa baadhi ya wanafunzi wa Yesu waliondoka na hawakumfuata tena. Miongoni mwao wanaweza kuwa Wasamaria na Wayahudi pia.

 

S: Kwenye Mat 16:4 na Mak 8:12, je hakuna ishara itakayotolewa kwa watu, au hakuna ishara itakayotolewa isipokuwa ishara ya Yona kwenye Luk 11:29-30?

J: Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

1. Ingawa Yona alipata muujiza, watu wa Ninawi hawakuuona. Yona hakuwapa watu wa Ninawi ishara zozote za miujiza lakini aliwaambia watu watubu; waliweza tu kumwona Yona na kusikia ujumbe wake. "Ishara" pekee waliyokuwa nayo haikuwa muujiza ambao wangeweza kuuona bali mtu. Yona aliwahubiria watu wa Ninawi, na hili ndili jambo pekee waliloweza kuliona. Tunaweza kusema kuwa ujumbe wa Yona ulithibitishwa na muujiza wa kumezwa kwake na samaki mkubwa na kuweza kuendelea kuishi. Hata hivy, watu wa Ninawi waliweza kusikia tu kuhusu muujiza huo; hawakuuona wao wenyewe.

2. Jambo hili ni tofauti na Kutoka kwa Waisraeli Misri (the Exodus), ambako Waisrali wote waliweza kuliona wingu la kimiujiza kama nguzo wakati wa mchana na moto wakati wa usiku.

3. Yesu alikuja "kwa mtindo wa Yona", si ule wa Kutoka. Yesu hakuja na utukufu wa mbinguni, na ingawa alifanya miujiza iliyouthibitisha ujumbe wake, watu wengi hawakuiona miujiza hiyo, walisikia tu.

Muhtasari: Kutokea ghafla kwa Yesu kunafanana na kwenda kwa Yoha Ninawi. Mara nyingine watu wanapenda kuamini kitu endapo tu ushahidi wake upo katika namna wanayoipenda. Kwa kuwa watu waliowasikia Yona na Yesu, walitakiwa kusikiliza ujumbe na si kufunga macho yao na kushindwa kuona vitu ambavyo hawakuvitarajia.

 

S: Kwenye Mat 16:4, Mak 8:12 na Luk 11:29-30, kwa nini ishara hazitatolewa kwa watu, kwani Yesu alifanya miujiza mingi?

J: Ingawa kila mmoja alisikia miujiza ambayo Yesu aliifanya, watu wengi hawakuona muujiza wowote ule wa Yesu. Wengi wa watu walioiona miujiza mikubwa, kama wa kulisha watu 5,000 waliokuwa wamekaa kwenye majani, kulisha watu 4,000 waliokaa sehemu isiyokuwa na majani, walikuwa ni sehemu kidogo ya watu waliokuwa wanaishi Palestina ya wakati ule.

Wakai ule na hata baadaye, miujiza inasaidia kuimarisha imani, lakini miujiza peke yake huwa haisaidii kumbadilisha mtu kutoka kuwa mtu asiyeamini na kuwa mtu anayeamini, hasa kama mtu huyo hapendi kuamini. Kumbuka kuwa baadhi ya mafarisayo waliuona mkono wa mtu aliyekuwa amepooza ukiponywa mbele ya macho yao wenyewe, lakini bado hawakutaka kumfuata Yesu.

 

S: Kwenye Mat 16:16; Mak 8:29, na Luk 9:20, maneno halisi ya Yesu yalikuwa yapi? Mat 16:16 inasema, "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai." Mak 8:29 inasema, "Wewe ndiwe Kristo." Luk 9:20 inasema, "Wewe ndiwe Kristo wa Mungu."

J: Bila kujali endapo maneno haya yalisemwa awali kwa Kigiriki, au Kiaramu na kutafsiriwa kwenye Kigiriki, waandishi wa injili waliyafafanua, hivyo ingawa tunajua maana ya tamko la Petro, hatuyafahamu maneno halisi.

 

S: Kwenye Luk 18:7, je maombi yanatakiwa yaendelee tu (bila kusimama wala kwisha), au Yesu alikuwa anawapinga watu waliodhani kuwa maombi yao yatasikiwa kwa sababu ya uwingi wa maneno yake kwenye Mat 6:7?

J: Yote ni sahihi. Mungu huangalia nguvu ya maombi yetu, si urefu wake. Tunatakiwa kuomba bila kukoma (1 The 5:17), lakini usifikiri kuwa ni maneno yasiyokuwa na mwisho yenye kusaidia, lakini mioyo yetu. Vivyo hivyo wakati wa Nehemia, walitakiwa kujenga ukuta kwa ajili ya kujilinda, lakini hawakutakiwa kuutegemea ukuta kuwalinda, bali kumtegemea Mungu.

 

S: Kwenye injili, je mpangilio upi wa habari zilizoripotiwa unafuata mtiririko halisi wa matukio kwenye sehemu ya mwisho ya huduma ya Yesu?

J: Ni muhimu kutenganisha kati ya mpangilio unaodhaniwa na mpangilio wenyewe. Kwenye matukio haya 67, tarakimu zinawakilisha matukio ambayo yanatakiwa kuzifuata namba zinazotangulia. Herufi kama a, b, c zinawakilisha matukio ambayo yanaweza kuwa yalitokea kwa kufuata mfuatano wowote ule. Maneno yaliyoandikwa kwa wino mzito yanaonyesha viashiria vya muda, mpangilio, na mahali. Kama kuna mtu anaamini kuwa injili zote ziliandikwa kwa kufuata mtiririkoo halisi wa matukio yaliyoripotiwa ya sehemu hii ya huduma ya Yesu, hataona shida yeyote.

Sehemu ya Mwisho ya Huduma ya Yesu: Mat 17:1-20:34; Mak 9:2-10:52; Luk 9:28-19:28; Yoh 7:10-11:57

L1. Baada ya siku kama nane (au sita) hivi, Yesu alimchukua Petro, Yakobo, na Yohana kwenda kwenye Mlima ambao Sura ya Yesu Ilibadilika (huenda ni Mlima Tabori) [Mat 17:1-8; Mak 9:2-8; Luk 9:28-35].

L2. Msiseme mpaka baada ya kufufuka (Mat 17:9; Mak 9:9-10; Luk 19:36).

L3. Yesu anaongea kuhusu Elia (Mat 17:10-13; Mak 9:11-13).

L4. Siku iliyofuatia, Yesu mvulana aliyekuwa na kifafa ambaye wanafunzi hawakuweza kumponya (Mat 17:14-21; Mak 9:14-29; Luk 9:37-45).

L5. Akiwa Galilaya, Yesu anatabiri tena kuhusu kifo chake (Mat 17:22-23; Mak 9:30-32).

L6a. Akiwa Kapernaumu (kwenye pwani ya kaskazini ya Bahari ya Galilaya), Yesu analipa kodi ya hekalu kwa kutumia sarafu toka kwenye mdomo wa samaki (Mat 17:24-27).

L6b. Wakati ule, wanafunzi walibishana kuhusu mtu aliye mkubwa miongoni mwao (huenda waliwahibishana mara kadhaa) [Mat 18:1-9; Mak 9:33-37; Luk 9:46-48).

L6c. Yohana na wanafunzi wengine wanawaambia watu wengine kuacha kutoa mapepo kwa kutumia jina la Yesu (Mak 9:38-41; Luk 9:49-50).

L6d1. Akiwa njiani kuelekea Yerusalemu, Wasamaria hawakumkaribisha Yesu (Luk 9:51-56).

L6d2. Akiwa anatembea njiani, kujitoa kunapaswa kuwepo kwa wanafunzi: mbweha, wafu, familia (Luk 9:57-62).

L6d3. Yesu awatuma wanafunzi sabini na wawili (Luk 10:1-24).

L7a1. Akiwa Yerusalemu kwenye sikukuu ya vibanda (siku ya tano ya mwezi wa saba), Yesu anakwenda (Yoh 7:10-52).

L7a2. Akiwa Yerusalemu, mwanamke aliyekutwa akizini (Yoh 8:1-11).

L7a3. Ushuhuda wa Yesu ni wa kweli (Yoh 8:12-59).

L7b. Yesu anamponya kipofu, ambaye anakwenda kwa Mafarisayo (Yoh 9:1-41).

L7c1. Yesu anafundisha kuhusu mchungaji (Yoh 10:1-21).

L7c2. Kwenye Sikukuu ya Kutabaruku [majira ya baridi kali] kwenye eneo la hekalu huko Yerusalemu, Yesu alisema, "Mimi na Baba tu umoja" (Yoh 10:22-39).

L7c3. Yesu anakwenda mahali ambako Yohana Mbatizaji alikuwa anabatiza watu (Yoh 10:40-42).

L7d1. Swali la mwanasheria kuwa jirani yangu ni nani (Luk 10:25-28).

L7d2. Mfano wa Msamaria mwema (Luk 10:29-37).

L7d3. [Huenda ilikuwa Bethani ya Uyahudi], Maria aliyejitoa, na Martha mchapakazi (Luk 10:38-42).

L7e. Akiwa Bethani ya Uyahudi, Yesu anamfufua Lazaro kutoka wafu (Yoh 11:1-44).

L7f. Siku moja, Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kusali, akitumia sala ya Bwana (huenda ilikuwa ni mara ya pili) [Luk 11:1-13].

L7g1. Yesu anamtoa pepo bubu, anashutumiwa kushirikiana na Beelzebuli (Luk 11:14-26).

L7g2. Mwanamke anambariki mama wa Yesu, Yesu hakubaliani naye (Luk Lk 11:27-28).

L7h. Makutano walipoongezeka, Yesu alisema watapewa ishara moja tu ya Yona (Luk 11:29-32).

L7i1. Taa ya mwili (Luk 11:33-36).

L7i2. Kwenye nyumba ya Farisayo, Yesu anatoa ole sita (Luk 11:37-53).

L7i3a1. Wakati huo huo, anafundisha kuhusu kufunuliwa kwa mambo yaliyofichika (Luk 12:1-7).

L7i3a2. Kumkiri Yesu mbele ya watu na kumkufuru Roho Mtakatifu (Luk 12:8-12).

L7i3b. Mfano wa tajiri mjinga (Luk 12:13-21).

L7i3c. Mfano wa kuwa tayari kwa ajili ya kurudi kwa bwana (Luk 12:35-48).

L7i3d. Unabii juu ya migawanyikano kwenye familia (Luk 12:49-53).

L7i3e. Kuyatambua majira (Luk 12:54-59).

L7i3f Yesu anawataja Wagalilaya waliouawa wakati mnara wa Siloamu ulipoaguka (Luka 13:1-9).

L7j Kwenye siku ya sabato, Yesu anamponya mwanamke aliye kiwete (Luk 13:10-17).

L6k. Mifano ya punje ya haradali (Luk13:18-21).

L6l1. Akiwa anapita kwenye miji na vijiji, mifano ya mlango mwembamba, na kusikitishwa na Yerusalemu (Luk 13:22-30).

L6l2. Wakati ule, Yesu anaomboleza kwa ajili ya Yerusalemu (Luk 13:31-35).

L6m. Sabato moja kwenye nyumba ya Farisayo mmoja mashuhuri, Yesu anamponya mtu mwenye safura na mfano wa karamu kuu (Luk 14:1-24).

L6n. Wakati makutano wengi walipokuwa na Yesu, alifundisha juu ya gharama kuwa mwanafunzi, kwa mara ya pili: wazazi, mifano wa mnara, mfalme, na chumvi (Luk 14:25-35).

L6o. Mafundisho kuhusu watoto wadogo (Luk 18:10-11).

L6p. Mfano wa kondoo aliyepotea (Mat 18:12-14; Lk 15:1-7).

L6q1. Mfano wa sarafu iliyopotea (Luk 15:8-10).

L6q2. Yesu anaendelea kufundisha, mfano wa mwana mpotevu (Luk 15:11-32).

L6r. Mfano wa wakili mwenye busara (Luk 16:1-15).

L6s. Mafundisho kuhusu kusamehe na mtumwa asiyekuwa na huruma (Mat 18:15-35).

L6t. Mafundisho kuhusu Yohana na sheria (Luk 16:16-17).

L6u. Yesu asafiri kutoka Galilaya kuelekea ng'ambo ya Yordani (Mat 19:1-2; Mak 10:1).

L6v. Mafundisho kuhusu talaka (Mat 19:3-12; Mak 10:2-12; Luk 16:18).

L6w. Mfano wa tajiri na Lazaro (Luk 16:19-31).

L6x. Kwa wanafunzi wake, Yesu anafundisha kuhusu dhambi, mfano wa mti uliopnadwa baharini, na mfano wa wajibu wa mtumwa (Luk 17:1-10).

L6y. Akiwa kati ya Galilaya na Samaria njini kuelekea Yerusalemu, Yesu awaponya wenye ukoma 10 (. . . wale kenda wako wapi?) [Luk 17:11-19].

L6z. Mafarisayo wanauliza ufalme wa Mungu unakujaje (Luk 17:20-37).

L7a. Mfano wa mjane asiyekata tamaa (Luk 18:1-8).

L7b. Mfano wa Farisayo na mtoza ushuru (Luk 18:9-14).

L7c. Watu waliokuwa wanaleta watoto wao kwa Yesu ili awabariki; wanafunzi wanawakataza (Mat 19:13-15; Mak 10:13-16; Luk 18:15-17).

L7d. Tajiri kijana anauliza swali (Mat 19:16-30; Mak 10:17-31; Luk 18:18-30).

L8. Mfano wa wafanyakazi kwenye shamba la mizabibu (Mat 20:1-16).

L9. Akiwa njiani kuelekea Yerusalemu, Yesu anatabiri kifo na kufufuka kwake (Mat 20:17-19; Mak 10:32-34; Luk 18:31-34).

L10a. Mama wa Yakobo na Yohana wanamwomba Yesu (Mat 20:20-28; Mak 10:35-45).

L10b. Yesu anaondoka Yeriko (huenda ni Yeriko ya zamani), Yesu anawaponya vipofu wawili waliopaza sauti zao na kusema, "Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi" (Mat 20:29-34).

L10c. Yesu anaingia Yeriko (huenda ni Yeriko mpya), Yesu anamponya kipofu Bartimayo, aliyepaza sauti na kusema, "Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu" (Mak 10:46-52; Luk 18:35-43).

L11a. Akiwa Yeriko, Yesu anakutana na Zakayo (Luk 19:1-10).

L11b. Akiwa karibu na Yerusalemu (miji miwili iliyofahamika kama ‘Yeriko' ilikuwa karibu kilomita 24-27, au maili 15-17 kaskazini mashariki ya Yerusalemu), Yesu anatoa mfano wa watumwa kumi na mafungu kumi ya fedha (Luk 19:11-28).

L12. Kayafa na baraza la Wayahudi wanapanga kumuua Yesu (Yoh 11:45-53).

L13. Hivyo, Yesu anaondoka na kuelekea kwenye kijiji cha Efraimi (Yoh 11:54).

 

S: Kwenye injili, ni mambo gani ya msingi yanayodhaniwa kuhusiana na mpangilio wa wa masimulizi unaofuata mtiririko halisi wa matukio ya kwenye kipindi cha mwisho cha huduma ya Yesu?

J: Kila kitu kinakuwa na mambo ya msingi yanayodhaniwa, na kama mtu mwingine atatumia mambo hayo hayo ya msingi, ataishia kupata orodha kama hii. Yafuatayo ni mambo ya msingi ambayo yamedhaniwa kwenye mtiririko wa matukio uliotangulia.

a) Injili zote zinafuata mtiririko haliso wa matukio ya kipindi cha mwisho cha huduma ya Yesu. Ingawa kuna uwezekano kuwa mpangilio huu unaweza usiwe unafuata mtiririko halisi, hakuna sababu ya kudhania hivyo.

b) Baadhi ya vifungu vya Yohana, vimewekwa hapa, vingeweza kuwa kwenye kipindi cha kati cha huduma ya Yesu.

c) Matukio yafuatayo yalitokea kipindi kimoja tu: Kugeuka kwa sura ya Yesu, mfalme wa kondoo aliyepotea, tajiri kijana.

d) Kufufuliwa kwa Lazaro, kaka wa Mariamu na Martha, kulitokea karibu wakati ule ule Yesu alipokuwa kwenye nyumba yao.

 

S: Je Mat 19:16-17; Mak 10:18 na Luk 18:19 zinathibitisha kuwa Yesu ni Mungu? (Waislamu wanasema hivi)

J: Hapana, lakini ni vema kuwa tunatambua hapa kuwa Yesu anahusisha mtu anayemwita mwema na maneno kuwa Yesu ni Mungu. Ama:

a) Yesu alikuwa Mungu, na alikuwa anamuuliza mtu huyu kwa nini anamwita mwema isipokuwa anamkiri Yesu kuwa Mungu, au

b) Yesu anakana kuwa yeye ni Mungu kama ilivyodhihirishwa kuwa Yesu hakuwa mwema kabisa.

Jibu haliwezi kuwa maoni haya yote mawili. Je unaafiki?

Je jibu ni lipi basi? Je Yesu alikuwa mwema kabisa (na Mungu) au la?

Je unaamini basi kuwa Yesu hakuwahi kutenda dhambi?

Kwenye Biblia, 2 Kor 5:21, Ebr 4:15, na 1 Pet 1:18-19 zinasema kuwa Yesu hakuwa na dhambi.

Yesu hata aliuliza kwenye Yoh 8:46a, "Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi?"

Yesu alikuwa mwangalifu kwa kutotumia kiurahisi neno "mwema", ingawa alijiita yeye mwenyewe mchungaji mwema kwenye Yoh 10:11.

Kwa Waislamu, Kurani inasema kuwa Yesu alikuwa msafi kwenye Sura 3:45. Hadithi za Kiislamu zinasema Yesu hakuwahi kutenda dhambi yeyote kwenye Sahih Muslim juzuu ya 4 na.64, uk.5837 (uk.1261), Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 38 na.641, uk.426, na Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 10 na.506, uk.324.

 

S: Kwenye Mat 19:16-30; Mak 10:17-31 na Luk 18:18-30, Yesu anasema ni jambo gani hasa lisilowezekana kwa mwanadamu lakini mambo yote (likiwemo hili) yanawezekana kwa Mungu?

J: Kuingia ufalme wa Mungu (wokovu) ni vigumu na pia haiwezekani bila Mungu. Hebu tumwangalie kwanza huyu kiongozi tajiri kijana kisha mambo mengine ye ujumla ili kuona mambo mawili ya kufanya.

Kiongozi tajiri na kijana alionekana mzuri sana mwanzoni, kwa ufahamu wake wa sheria ya Mungu. Lakini alipungukiwa haki inayotakiwa kwenda mbinguni, kwa sababu alionyesha kuwa endapo angetakiwa kuchagua kati ya utajiri wake na kumfuata Yesu, hangekuwa tayari kuuacha utajiri wake.

Jambo la kwanza la kufanya ni kuwa mara nyingi ni vigumu zaidi kwa watu matajiri kuliko watu wengine kuwa na haki ya kutosha kwenda mbinguni, kwa sababu ni vigumu sana kwao kumtumaini Mungu endapo kwa kufanya hivyo itawabidi kuuacha utajiri wao. Abrahamu alikuwa tajiri sasa, na alikwenda mbinguni, hivyo si kwamba tatizo ni utajiri wenyewe. Tatizo ni kupenda fedha ambako ndio shina la maovu yote.

Hata hivyo, kwa kuangalia kwa ujumla zaidi, watu wasiokuwa matajiri nao wana shida pia. Watu wanaweza kutumaini uwezo wao wenyewe, kutamani mazoea yao maovu, kuwa na upendo hafifu, na hata chuki kiasi kwamba kama Yesu angewaita waache mambo hayo na kumfuata yeye wasingependa kuyaacha.

Kwa kweli, jambo la pili la kufanya ni kuwa watu wote ambao wamewahi kuishi, isipokuwa Yesu, wanapungukiwa haki wanayotakiwa kuwa nayo ili kwenda mbinguni. Hata kama Mungu angewasamehe dhambi zao zote za zamani, na kusema "Kuanzia sasa usifanye dhambi tena na utakwenda mbinguni", hata hivyo, bado tusingeweza kwenda mbinguni. Mioyo yetu si mikamilifu; tuna asili ya dhambi, na tunatakiwa kutakaswa.

Hivyo, kwa ajili ya mioyo yetu, hatuwawezi kwenda mbinguni; na kama jambo hili lingekuwa ndio mwisho wa habari yetu, mbingu zisingekuwa na watu. Hata hivyo, jambo lisilowezekana kwa wanadamu linawezekana kwa Mungu. Ingawa mioyo yetu si mikamilifu, tumefanya dhambi wakati ulitangulia, na bado tutafanya dhambi wakati ujao, Mungu ambaye mambo yote yanawezekana kwake, amefanya njia kwa wanadamu wenye dhambi kwenda mbinguni. Njia hiyo ni Yesu Kristo. Ni kama vile mtu aliyekwenda kwa Yesu ili amponye binti yake, na Yesu alimuuliza endapo anaamini. Yule mtu akajibu akasema, "Bwana, naamini. Nisaidie kutokuamini kwangu." Tunatakiwa tuseme ukweli na kuwa waaminifu kabisa kwa Mungu, lakini kuwa waaminifu kwa Mungu kunahusisha kukiri wakati tunapokuwa waongo na wanafiki.

Kiongozi tajiri na kijana angeweza kusema, "Yesu, nasikitika kwa ajili ya uovu wangi, lakini siwezi kuuacha utajiri wangu sasa; ninatumikishwa nao. Nirehemu, nifungue toka kwenye kifungo cha dhambi, na yachukue maisha yangu jinsi yalivyo ili niweze kukufuata wewe." Badala yake, kiongozi tajiri na kijana aliondoka na kuenda zake. Corrie ten Boom ni Mkristo mwanamke aliyenusurika kufa kwenye kambi ya mateka wa Kiyahudi huko Bergen Belsen ambako Wayahudi walifanyishwa kazi nzito wakisubiri kifo chini ya utawala wa Kinazi wa Ujerumani ulioishikilia Ulaya miaka ya 1933-45. Mara baada ya vita, akiwa anaongea kuhusu upendo wa Mungu, mwanaume mmoja alimfuata kumpa mkono. Mwanamke huyu alimtambua kuwa alikuwa mmoja wa walinzi makatili zaidi kwenye makambi ya mateso. Baada ya vita kwisha, mlinzi huyu alikutana na Yesu, hata hivyo Corrie, licha ya maneno aliyokuwa amesema kwa watu wote, hakuweza kumpa mlinzi huyu mkono. Badala yake aliomba kimya, "Yesu, siwezi kumsahau. Nipe msamaha wako." Kisha, kwa namna ya ajabu sana, mkono wake ukatoka na akampa mlinzi yule (The Hiding Place, uk.238).

Kwenye jamii yetu iliyokuwa na mali nyingi, wakati mwingine kama Wakristo tunaweza kusahau kirahisi dhana muhimu ya kumtegemea Mungu tuliko nako. Kama unadhani unaweza kufanya mambo yote bila Mungu, basi malengo unayoweka ni madogo sana. Jambo moja zuri kuhusu watu maskini, ambao hawajui jinsi watakavyokula siku mbili zijazoa, ni kuwa wanajua kwamba kujitegemea halisi ni dhana isiyokuwa sahihi kwao. Ingawa, ukweli ni kwamba kujitegemea ni dhana isiyokuwa sahihi kwa kila mtu.

 

S: Kwenye Mat 20:20, je mama wa Yakobo na Yohana alimwomba Yesu jambo hili, au Yakobo na Yohana ndio waliomwomba Yesu kama Mak 10:35 inavyosema?

J: Mama na watoto wake wa kiume walikwenda kwa Yesu. Kwenye Mat 20:22, Yesu aliwauliza (Yakobo na Yohana) endapo wanaweza kunywea kikombe ambacho atakinywea. Walimjibu kuwa wanaweza.

 

S: Kwenye Yoh 14:2, kwa nini Yesu alikwenda kuandaa mahali kwa ajili yao, kwani mbingu ilikwisha andaliwa kwa ajili yao kabla ya kuwekwa kwa misingi ya dunia kwenye Mat 25:24?

J: Mungu yuko ndani ya muda, na zaidi ya muda. Kabla ya muda kuanza, Mungu alijua nani atakayekwenda mbinguni, jambo ambalo linamaanisha kuwa Mungu alijua kuwa ataandaa mahali kwa ajili yao. Kifo cha Yesu kilihitajika ili kufungua mbingu kwa ajili ya watu wote watakaoenda.

Kama kilinganishi rahisi, wanandoa wanapoasili mtoto, wanatakiwa kuandaa nyumba kwa ajili ya mtoto. Nyumba iliishajengwa, lakini wanandoa wanaweza kununua kitanda cha mtoto, na chakula na huenda hata na mapambo kwa ajili ya kusheherekea kuja kwake.

Isitoshe, 1 Kor 3:11-15 inaonyesha kuwa watu tofauti watapokea thawabu tofauti mbinguni.

 

S: Kwenye Mat 20:29-34, je Yesu aliponya watu wawili vipofu alipokuwa anaondoka kuelekea Yeriko, au mtu mmoja kipofu alipokuwa anaondoka Yeriko kama Mak 10:46-52 inavyosema?

J: Kuna mambo mawili yanayowezakana hapa.

Matukio mawili: Yesu anaweza kuwa alimponya kipofu Bartimayo, na pia aliwaponya watu wengine vipofu kabla au baada ya Bartimayo. Mara baada ya Yesu kumponya angalau mtu mmoja kipofu, ingeshangaza endapo watu wa mji ule wasingejua jambo hili, na mtu mwingine zaidi kipofu asingekwenda kwa Yesu kuponywa. Inawezekana kuwa Yesu aliwaponya hata watu zaidi Yeriko kuliko waandishi wa injili wanavyotuambia. Kama Yesu alimponya mtu mmoja kipofu alipokuwa anaingia Yeriko, na mtu mmoja aliliona tendo hili na akawaambia wengine, unaweza kuwa na uhakika kuwa palikuwa na watu wengine vipofu waliokuwa wakimsubiri alipokuwa anatoka Yeriko.

Tukio moja: Mak 10:46-52 inataja mtu mmoja tu kipofu (Bartimayo). Huenda Marko hakufahamu kuhusu vipofu wengine wawili. Ni kweli kama palikuwa na watu wawili vipofu, mmoja wao aliitwa Bartimayo, basi kusema kuwa palikuwa na kipofu mmoja ni sahihi ila hakutoi undani wote. Angalia swali linalofuatia kwa habari kamili kuhusu miji miwili iliyoitwa Yeriko.

 

S: Kwenye Mat 20:29-34 na Mak 10:34-52, je Yesu alimponya mtu kipofu alipokuwa anaondoka Yeriko, au alipokuwa anaondika kama Luk 18:35 inavyosema?

J: Hili linaweza kuwa tukio moja tu lililotokea wakati Yesu alipokuwa anasafiri kati ya miji miwili inayoitwa Yeriko.

Yeriko ya zamani (Tell es-Sultan) ipo kaskazini magharibi mwa Yeriko ya sasa (er-Riha). Mji huu wa Yeriko uliteketezwa na Yoshua, lakini ulijengwa upya kwenye 1 Fal 16:34. Wayahudi ndio waliokuwa wakazi wengi zaidi wa mji huu wakati wa huduma ya Yesu.

Yeriko ya Agano Jipya (iliyopo Tulul Abu el-'Alayiq) ulikuwa ni mji wa watu wa mataifa zaidi uliojengwa karibu na jumba la msimu wa baridi kali la Herode Mkuu, aliyekufa karibu mwaka 4 KK. Sehemu hii ipo kiasi cha kilomita 1.2 au 1.6 (robotatu ya maili au maili moja) kusini au kusini magharibi mwa Yeriko ya zamani. Jumba la msimu wa baridi kali lilikuwa na mabwawa mawili, bafu kubwa la Kiroma, na mabafu sita ya Kiyahudi ambayo yalikuwwa yanatumika kujitakasa.

Sehemu mbili tofauti za Yeriko zilitajwa pia kwenye vyanzo vingi.

 

S: Kwenye injili, ni mpangilio upi unaofuata mtiririko halisi wa matukio ya Juma la Mateso ya Yesu, juma la mwisho kabla ya Kufufuka kwa Yesu?

J: Ni muhimu kutenganisha kati ya mpangilio unaosemwa kuwa ndio mtiririko halisi na mpangilio ambao ndio mtiririko halisi. Kwa matukio haya 105, tarakimu zinawakilisha matukio ambayo yanatakiwa kufuata namba zilizotangulia. Harufi kama a, b, c zinawakilisha matukio ambayo yangeweza kutokea kwa kufuata mtiririko wowote ule. Maneno yaliyoandikwa kwa wino mzito yanaonyeha viashiria muda, mfuatano, na mahali. Ikiwa mtu anaamini kuwa injili zinafuata mtiririko halisi wa matukio kwenye sehemu hii, hataona shida yeyote.

Juma la Mateso ya Yesu: Mat 21:1-27:66; Mak 11:14-15:47; Luk 19:29-23:56 na Yoh 12:11-19:42

P1. Akiwa Bethani, siku moja kabla kuingia kwa shangwe, Yesu alikwenda kwenye chakula cha jioni kwenye nyunba ya Maiamau, Martha, na Lazaro (Yoh 12:1-12a).

P2. Yesu akiwa Bethfage kwenye Mlima wa Mizeituni (Mat 21:1; Mak 11:1-6; Luk 19:29-34).

P3. Yesu anawaagiza kumleta mwana punda na mamaye (Mat 21:2-6; Mak 11:2-6; Luk 19:29-34).

P4. Wanafunzi wanarudi na punda na mtoto wa punda (Mat 21:7a; Mak 11:7-10; Luk 19:35-35; Yoh 12:14-15).

P5. Kwenye Juma la Mitende, Yesu anaingia Yerusalemu kwa shangwe (Mat 21:7b-11; Mak 11:7-11a; Luk 19:35-44; Yoh 12:12b-19).

P6a. Yesu anatabiri kifo chake, na Baba anaongea kutoka mbinguni (Yoh 12:20-50).

P6b. Yesu analala Bethani (Mak 11:11b).

P6c. [Jumapili au jumatatu au siku zote hizi mbili] Yesu anawafukuza watu wanaobadilisha fedha hekaluni kwa mara ya pili (Mat 21:12-13; Luk 19:45-48).

P6d1. Akiwa hekaluni, Yesu anamponya mtu aliyekuwa kipofu na kiwete (Mat 21:14-16).

P6d2. Yesu analala Bethani (Mat 21:17).

P7. Asubuhi mapema siku iliyofuata [jumatatu au jumanne], akiwa anarudi Yerusalemu, Yesu anaulaani mti mtini (Mak 11:12-14). Kumbuka hii ni safari ya pili ya Yesu kwenda hekaluni kama When Critics Ask, uk.354 -355 inavyosema.

P8. Asubuhi na mapema [jumanne au jumatano], Yesu anaulaani mti mtini kwa mara ya pili (Mat 21:18-19a).

P9a. Mara mti mtini unanyauka (Mat 21:19b-22).

P9b. Mti mtini unanyauka (Mak 11:20-25).

P10. Yesu anaingia hekaluni, anafundisha kuhusu mamlaka (Mat 21:23-32) na anawafukuza watu wanaobadilisha fedha kwa mara ya tatu (Mak 11:15-18). Kumbuka: ingekuwa ajabu endapo Yesu angewafukuza siku moja na kuwaruhusu siku iliyofuata.

P11. Ilipofika jioni, waliondoka mjini (Mak 11:19).

P12. Siku moja akiwa hekaluni [jumanne au jumatano] Yesu anaulizwa kuhusu mamlaka yake (Mak 11:27-33; Luk 20:1-8).

P13. Mfano wa wakulima wabaya (Mat 21:33-46; Mak 12:1-12; Luk 20:9-19).

P14. Yesu anatoa mfano wa karamu ya harusi (Mat 22:1-14).

P15a. Mafarisayo na Maherode wanamuuliza Yesu juu ya kulipa kodi kwa Kaisari (Mat 22:15-22; Mak 12:13-17; Luk 20:20-26).

P15b. Masadukayo wanamuuliza Yesu kuhusu kufufuka (Mat 22:23-33; Mak 12:23-27; Luk 20:27-39).

P16. Baada ya Masadukayo, Farisayo anauliza kuhusu amri iliyo kubwa zaidi (Mat 22:34-40; Mak 12:28-33).

P17a. Hakuna mtu aliyemuuliza Yesu swali lolote tena (Mat 22:46; Mak 12:34; Luk 20:40).

P17b. Wakati Mafarisayo wakiwa pamoja, Yesu anauliza swali kuhusu Zab 110:1 (Mat 22:41-45; Mak 12:35-37; Luk 20:41-44).

P18a. Yesu anawakemea waandishi na Mafarisayo (Mathayo 23; Mak 12:38-40; Luk 20:45-47).

P18b. Yesu anaisifia sadaka ya mjane (Mak 12:41-44; Luk 21:1-4).

P19. Akiwa anaondoka hekaluni, Yesu anatabiri juu ya kubomolewa kwa hekalu (mat 24:1-2; Mak 13:1-2; Luk 21:5-6).

P20. Akiwa Mlima wa Mizeituni, Yesu anafundhisha kuhusu siku za mwisho (Mat 24:3-44; Mak 13:3-37; Luk 21:7-36).

P21. Kila siku hekaluni Yesu anafundisha na kwenda kwenye Mlima wa Mizeituni usiku wote (Luk 21:37-38).

P22. Mifano mitatu ya kurudi kwa Bwana (Mat 24:45-25:30).

P23a. Hukumu ya kondoo na mbuzi kwenye kiti cha enzo cha Yesu (Mat 25:31-46).

P23b. Siku mbili kabla ya Pasaka (jumatano), wakuu wa makuhani na wazee wanapanga kumkamata Yesu (Mat 26:1-5; Mak 14:1-2; Luk 22:1-2).

P24. Akiwa Bethani, siku sita kabla ya Pasaka Yesu anahudhuria karamu iliyoandaliwa kwa heshima yake kwenye nyumba ya Simoni mkoma, ambapo Mariamu alihudumu. Yesu anapakwa mafuta, kwa mara ya pili, na Mariamu panti ya marhamu yenye thamani ya mshahara wa mwaka mzima, kutoka kwenye kibweta cha marhamu. (Kumbuka huu ni mji ambao Lazaro alikuwa anaishi, siyo nyumba). Yuda Iskariote na wanafunzi wanalalamika (Mat 26:6-13; Mak 14:3-9; Yoh 12:1-11).

P25. Yuda anaongea na makuhani (Mat 26:14-16; Mak 14:10-11; Luk 22:2-6).

P26. Siku ya kwanza ya sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu (alhamisi), wanafunzi wanaandaa karamu ya mwisho (Mat 26:17-19; Mak 14:12-16; Luk 22:7-13).

P27. Yesu anaosha miguu ya wanafunzi (Yoh 13:1-18).

P28. Kwenye chumba kikubwa cha juu (Mak 14:15), Yesu na wanafunzi wake wanakula karamu ya mwisho (Mat 26:20-29; Mak 14:17-25; Luk 22:14-23; 1 Kor 11:23-26).

P29. Yesu anasema kuwa Yuda atamsaliti (Yoh 13:18-28a).

P30. Amri mpya ya Yesu, kupendana (Yoh 13:31-35).

P31. Wakati wa karamu ya mwisho inaendelea, Yuda Iskariote anaondoka (Yoh 13:28b-30).

P32. Ama wakati wa karamu ya mwisho au muda mfupi baadaye, mabishano mengine kuhusu nani aliye mkubwa (Luk 22:24-30).

P33a1. Baada ya Yuda kuondoka, wakiwa njiani kuelekea kwenye Mlima wa Mizeituni, Yesu anatabiri kuwa Petro atamkana mara tatu (Mat 26:30-35; Mak 14:26-31; Luk 22:31-38; Yoh 13:36-38).

P33a2. Kwenye bustani ya Gethsemane kwenye Mlima wa Mizeituni (Mat 26:36-46; Mak 14:32-43a; Luk 22:39-46).

P33b. Kutoka kwenye karamu ya mwisho hadi kwenye Mlima wa Mizeituni, Yesu anaongea (Yoh 14:1-16:33).

P34. Maombi ya Yesu kabla ya kukamatwa kwake (Yoh 17:1-26).

P35. Baada ya Yesu kumaliza kuomba, yeye na wanafunzi wanavuka kijito Kedroni na wanakwenda kwenye kijisitu cha mizeituni (Yoh 18:1).

P36. Kukamatwa kwa Yesu (Mat 26:47-56; Mak 14:43b-52; Luk 22:47-53; Yoh 18:2-11).

P37. Wanakwenda kwenye nyumba ya Anasi, baba mkwe wa Kayafa, kuhani mkuu (Luk 22:54; Jn 18:12-13).

P38. Yesu anaelekezwa aende kwenye nyumba ya Kayafa (Yoh 18:24). Kwenye Mat 26:56-57 na Mak 14:51-53 hakuna maelezo ya tukio linalolitangulia hapo juu, badala yake vifungu hivyo vinataja tukio hili tu.

P39a1. Kwenye/karibu na ua wa kuhani mkuu, Yesu anashitakiwa na baraza la Wayahudi (Mat 26:57-68; Mak 14:53-65; Luk 22:66-71; Yoh 18:12-14; 18:19-23).

P39b1. Kwa sababu "mwanafunzi huyu" [Yohana] alifahamika na kuhani mkuu, alikwenda ndani ya ua. Kisha alitoka nje na kuongea na michana/mjakazi/mtumishi wa kike aliyekuwa zamu na kumuingiza Petro kupitia kwenye mlango (Yoh 18:15-16).

P39b2. Shitaka la kwanza: Kwenye ua, msichana/mjakazi/mtumishi mmoja wa kike wa kuhani mkuu aliyekuwa mlangoni, alikjwenda kwa Petro (Mathayo), alimsogelea (Marko) na alimwangalia Petro kwenye mwanga wa moto, na kumwambia Petro kuwa alikuwa na Yesu. Petro alikuwa anajipasha moto kwenye ua (Mat 26:69; Mak 14:66-67; Luk 22:54-56; Yoh 18:17a).

P39b3. Kukana kwa mara ya kwanza: Petro alimkana Yesu akisema, "Si mimi" (Yoh 18:17), "Ee mwanamke, simjui" (Luk 22:57) "Sijui usemalo" (Mat 26:70) au "Sijui wala sisikii unayoyasema wewe" (Mak 14:68) mbele ya wote (Mat 26:70.

P39b4. Mzunguko wa pili wa mashitaka: Kisha Petro alikwenda mlangoni (Mathayo), na msichana [allu] mwingine aliuambia umati uliokuwepo, "Huyu alikuwapo pamoja na Yesu Mnazareti" (Mat 26:71). Petro alishutumiwa, "Wewe nawe u mmoja wao" (Luk 22:58). Mjakazi alipomwona tena Petro alisema kwa umati uliokuwepo, "Huyu ni mmoja wao" (Mak 14:69). Petro aliulizwa, "Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmojawapo?"(Yoh 18:25).

P39b5. Kukana kwa mara ya pili: Petro alisema kwa kuapa, "Si mimi" (Yoh 18:25), "Ee mtu [anthrope], si mimi" (Luk 22:58), "Simjui mtu huyu" (Mat 26:72), na alimkana Yesu kwa mara ya pili.

P39b6a. Mzunguko wa tatu wa mashitaka: karibu saa moja baadaye (Luk 22:59) watu waliokuwa wamesimama karibu [kundi dogo la watu?] walisema Petro alikuwa mmoja wao na walisema lafudhi ya Kigalilaya (Mat 26:73; Mak 14:70b; Luk 22:59).

P39b6b Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ndugu wa mtu aliyekatwa sikio lake na Petro, alimwambia Petro kuwa alimwona kwenye kijisitu cha mizeituni (Yoh 18:26).

P39b7. Kukana kwa mara ya tatu: Petro alilaani na kuapa, "Ee mtu, sijui usemalo" (Luk 22:60), "Simjui mtu huyu" (Mat 26:74) au "Simjui mtu huyu mnayemnena" (Mak 14:71; Yoh 18:27), na akamkana Yesu mara ya tatu. Mara, walipokuwa bado wamo ndani ya nyumba, jogoo aliwika. Yesu aligeuka na kumwangalia Petro (Mat 26:74-75; Mak 14:71-72; Luk 22:60-62; Yoh 18:27).

P39c. Akiwa Akeldama, Yuda anajinyonga. Kamba ilikatika ama kabla au baada ya kufa (Mat 27:1-10; Mdo 1:18-19).

P39a2. Askari wanamdhihaki, wanampiga, na kumfunika uso Yesu (Luk 22:63-65).

P40. Asubuhi, baraza la Wayahudi lilimuuliza Yesu (au lilimuuliza tena) "Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie." Wakafanya uamuzi (Mat 27:1; Mak 15:1; Luk 22:66-71).

P41. Kwa sasa ilikuwa mapema asubuhi, na Yesu akiwa amesindikizwa na makuhani aliondoka kwenye nyumba ya Kayafa na kwenda kuhukumiwa na liwali wa Roma, Pontio Pilato (Mat 27:2; Mak 15:1; Luk 23:1; Yoh 18:28-38).

P41b. Usiku kabla ya kwenda kuhukumiwa na Pilato, mke wa Pilato aliota ndoto iliyomwonya liwali kutokumfanyia Yesu kitu chochote chenye kumhukumu (Mat 27:19).

P42. Yesu anahukumiwa na Pilato (Mat 27:11-14; Mak 15:1-15; Luk 23:1-6; Yoh 18:28-37).

P43. Pilato anamtuma Yesu kwa Herode (Luk 23:7-11a).

P44a. Herode anamrudisha Yesu kwa Pilato (Luk 23:11b-12).

P45. Yesu anarudishwa kwa Pilato (Luk 23:13-16).

P46. Pilato anasema hana hatia na damu ya Yesu, anawasihi watu waliokuwepo na anamfungua Baraba (Mat 27:15-26; Luk 23:17-25; Yoh 18:38-40).

P47. Askari wa Kiroma wanampiga viboko Yesu na kumdhihaki na kumvisha kanzu la zambarau na taji la miiba (Mat 27:27-31a; Mak 15:16-20a; Yoh 19:1-3).

P48. Pilato anawaendea Wayahudi tena (Yoh 19:4-15).

P49. Yesu anapelekwa kusulubiwa (Mat 27:31b; Mak 15:20b; Luk 23:26a; Yoh 19:16).

P50. Yesu [mwanzoni] anaubeba msalaba wake mwenyewe (Yoh 19:17a).

P51.[Kisha]Simoni Mkirene anabebeshwa msalaba wa Yesu (Mat 27:32; Mak 15:21; Luk 23:26b).

P52. Yesu anasema, "Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu . . ." (Luk 23:28-31).

P53a. Ilipofika saa tatu [asubuhi] huko Golgotha, Yesu anasulubiwa (Mat 27:33; Mak 15:22, 25; Luk 23:33; Yoh 19:16b-22).

P53b. Anuani ya mashtaka iliandikwa kwa lugha tatu na kuwekwa juu ya kichwa cha Yesu (Mat 27:37; Mak 15:26; Luk 23:38).

P53c. Wahalifu wawili wanasulubiwa mmoja upande wa kushoto na mwingine kulia kwa Yesu (Mat 27:38; Mak 15:27; Luk 23:32-33).

P54a. Yesu anasema, "Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo" (Luk 23:34a)

P54b. Kuna watu waliompa Yesu divai iliyochanganyika na nyongo (Mat 27:34; Mak 15:23).

P54c.Nguo za Yesu zinagawanywa kwa kupiga kura (Mat 27:35-36; Mak 15:24; Luk 23:34b; Yoh 10:23-24).

P55a. Yesu asema, "Mama, tazama, mwanao . . . [mwana], tazama, mama yako" (Yoh 19:25-27).

P55b. Watu wengine wanasema, "Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe . . ." (Mat 27:40-43; Mak 15:29-30; Luk 23:35a).

P55c. Makuhani nao wamdhihaki Yesu (Mak 15:31-32; Luk 23:35b).

P55d. Askari wamdhihaki Yesu akiwa msalabani (Luk 23:36-37).

P55e.1 Mwizi aliyekuwa upande wa kushoto wa Yesu (Mat 27:44; Luk 23:39).

P55.e.2 Mwizi aliyekuwa upande anamtetea Yesu (Luk 23:40-43a).

P55.e.3 Yesu asema, ". . . Leo hivi utakuwa pamoja nami peponi" (Luk 23:43b).

P55.f. Yesu asema, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha" (Mat 27:45-47; Mak 34-36).

P55.g. Yesu asema, "Naona kiu" na kwa mara ya pili akapewa iliyokuwa kwenye sifongo (Mat 27:48; Jn 19:28-29).

P55.h Baadhi ya watu wanasubiri kuona kama Elia atakuja (Mat 27:49).

P55.i. Giza latanda kuanzia saa ya sita mchana hadi ya tisa alasiri (Mak 15:33; Luk 23:44-45a).

P56a. Yesu asema, "Imekwisha" (Yoh 19:30).

P56b. Muda mfupi kabla ya kufa Yesu asema, "Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu" (Luk 23:46a).

P57a. Yesu anakufa (Mat 27:50; Mak 15:37; Luk 23:46b).

P57b. Wakati ule, pazia la hekalu lilipasuka katikati (Mat 51a; Mak 15:38-39, Luk 23:45b; pia Thales aliyeandiaka mwaka 52 BK).

P57c. Tetemeko la ardhi lilitokea, makaburi yalifunguka na wafu wakatokea (Mat 51b-53).

P58a. Askari wakata miguu ya watu waliosulubiwa pamoja na Yesu, lakini hawakuikata miguu ya Yesu (Yoh 19:31-37).

P58b. Akida asema, "Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki" (Luk 23:47-49).

P58c. Akiba asema, "Hakika huyu alikuwa mwana wa Mungu" (Mat 27:54; Mak 15:39).

P58d. Wanawake wengi walikuwa wakitazama (Mat 27:55-56).

P59. Ilipofika jioni, Yusufu wa Arimathayo amwomba Pilato mwili wa Yesu (Mat 27:57-58; Yoh 19:38).

P60a. Kwenye kaburi la Yusufu wa Arimathayo, Yusufu na Nikodemo wauzika mwili wa Kristo na jiwe kubwa liliwekwa kwenye mlango wa kaburi (Mat 27:59-61; Mak 15:42-47; Luk 23:50-54; Yoh 19:39-42).

P60b. Kabla ya sabato, wanawake watayarisha manukato na marhamu (Luk 23:55-56).

P60c. Pilato akubali walinzi wawekwe kulilinda kaburi la Yesu (Mat 27:62-65).

P61. Wakuu wa makuhani na Mafarisayo walitia jiwe la kaburini muhuri na kuweka walinzi (Mat 27:66).

 

S: Kwenye injili, ni mambo gani ya msingi yaliyodhaniwa kuhusiana na mpangilio wa masimulizi unaofuata mtiririko halisi wa matukio ya kwenye Juma la Mateso ya Yesu?

J: Mtu yeyote atakayetumia mambo haya yanayodhaniwa, anaweza kupata mpangilio unaofanana sana na mtiririko wa matukio halisi ya Juma la Mateso ya Yesu.

a) Yesu alifanya huduma siku ya jumatano

b) Yesu aliondoka Yerusalemu usiku zaidi ya mmoja.

c) Yesu aliwafukuza watu waliokuwa wanabadilisha hela hekaluni angalau mara mbili.

d) Yesu aliulaani mti mtini siku moja kabla haujakauka, na siku ya pili alifanya hivyo pia.

e) Kila kitu kwenye injili kinafuata mtiririko halisi wa matukio ya Juma la Mateso ya Yesu, isipokuwa Mak 22:46; Luk 22:54-62, na Luk 23:38.

 

S: Kwenye Mat 21:1-3, Mak 11:4-7, Luk 19:30, na Yoh 12:13-15, je Yesu alipanda punda au mwana punda?

J: Maelezo haya si jibu la swali hili: Kuna watu wanaodhani kuwa huenda alikuwa mnyama mmoja au wawili, kwani neno la Kigiriki kai linaweza kumaanisha "na" au "hata/yaani." Neno la Kiebrania kwenye Zak 9:9 pia linamaanisha "na" au "au." Hata hivyo, kama maandishi ya sehemu inayofuata yanavyoonyesha, kulikuwa na wanyama wawili.

Jibu la swali: Kulikuwa na wanyama wawili, kwani wakati Yesu anaingia Yerusalemu kwa shangwe kwenye Mat 11:4-7 inavyosema, punda na mwanawe walikuwepo wote hapo. Haikosi mtoto wa punda alikuwa mdogo sana, kwa sababu alikuwa hajapandwa na mtu bado. Inaelekea punda hawakuwa wanatenganishwa na wanao, bali waliletwa pamoja. Katika mtazamo wa kawaida watu walikuwa wanafanya hivyo ili kuwatuliza wanyama. Kama mwana punda alikuwa na mamaye, na mama punda hakujali kuwa mwanawe anapandwa, basi hata mwana punda hakujali pia. Kuna njia gani nzuri zaidi ya kumwongoza ndama, ambaye ni mnyama mwoga, kuliko kumfanya amfuate mama yake?

Nje ya Biblia, Justin Martyr (aliyeandika karibu mwaka 138-165 BK) pia aliongelea kuhusu kuletwa kwa punda na ndama wake kwenye Dialogue with Trypho the Jew sura ya 53 (ANF juzuu 1, uk.222).

 

S: Kwenye Mat 21:12-13, Mak 11:11-17, na Luk 19:37-46, je Yesu aliwafukuza watu waliokuwa wanabadilisha fedha hekaluni siku ya jumapili au jumatatu?

J: Mat 12:12-13 na Luk 19:37-46 havisemi bayana endapo Yesu aliwafukuza watu waliokuwa wanabadilisha fedha siku ile ile aliyoingia Yerusaalemu kwa shangwe (jumapili) au siku iliyofuata. Hata hivyo, Mak 11:11-17 inaonyesha kuwa ilikuwa siku iliyofuata.

 

S: Kwenye Mat 21:12-13, Mak 11:12-19, na Luk 19:43-48, Yesu aliwezaje kupindia meza za wabadilisha fedha hapa, kwani alifanya mwanzoni mwa huduma yake kwenye Yoh 2:13-19?

J: Yesu aliwafukuza watu waliokuwa wanabadilisha fedha mara mbili, kwa sababu maoni yake kuhusu biashara hii hekaluni hayakubadilika. Yesu hakufanya hivi mara ya kwanza na kuangalia tu mara nyingine alipowaona wabadilisha fedha hekaluni.

Hapakuwa na jambo moja tu lililokuwa na walakini bali matatu kuhusiana na wabadilisha fedha hekaluni:

1. Hawakuwa watumwa wa Mungu, lakini walikuwa wakipata hela ndani ya hekalu la Mungu.

2. Ingawa watu wangeweza kuwa wanakuja na fikra za kuabudu, walianza kufikiria biashara ya kubadilishana bidhaa, na mambo mengine yahusuyo fedha katika "kulipia ibada kwa Mungu."

3. Zaidi ya hapo, walikuwa wanawaibia watu kwa kutoza bei kubwa. Kwa mfano, hawakuwaruhusu watu kutumia hela za kawaida kununua wanyama hawa. Watu walitakiwa kubadilisha hela ili kupata sarafu maalumu za hekaluni zilizotumika kununua wanyama.

 

S: Kwenye Mat 21:12-19, je Yesu aliulaani mti mtini siku moja baada ya kulisafisha hekalu, au kabla kama Mak 11:12-14, 20-24 inavyoelekea kumaanisha?

J: Yesu aliulaani mti mtini baada ya kuwafukuza watu waliokuwa wanabadilisha fedha hekaluni, kama Injii ya Mathayo inavyosema. Injili ya Marko haina maelezo mengi, lakini nayo inasema, "Hata asubuhi yake" kuonyesha kuwa ilikuwa baada.

 

S: Kwenye Mat 22:37 na Mak 12:29-30, je kuitii amri kubwa kuliko zote kunaleta umoja wa dini za hapa duniani, kama baadhi ya wafuasi wa ‘New Age' wanavyodai?

J: Hapana. Kwanza kabisa, hapa pana amri mbili siyo moja. Pili, amri ya kwanza, kumpenda Mungu kwa vitu vyote alivyo navyo mtu, ni kubwa kuliko amri ya pili, kuwapenda watu wengine kama nafsi yako mwenyewe. Tofauti na jinsi wafuasi wa New Agers wanavyoamini, dini zote HAZIPELEKI watu kwa Mungu. Kwenye hukumu ya mwisho, Yesu atawaambia watu waliodai kumfuata lakini hawafanyi hivyo, "Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu" (Mat 7:23). Hutapenda Yesu akwambie "Ondoka kwangu."

 

S: Kwenye Mathayo 24-25 na Mak 13:5-30, je mambo haya tatatimia lini?

J: Mambo haya yatatimia kwa kipindi kirefu. Kwenye Mat 24:2, hekalu lilibomolewa mwaka 70 BK. Sehemu nyingine zinasubiri kuja kwa Yesu kwa mara ya pili. Matukio ya kwenye nyakati za mwisho "yapo karibu sana kutimia", ikimaanisha kuwa Biblia haisemi kuwa yatatokea siku za karibuni, bali yanaweza kutokea wakati wowote ule.

 

S: Kwenye Mat 24:19 na Mak 13:17, kwa nini itakuwa vigumu sana kwa wanawake wajawazito na kina mama wanyonyeshao?

J: Kunaweza kuwa na sababu mbili. Kwanza, kukimbia kwa haraka wakati wa safari ngumu ni jambo gumu kwa wanawake wajawazito na wale walio na watoto wadogo. Pili, inaweza kuwa vibaya sana kwa kina mama watakaokutwa, kuhusiana na mambo yatakayotokea kwa watoto wao wadogo, au wale walio bado kuzaliwa.

 

S: Kwenye Mat 24:24 na Mak 13:22, inawezekanaje kuwa hata wateule wadanganywe?

J: Wateule si waumini. Badala yake wao ni watu watakaokuwa waumini. Ni kweli kuwa kama mtoto akifa na kwenda mbinguni, hata yeye atakuwa muumini mbinguni.

Mistari hii inasema wateule wanaweza kudanganywa, lakini haisemi kuwa watadanganywa wakati wote. Binafsi namfahamu mtu ambaye alikuwa muumini wa kweli, aliyejiunga na kanisa wa, na muda mfupi baadaye aliondoka akauacha Umormoni na kuurudia Ukristo.

 

S: Kwenye Mat 24:28, je Yesu alikuwa anauongelea "mwili uliokufa", au ulikuwa ni mwili tu, uliokuwa hai au umekufa, kama Kigiriki cha kwenye Luk 17:37 kinavyosema?

J: Hakuna ushahidi kuwa mwandishi yeyote kati ya hawa wawili alinukuu maneno yote aliyoyasema Yesu; mara nyingi waandishi walikuwa wakifafanua. Huenda Yesu hakutumia neno lolote kati ya haya mawili ya Kigiriki, kama inavyoelekea, Yesu alitumia Kiaramu.

 

S: Kwenye Mat 24:29, je Yesu atakuja mara baada ya dhiki kuu, au patakuwa na "muda wa watu wa mataifa" kama Luk 21:24, 27 inavyoonyesha?

J: Yote. Dhiki kuu itakuwa mwishoni mwa kipindi cha watu wa mataifa.

 

S: Kwenye Mat 24:30-31 na Mak 13:26-27, je wateule watakusanywa kabla ya Yesu kurudi kwenye mawingu kwa utukufu mkubwa, au baada ya hapo?

J: Ingawa kurudi kwa Yesu kumetajwa kwanza kwenye vifungu vyote hivi viwili, hakuna kifungu kinachotoa mfuatano wa matukio haya.

 

S: Kwenye Mat 24:34 na Mak 13:30, kutatokea kitu gani kabla ya kizazi kupita?

J: Kwanza, jambo ambalo siyo jibu la swali hili, kisha jibu.

Jambo ambalo siyo jibu: Yesu alisema maneno haya karibu mwaka 33 BK. Kwenye fikra za Kiebrania, kizazi kilikuwa karibu miaka 40. Kusulubiwa, kufufuka, kupaa mbinguni kwa Kristo kungetokea muda mfupi baadaye, na kubomolewa kwa hekalu la Yerusalemu kungetokea mwaka 70 BK, muda ambao haukuzidi miaka 40. Wakristo ambao ni Wapreteristi (Wakristo wanaoamini kuwa baadhi ya nabii za mwisho wa dunia zilitimia katika karne ya kwanza ya kifo cha Yesu) kwa kiasi wanafuta maoni haya. Hata hivyo, Yesu alisema "Hayo yote", jambo ambalo linamaanisha kuwa ni pamoja na nabii za kuja kwake mara ya pili.

Jibu la swali: Jambo hili yaelekea kuwa kosa la kunakiri kwani maneno ya Kigiriki "kizazi" na "mbari/jamii" yanatofautiana kwa konsonati moja tu. Yesu alisema kuwa jamii ya Kiyahudi haitapita kabla ya kurudi kwa Kriso kwa mara ya pili.

 

S: Kwenye Mat 24:42 na Mak 13:35-37, ni wakati gani Wakristo wanatakiwa kuanza kuangalia ishara za kuja kwa mara ya pili kwa Kristo?

J: Yesus aliamuru kuangalia kuanzia mara moja. Hivyo, kanisa lilipaswa kuwa liwe linaangalia kuanzia miaka 2,000 iliyopita. Dhana hii, inayoitwa "kurudi kuliko karibia kwa Kristo", kunahimiza kuwa tuwe macho wakati wote, kwa kuwa hatujui siku wala saa, Mungu ametuagiza ili tuwe makini na neno lake.

 

S: Kwa nini Mat 26:6-13, Mak 14:1-11 na Yoh 12:1-11 zinatofautiana sana na Luk 7:36-50 kuhusu Yesu kupakwa mafuta?

J: Luk 7:36-50 inaripoti tukio tofauti. Kwa ufasaha, Luka anaripoti mwanamke mwenye dhambi kupaka mafuta miguu ya Yesu akiwa kwenye nyumba ya Farisayo muda mfupi baada ya wanafunzi wa Yohana Mbatizaji kumuuliza Yesu kuwa lini atajidhihirisha kuwa masihi. Vifungu vitatu vingine vinaripoi Mariamu Magdalena akimpaka Yesu mafuta kwenye nyumba ya mwenye ukoma aliyeponywa, huku Lazaro akiwepo, muda mfupi kabla ya Pasaka.

Miongoni mwa watu wa kwanza kujibu swali hili alikuwa Augustino wa Hippo (mwaka 354-430 BK) kwenye Harmony of the Gospels kitabu cha 2 sura ya 79:154 (NPNF1 juzuu ya 6, uk.173-164).

 

S: Kwa nini Mat Mt 26:6-13 inasema kichwa cha Yesu kilipakwa mafuta, wakati Yoh 12:1-11 inasema kuwa ni miguu?

J: Mariamu Magdalene alimpaka mafuta kwanza kisha mtu mwingine.

 

S: Kwenye Mak 14:1, je Mariamu alimpaka Yesu mafuta siku mbili kabla ya, au siku sita kabla kama Yoh 12:1 inavyosema?

J: Yote. Tukio hili moja limethibitishwa kuwa lilitokea siku ya 8 ya mwezi wa Nisani, ambayo ni siku mbili kabla ya kuanza sherehe ya siku nne ya Pasaka, ambayo ilikuwa inakamilishwa na mlo wa Pasaka, kama Kut 12:1-11 inavyonyesha.

 

S: Kwenye Mat 26:17, Mak 14:12, Luk 22:1, na Yoh 13:1-2, je Karamu ya Mwisho ilikuwa usiku wa ijumaa au alhamisi?

J: Makisio ya watu mbalimbali yanazitaja siku mbalimbali kutoka jumatano hadi jumamosi. Kwa muhtasari, siku za jumatano na jumamosi haziwezi kuwemo. Siku ya ijumaa inaendana vizuri na mtiririko halisi wa matukio, lakini alhamisi nayo pia inafaa. Hata hivyo, Wakristo wa awali wanasema ilikuwa ijumaa, isipokuwa Origen, aliyesema kuwa ilikuwa ama ijumaa ama siku iliyotangulia.

Justin Martyr (mwaka 151-155 BK) Yesu alisulubiwa siku moja kabla ya jumamosi [Ijumaa] na alifufuka siku moja baada ya jumamosi [Jumapili] (First Apology of Justin Martyr sura ya 67, uk.186.

Victorinus wa Petau (aliyeuawa kwa ajili ya imani yake mwaka 304 BK) "Siku ya sita [yaani Ujumaa], . . . Katika siku hii kwa ajili ya mateso ya Bwana Yesu, ama tunaweka kituo kwa Mungu ama tunafunga. Siku ya saba . . ." (On the Creation of the World, uk.341).

Petro wa Alexandria (mwaka 306, 285-311 BK) inaongelea siku ya nne na kuwa Yesu aliteswa siku ya sita [Ijumaa] kwa ajili yetu. Kisha inasema, "Lakini ya Bwana tunaosherehekea ni siku ya furaha, kwani katika siku hiyo alifufuka tena, siku hiyo tumeipokea kama desturi kutokupiga goti" (Canonical Epistle, Canon 15, uk.278).

Origen (mwaka 225-254 BK) "Yeye aliyeongelewa na manabii, lakini pia na mataifa ya kipagani, kwamba alisulubiwa jana au siku iliyotangulia alikufa kwa hiari kwa ajili ya wanadamu" (Origen Against Celsus kitabu cha 1 sura ya 31, uk.409).

Hata hivyo, kati ya waandishi 80 au zaidi baada ya Biblia na kabla ya Nikea, waandishi watatu wenye wazo moja si wengi. Tazama majadiliano kwenye swali lililotangulia. Tazama Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.375-376 kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Mat 12:40, je Yesu alikuwa kaburini siku tatu mchana na usiku, au alifufuka siku ya tatu kwenye Mak 8:31, au katika siku tatu kwenye Mak 14:58 na Yoh 2:19 au siku ya tatu ni leo kwenye Luk 24:21?

J: Baada ya siku tatu ni msemo wa Kiebrania uliokuwa unafahamika sana kwenye Biblia unaomaanisha sehemu au siku nzima ya hizo tatu.

Usiku na mchana vinachukuliwa kuwa sehemu moja. Rabi Eleazar ben Azariah (karne ya 1 BK) anasema, "Mchana na usiku ni kipindi kimoja, "Onah" [sehemu ya muda], na sehemu ya muda ni muda wote" (Mishnah, Jerusalem Talmud: Shabbath, Suraya 9, kufungu cha 3, Babylonian Talmud: Pesahim 4a).

Sehemu ya siku inachukuliwa kuwa siku nzima. Licha ya nukuu iliyotangulia, Rabi Simeon ben Gamaliel pia aliongelea jambo hili na watu wengine. "Na kipindi cha muda [Onah] kina urefu gani? - Rabi Simeon ben Gamaliel alieleza: Usiku na nusu ya siku. Lakini je ni lazima kipindi hiki kiwe kirefu namna hiyo? Si lazima ila haifanani na maelezo haya yafuatayo: Ikiwa kishinikizo vishinikizo vya zabibu vya mtu ni vichafu na alitaka kuandaa mvinyo wake na mafuta kwa usafi, atapaswa kufanyaje? Atasuza vibao, vitawi na vyombo vya kukandia" (Babylonian Talmud Tractate Niddah folio ya 65a.

Kuna watu waliojaribu kusema kuwa onah ilimaanisha tu siku za unajisi za mwanamke, lakini nukuu iliyotangulia inaonyesha kuwa onah ni kipindi cha ujumla cha muda.

Mara nyingi muda wenye kuhusisha vipindi zaidi ya kimoja siku hizi. http://www.apologeticspress.org/apcontent.aspx?category=6&article=756 inasema kuwa hata siku hizi mtu akipanga chumba kwenye usiku, na asiondoke muda wa kundoko ukifika, atatakiwa kulipa siku mbili nzima.

Mfano wa kibiblia ni matumizi ya Law 12:2-3. Unasema kuwa watoto wa kume wa Kiyahudi wanatakiwa kutahiriwa siku ya nane. Hivyo kama mvulana wa Kiyahudi alizaliwa jumatatu, anatahiriwa lini? Atatahiriwa jumatatu juma linalofuata. Vipi kama alizaliwa jumatatu saa 5:59 uskiu? Bado atatahiriwa jumatatu juma linalofuata. Hivi ndivyo kuhusisha vipindi zaidi ya kimoja vya muda kulivyo.

Ifuatayo ni mifano mingine tisa kutoka kwenye Biblia inayohusu kuhusisha vipindi zaidi ya kimoja vya muda.

1. Kwenye Mwa 42:17, Yusufu aliwafunga kaka zake muda wa siku tatu. Lakini kwenye mstari wa 18, aliwatoa kumi yao siku ya tatu.

2. Rehoboamu kwenye 2 Nya 10:5, aliwaambia watu, "Mnirudie baada ya siku tatu." Lakini kwenye 2 Nya 10:12, watu walirudi "siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru."

3. Kwenye 1 Sam 30:12, mtumwa wa Kimisri aliyekuwa anaumwa alimwambia Daudi kuwa hakula chakula chochote au kunywa kiasi chochote cha maji siku tatu mchana na usiku. Lakini hakuna mtu ambaye angeweza kuendelea kuishi jangwani bila kunywa kiasi chochote cha maji kwa masaa 72. Bila shaka mtumwa huyu alimaanisha sehemu ya siku tatu.

4. Kwenye Est 4:16, Esta aliwaagiza watu kuomba kwa ajili yake, "muda wa siku tatu, usiku wala mchana", naye pia angefanya hivyo hivyo. Lakini Est 5:1 inasema "Siku ya tatu" Esta aliandaa karamu, kwa hiyo huu ni muda unaofana na huo hapo juu.

5. Mat 27:62b-63a wakuu wa makuhani na Mafarisayo walimwambia Pilato, "Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema alipokuwa akali hai, Baada ya siku tatu nitafufuka. Basi amuru kwamba kaburi lilindwe salama hata siku ya tatu."

6. Yesu alipokuwa anaongelea kifo chake alisema, "siku tatu mchana na usiku" (Mat 12:40), ". . . baada ya siku tatu kufufuka" (Mak 8:31), ". . . katika siku tatu" (Mak 14:58; Yoh 2:19), ". . . leo ni siku ya tatu" (Luk 24:21).

7. Hivyo, "siku tatu mchana na usiku" (Mat 12:40; Yon 1:17) ni sawa na "siku ya tatu" (Mat 16:21; 17:23; 20:19 na Luk 13:32. Pia ni sawa na "ni siku ya tatu" (Luk 24:21).

8. Lakini hakuna jambo lolote maalumu kuhusu namba tatu hapa. Misemo, "siku saba" na "siku ya saba" inaweza kutumiwa kwa kubadilishana pia. Kwenye 1 Fal 20:29a, Biblia inasema, "Wakatua kuelekeana muda wa siku saba. Ikawa siku ya saba vikapigwa vita."

9. Msemo "siku tatu zilizopita" (Mdo 10:30) unamaanisha sehemu za siku nne (Mdo 10:3, 9, 23, 24).

 

S: Kwenye Luk 22:3-4, 7, je shetani alimwingia Yuda wakati alipokwenda kwa wakuu wa makuhani kumsaliti Yesu, au ilikuwa wakati wa Karamu ya Mwisho wakati Yesu alipompa mkata kwenye Yoh Jn 13:27?

J: Yote yalitukia. Shetani alimwingia Yuda wakati Yuda ameamua koungea na makuhani kuhusu kumsaliti Yeu, na shetani alimwingia Yuda tena wakati Yuda aliporudi kwa wakuu wa makuhani kuwaambia mahali ambako Yesu atakuwa.

 

S: Kwenye Mat 26:34, Mak 14:30-71, na Luk 22:34, je Petor alimkana Yesu mara ngapi, na jogoo aliwika mara ngapi?

J: Mat 26:34, Luk 22:34, na Yoh 13:38 zinasema kuwa kabla jogoo/wimbi hajawika (mara zisizotajwa) Petro atamkana Yesu mara tatu. Mak 14:30 inasema kuwa kabla jogoo hajawika mara 2, Petro atamkana Yesu mara 3.

1. Kukana kwa mara ya kwanza kupo kwenye Mat 26:70; Mak 14:68, na Luk 22:57.

2. Kukana kwa mara ya pili kupo kwenye Mat 26:72; Mak 14:70, na Luk 22:58.

3. Kukana kwa mara ya tatu kupo kwenye Mat 26:74; Mak 14:71, na Luk 22:60.

Jogoo aliwika mara ya pili kwenye Mat 26:75; Mak 14:72, na Luk 22:60. Maandiko hayasemi bayana endapo jogoo aliwika mara zote mbili baada ya Petro kumkana Yesu mara ya tatu, au endapo jogoo aliwika mara moja kabla ya, na mara ya pili baada ya Petro kukana kwa mara ya tatu. Kwa namna yeyote ile, haijalishi.

 

S: Kwenye Mat 26:40, 42, 44 na Mak 14:27, 40, 41, kwa nini wanafunzi walilala, kwani Yesu aliwaambia bayana kabisa kuwa wasifanye hivyo, bali wakeshe na wamwombee?

J: Hawakupaswa kulala. Wanafunzi wanaweza kuwa walichoka sana baada ya msongo wa mawazo ya kufahamu kuwa viongozi walitaka kumkamata Yesu. Huenda walifikiri kuwa bustani ilikuwa mahali salama, na kwa sababu ya kuwa kwenye mandhari salama walichoka.

Yesu hata hakupata msaada wa maombi yao na kujishughulisha kwao, bali kukoroma kwao.

 

S: Kwenye Mat 26:69-75; Mak 14:66-72; Luk 22:54-62, na Yoh 18:15-18, 25-27, je unawezaje kulinganisha masimulizi haya manne hapa, hasa linalohusu kukana kwa mara ya pili?

J: Hakuna shida endapo utakumbuka kuwa makutano huwa hawawi kimya. Kwanza, hebu tuangalie mfuatano wa matukio, kisha tuyaondoe maelezo yasiyokuwa sehemu ya jibu, ndipo tutoe jibu.

Mfuatano wa matukio:

1. Kwa sababu "mwanafunzi huyo" [Yohana] alifahamika na kuhani mkuu, aliingia katika behewa la kuhani mkuu. Kisha alitoka nje tena na kungea na kijazazi aliyekuwa zamu wakati ule alimleta Petro kupitia mlangoni (Yoh 18:15-16).

2. Shitaka la kwanza: Akiwa behewani, mmoja wa vijakazi wa kuhani mkuu aliyekuwa mlangoni, alimjia (Mat 26:69), alikwenda karibu naye (Mak 14:66) na alimwangalia Petro kwenye mwanga wa moto, na kumwambia Petore kuwa alikuwa na Yesu. Petro alikuwa anajipasha moto behewani (Mat 26:69; Mak 14:66-67; Luk 22:54-56; Yoh 18:17a).

3. Kukana kwa mara ya kwanza: Petro alikana akisema, "Ee mwanamke, simjui" (Luk 22:57), "Sijui usemalo" mbele yao wote (Mat 26:70) [Mat 26:70; Mak 14:68; Luk 22:57; John 18:17].

4. Mzunguko wa pili wa mashitaka: Kisha Petro alitoka nje hadi ukumbini, na binti [allu] mwingine aliuambia umati uliokuwepo, "Huyu alikuwapo pamoja na Yesu Mnazareti" (Mat 26:71). Petro alishutumiwa, "Wewe nawe u mmoja wao" (Luk 22:58a). Kijakazi alipomwona Petro tena, aliuambia umati uliokuwepo, "Huyu ni mmoja wao" (Mak 14:69). Petro aulizwa, "Wewe nawe, je! Hu mwanafunzi wake mmojawapo" (Yoh 18:25a).

5. Kukana kwa mara ya pili: Petro aliapa na kusema, "si mimi" (Yoh 18:25b), "Ee mtu [anthrope], si mimi" (Luk 22:58b), "Simjui mtu huyu" (Mat 26:72), na akamkana Yesu mara ya pili (Mak 14:70a).

6a. Mzunguko wa tatu wa mashtaka: Baada ya karibu saa moja (Luk 22:59), watu waliosimama karibu [kundi dogo la watu?] walisema kuwa Petro alikuwa mmojawapo na kuwa ana lafudhi ya Kigalilaya (Mat 26:73; Mak 14:70b).

6b Ama kabla ama baada ya 6a, mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ndugu wa mtu ambaye sikio lake lilikatwa na Petro, alimpinga Petro kuwa alimwona kwenye kijisitu cha mizeituni (Yoh 18:26).

7. Kukana kwa mara ya tatu: Petro alaani na kusema, ". . . sijui usemalo" (Luk 22:60), ". . . simjui mtu huyu" (Mat 26:74). Kisha Petro amkana Yesu kwa mara ya tatu (Mak 14:71-72; Yoh 18:27). Mara, walipokuwa bado wapo kwenye nyunba, jogoo aliwika. Yesu alimwangalia Petro (Mat 26:74-75; Mak 14:71-72; Luk 22:60-62; Yoh 18:27).

Kitu gani siyo jibu la swali hili:

Mfuatano tofauti si jibu, kwa sababu masimulizi ya injili yanatumia maneno kama "baadaye", "baada", na "saa moja baadaye."

Kukana zaidi ya mara tatu ni karibu haiwezekani, kama mtu mmoja alivyopendekeza, lakini hakuna sababu ya lazima ya Yesu kusema kuwa Petro atamkana mara tatu na ilikuwa zaidi ya mara tatu.

Jibu la swali: (Umati hauko kimya)

Baada ya Petro kumkana Yesu kwa mara ya kwanza, muda mfupi baaday kijakazi wa pili aliuambia umati kuhusu Petro. Behewa lilikuwa ndani ya nyumba, na huenda halikuwa kubwa sana. Je unategemea kijakazi wa kwanza kukaa kimya? – kuna uwezekano mkubwa kuwa sivyo hivyo. Alirudia maneno aliyomwambia Petro. Je unategemea umati ungekaa kimya baada ya kusikia mashtaka makubwa namna hii? – si rahisi sana. Mtu mwingine hakumshutumu Petro, lakini alimuuliza endapo alikuwa na Yesu. Hii ndiyo sababu ingawa vijakazi hawa walimshutumu Petro, yeye alimjibu mwanamke.

Vivyo hivyo, kuhusu kukana kwa mara ya tatu, je unategemea mtu auambie umati, lakini pasiwe na mtu yeyote kwenye kwenye umati wa kusema kitu chochote? Isitoshe, mambo haya mawili yaliyosemwa, huenda palikuwa na mambo mengine zaidi yaliyosemwa pia.

 

S: Kwenye Mak 15:25, je Yesu alisulubiwa saa tatu, au mashtaka yake yalikuwa saa sita kama Yoh 19:14 inavyosema?

J: Kwanza, jambo si sehemu ya jibu la swali, kisha jibu.

Jambo ambalo si sehemu ya jibu la swali: Kama ambavyo Eusebius na watu wengine walivyosema, namba tatu na sita za Kigiriki zilitofautiana kwa mstari mmoja tu, hivyo huenda lilikuwa kosa la kunakiri. Hili si jibu kwani sehemu inayofuata inaonyesha kwa nini nyakati hizo mbili ni tofauti.

Jibu la swali:

Marko alitumia siku ya Kiyahudi inayoanza saa 12 asubuhi, hivyo Yesu alisulubiwa karibu saa 3 asubuhi; Yohana, ambaye kimsingi alikuwa akiwaandikia watu wa mataifa, alitumia siku ya Kiroma kwenye Yoh 1:39; 4:6; 19:14, ambayo ilianza saa 6 usiku, hivyo mashtaka yalianza karibu saa 12 asubuhi.

Kama jambo la kuzingatia kihistoria, mtaalamu wa mambo ya anga Claudius Ptolemy (karne ya 2 BK) alianza kila nusu ya siku saa 6 usiku na saa 6 mchana, na yaelekea hii ndiyo sababu ya Waingereza wanaigawa siku asubuhi na mchana, yaani A.M na P.M.

 

S: Mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anasema kuwa Yesu alikuwa mtabiri wa kuangamizwa kwa ulimwengu (alisistizia mwisho wa ulimwengu) kwenye Marko, lakini siyo Yohana (Jesus, Interrupted, uk.81)

J: Yesu alikuwa mtabiri wa kuangamizwa kwa ulimwengu (alizungumzia mwisho wa ulimwengu), kwenye injili tatu: Mathayo 24-25, Marko 13, na Luk 17:20-37. Inafahamika kwa ujumla kuwa Injili ya Yohana iliandikwa baada ya injili nyingine. Injili ya Yohana ina urefu karibu sawa na injili nyingine. Mtume Yohana anatoa maelezo kuhusu mahubiri ambayo hayamo kwenye injili nyingine, lakini anaelekea kuwa hakupenda kurudia mambo ambayo yameongelewa vizuri kabisa na injili nyingine. Ni kweli kuwa, kwenye Biblia, kitabu chenye habari nyingi zaidi za utabiri wa kuangamizwa kwa ulimwengu ni Ufunuo wa Yohana, kilichoandikwa na Mtume Yohana.

 

S: Kwenye Mat 26:14-16; Mak 14:43-45; Luk 22:1-6 na Yoh 18:2, Ehrman anafikiri kuwa kitendo cha Yuda kuwaambia Wayahudi mahali alikokuweko Yesu hakikuwa cha muhimu sana; badala yake watu wengine waliwaambia Wayahudi Yesu alijifanya kuwa mfalme wa Wayahudi, na walingeweza kutumia jambo hilo kumuua. Ehrman anakiri kuwa hii "ni tafsiri isiyokuwa ya ajabu zaidi." [Vipi kuhusu kuingia kwa Yesu Yerusalemu kwa shangwe?] (Jesus, Interrupted, uk.170-171).

J: Huyu ni mtu pekee ambaye nimewahi kumsikia mwenye kutafsiri jambo hili kwa namna hii isiyo ya kawaida. Ehrman anasema viongozi wa Kiyahudi wangeweza kumfuata Yesu na kumkamata, lakini hawakuwa na mashtaka makubwa ya kutosha kuwafanya Waroma wamhukumu. Hivyo kimsingi Ehrman anasema kuwa ilikuwa muhimu kwa viongozi wa Kiyahudi: 1) kuthibitisha kuwa Yesu alidai kuwa mfalme, na b) kuweza kumshika Yesu wakati makutano hawangeweza kumlinda.

Lakini vipi kuhusu matawi ya mitende na kuingia Yerusalemu kwa shangwe? Jambo hilo tayari lingewapa sababu ambayo wangeweza kuitumia kumshtaki. Kuhusu kumfuata Yesu wakati alipokuwa anaondoka kwa wafuasi wake kila usiku bila kuonekana walihitaji mpelelezi, mtu ambaye angejichanganya miongoni mwa wafuasi wake na kutoa taarifa kwao. Viongozi wa Kiyahudi walikuwa na mpelelezi: Yuda.

 

S: Kwenye Mat 26:26-29 na Mak 14:22-23, je Yesu mwenyewe alikuwa mkate na kunywa kikombe wakati wa Karamu ya Mwisho?

J: Ndiyo. Yesu alikuwa pamoja nao kwa mujibu wa Luk 22:15-16. Lingekuwa jambo la ajabu sana kwa wanafunzi kula mlo kamili wakati Yesu hajala kitu chochote.

 

S: Kwenye Mat 26:26-29; Mak 14:17-26; Luk 22:15-38; Yoh 13:3-29 na 1 Kor 11:24-25, Yesu alisema kitu gani hasa kwenye Karamu ya Mwisho?

J: Hakuna habari inayoeleza maneno hasa yaliyosemwa na Yesu wakati huo.

Yafuatayo ni mambo tunayoweza kuyaona

Kabla ya Karamu

Yesu aliwaosha wanafunzi wake miguu na aliongea kuhusu utumishi (Yoh 13:3-20).

Maneno aliyosema kwanza

"Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu" (Luk 22:15-16). Maneno haya yanaweza kuwa yalisemwa pia kabla au baada ya maneno aliyosema mara ya tano.

Maneno aliyosema mara ya pili

"Amin, nawaambia, Mmoja wenu atanisaliti (Mat 26:21).

"Amin, nawaambia, Mmoja wenu, naye anakula pamoja nami, atanisaliti" (Mak 14:18).

"Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti" (Yoh 13:21b).

Maneno aliyosema mara ya tatu

"Yeye aliyetia moko wake pamoja nami katika kikombe, ndiye atanisaliti . . ." (Mat 26:23-24).

"Ni mmoja wa hao Thenashara, ambaye achovya pamoja nami katika kombe. Kwa maana Mwana wa Adamu aenda zake kama ilivyoandikwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu; ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa" (Mak 14:20b-21).

Yesu alijibu, "Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge" (Yoh 13:26a).

Maneno aliyosema mara ya nne

"Wewe umesema" (Mat 26:25).

Maneno aliyosema mara ya tano

"Uyatendayo yatende upesi" (Yoh 13:27f).

Maneno aliyosema mara ya sita

"Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja" (Luk 22:17b-18).

Maneno aliyosema mara ya saba

"Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu" (Mat 26:26).

"Twaeni; huu ndio mwili wangu" (Mak 14:22).

"Huu ndi mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu" (Luk 22:19b).

"Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu" (1 Kor 11:24).

Maombi

Alimshukuru Mungu kwa ajili ya kikombe (Mat 26:27).

Maneno aliyosema mara ya nane

"Nyweni nyote katika hiki; kwa maana ndio damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa indoleo la dhambi. Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu" (Mat 26:27b-29).

"Hii ndio damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu" (Mak 14:24b-25).

"Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, imwagikayo kwa ajili yenu. Walakini, tazama mkono wake yeye anayenisaliti upo hapa pamoja nami mezani, Kwa kuwa Mwana wa Adamu aenda zake kama ilivyokusudiwa; lakini, ole wake mtu yule amsalitiye" (Luk 22:20b-22).

"Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu" (1 Kor 11:25b).

Mabishano kuhusu mtu mkubwa zaidi (Luk 22:25-31).

Petro anaambiwa kuwa jogoo atawika baada yay eye kumkana Yesu mara tatu (Luk 22:34).

Majadiliana kuhusu mikoba a mapanga (Luk 22:35-38).

Waimba wimbo (Mat 26:30; Mak 14:26).

 

S: Kwenye Mat 26:26-28; Mak 14:22-24; Luk 22:19-21 na 1 Kor 11:23-26, mwandishi mwenye kushuku alisema kuwa Karamu ya Mwisho iliyoelezwa kwenye Biblia ni ya uongo kabisa, kwa sababu Wayahudi hawakuipenda dhana ya kushiriki "mwili na damu", hivyo sio tu kuwa Yesu alifahamu jambo hili bali pia wanafunzi wake na Wayahudi wengine wangekasirishwa na jambo hili na wangeyakataa mafundisho yake. Je kuna jambo lolote linaloweza kuwa limesababisha madai haya?

J: Hapana, sijawahi kusikia madai kuwa Karamu ya Mwisho ni ya uongo. Hata hivyo, hebu na tuangalie jambo hili.

Kama Wayahudi wote hawakuyakubali, vipi kuhusu Paulo ambaye mwanzoni alikuwa Farisayo? Kwanza, hakukataa alipokuwa Mkristo, na pia aliwafundisha watu wengine, wakiwemo Wayahudi.

Wakati wa Pasaka, damu ya mwana kondoo iliwekwa kwenye miimo ya milango, kwa hiyo Wayahudi walifahamu kafara ya damu na kafara ya wana kondoo.

Yohana Mbatizaji alimwita Yesu Mwana Kondoo wa Mungu anayechukua dhambi ya ulimwengu kwenye Yoh

1:29.

Jambo hili linaonekana kama madai ya karne ya 20 yasiyokuwa na mandhari ya kihistoria. Kwanza wanatakiwa kuyaangalia kwenye Talmudi (sheria za kijamii na kidini na mapokeo yasiyothibitishwa vya Kiyahudi yenye kuhusisha Mishna na Gemara), maandiko ya Kiyahudi ya baadaye, maandiko ya awali nay a baadaye ya kikristo, maandiko ya Kiroma, au mahali pengine, angalau ushahidi wa namna fulani kuwa Wayahudi hawakukubaliana na jambo hili, Wakristo hawakufanya hivi, n.k. Mtu anaweza kudai kuwa mahali halisi alikotokea Yesu ni New Zealand, lakini kutoa ushahidi halisi watu watamwamini naye pia?

Kwa vyovyote vile, ufuatao ni ushahidi mbali ya Biblia kuwa Karamu ya Mwisho ni tukio halisi. Maelfu ya Wakristo wa awali walikufa kwa ajili ya imani yao. Walishtakiwa kwa kutokumwamini Mungu (kwa sababu hawakuiamini miungu ya Kiroma), na kuwa wala nyama ya binadamu (maoni potofu yatokanayo na kula na kunywa mwili na damu vya Yesu wakati wa Karamu ya Mwisho). Kwa nini basi washutumiwe kwa uongo kuwa wanakula nyama ya binadamu kama hawakushiriki Karamu ya Mwisho?

Ignatius, mwanafunzu wa Mtume Yohana aliyekufa kabla ya mwaka 116 BK, anaongelea kuwa Karamu ya Mwisho kwenye kazi yake Letter to the Romans sura ya 7, uk.77. "Ninapenda mkate wa Mungu, mkate wa mbinguni, mkate wa uzima, ambao ni mwili wa Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye baadaye alikuja kuwa mzao wa daudi na Abrahamu; na ninapenda kunywa kikombe cha Mungu, yaani damu yake, ambacho ni upendo usiohakibika na uzima wa milele."

"Angalia basi, iwe Ekaristi moja tu. Kwa sababu kuna mwili mmoja wa Bwana wetu Yesu Kristo na kikombe kimoja [kuonyesha] umoja wa damu yake" (Ignatius, Letter to the Philadelphians, sura 4, uk.81).

Justin Martyr kwenye kazi yake First Apology (mwaka 147-151 BK) sura ya 66, uk.185, "Na chakula hiki kinaitwa miongoni mwetu Eucharistia [Ekaristi], ambacho hakuna mtu anayeruhusiwa kushiriki isipokuwa yeye anayeamini kuwa mambo tunayofundisha ni ya kweli, na yeye aliyeoshwa kwa utakaso wa ondoleo la dhambi, na kuzaliwa upya, na kuishi kama Kristo alivyoagiza. Kwa sababu hatupokei vitu hivi kama mkate wa kawaida na kikombe cha kawaida; lakini kwa namna hiyo hiyo kama Kristo Mwokozi wetu, akisha kufanyika mwili kwa neno la Mungu, alikuwa na mwili na damu kwa ajili ya wokovu wetu, hivyo kwa namna hiyo hiyo tumefunzwa kuwa chakula kilichobarikiwa kwa maombi ya neno lake, na kutokana na hicho damu na mwili wetu hubadilishwa na kustawishwa, ni mwili na damu ya Yesu vilivyofanyika mwili."

 Irenaeus (mwaka 182-188 BK) kwenye kazi yate Irenaeus Against Heresies kitabu cha 5 sura ya 2, uk.528 aliandika, "Lakini kama hii haikufikia wokovu, basi Bwana hakutukomboa kwa damu yake, wala kikombe cha Ekaristi si ushirika wa damu yake, wala mkate tuumegao si ushirika wa mwili wake."

Hivyo, huenda

a) Yesu alifanya Karamu ya Mwisho kweli, au

b) Mathayo, marko, Luka, Paulo, Ignatius, Justin Mfia dini, Irenaeus, na waandishi wote wa kale wa kikristo walikosea.

c) Hawakuliandika jambo hili; badala yake jambo hili limekuwa likiongezwa kwenye maandiko miaka hii yote.

Ili kukabiliana na pingamizi c), tunahitaji kujua tarehe za maandishi ya kale zaidi yaliyokuwa na aya hizi zinazoongelewa. Zifuatazo ni aya ambazo zinataja bayana wakati wa Karamu ya Mwisho damu na mwili wa Yesu.

Mat 26:26-28

p45 Chester Beatty I (ina injili nne na Kitabu cha Matendo) [mwaka 100-150 BK]. Awali, hati hii ya maandishi ya kale ilidhaniwa kuwa iliandikwa karne ya 2 au 3 BK) [Mat 20:24-32; 21:13-19; 25:41-26:39].

p37 (=Ann Arbor 1570) Mat 26:19-52 [iliandikwa katikati ya karne ya 3]

Vaticanus (mwaka 325-350 BK) na Sinaiticus (iliandikwa mwaka 340-350 mwaka) ina injili yote ya Mathayo.

Alexandrinus [A] (iliyoandikwa karibu mwaka 450 BK) ina Mat 25:7 hadi mwisho tu.

Mak 14:22-24

Vaticanus [B] (iliyoandikwa mwaka 325-350 BK), Sinaiticus [Si] (iliyoandikwa mwaka 340-350 BK), na Alexandrinus [A] (iliyoandikwa karibu mwaka 450 BK) ina injili yote ya Mathayo.

Luk 22:19-21

p75 Bodmer makaratasi ya mafunjo 14/15 (sehemu kubwa ya Luka na Yohana) Ina Luk 3:18-22; 3:33-4:2; 4:34-5:10; 5:37-6:4; 6:10-7:32; 7:35-39,41-43; 7:46-9:2; 9:4-17:15; 17:19-18:18; 22:4-24:53. Inachukuliwa kuwa iliandikwa mwaka 175-200 BK, au mwaka 175-225 BK. Lakini, mwandiko wake unafanana sana na hati nyingine, Papyrus Fuad XIX, inayofahamika kuwa iliandikwa mwaka 145-146 BK.

Vaticanus [B] (iliyoandikwa mwaka 325-350 BK), Sinaiticus [Si] (iliyoandikwa mwaka 340-350 BK), na [A] (iliyoandikwa karibu mwaka 450 BK) ina injili yote ya Luka.

1 Kor 11:23-26

p46 Chester Beatty II (iliyoandikwa mwaka 100-150 BK) Ina 1 Kor 1:1-9:2; 9:4-14:14; 14:16-15:15 na 15:17-16:22.

Vaticanus [B] (iliyoandikwa mwaka 325-350 BK), Sinaiticus [Si] (iliyoandikwa mwaka 340-350 BK), na Alexandrinus [A] (iliyoandikwa karibu mwaka 450 BK) ina 1 Korintho yote.

 

S: Kwenye Mat 26:27b-29, Mak 14:24b-25, Luk 22:20b-22, na 1 Kor 11:25b, je walikunywa kikombe baada ya mkate, au kabla ya mkate kama Luk 22:17b-18 inavyoonyesha wazi?

J: Yote. Wakati wa Pasaka ya Wayahudi, vikombe vinne vilinywewa nyakati mbalimbali kwenye mlo. Kikombe cha mwisho, baada ya mlo, kilikuwa ni pale Yesu aliposema, "Hii ni damu yangu ya agano jipya . . ." Hata kama mtu hafahamu desturi za Kiyahudi bado ataona jibu, kwani Luka 22 inataja kikombe mar azote kabla ya mkate na baada ya mkate.

 

S: Kwenye Luk 22:31, 34, je Yesu alisema Petro atamkana wakati wa Pasaka, au watakapokuwa wameondoka kama Mat 26:34, Mak 14:30, na Yoh Jn 13:38 zinavyosema?

J: Maneno haya yanaweza kuwa yalimshangaza sana Petro, huenda alifikiri kuwa hakusikia vizuri, kama Yesu asingeyarudia baada ya Pasaka. Isitoshe, Maandiko hayasemi pia kuwa Yesu alisema maneno haya mara mbili tu.

 

S: Kwenye Mat 26:57-68 na Mak 14:53-65, je Yesu aslishtakiwa usiku, au asubuhi kama Luk 21:54-71 na Mat 27:1, 2, 11-26 zinavyosema?

J: Yote, kwa sababu kulikuwa na mashtaka yaliyoendeshwa na baraza kuu la Wayahudi (Sanhedrini), na yale yaliyoendeshwa na Pilato.

Mashtaka yaliyoendeshwa na baraza kuu la Wayahudi kwenye Mat 26:57-68 na Mak 14:53-65 yalianza katikati ya usiku na yaliisha kulipokuwa kunakucha. Isitoshe, sheria za Kiyahudi hazikuruhusu kuendesha mashtaka usiku.

Luka hasemi kitu chochote kuhusu mashtaka, isipokuwa alipokuwa anaongelea Petro kusimama nje. Yesu aliingia kwenye nyumba ya kuhani mkuu, na kisha makuhani walikuja kutoka ndani ya nyumba.

Jogoo aliwika muda mfupi kabla ya jua kuchomoza kwenye Mat 26:74-75, Mak 14:27, na Luk 22:60-62.

Kisha kulipopambazuka kwenye Mat 27:1; Mak 15:1 na Luk 22:66.

Kisha Yesu alishtakiwa na gavana wa Kiroma Pontion Pilato kwenye Mat 27:1-2, 11-26; Mak 15:1-5 na Luk 23:1-5. Angalia pia swali linalofuata.

 

S: Kwenye Mat 26:57-68, Mak 14:53-65 na Luk 22:60-62, palikuwa na mfuatano gani wa matukio kabla ya mashtaka kweney baraza kuu la Wayahudi?

J: Huu ndio mfuatano.

1. Kwanza, walikwenda kwenye nyumba ya Anasi, baba mkwe wa Kayafa kuhani mkuu mara baada ya Yesu kukamatwa Gethsemane (Luk 22:54; Yoh 18:12-13).

2. Ama kwenye Yoh 18:24 au mapema, Yesu alitumwa kwenye nyumba ya Kayafa. Mat 26:56-57 na Mar 14:51-53 hazitoi maelezo yaliyotangulia na zinasema tu kuhusu kwenda kwenye nyumba ya Kayafa.

3. Petro anamkana Yesu mara moja (Mat 26:60; Mak 14:68; Luk 22:57 na Yoh 18:17).

4. Muda mfupi baadaye, Petro alimkana Yesu mara ya pili (Mat 26:71; Mak 14:69; Luk 22:58; Yoh 18:25).

5. Karibu saa moja baadaye, Petro alimkana Yesu mara ya tatu. Walipokuwa bado wamo ndani ya nyumba jogoo aliwika (Mat 26:74; Mak 14:71-72; Luk 22:59-62 na Yoh 18:27).

6. Kulipopambazuka, baraza kuu la Wayahudi lilimuuliza Yesu (au lilimuuliza tena) "Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie." Na wakafanya uamuzi (Mat 27:1; Mak 15:1; Luk 22:66-71).

7. Kufikia wakati huu ilikuwa asubuhi na mapema, na Yesu, akiwa anafuatana na makuhani, aliondoka kwenye nyumba ya Kayafa na kwenda kushtakiwa kwa gavana wa Kiroma Pilato (Mat 27:2; Mak 15:1; Luk 23:1 na Yoh 18:28-38).

8. Pilato alimtuma Yesu kwa Herode kwenye Luk 23:7-11a.

9. Herode alimtuma Yesu tena kwa Pilato kwenye Luk 23:11b-12.

10. Usiku uliokuwa umetangulia, mke wa Pilato aliota ndoto yenye kumwonya Pilato asishiriki kumhukumu Yesu (Mat 27:19).

11. Pilato aliwauliza kama walitaka Barnaba au Yesu afunguliwe (Mat 27:15-27; Luk 23:18-25; Yoh18:39-40).

 

S: Kwenye Mat 27:2, kwa nini Pontio Pilato anaitwa gavana, wakati yeye hasa ni liwali?

J: Liwali (praefectus) lilikuwa ni jina bayana zaidi la gavana wa eneo dogo lililokuwa gumu kulitawala.

 

S: Kwenye Mat 27:2, 11-26, kwa kuwa Pilato alifahamika nje ya Biblia kuwa mtawala katili na dhalimu, kwa nini injili zinmwonyesha Pilato kuwa mnyonge na mwenye kutaka kutenda haki?

J: Kuna maelezo mawili ya nyongeza.

Msingi usiokuwa imara: Huenda tabia ya Pilato ilibadilika baada ya mwaka 33 BK, kwani wakati huu Pilato alitambua kuwa uhusiano wake na mfalme ni dhaifu sana. Pilato aliamuru ngao zenye jina la mfalme ziwekwe jumba la gavana Yerusalemu. Wayahudi walilalamika kwa mfalme wa Roma, na Tiberio mwenyewe alimuamuru Pilato kuondoa ngao hizo.

Jambo la pili lenye kuonyesha fikra za kutokuwa salama lilikuwa kwamba Pilato alipewa madaraka kupitia ushawishi wa mnasihi wake, Sejanus, mtu aliyekuwa anawapinga Wayahudi. Sejanus aliuawa na Tiberio tareha 9 Oktoba, 31 BK, na Pilato huenda alisikia habari hizo kufikia mwaka 33 BK. Kabla ya hapo, Tiberio hakusita kuwaadhibu Waroma wenzake kwa kujipatia mali kwa nguvu na kutaka kupindua serikali. Pilato mwenyewe aliondolewa madarakani mwaka 36/37 BK.

Pande mbili: kwa nyongeza, Expositor's Bible Commentary juzuu ya 8, uk.559-560 pia inaitaja sababu ya pili. "Kisaikolojia, mtu ambaye ndani mwake ni mnyonge, hana usalama, mbinafsi, anapopewa madaraka, ana uwezekano wa kuwa mkandamizaji, katili na asiye fikiria hisia za wengine. Kwa maneno mengine, tabia ya Pilato haikubadilika, ukweli ni kwamba alikuwa tu anaonyesha upande mwingine. Ingawa Pilato alionekana kama anamtetea Yesu kwa namna fulani, hakuwa hivyo kwa kweli, kama ambavyo mateso na kusulubiwa kwa Yesu kunavyoonyesha. Badala ya kumtetea Yesu, Pilato alikuwa akipingana na baraza kuu la Wayahudi.

Pontio Pilato alikuwa na mashaka. Baada ya Tiberio kumuondoa madarakani mwaka 36/37 BK, Pilato alijiua kwa mujibu wa Eusebius.

 

S: Kwenye Mat 27:2-14; Mak 15:2-15; Luk 23:1-24 na Yoh 19:1-15, kuna ushahidi gani nje ya Biblia kuwa Pilato ni mtu halisi aliyewahi kuishi duniani?

J: Kuna aina sita zinazojitegemea za ushahidi nje ya Biblia.

1. Mwana historia wa Kiroma ambaye hakuwa Mkristo, Tacitus (mwaka 100 BK), kwenye Annals 15:44 aliandika, "Kristus, ambaye kutokana na yeye [Wakrtisto] wanaitwa, aliuawa tokana na hukumu ya gavana Pontio Pilato wakati Tiberio alipokuwa mfalme."

2. Tunayo sarafu iliyotolewa na gavana wa Kiroma, Pontio Pilato.

3. Maandishi yenye kumtaja Pontio Pilato yalipatikana kwenye ukumbi wa maonyesho kwenye mji wa pwani wa Kaisaria mwaka 1961. Sehemu zilizopo zinasomeka hivi:

Kwa watu wa Kaisaria

Tiberieum

Pontio Pilato

Liwali wa Yuda

4. Philo Myahudi pia alisema kuwa Pontion Pilato alileta ngao za dhahabu zenye jina la Mfalme Tiberio na kuzitungika kwenye jumba la Herode. Wayahudi walikasirishwa, na kulalamika kwa Tiberio, jambo ambalo huenda lilimuaibisha Pilato (On the Embassy to Gaius 38-39 [mwaka 299-306], uk.784-785).

5. Josephus kwenye Antiquities of the Jews 18.3.1 (iliyoandikwa karibu mwaka 93-94 BK) na Wars of the Jews 2.9.2, pia anamtaja Pontio Pilato kuwa gavana.

6. Wakristo wa awali.

Ignatius (aliyekufa mwaka 107/116 BK) kwenye Letter to the Magnesians sura ya 11-12, uk.64 anamtaja Pontion Pilato.

Ni kweli Yesu alisulubiwa wakati wa utawala wa Pontion Pilato, alikufa, na kisha akafufuka kutoka kwa wafu (Ignatius' Letter to the Trallians sura ya 9, uk.70).

Justin Martyr (aliyekufa karibu mwaka 150 BK) Yesu Kristo alisulubiwa wakati wa utawala wa Pontio Pilato. ". . . na tunamuabudu kwa usahihi, tukiwa tumejifunza kuwa yeye ni Mwana wa Mungu mwenyewe wa kweli, na tunamuweka mahali pa pili, na Roho wa unabii mahali pa tatu, na tutathibitisha" (First Apology of Justin Martyr sura ya 13, uk.166-167).

Alisulubiwa wakati wa utawala wa Pontio Pilato (First Apology of Justin Martyr sura ya 61, uk.183).

Melito wa Sardis (mwaka 170-180 BK) Ante-Nicene Fathers juzuu ya 8 sura ya 4, uk.757 inasema Yesu alihukumiwa na Pilato.

Irenaeus Against Heresies (mwaka 182-188 BK) kitabu cha 3 sura ya 42, uk.417 inasema kuwa Yesu, "amemuunganisha mwanadamu na Mungu kupitia nafsi yake mwenyewe", alisulubiwa wakati wa utawala wa Pontio Pilato, na akafufuka. Yesu Hakimu wa wanaohukumiwa.

Clement wa Alexandria (mwaka 193-217/220 BK) alinukuu 1 Tim 6:13 na kumtaja Pontio Pilato (Kipande cha 4, uk.579 Eusebius' Ecclesiastical History kitabu cha 6 sura ya 14).

Tertullian (mwaka 198-220 BK) alimtaja Pontion Pilato kwenye Tertullian's Apology sura ya 21, uk.35.

Hippolytus askofu wa Portus (mwaka 222-235/6 BK) alimtaja Kayafa, Herode, na Yesu kupigwa viboko na Pilato (Against the Heresy of One Noetus sura ya 18, uk.230).

Origen (mwaka 225-254 BK) anasema kuwa umati ulimshawishi Pilato amhukumu Yesu. Pia anautaja uadui wake na Herode na urafiki wanaoonyesha kuwa nao (Origen's Commentary on Matthew kitabu cha 12 sura ya 1, uk.449-450). Tazama pia (dokezo) de Principiis kitabu cha 3 sura ya 25, uk.332.

Cyprian wa Carthage (karibu mwaka 246-258 BK) "mwishowe walimshika [Yesu] na kumpeleka kwa Pontio Pilato, ambaye alikuwa liwali wa Shamu kwa niaba ya Waroma, wakidai kwa ukatili na msistizio wa usumbufu kuwa asulubiwa na kuuawa" (Treatises of Cyprian Makala ya 7 sura ya 13, uk.468).

Peter wa Alexandria (mwaka 306, 285-311 BK) alisema kuwa Yesu alipelekwa kwa Pilato (Canonical Epistle Orodha ya 9, uk.273).

Lactantius (karibu mwaka 303-c.325 BK) alisema kuwa baada ya Yuda kumsaliti Yesu, Wayahudi walimpeleka Yesu kwa Pilato (Divine Institutes kitabu cha 4 sura ya 18, uk.119). Anamtaja Herode kwenye sura ya 18, uk.120.

Athanasius (mwaka 331 BK) alisema kuwa Pilato alinawa mikono wakati Yesu aliposulubiwa (History of the Arians sura ya 68, uk.295).

Eusebius mwana historia Mkristo (karibu mwaka 325 BK) anamtaja Pontio Pilato, na anasema kuwa baada ya kuondolewa kwake madarakani alijiua.

Pontio Pilato alikuwa gavana wa Yuda, baada ya Gratus, mwaka 26-36/37 BK.

 

S: Kwenye Mat 27:2-14, Mak 15:2-15; Luk 23:1-24 na Yoh 19:1-15, mbali na Biblia, tunajua kitu gani kuhusu Pontio Pilato?

J: "Pontio" ulikuwa ni ukoo wa Kiroma. "Pilatus" inamaanisha mtu aliyebeba pilum (mkuki uliokuwa unatumika sana na jeshi la Kiroma la kale). Mambo tunayoyajua kuhusu Pontio Pilato yanatoka kwa Josephus. Mfalme Tiberio alikuwa na rafiki aliyeitwa Sejanus, ambaye alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote, na Pontio Pilato na Flaccus, mtu aliishi wakati mmoja na yeye, walikuwa wafuasi wa Sejanus. Wakati Pontion Pilato amekuwa gavana (au iwali) wa Wayahudi mwaka 26 BK, alikuwa mtu wa kwanza kuleta Yerusalemu bendera zenye sura ya Kaisari. Wakati Wayahudi wameomba rasmi kuwa ziondelewe, Pilato alizizingira na askari walitishia kuwaua (Wayahudi). Josephus anaripoti kuwa Wayahudi walijitupa chini kuonyesha kuwa wako tayari kufa kuliko kuvunja sheria zao. Pilato aliziondoa bendara na kuzipeleka Kaisari.

Kisha Pilato alichukua hela kutoka kwenye hazina ya hekalu na kujenga mfereji wa kuleta maji Yerusalemu. Wayahudi walipopinga, Pilato alikuwa na askari waliovaa kama raia miongoni mwa umati wa watu, ambao waliwaua watu wengi waliokuwa wamekusanyika. Luk 13:1 pia inaripoti kuwa Pilato aliwaua baadhi ya watu wa Galilaya ambao damu yao aliichanganya na kafara zao.

Wakati Wasamaria wamekusanyika kwenye mlima ili kuangalia vyombo vitakatifu ambavyo inadhaniwa Musa aliviweka hapo, Pilato alituma vikosi kuwavizia na kuwaua. Wasamaria walilalamika kwa Vitellius, legate (jenerali au gavana wa jimbo la Roma) la Shamu, ambaye alimtuma Marcellus kuongoza Yuda kwa muda na kumwamuru Pilato kwenda Roma mwaka 36/37 BK kutoa maelezo ya mambo aliyoyafanya kwa Kaisari. Sejanus aliuawa tarehe 18 Oktoba 31 BK, na Tiberio alikuwa anajaribu kubadilisha sera zilzokuwa zinawapinga Wayahudi. Kaisari Tiberio alikufa tarehe 16 Machi 37 BK, wakati Pilato akiwa njiani kuelekea Roma. Pilato hakurudi tena Yuda. Mapokeo yanasema kuwa alijiua kwenye nchi ya sasa ya Austria au Uswiss kwa kuzama kwenye maji.

Philo Myahudi anasema Herode Agrippa I alimwita Pilato "mtu mwenye asili ya kutokubadilika, mchanganyiko wa ushupavu na kutokuwa na huruma."

Yaelekea uhusiano wa Pilato na mfalme haukuwa na uhakika. Ingawa mfalme (Kaisari) alitaka utengamano, Pilato alikaribia kusababisha mapinduzi mara tatu. Mfalme Tiberio alikuwa amewaua maafisa wake kadhaa kwa usaliti. Endapo Pilato angeonekana akimvumilia mtu anayedai kuwa mfalme, au hakulipa kodi, au alitaka kuwa na ufalme wake mwenyewe, Pilato angekuwa mmoja wa watu wengine wengi ambao Tiberio aliwaua. Wayahudi hawakusahau jambo hili. Walimwambia Pilato kwa ujasiri kuwa endapo utamwachia mfalme huru, hutakuwa rafiki wa Kaisari.

 

S: Kwenye Mat 27:19-28; Luk 23:23-25 na Yoh 18:38-40, watu wangapi walikuwapo kwenye umati uliokuwa mbele ya Pilato, Yesu na Barabba?

J:Wanaakiolojia (elimukale) wamechimbua eneo mbele ya kiti cha Hukumu cha Pilato na kusema kwamba watu wasiozidi 150 wangeweza kuwapo kwenye eneo hilo. Wakati wa Pasaka pangeweza kuwa na mamia ya maelfu ya watu Yerusalamu, lakini ni watu 150 tu ambao wangeweza kuwapo mbele ya Pilato. Ingekuwa rahisi kwa makuhani kujichagulia watu waliowataka mbele ya Pilato alipopendekeza kumfungulia mfungwa mmoja.

 

S: Kwenye Mat 27:26; Mak 15:15; Luk 23:20-25; Yoh 19:16; Mdo 2:23 na Ebr 12:2, tunajua kitu gani kuhusu kusulubisha kabla ya Kristo?

J: Kusulubiwa kulikuwa ni namna ya kuchukiza lakini lakini ya kawaida ya kuua wahalifu miongoni mwa watu wengi.

Nani na Lini: Namna hii ya kuua wahalifu ilitumiwa na Wafoenike, watu wa Carthage, na Wamisri. Herodotus katika kazi yake iitwayo History 3.125 aliwataja Waajemi kuwa walikuwa wakiwasulubisha watu walio hai. Kwenye History 3.159, Herodotus pia anasema kuwa Dario (mwaka 512-485 KK) aliwasulubisha wananchi mashuhuri 3,000 wa Babeli. Vyanzo vingine vya kale, visivyo na uhakika wa kuwa vinasadikika, vinasema kuwa kusulubu kulitumiwa na watu wa India, Scythia, Tauria, Waashuri, Waseltiki, Wajerumani na Waingereza. Kaisari Julius aliripoti kuwa Wanumidia walikuwa wanasulubisha watu. Wakati Alexander Mkuu alipouteka mji wa Wafoenike wa Tiro mwaka 332 KK, aliwaua watu 6,000-8,000 mara moja na kuwasulubisha 2,000 wengine baadayekwa mateso ya msalaba wapatao 2,000.

Wayahudi walisulibiwa na Mselusidi Antiochus IV (267 BK) kwa mujibu wa Josephus kwenye Antiquities of the Jews kitabu cha 12 sura ya 5, uk.257. Kwenye Antiquities of the Jews kitabu cha 13 sura ya14.2, uk.285 Josephus pia anasema kiongozi Msadukayo Alexander Jannaeus (mwaka 103-76 KK) aliwasulubisha Mafarisayo 800 Yerusalemu, baada ya kuwaua wake zao na watoto wao mbele ya macho yao.

Miongoni mwa Waroma, Plautus (aliyekufa mwaka 184 KK) alikuwa mwandishi wa kwanza aliyetoa ushahidi juu ya kusulubisha kwa Waroma, na hawa walikuwa watu waliosulibishwa kabla yay eye kuzaliwa. Kwa mfano, watumwa wa kiume wahaini 25 huko Roma walisulibiwa mwaka 217 KK. Josephus alisema kulikuwa na aina kuu tatu za kuua wahalifu za Kiroma: kukata kichwa/kutupwa kwa wanyama, kuchomwa moto, na kusulibiwa. Pia alisema kuwa kuuawa kwa kuchomwa moto kulichukuliwa kuwa afadhali kuliko kusulubiwa.

Waroma Walijifunza wapi kusulubisha: Wagiriki na Waroma walijifunza kusulubisha kutoka kwa Wafoenike. (Watu wa Carthage wanaweza kuchukuliwa kuwa "Wafoenike wa Magharibi"). Vyanzo kadhaa vinashuhudia usulubishaji uliofanywa na watu wa Carthage, na kuwa Waroma wanaweza kuwa wamejifunza jambo hili kutoka kwao.

Kama alama ya ukristo: Kuna ugunduzi wenye kufurahisha wa kiakiolojia unaohusu matumizi ya msalaba kama alama. Kwa hakika Paulo (karibu na mwaka 52 BK) alimhubiri Yesu aliyesulibiwa (1 Kor 2:2), aliona fahari juu ya msalaba (Gal 6:14), na aliteswa kwa ajili ya msalaba (Gal 5:7; 6:12). Lakini tunawezaje kujua kwa hakika jinsi msalaba ulivyokuwa?

Wakati mji wa Herculaneaum ulipoharibiwa na mlipuko wa volkano ya Mlima Vesuvius mwaka 79 BK, nyumba iliyochimbuliwa inaonyesha msalaba (msalaba wa Kilatini kama herufi ndogo ‘t').

Huko Talpioth, kitongoji cha Yerusalemu, hifadhi za mifupa ya watu zilipatikana kabla ya mwaka 70 BK zikionesha sehemu nne zilizowekewa alama ya msalaba iliyokuwa inaonekana kama alama ya kujumlisha.

Kwa mujibu wa Justin Martyr (karibu mwaka 138-165 BK), alilinganisha msalaba wenye sanamu ya Yesu Kristo na herufi ya Kigiriki ‘Chi' (kama X) kwenye kazi yake iitwayo First Apology sura ya 60.

Msalaba ulionekana kama herufi ya Kiyunani ‘Tau' kwa ujibu wa kazi ya Tertullian Five Books in Reply to Marcion kitabu cha 3 juzuu ya 120, uk.153.

Athanasius (mwaka 326-323 BK) alisema kwenye Incarnation 25:3, kuwa ni msalabani pekee yake ambapo mtu anakufa huku mikono yake imetawanywa.

Pia, michoro ya kukwangua ukutani ya Kiroma ilipatikana Roma kwenye kilima cha Paletine ikiwakejeli Wakristo. Michoro hii inaonyesha msalaba na mikono iliyotawanywa.

S: Kwenye Mat 27:15-19; Mak 15:6-7; Luk 23:16-18 na Yoh 18:39-40, kwa nini Yesu, ambaye hakuwa amekutwa na hatia, aliingizwa kwenye ‘mpango wa hisani wa kuwaachia huru wafungwa'?

J: Hakuna mtu aliyesema mfumo wa sheria wa Kiroma ulikuwa wa haki wakati wote. Kwa kuwa kuhukumiwa kwa Yesu kunaonekana kuwa kulikwisha amuliwa, nadhani ilikuwa muhimu kwa Pilato kumpendekeza kupata msamaha ingawa hakuwa amethibitishwa kuwa ana hatia. Wakati mwingine hata matendo ya rehema yanaweza kutumika kwa makusudi yasiyo haki.

S: Kwenye Mat 27:19, kwanini mke wa Pilato alikuwa Yerusalemu?

J: Wake walikuwa wanaongozana na magavana wa Kiroma. Kabla ya wakati huu, Tacitus kwenye Annals 3:34-35 anasema kuwa baraza la seneti (sehemu moja ya bunge) ilijadili pendekezo la Severus Caecina la kuwazuia wake kuongozana na mahakimu, lakini pendekezo hilo lilikataliwa.

 

S: Kwenye Mat 27:34 na Mak 15:23, je kuna watu waliompa Yesu kitu cha kunywa ila alikataa, au Yesu alisema "nina kiu" na akakubali kama Yoh 19:28-29 inavyoashiria?

J: Watu waliokuwa wakisulibiwa walikuwa wanashikwa na kiu kubwa sana, na inaelekea Yesu hakuwa tofauti hapa, kwa kusema kuwa ana kiu. Walimpa sifongo iliyokuwa imechovywa kwenye siki. Kinywaji hiki kilikuwa na nyongo, ambayo ilidhoofisha maumivu. Mwanzoni Yesu aliikubali sifongo na akaonja kile kinywaji, lakini baadaye aliikataa. Yesu hakutaka kutumia dawa za kuondoa maumivu wakati alipoteswa kwa ajili ya dhambi zetu.

 

S: Kwenye Mat 27:38, Mak 15:32, na Luk 23:39, je wanyang'anyi pale msalabani walimtukana Yesu, au mmoja wao alitubu na kumgeukia Yesu kwenye Luk 23:39?

J: Wanyang'anyi wote wawili walimtukana Yesu mwanzoni. Lakin mara baada ya kufanya hivyo, mnyang'anyi aliyekuwa mkono wa kulia wa Yesu alibadilisha moyo wake na kumwamwamini Yesu. Yesu alimwambia kuwa siku hiyo atakuwa pamoja naye Paradiso.

 

S: Kwenye Mat 27:44 na Mak 15:31-32, ni wakati gani hasa wanyang'anyi walimtukana Yesu?

J: Maandiko hayasemi ni wakati gani hasa. Mathayo na Marko wanataja makundi matatu ya watu waliomtukana Yesu: wapita njia, makuhani, na wanyang'anyi msalabani. Hata hivyo, mistari hii haibainishi ama mfuatano endapo walisema hivyo mara moja tu, ama walisema mara ngapi. Kwa ujumla, si kawaida mtu kusema neno baya mara moja tu na kuishia hapo.

Leo Wakristo wanaweza kukejeliwa kwa sababu ya imani yao na wahalifu, watu wasiowajua kabisa, na hata viongozi potofu wa kidini.

 

S: Kwenye Luk 21:7, je, Yesu alifundisha juu ya siku za mwisho akiwa hekaluni, au kwenye Mlima wa Mizeituni kama Mat 24:3-44 na Mak 13:3-37 zinavyoonyesha?

J: Yesu alifundisha jambo hili kwenye Mlima wa Mizeituni, na yawezekana ilikuwa wakati walipokuwa wakielekea huko. Luka 21 haisemi kwamba Yesu alikuwa hekaluni wakati alipofundisha jambo hili.

 

S: Kwenye Mat 27:32; Mak 15:21, na Luk 23:26, je Simoni Mkirene aliubeba msalaba wa Yesu, au Yesu ndiye aliyeubeba kama Yoh 19:17 inavyoonyesha?

J: Vyote. Kwa ujumla, ilikuwa desturi kwa mhukumiwa kuubeba msalaba wake mwenyewe kama Yoh 19:17 inavyosema. Hata hivyo, Yesu alikuwa amedhoofika sana, baada ya kuchapwa mijeredi, na mapigo mbalimbali, hata hakuweza kuubeba msalaba wake mpaka mwisho. Hivyo Waroma walimwamuru Simoni Mkirene, aliyekuwa anapita njiani, aubebe sehemu iliyobaki ya safari.

S: Kwenye Mat 27:48; Mak 15:23; Luk 23:36 na Yoh 19:29, je Yesu alipewa kitu gani hasa kunywa pale msalabani?

J: Matthew 27:48 says "sour wine / wine Mat 27:48 inasema, "siki", Mak 15:23 inasema "mvinyo iliyotiwa manemane", Luk 23:36 inasema, "siki", na Yoh 19:29 inasema "siki." Hata hivyo "nyongo/siki" haikuwa kimimika halisia bali kielelezo cha kitu kichungu, na manemane ilikuwa chungu.

 

S: Kwenye Mat 27:37; Mak 15:26; Lk 23:38 na Yoh 19:19, ni maneno gani hasa yaliyoandikwa kwenye anwani juu ya kichwa cha Yesu?

J: Kwanza tuangalie mambo matano yanayohusiana na jibu, na kisha majibu mawili.

1. Kwanza kabisa hapakuwa na ujumbe mmoja, lakini kulikuwa na jumbe tatu, kama Yoh 19:29 inavyosema, anwani iliandikwa Kiaramu, Kilatini na Kigiriki.

2. Hivi ndivyo waandishi wa injili wanavyo ripoti:

Mat 27:37 inasema, "Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi."

Mak 15:26, "Mfalme wa Wayahudi."

Luk 23:38, "Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi."

Yoh 19:19, "Yesu Mnazareti, Mfalme wa Wayahudi."

3. Waandishi wa kale walikuwa na kawaida ya kufafanua maneno badala ya kunukuru. Ripoti Tulizo nazo hapa ni sahihi, lakini hazina maelezo ya kina. Hivyo, kwa mfano, kama mwandishi mmoja alisema "Huyu ndiye Yesu, Mfalme wa Wayahudi", na mwingine alisema "Mfalme wa Wayahudi", wote wanaweza kuwa wanaripoti maneno yale yale. Mwandishi wa kwanza anaripoti maneno zaidi kuliko yule wa pili.

4. Papias, mwanafunzi wa Mtume Yohana, anaripoti kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwanza kwa lugha ya Kiebrania (au Kiaramu?) na kisha ikatafsiriwa kwenye Kigiriki. Waandishi wengine waliandiki Kigiriki. Hivyo, kuna tafsiri kati ya maneno yaliyosemwa na yale yaliyoandikwa na waandishi wa Injili.

5. Bila kujali tofauti zilizopo kati ya anwani hizi tatu, Marko anaelekea kuripoti maneno yaliyopo kwa waandishi wote watatu.

Jibu la Kwanza: Jumbe hizi tatu kwenye lugha tatu tofauti zimeripotiwa kwenye Mathayo, Luka, na Yohana. Marko anaripoti maneno yaliyomo kwa waandishi wote watatu. Pilato huenda hakujua Kiaramu kwa hiyo ujumbe ungeweza kuandikwa kwa Kilatini, na kutafsriwa kwenye Kigiriki na Kiaramu ili kila mtu aweze kuusoma.

Jibu la Pili: Kwa kuwa waandishi wa injili waliripoti maneno yaliyokuwa yametafsiriwa, na mambo kama "Hii ni" yalitokea mara kwa mara kwenye tafsiri, tuna uhakika na ujumbe wa anwani, lakini hatuna uhakika na maneno halisi. Hata hivyo, kitu muhimu hapa ni ujumbe, siyo maneno halisi.

 

S: Ni maneno gani hasa saba aliyoyasema Yesu msalabani, kwa kufuata mtiririko wake halisi?

J: Ingawa mfuatano uliotolewa kwenye injili si lazima uwe ule ambao yalisemwa, ni rahisi zaidi kudhani kuwa yalikuwa katika mtiririko halisi, ambao ni:

1. Baba uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo (Luk 23:34a)Kw

2. Mama, tazama mwanao, na mwana tazama mama yako (Yoh 19:25-27).

3. Amin nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi (Luk 23:43b).

4. Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha (Mat 27:46; Mak 15:34).

5. Naona kiu (Yoh 19:28-29).

6. Imekwisha (Yoh 19:30).

7. Muda mfupi kabla ya kufa, Yesu alisema, "Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu" (Luk 23:46a).

Ni kweli kuwa Yesu anaweza kuwa alisema maneno mengine pia.

 

S: Kwenye injili, je ni kweli kuwa Yesu alikufa msalabani, au Mungu alimweka mtu mwingine badala yake kimiujiza na bila kutambulika kama Korani inavyodai?

J: Tofauti za mitizamo ya Wakristo na Waislamu ni tofauti ya msingi kati ya dini zao mbili.

Wakristo wanasema alikuwa ni Yesu kweli kwa sababu simulizi zote za kikristo na zisizo za kristo zinasema kuwa alikuwa Yesu. Mungu (Allah) wa Waislamu ni tofauti kabisa na Mungu wa kwenye Biblia, na Allah amewapumbaza na kuwadanganya watu wake wote kufikiri kuwa alimweka mtu mwingine badala ya Yesu.

Waislamu wanasema Allah ni Mungu yule yule wa kwenye Biblia. Kitando cha Allah kumbadilisha Yesu kisingetambulika na mtu yeyote, na kwa hiyo pasingekuwa na ushahidi wowote wa kihistoria wa kubadilishwa huko.

Wote Wakristo na Waislamu wanaweza kukubaliana katika mambo mawili: 1) Angalau inaonekana kuwa Yesu alikufa msalabani 2) Wakati fulani, Allah aliwapumbuza kabisa na kuwahadaa watu wake kwa makusudi mazima.

 

S: Kwenye injili, kuna ushahidi gani usiotoka kwenye Biblia kuhusu "giza kutanda juu ya nchi" wakati wa kusulibiwa kwa Yesu?

J: Si sahihi kutegemea kuwa kila jamii ingeweka kumbukumbu za giza. Kwa mfano imekadiriwa kimahesabu kuwa kupatwa kwa jua kulisababisha giza Misri tarehe 12 Desemba 504 KK, na bado hakuna kumbukumbu za kihistoria, miongoni mwa Wamisri waliostaarabika sana, au watu wengine wote kuhusiana na jambo hili. Angalia http://www.informationblast.com/500s_BC.html

kwa maelezo zaidi.

Hata hivyo, mwanahistoria Mpalestina asiye Mkristo Thales (pia huandikwa Thallus), aliandika mwaka 52 BK, miaka chini ya 20 baada ya kusulibiwa kwa Yesu. Thales aliandika kuwa giza liliambatana na kusulubiwa kwa Yesu.

Angalia usimchanganye mwanahistoria Msamaria Thallus, na Mwanafalsafa Mgiriki Thales, aliyekuwa anajulikana kiasi cha kutosha.

Justin Martyr's Hortatory Address to the Greeks sura ya 9, uk.277 inamtaja Thallus, Philo, Josephus, na wengine.

Theophilus to Autolychus sura ya 29, uk.120 inamtaja Thallus, pia mwanahistoria aliyetangulia Berosus kwenye uk.121.

The Octavius of Minucius Felix sura ya 22, uk.186 inamtaja mwanahistoria Thallus.

Tertullian's Apology sura ya 19, uk.33 inawataja Thallus na Josephus.

Julius Africanus kipande cha 18, uk.136.

Phlegon alikuwa mwandishi wa Kigiriki wa Caria (kusini magharibi mwa Asia Ndogo) aliyeandika muda mfupi baada ya mwaka 137 BK. Aliandika kuwa mwaka wa nne wa kipindi cha 202 cha miaka mine baina ya michezo ya Olimpiki [33 BK] kulikuwa na "kupatwa kwa jua kukubwa zaidi" na kwamba "giza liliingia saa sita mchana kiasi kwamba hata nyota zilitokea mbinguni. Kulikuwa na tetemeko kuu la ardhi kule Bithinia, na vitu vingi vilipinduliwa huko Nikea." Origen (mwaka 225-254 BK) pia anasema Phlegon aliandika juu giza kwenye kitabu chake cha 13 au 14 (Origen Against Celsus kitabu cha 2 sura ya 14, uk.437, kitabu cha 2 sura ya 33, uk.445; kitabu cha 2 sura ya 59 uk.455).

Justin Martyr (karibu mwaka 150 BK) Hortatory Address to the Greeks sura ya 9, uk.277 anamtaja Thallus, akiandika kuhusu ya giza kutanda juu ya nchi kwa wakati ule.

Melito of Sardis (mwaka 170-177 BK) anasema kuwa dunia ilitikisika, jua likatoweka, na siku ilibadilishwa, kwa kuwa havikuhimili Bwana wao kuwambwa mtini (From the Discourse on the Soul and the Body sura ya 2 Ante-Nicene Fathers juzuu ya 8, uk.756).

Irenaeus in Against Heresies (mwaka 182-188 BK) kitabu cha 4 sura ya 34, uk.512 anasema, "Na mambo yanayohusika na mateso ya Bwana, ambayo yaliyotabiriwa, hayakutimilika katika tukio jingine. Kwa kuwa tukio hili halikutokea kwenye kifo cha mtu yeyote kati ya watu wa kale kuwa jua lizame saa sita mchana, wala pazia la hekalu lipasuke, wala tetemeko la ardhi litokee, wala miamba ipasuke, wala wafu wafufuke kutoka kwa wafu, wala mtu yeyote kati ya hawa [wa kale] afufuke siku ya tatu, wala kupokelewa . . . Kwa hiyo manabii hawakumwongelea mtu yeyote yule mwingine isipokuwa Bwana, ambaye ndani mwake ishara zote hizi ziliyotabiriwa zinakubalianayalitokea sambamba."

Mwandishi Mkristo Tertullian, akiandika mwaka 200 BK, kwenye On Fasting sura ya 10 juzuu ya 4, uk.109 pia alilitaja giza lililoambatana na kusulubiwa kwa Yesu. Analitaja jambo hili pia kwenye An Answer to the Jews sura ya 12, uk.170.

Hippolytus alikuwa askofu wa Portus (mwaka 222-235/6 BK). Alisema kuwa kwa ajili ya Yesu "jua lilitiwa giza, siku haikuwa na nuru, miamba ilipasuliwa, pazia lilipasuka, misingi ya dunia ilitikitiswa, makaburi yalifumuliwa, na watu walifufuliwa" (Against the Heresy of One Noetus sura ya 17, uk.230).

Mwandishi wa kale Origen (akiandika mwaka 225-254 BK) alilitaja giza lililotanda juu ya nchi, na makaburi yaliyofumuka kwenye Against Celsus kitabu cha 2 sura ya 33, uk.445.

Mwandishi Mkristo Cyprian wa Carthage (karibu mwaka 246-258 BK) "Neno la Mungu lilipelekwa kimya machinjoni. Na wakati akiwa kwenye msalaba wa Bwana, nyota zilichanganywa, vitu vya asili vilitikiswa, dunia ilitetemeka, giza liliugubika mchana, jua . . ." (Treatises of Cyprian makala ya 9 sura ya 7, uk.486).

Dionysius of Alexandria (mwaka 246-265 BK) alilitaja tetemeko la kwenye Mathayo (Letter to the Bishop Basilides orodha ya 1, uk.94).

Arnobius (mwaka 297-303 BK) kwenye Against the Heathen kitabu cha 1 sura ya 53, uk.428 alitaja giza wakati wa kifo cha Yesu.

Lactantius (mwaka 260-325 BK) tetemeko la ardhi saa ile ile aliyokufa Yesu na jua likaondoa nuru yake mara moja na kulikuwa na giza tangu saa ya sita hadi saa tisa (The Divine Institutes kitabu cha 4 sura ya 19, uk.122).

Alexander of Alexandria (mwaka 313-326 BK) asema jinsi makaburi yalivyofunguliwa, dunia ikiyumbayumba, na mianga ilitishiwa, na jua pamoja na mwezi vilitoweka, nyote ziliondoa mng'ao wao wakati Yesu alikuwa akiteseka msalabani (Epistles on the Arian Heresy Epistle 5.6, uk.301).

Cyril of Jerusalem (karibu mwaka 315-335-386 BK) alisema kuwa jua lilirudi nyuma wakati wa Hezekia, na jua lilipatwa wakati wa Kristo (First Catechetical Lecture 2 Nicene & Post-Nicene Fathers juzuu ya 7, uk.12).

 

S: Kwenye injili, je kutajwa kwa giza na tetemeko la ardhi na kupasuka kwa pazia wakati Kristo aliposulibiwa ni mambo kistiari tu na hayakutokea kwa hakika, kwani hayakuandikwa mahali pengine popote, kama Some Answered Questions, uk.37-38 inavyosema?

J: Hapana. Angalia swali lililotangulia kwa uthibitisho wa giza, na swali kuhusu Mat 27:51 kwa ushahidi wa tetemeko la ardhi.

 

S: Kwenye Luk 23:45-46, mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anasema kuwa pazia la hekalu lilipasuka wakati Yesu akiwa hai, lakini lilipasuka baada ya Yesu kufa kwenye Injili ya Marko (Jesus, Interrupted, uk.68). Kisha anauliza kama pazia lilipasuka linawakilisha Mungu kuukataa mfumo wa kuabudu wa Kiyahudi, au linaashiria Yesu kutupaka mafuta (pia kwenye Jesus, Interrupted, uk.52).

J: Mambo mawili ya kuzingatia katika kujibu swali hili. 1) Kwa kweli kutatuka kwa pazia kunaweza kuwa kunawakilisha zaidi ya jambo moja, hasa mambo hayo mawili yanapokuwa yanahusiana kwa karibu. Kwa hakika hakuashirii kuwa Mungu aliukataa mfumo wa kuabudu wa Kiyahudi; bali kuwa sasa Yesu amelipia dhambi, mfumo wa kuabudu wa Kiyahudi umemalizika (Na kwa hakika hekalu liliharibomolewa baada ya miaka 40).

2) Luka habainishi wakati pazia lilipopasuliwa vipande viwili. Luk 23:44-45 inasema kulikuwa na giza tangu saa ya 6 hadi saa ya 9 mchana, na pazia la hekalu lilipasuka vipande viwili, na Yesu akalia kwa sauti kuu kabla hajafa. Maealeao haya hayabainishi mpangilio wa matukio.

 

S: Kwenye Injili ya Luka, mwandishi mwenye kushuku Bart Ehrman anasema kwenye Jesus, Interrupted uk.46-47, "Kifo cha Yesu ni muhimu kwa wote Marko na Luka. Lakini kwa Marko, kifo chake ni sadaka ya ondoleo la dhambi; kwa Luka ni sababu ya watu kutambua kuwa ni wenye dhambi na kuhitaji kumgeukia Mungu kupata msamaha. Hivyo basi, sababu ya kufa kwa Yesu ni tofauti kabisa, kutegemeana na mwandishi unayemsoma." (pia kwenye Jesus, Interrupted, uk.94).

J: Erhman anajaribu kuweka tofauti ya imani kati ya injili za Marko na Luka wakati hazipo. Hata Erhman anatambua kuwa Luka na Matendo ya Mitume vimeandikwa na mwandishi mmoja. Pengine moja ya kauli zilizo wazi zaidi kuhusu sadaka ya ondoleo la dhambi aliyoisema Luka imo katika Matendo 5:30-31: "Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkitundika katika mti. Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi" (mstari imeongezwa ili kuonesha mahali ambapo Erhman amekosea).

 

S: Kwenye Mat 27:53 na Mak 15:39, je akida alisema, "huyu alikuwa Mwana wa Mungu", au "huyu alikuwa mwenye haki" kama Luk 23:47 inavyosema?

J: Yote. Akida hakufungwa kusema sentensi moja tu. Mara nyingi injili hazikunukuu neno kwa neno, na hazikuandika kila neno, kwa hiyo akida, kwa hiyo kuna uwezekano kuwa akida alisema maneno ya ziada pia.

Watu wengi zaidi wanaafiki kuwa wakati wote tangu Yesu alipokufa hadi wakati walipotaka kuhakikisha kuwa alikuwa amekufa kweli, hadi kuutelemsha mwili wake kutoka msalabani, akida alikuwa na muda wa kutosha kusema zaidi ya sentensi moja. Ingekuwa jambo la ajabu kama jemedari angekuwa kimya kabisa isipokuwa alipoisema hiyo sentensi moja.

 

S: Ni mpangilio upi wa injili unaofuata mtiririko halisi wa matukio?

J: Kwanza kabisa nawiwa kukiri kuwa kwa kiasi nimepoteza kuunda kitu ambacho tayari kipo. Zamani za mwaka 246-265 BK, Dionysius, askofu wa Alexandria, alithibitisha kuwa waandishi wa injili "hawakutofautiana wala kupingana" na alitoa mpangilio mzuri na mkamilifu wa injili unafuata mtiririko halisi wa matukio baada ya kufufuka kwa Yesu kwenye kazi yake, Letter 5-to Bishop Basilides orodha ya 1 Ante-Nicene Fathers juzuu ya 6, uk.94-95. Vyovyote vile, huu hapa ndio mpangilio wa matukio 29 unaofuata mtiririko halisi wa kutokea kwao, na unakubaliana na ule wake.

Namba zinawakilisha matukio ambayo ni lazima yawe na mpangilio, na herufi a, b, c zinawakilisha matukio ambayo yangeweza kutokea kwa kufuata mpangilio wowote. Maneno yaliyo kwenye wino mzito yanaonyesha viashiria muda, mfuatano, na mahali. Mistari iliyopigiwa mstari inaonyesha mahali ambapo vifungu havifuati mtiririko halisi.

Baada ya Yesu kufufuka kutoka kwa wafu: Mat 28; Mak 16; Luka 24 na Yoh 20-21

R1a. Sabato ilipokwisha, Mariamu Magdalena, Mariamu mwingine [mama wa Yakobo] Salome, na wanawake wanaanza safari ya kwenda kaburini (Mat 28:1b; Mak 16:1-3; Luk 24:1 na Yoh 20:1).

R2a. Tetemeko la ardhi linatokea wakati malaika alipoliviringisha jiwe kuliondoa mlangoni pa kaburi. Walinzi wakawa kama wafu (Mat 28:2-4).

R2b. Malaika analiviringisha jiwe kutoka kaburini (Mak 16:4; Lk 24:2).

R1b. Mwili haukuonekana, na "wanaume" wawili wanaongea na wanawake (Luk 24:3-8; Yoh 20:2).

R3. Asubuhi ile Yesu alipofufuka, malaika anawatokea wanawake na kuwaagiza wawaambie wanafunzi kwenda Galilaya Mat 28:5-7; Mk 16:5-8

R4a. Wakati wanawake wakirudi upesi, Yesu pia anawatokea na anawaambia wakawaambie wanafunzi waende Galilaya (Mat 28:8-10).

R4b1. Wakati wanawake waliporudi kutoka kaburini, wanafunzi hawakuwaamini (Luk 24:9-11).

R4b2. Petro na Yohana wanakimbia kwenda kaburini; Yohana anafika kwanza (Luk 24:12; Yoh 20:3-9).

R4b3. Kisha wanafunzi walirudi majumbani mwao [Yerusalemu] (Yoh 20:10).

R4c. Walinzi wanawaambia makuhani; kisha makuhani wakawapata rushwa (Mat 28:11-15).

R4d. Wakati Mariamu analia, wanaume wawili, na baadaye Yesu, wanamtokea Mariamu Magdalena (Mak 16:9-11; Yoh 20:11-18).

R5. Siku hiyo hiyo kwenye njia ya kwenda Emau, Yesu anawatokea wanafunzi wawili (si miongoni mwa wale kumi na mmoja). Anakaa nao hadi jioni (Mak 16:12; Luk 24:13-29).

R6. Mara wanafunzi wale wawili wanarudi kwa haraka Yerusalemu (kilomita 11, au maili 7) na wanawaambia wanafunzi 11 (Mak 16:13; Luk 24:33-35).

R7. Huko Yerusalemu, jioni ya siku ile ile Yesu aliyofufuka, wakati wanafunzi wale wawili walipokuwa wakizungumza na wanafunzi 11, Yesu anatokea, kwa mara ya kwanza, kwa wanafunzi kumi (Yoh 20:19-23).

R8. Wanafunzi wengine wanamwambia Tomaso kuwa wamemwona Yesu (Yoh 20:25).

R9. Siku nane baadaye, Yesu anatokea, kwa mara ya pili, kwa wanafunzi kumi na mmoja akiwemo Tomaso (Mak 16:14; Yoh 20:19, 26-31).

R10. Yesu anawatokea (mara ya tatu), kandoni mwa Bahari ya Taiberia [Galilaya]. Wanavua samaki 153 (Mat 28:19-20; Yoh 21:1-14).

R11a. Mara tatu, Yesu anamuuliza Petro kama ampenda (Yoh 21:15-23).

R11b1. Yesu anawatokea wafuasi wake zaidi ya 500 (1 Kor 15:6).

R11b2. Yesu anamtokea Yakobo, ndugu yake (1 Kor 15:6).

R12. Huko Galilaya, Yesu anawatokea wanafunzi na kuwapa agizo kuu (Mat 28:16-20; Mak 16:15-18).

R13. Wanafunzi wanarudi Yerusalemu, aidha wanakaa huko au Bethania, kitongoji chake.

R14. Walipokuwa wanakula, Yesu anawaagiza wabaki Yerusalemu hadi watakapopokea nguvu kutoka juu (Luk 24:49; Mdo 1:4). Wanaitii amri hii (Luk 24:52).

R15. Yesu awaongoza wanafunzi kwenda Bethania, kitongoji cha Yerusalemu kwenye mteremko wa Mlima wa Mizeituni (Luk 24:50).

R16. Siku arobaini baada ya ufufuo (Mdo 1:3), Yesu anapaa mbinguni kupitia kwenye (Mak 16:19; Luk 24:50-51; Mdo 1:9-11).

R17a1. Mitume wanarudi Yerusalemu, na kubaki hekaluni (Luk 24:52-53).

R17b. Mitume 11 walimchagua Mathiya achukue nafasi ya Yuda (Mdo 1:15-26).

R18. Huko Yerusalemu siku ya Pentekoste (siku 50 baada ya Pasaka), mitume wakiwa wamejazwa na Roho Mtakatifu (Matendo 2).

R19. Baada ya haya, mitume wasafiri kwa uhuru (Mak 16:20).

 

S: Kwenye Mat 28:1; Mak 16:2 na Luk 24:1, je Mariamu alikuwa kaburini mara baada ya jua kuchomoza, au alikwenda kaburini wakati kungali giza kama Yoh 20:1 isemavyo?

J: Yote ni kweli. Yoh 20:1 inasema walikwenda kaburini wakati kungali giza, lakini Mak 16:2 inaonyesha kuwa walifika kaburini wakati jua limechomoza. Kama walikuwa Bethania, na kaburi lilikuwa pembeni mwa Yerusalemu, ingewachukua muda kiasi kutembea kutoka kwenye kitongoji hicho kwenda Yerusalemu.

S: Kwenye Mat 28:1; Mak 16:1-2; Luk 24:1 na Yoh 20:1, kwa nini wanawake walikwenda kaburini, kwa kuwa kulikuwa na muhuri wa Kiroma kwenye jiwe lililofunika katika lango lake kwenye Mat 37:62-66?

J: Kuna majibu mawili yanayowezekana, lakini la pili lina uwezekano zaidi.

Wanawake walitaraji kuwa wangeruhusiwa: Haikuwa desturi ya kawaida kuweka muhuri na askari wa Kiroma kulinda makaburi. Makuhani wakuu na Mafarisayo walimwomba Pilato bayana kuwa "kaburi lilindwe vizuri mpaka siku ya tatu" kwenye Mat 27:64. Watawala hawakutaka kuzuia desturi za mazishi, walihakikisha tu kuwa hakuna mtu atakayeuiba mwili, hivyo wanawake wanaweza kudhaniwa kuwa walitegemea kuruhusiwa kuingia kaburini.

Wanawake hawakujua kuhusu muhuri na mlinzi: Kulinda kaburi la mhalifu na kuweka askari na muhuri vya Kiroma kulizunguka kaburi lilikuwa jambo lisilo la kawaida kabisa. Luk 23:55-56 inasema wanawake walimfuata Yusufu ili kuona mahali ambapo mwili wa Yesu ulilazwa, na kisha walirudi nyumbani kuandaa marhamu na manukato. Kwa maneno mengine, hawakuwa wanazunguka zunguka pale wakiliangalia kaburi. Ombi la kuweka muhuri na mlinzi haliwekwa hadi siku iliyofuata kwa mujibu wa Mat 27:62. Hivyo inawezekana wanawake hawakufahamu kuhusu muhuri na mlinzi.

 

S: Kwenye Mat 28:1; Mak 16:1-2; Lk 24:1 na Yoh 20:1, kwa nini wanawake walikwenda kaburini kuuviringishia mwili wa Yesu wakati Yusufu wa Arimathaya na Nikedemo walikuwa wameshaubingirishia kwenye Yoh 19:39?

J: Yesu alikufa karibu saa 9:00 alasiri, na kutakuwa na muda uliopita toka Yusufu wa Arimathaya kuuomba mwili, Pilato kuhakikisha kuwa Yesu alikuwa amekufa kweli, na wawili hawa kuushusha mwili na kuupeleka kaburini. Hawakuwa na muda wa kutosha kabla ya jua kuzama kufanya mazishi yaliyotakiwa (fikiria taratibu zinazofanana na za Kimisri ya kuhifadhi miili). Hivyo Yusufu na Nikodemo kwenye Yoh 19:38-39 walifanya sehemu ya kwanza, iliyohususha manukato, kuzuia mwili usioze kwa siku kadhaa, na kisha wangerudi na kuubingirishia mwili kwa namna ipasavyo, yaani vitambaa vya kuviringishia mikono yake, miguu, kiwiliwili, na kichwa wakati wa jua kupambazuka siku ya Jumapili. Kazi hii inaweza kuonekana kuwa ya kuchukiza, lakini ilikuwa desturi ya kawaida kabisa siku zile.

Isitoshe, ingawa hatujui sana namna Wayahudi walivyokuwa wanazika wafu wakati ule, lakini kwa upande wa Wamisri, baadhi ya hatua za matayarisho ya mwili hazikufanyika hadi siku kadhaa baadaye.

 

S: Kwenye Mak 15:47, je Mariamu Magdalena na Mariamu mamaye Yose walipaona mahali alipolazwa Yesu, ni wanawake waliokuwa wamekuja na Yesu kutoka Galilaya kama Luk 23:55 inavyosema?

J: Yote mawili. Kwa upande mmoja, wanawake kutoka Galilaya inaweza kumaanisha wanawake waliosafiri na Yesu kutoka Galilaya, si lazima wawe wazaliwa wa Galilaya. Kwa upande mwingine, Magdala ulikuwa mji wa Galilaya, pwani ya mashariki ya Bahari ya Galilaya.

 

S: Kwenye Mat 28:1, je kaburi lilifunikwa, au jiwe lilibingirishwa kutoka mlangoni kama Luk 24:2 inavyosema?

J: Luk 24:2 inasema jiwe lilikuwa limebingirishwa kutoka mlangoni wakati wanawake wanafika kaburini. Mat 28:2 pia inasema kuwa jiwe lilibingirishwa kutoka mlangoni, wakati inapoelezea Mat 28:1. Hakuna kifungu kinachosema kuwa wanawake walikuwepo wakati jiwe linabingirishwa kutoka mlangoni mwa kaburi.

 

S: Kwenye Mak 16:4, je jiwe lilikuwa limeshabingirishwa kutoka kaburini, au lilibingirishwa na malaika [kama inavyodaiwa] wakati wanawake wapo pale (Mat 28:2)?

J: Kwenye injili zote mbili, jiwe lilibingirishwa kutoka kaburini kabla ya malaika kuongea na wale wanawake. Mat 28:2 haisemi kuwa wanawake walikuwapo wakati jiwe linabingirishwa kutoka kwenye mlango wa kaburi.

S: Kwenye Mat 28:1-8, Mak 16:1-8; Luk 24:1-10 na Yoh 20:1-8, kitu gani kilitokea Yesu alipofufuka?

J: Yesu alikuwa hai katika mwili wake tena. Mwili wake uliweza kuguswa (Yoh 20:27; Mat 28:9; Luk 24:39), na kula (Luk 24:41-43). Yesu alisema mwili wake baada ya kufufuka ulikuwa na nyama na mifupa (Luk 24:39), na ninadhani unaamini kuwa Yesu alijua vema zaidi kuliko mtu mwingine yeyote! Hata hivyo, mwili wa Yesu ulikuwa mwili uliotukuzwa ambao uliweza kupenya kuta (Yoh 20:19-20) na kutoweka (Luk 24:31).

Tertullian (mwaka 198-220/240 BK) Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuka katika mwili wake. Huu ni msingi hasa wa injili, wokovu wetu. Five Books Against Marcion kitabu cha 3 sura ya 8, uk.328.

Novatian (mwaka 250/254-256/7 BK) [Yesu] Alifufuliwa tena katika mwili ule ule alimofia, jambo hili limethibitishwa na majeraha ya mwili ule ule, na hivyo anaonyesha kanuni za kufufuka kwetu katika mwili wake, kuwa aliurejesha katika kufufuka kwake mwili ule ule aliokuwa nao kwa ajili yetu" [Treatise Concerning the Trinity sura ya 10, uk.620].

Adamantius (karibu mwaka 300 BK) anajadili kuwa ingekuwaje endapo Yesu aliteseka katika hali ya mwonekano tu. "Kama aliteseka katika mwonekano tu, na si katika uhalisia, Herode alikaa katika kiti cha hukumu katika mwonekano tu; katika mwonekano tu Pilato alinawa mikono yake, na katika mwonekano Yuda alimsaliti. Kayafa vile vile alimtoa ahukumiwe katika mwonekano; Wayahudi walimkamata katika mwonekano tu, na mitume . . . Hata damu yake ilichuruzika katika mwonekano tu; wainjilisti walihubiri Injili katika mwonekano; Kristo alikuja kutoka mbinguni katika mwonekano, na alipaa katika mwonekano. Wokovu wa wanadamu ulikuwa katika mwonekano pia, na si katika kweli. Kwanini sasa Kristo aseme, ‘Mimi ni kweli'" (Dialogue on the True Faith sehemu ya 5 sura ya 851a, uk.149.

 

S: Kwenye Yoh 20:1, je Mariamu Magdalena alikwenda kaburini peke, yake au Mariamu Magdalena na Mariamu yule mwingine (Mat 28:1), au Magdalena, Mariamu, mamaye Yakobo, na Salome kwenye Mak 16:1, au Magdalena, Yoana, na wanawake wengine katika Luka 24:10?

 

J: Mariamu Magdalene, Yoana, Mariamu mamaye Yakobo, na wale wanawake wote walikwenda. Yoh 20:1 HAISEMI Mariamu alikwenda pekee yake. Kama namba ya wanawake waliokwenda bado ni sahihi, japokuwa si kwa ufahasa kabisa, kumtaja mmoja, wawili au watatu kati yao. Kama kuna waliokwenda mapema na wengine mara baadaye, bado ni sahihi kwa simulizi hii kusema kuwa wako waliokwenda, na simulizi nyingine kulitaja kundi zima.

 

S: Kwenye Mat 28:2-5 na Mak 16:5, je palikuwa na malaika mmoja tu, au palikuwa na malaika wawili kulingana na Luk 24:4 na Yoh 20:12?

J: Kama palikuwa na malaika wawili au zaidi, basi ni sahihi pia kusema palikuwa na malaika mmoja. Huu ni mmoja wa mifano mingi ambapo masimulizi ya Injili ni sahihi, lakini hayawi na maelezo ya kina.

 

S: Kwenye Mat 28:8 je, wanawake waliwaambia wanafunzi, au hawakumwambia mtu yeyote kama Mak 16:8 isemavyo (Jesus Interrupted, uk. 48)?

J: Ni dhahiri Marko hakumaanisha kuwa wanawake hawakumwambia yeyote maisha yao yote. Kwa hakika hawakumwambia mtu yeyote mambo waliyoyaona wakati wakikimbia kutoka kaburini. Ukisoma Mat 28:8-10, wanawake walikimbia bila kumwambia mtu yeyote, kisha Yesu akawatokea. Yesu aliwaagiza wakawaambie ndugu zake (yaani wanafunzi wake). Kama mtu anataka kufuatilia mambo yasiyokuwa ya lazima, Mathayo 28 haisemi hasa hasa kuwa wanawake walitii na kumwambia mtu yeyote. Hata hivyo, matendo ya wanafunzi yanaonesha bayana kuwa wanawake waliwaambia wanafunzi.

 

S: Kwenye Mat 28:9, je Mariamu Magdalena alimjua Yesu alipomtokea kwa mara ya kwanza, au hakumjua kama Yoh 20:14 inavyosema?

J: Mat 28:9 haisemi ni mapema kiasi gani Mariamu alimtambua Yesu; inasema tu kuwa walimtambua Yesu muda mfupi baadaye. Kwenye Yoh 20:14 mwanzoni Mariamu hakujua kuwa alikuwa ni Yesu. Lakini Yoh 20:15-17 pia inaonyesha kuwa hatimaye ALIMTAMBUA Yesu.

 

S: Kwenye Yoh 20:29 je, wale waaminio bila kuona wana heri, au wale waonao wana heri kwenye Luk 10:23?

J: Yesu alisema mambo mawili tofauti katika mikutadha miwili tofauti, na wote wawili wana heri, lakini katika njia mbili tofauti.

Kwenye Yoh 20:29 Yesu HAKUSEMA wale waliomwona kwa macho yao baada ya kufufuka hawana heri. Isipokuwa Yesu alimwambia Tomaso mwenye mashaka, "[Sasa] Kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wasadiki." Tomaso alilifanya tukio la ufufuo kuwa msingi wa imani yake. Yesu alisema kuwa heri wale (wanaosifiwa, wamekubalika) wale ambao ingawa wanaichukulia miujiza kuwa husaidia imani yao, hawaifanyi miujiza kuwa msingi wa imani yao, kama alivyofanya Tomaso.

Kwenye Luka 10:23, Yesu anawaambia wanafunzi (akiwemo Tomaso) kwamba walikuwa wenye heri [waliobarikiwa] (kuoneshwa kuwa wale walioridhiwa sana) kuyaona ana kwa ana mambo waliyoyaona.

Msingi wa imani yako katika Kristo ni nini? Kama ni miujiza tu, itakuwaje kama Shetani atatenda miujiza ya kukugushi? Kama itakuwa ujuzi wa kutetea imani, itakuwaje wakati utakapokutana na mtu asiye Mkristo ambaye ni mfanya mihadalo mzuri kwa kujenga hoja? Kama ni kuwa na jibu la kila upinzani dhidi ya Biblia, itakuwaje ikiwa mtu ataleta hoja mpya ya pingamizi dhidi ya Biblia na huna jibu lake? Msingi wa imani unapaswa kuwa uhusiano wetu na Kristo; mambo haya mengine yanafaa kuthibitisha imani yetu, lakini hayapaswi kuwa msingi wa imani yetu.

 

S: Kwenye Luk 24:44, je Wayahudi waliigawa Biblia katika sehemu tatu, au mbili tu kama Mat 5:17 inavyoonyesha?

J: Wayahudi waliiita namna zote mbili, kama Yesu alivyofanya.

Sheria na Manabii: Wayahudi waliliita Agano la Kale Torati na Manabii kufuatana na Mat 5:17-18; Luk 24:27 (Musa na Manabii); Zakaria 7:12 (Torati au manabii wa awali kabisa); 2 Maccabees 15:9; ‘Qumran Manual' ya Discipline 9.11.

Mgawanyo wa sehemu tatu (Torati, Manabii, Maandishi) Utangulizi wa Ecclesiasticus (karibu mwaka 132 KK), Philo wa Alexandria (karibu mwaka 40 BK) ". . . kujifunza mahali hapo sheria na maneno matakatifu ya Mungu yaliyotamkwa kwa ufasaha kabisa na manabii watakatifu, na nyimbo za kiroho, na zaburi, na vitu vingine vya aina nyingine zote . . ." Contemplative Life 25 p.700, Josephus (37-100 A.D.) Against Apion 1.8, na Talmudi ya Kibabeli (karne ye 4 BK). Utangulizi wa Sirach una "Sheria, Manabii, na vitabu vingine vya mababa." Sirach 39:1 inasema, "sheria, hekima, unabii." Waraka wenye sheria za kidini kutoka Kumrani zina "kitabu cha Musa, Manabii, na Daudi na historia ya kizazi" (4QMMT).

Yesu haelekei kujali sana mgawanyo halisi almradi wasomaji walifahamu kitu alichokimaanisha wakati alipoongelea Torati ya Musa, Manabii, na Zaburi kwenye Luk 24:44.

J: Wayahudi walirejea kwake kwa njia zote mbili, kama Yesu alivyofanya.

 

Contemplative Life 25 uk.700, Josephus (37-100 B.K.) Against Apion 1.8, na Talmud ya Kibabeli (Karne ya 4 B.K.). Utangulizi kwa Sirach una "Torati, Manabii, na vitabu vingine vya mababa Kikanisa." Sirach 39:1 yasema, torati, hekima, unabii". Barua ya Halakhic kutoka Qumran "kitabu cha Musa, Manabii, na historia ya kizazi" (4QMMT).

Yesu kwa dhahiri hakujali sana mgawanyo halisi, ili mradi wasomaji walielewa alichokuwa akimaanisha, alirejea kwenye Torati, Manabii, na Zaburi katika Luka 24:44.

 

S: Kwenye Luk 24:49, je wanafunzi walitakiwa kuendelea kukaa Yerusalemu au walikwenda Galilaya kwenye Mat 28:10, 16?

J: Mwanzoni waliambiwa kwenda Galilaya, kitu ambacho walikifanya baada ya kungojea kwa siku nane. Kisha walirejea Yerusalemu, na Yesu aliwaambia wabaki hapo hadi watakapopokea nguvu kutoka juu. Ufuatao ni mpangilio wa matukio yaliyotokea siku 40 za kuwepo kwa Yesu duniani, baada ya kufufuka na kabla ya kupaa kwake.

R2. Enendeni . . . Galilaya, ndilo jambo ambalo malaika aliwaambia asubuhi ile aliyofufuka Yesu (Mak 16:7). Yesu pia aliwatokea wanawake waliokwenda kaburini na kuwaagiza wawaambie wanafunzi kwenda Galilaya (Mat 28:9-10).

R7. Huko Yerusalemu, jioni ya siku ile ile aliyofufuka Yesu, wakati wanawake wale wawili walipokuwa wanaongea na wanafunzi kumi na mmoja, Yesu aliwatokea wanafunzi kumi (Yoh 20:19-23).

R9. Siku nane baadaye, Yesu aliwatokea tena wanafunzi wote, akiwemo Tomaso (Yoh 20:19, 24-29).

R10. Walikwenda Galilaya, kupitia njia ya Bahari ya Tiberia [Galila] (Mat 28:19-20; Yoh 21:1-24).

R14. Wakarudi Yerusalemu, walikaa ama hapo ama kwenye kitongoji cha Bethania (kama inavyodokezwa).

R15. Walipokuwa wanakula, Yesu aliwaamuru kubaki Yerusalemu hadi watakapopokea nguvu kutoka juu (Luk 24:49; Mdo 1:4). Waliitii amri hii (Luk 24:52).

R16. Yesu aliwaongoza kwenda Bethania, kitongoji cha Yerusalemu kwenye mteremko wa Mlima wa Mizeituni (Luk 24:50).

R17. Siku arobaini baada ya kufufuka (Mdo 1:3), Yesu alipaa mbinguni akiinuliwa na mawingu (Mak 16:19; Luk 24:50-51; Mdo 1:9-11).

R19. Walijazwa nguvu za Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, ambayo ilikuwa siku 50 baada ya Pasaka (Matendo 2).

R20. Baada ya hayo, walikwenda kwa uhuru kati ya Yerusalemu na miji mingine.

Angalia swali juu ya mfuatano halisi wa matukio baada ya kufufuka ili kupata habari zaidi kuhusu mtiririko wa kina wa matukio.

 

S: Je "Ushuhuda wa Flavia" (Testimonium Flavianum) wa Josephus kwenye Antiquities of the Jews 18.63-64 ni sahhi kihistoria?

J: Kwanza tutaangalia kifungu hiki kinasema nini kwa Kiebrania, kisha mjadala. Kinasema, "Karibu na muda huu aliishi Yesu, mtu mwenye hekima, endapo ni sahihi kumwuita mtu. Kwani alikuwa mtu aliyetenda matendo makubwa ya ajabu na alikuwa mwalimu wa watu walioipokea kweli kwa furaha. Aliwavuta Wayahudi na Wagiriki. Alikuwa Masihi (Kristo). Wakati Pilato, baada ya kusikia watu mashuhuri sana miongoni mwetu wakimshtaki, alimhukumu asulibiwe, wale waliompenda kwa kina tangu mwanzo hawakuondoa mapenzi yao kwake. Siku ya tatu aliwatokea akiwa hai tena, kwani manabii wa Mungu walitabiri mambo haya na mengine mengi yasiyohesabika juu yake. Na kabila la Wakristo, walioipewa jina lake, hawajatoweka hadi leo."

Michael J. Wilkins na J.P. Moreland kwenye Jesus Under Fire: Modern Scholarship Reinvents the Historical Jesus, uk.212-213 inasema, "Maoni ya wanazuoni kuhusu kifungu hiki yanaweza kugawanywa katika makundi matatu; (1) wale wanaotetea mamlaka ya kifungu hiki; (2) wale wanaokikana hiki chote; (3) wale wanaoamini kuwa kifungu kina kiini sahihi lakini pia kinajumuisha mambo mengine yaliyoongezwa na Wakristo. Wengi wa wanazuoni wa sasa wanaunga mkono wazo la mwisho." Toleo la Kirabu, lililoandikwa na Agapius, askofu wa Kimelkite wa Hierapolis nchini Syria wa karne ya 11, linasema, "mwenendo mwema" neno linalofuata "miujiza" ni "taarifa", na "huenda" limeingizwa kabla ya "alikuwa Masihi." Eusebius wa Kaisaria (aliyeandika mwaka 325 BK), alinuu kifungu hiki, lakini Origen (mwaka 225-254 BK), anaeleza kuwa Josephus alimwongelea Yakobo, lakini HAKUMWONGELEA Kristo kwenye Origen Against Celsus kitabu cha 1 sura ya 47, uk.416; kitabu cha 2 sura ya 13, uk.

 

S: Ni waandishi gani wa awali walioziongelea injili kama injili?

J: Ifuatayo ni orodha yao:

To Diognetus

Kwa Diognetus (karibu mwaka 130 BK) sura ya 11, uk.29, ". . . imani ya injili imethibitishwa, na mapokeo ya Mitume yamehifadhiwa . . ."

Justin Martyr (mwaka 151-155 BK) "Kwa Mitume, katika habari za maisha yao walizoziandika, zinazoitwa injili, wametuletea mambo waliyoyaagiza" (First Apology of Justin sura ya, 66 uk.185).

Theophilus kwa Autolycus (mwaka 168-181/188 BK) kitabu cha 3 sura ya 12, uk.114 inasema, "ilipatikana kwenye manabii na katika injili, kwa sababu wote walinena kwa kuvuviwa na Roho mmoja wa Mungu."

Hegesippus (karibu mwaka 170 BK) Five Books of Commentaries on the Acts of the Church sura ya 3 juzuu ya 8, uk.764 anataja Maandiko ya injili.

Claudius Apollinaris (mwaka 160-180 BK) anataja Mathayo, injili, na torati (Ante-Nicene Fathers juzuu ya 8 sura ya 772).

Irenaeus (mwaka 182-188 BK) "Haiwezekani injili kuwa zaidi au pungufu kwa idadi kuliko jinsi zilivyo . . . ‘nguzo na msingi' wa kanisa ni injili na roho wa uzima; ni inafaa kwa kanisa kuwa na nguzo nne, ili liondoe mauti kupitia kila upande" (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 11.8).

Irenaeus anaongelea "kuzipima injili" kwenye Irenaeus Against Heresies kitabu cha 2 sura ya 22.3, uk.390.

Muratorian canon (karibu mwaka 190-217 BK) Kitabu cha tatu cha injili ni Luka. Orodha ya Muratorian 1 (Kwa hiyo injili za Mathayo na Marko zisizotajwa zinachukuliwa kuwa mbili).

Clement wa Alexandria (mwaka 193-217/220 BK) anataja unabii, injili na maneno ya mitume kwenye Who is the Rich Man That Shall be Saved sura ya 42, uk.604.

Tertullian (mwaka 198-220 BK) anasema Marcion "anafanya bidii kubwa sana kuharibu sifa ya zile injili ambazo ziliandikwa kama vitabu vya kweli, na kwa kutumia majina ya mitume, ili, kwa kweli, kuipa injili yake mwenyewe sifa ambayo anaichukua kutoka kwenye injili za mitume" (Tertullian's Five Books Against Marcion kitabu cha 4 sura ya 3, uk.348). Pia kitabu cha 5 sura ya 2, uk.432 na On the Resurrection of the Flesh sura ya 33, uk.568).

Tertullian (mwaka 198-220 BK) "Au pengine, baada ya yote, alikuwa akizishitumu injili kwa uongo, akisema kwa hakika "Achana na Mathayo, achana na Luka" (Against Praxeas sura ya 1, uk.597).

Hippolytus (mwaka 225-235/6 BK) anazitaja injili kwenye Refutation of All Heresies kitabu cha 6 sura ya 24, uk.85.

Origen (mwaka 225-254 BK) ana sura nzima mbili zinazoelezea sababu ya injili na siyo vitabu vingine huitwa hivyo kwenye Commentary of John kitabu cha 1 sura ya 7,8, uk.300, 301.

Origen (mwaka 225-254 BK) aliongelea Agano Jipya na kusema kulikuwa na injili nne tu (Origen's Commentary on John (mwaka 225-231 BK) kitabu cha 1 sura ya 1, uk.299).

Novatian (mwaka 250-247 BK) "Kwa kuwa unabii wa kale kama injili unamshuhudia kuwa mwana wa Ibrahimu na mwana wa Daudi" (Treatise on the Trinity sura ya 9, uk.618).

Treatise on Rebaptism sura ya 17, uk.677 (mwaka 250-258 BK) "Kwa kuwa ubatizo huu wa kikahaba, naam, wa kiuaji, kama kuna mtunzi yeyote, kwa hakika ni kitabu kilichotungwa na wapotoshaji hawa hawa kwa lengo la kosa lile lile lililoandikwa, The Preaching of Paul kwenye kitabu ambacho, tofauti na Maandiko yote, utamkuta Kristo akiungama dhambi zake mwenyewe—ingawa ni Yeye tu ambaye hakutenda dhambi kamwe—na ni kama alilazimishwa na mamaye Mariamu kuukubali ubatizo wa Yohana bila utashi wake. Pia, baada ya kubatizwa, moto ulionekana kuwa juu ya maji, jambo ambalo halijaandikwa kwenye injili yeyote ile."

Cyprian wa Carthage (mwaka 246-258 BK) anazitaja injili kwenye Barua ya 72 sura ya 17, uk.383.

Dionysius wa Alexandria (mwaka 246-265 BK) anawataja "wainjlisti" wanne kwa majina (Letter to Bishop Basilides orodha ya 1, uk. 94).

Archelaus (mwaka 262-278 BK) anazitaja "injili" kwenye Disputation with Manes sura ya 5, uk.182.

Diodorus (mwaka 262-278 BK) anawataja
"Mtume Paulo na injili" kama msingi wa hoja yake (Disputation with Manes sura ya 45, uk.221).

Adamantius (karibu mwaka 300 BK) awataja watu wanne walioihubiri injili, lakini waliihubiri injili ile ile, kwa hiyo injili ni moja (Dialogue on the True Faith Sehemu ya kwanza sura ya 6, uk.43).

Victorinus wa Petau (aliyeuawa mwaka 304 BK) anasema ulimwengu una vitu vinne, kama zilivyo injili nne, vizazi vinne kutoka Adamu hadi Nuhu, kutoka Ibrahimu hadi Musa, mito minne paradiso, askari wanne wakati wa kusulibiwa kwa Yesu, viumbe hai vinne, na majira manne (On the Creation of the World, uk.341).

Methodius (mwaka 280-312 BK) "Kwa kusudi hili pia injili nne zilitolewa, kwa sababu Mungu alitoa injili mara nne kwa kizazi cha mwanadamu" (Banquet of the Ten Virgins Mahubiri ya 10 sura ya 2, uk.348).

Athanasius (mwaka 318 BK) ananukuru Luk 19:10, "kama Yeye [Yesu] mwenyewe asemavyo kwenye injili: ‘Nilikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea' (Incarnation of the Word sura ya 14, uk.43).

Athanasius (mwaka 318 BK) ananukuru Yoh 3:3, 5, "Yeye [Yesu] mwenyewe anasema kwenye injili: ‘Nilikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea'" (Incarnation of the Word sura ya 14, uk.43).

Alexander wa Alexandria (mwaka 313-326 BK) amtaja Mungu aliyetupa Torati, manabii, na injili (Epistles on the Arian Heresy Waraka wa 1 sura ya 12, uk.295).

Baada ya Nikea Baada ya Nikea

Eusebius' Ecclesiastical History (mwaka 323-326 BK) kitabu cha 3 sura ya 24, uk.152 kinazijadili injili nne, Mathayo, Marko, Luka na Yohana (Nicene and Post-Nicene Fathers Second Series juzuu ya 1, uk.152).

Juvencus (mwaka 329 BK) (kwa sehemu) aliandika shairi la kishujaa akitumia injili nne, lakini hakuziita injili.

Hilary wa Poitiers (mwaka 355-367/368 BK) "Tena injili zinajazia mambo yanayopungua kwenye nyingine: tunajifunza kadhaa kutoka kwenye moja, na mengine kutoka kwa nyingine, na kadhalika, kwa sababu zote ni mahubiri ya roho yule yule" (The Trinity kitabu cha 10 sura ya 42, uk.193).

Athanasius (mwaka 367 BK) "Tena haichoshi kuongelea [vitabu] vya Agano Jipya. Hivi ni injili nne, za Mathayo, Marko, Luka, na Yohana" (Athanasius' Festal Letter 39 sura ya 5, uk.552).

Synopsis Scripturae Sacrae (mwaka 350-370 BK au karne ya tano).

Cheltenham Canon (=Orodha ya Mommsen) (karibu mwaka 360-370 BK) anazitaja injili. Ephraim/Ephrem, mwandishi nyimbo mwenye asili ya Shamu (mwaka 350-378 BK).

Basil wa Cappadocia (mwaka 357-378/379 BK).

Sinodi ya Laodicea (mwaka 343-381, 363 BK).

Cyril wa Yerusalemu (karibu mwaka 349-386 BK) alisema kuwa kulikuwa na injili nne tu kwenye Lecture 4:36, uk.27.

Gregory wa Nazianzen (mwaka 330-391 BK).

Pacian wa Barcelona (mwaka 342-379/392 BK).

Amphilochius Iambi ad Seleucum (kabla ya mwaka 394 BK).

Gregory wa Nyssa (karibu mwaka 356-397 BK) anazitaja injili kwenye Against Eunomius kitabu cha 2 sura ya 4, uk.104, na On Infant Early Deaths, uk.378.

Orodha ya Shamu ya Mt. Catherine (karibu mwaka 400 BK) anazitaja injili.

Epiphanius wa Salamis (mwaka 360-403 BK) anazitaja injili nne, nyaraka 14 za Paulo, Yakobo, Petro, Yohana, Yuda, Matendo, Ufunuo wa Yohana, Hekima za Sulemani na Sirach (=Ecclesiasticus).

Papa Innocent I wa Roma (karibu mwaka 405 BK) anazitaja injili nne.

Rufinus kwenye Commentary on the Apostles Creed (mwaka 374-406 BK) anazitaja injili nne.

John Chrysostom (aliyeuawa mwaka 406 BK) anajadili sehemu ambazo zina injili nne, si moja tu kwenye Gospel of Matthew Homily 1.6, uk.3 (juzuu ya 10).

Orosius/Hosius wa Braga (mwaka 414-418 BK) anazitaja injili Defense Against the Pelagians sura ya 7, uk.123).

Baraza la Carthage (maaskofu 218) (mwaka 393-419 BK).

Sulpicius/Sulpitius Severus (mwaka 363-420 BK) anazitaja injili kwenye Sulpitius Severus Dialog 1 sura ya 26, uk.37 na Dialog 2 sura ya 13, uk.45.

Jerome (mwaka 317-420 BK) anazitaja kila moja ya injili zote nne kwa jina kama timu ya Bwana ya watu wanne kwenye barua 53.9, uk. 101.

Sozomen (mwaka 370-380/425 BK) anazitaja injili katika Sozomen's Ecclesiastical History kitabu cha 2 sura ya 14, uk.267.

Augustine wa Hippo (mwaka 388-430 BK) anazitaja nyaraka za Paulo na kisha vitabu vinne vya injili (On The Profit of Believing sura ya 7, uk.350).

John Cassian (mwaka 419-430 BK)

Vincent wa Lerins (karibu mwaka 434 BK)

Socrates' Ecclesiastical History (karibu mwaka 400-439 BK) kitabu cha 3 sura ya 16, uk.87 anasema Apollinaris alizifafanua injili.

Socrates' Ecclesiastical History (karibu mwaka 400-439 BK) kitabu cha 3 sura ya 20, uk.89 anataja Wayahudi na Torati ya Musa na Kristo kwenye injili takatifu.

Ushahidi wa waasi na vitabu vya uongo

Mwasi wa Kienkrati Tatian (aliyeishi hadi mwaka 177 BK) aliandika mpangilio wa injili nne unaofuata mtiririko halisi wa matukio unaoitwa Diatessaron, ikiwa na maana ya "kupitia nne."

X Megethius (karibu mwaka 300 vurugu), mfuasi aliyejipa jina la ‘mfuasi wa Marcion', kwenye mdahalo wake na Adamantius alisema kuwa anazikana injili nne (Dialogue on the True Faith sehemu ya kwanza sura ya 1, uk.36).

Mwasi mwenye mlengo wa Kipelagia Theodore wa Mopsuestia (mwaka 392-423/429 BK) anukuru Mat 5:23-24 kama ilivyotolewa na Bwana kwenye injili (Commentary on Malachi sura ya 2, uk.410).

Mwasi mwenye mlengo wa Kipelagia Theodore wa Mopsuestia (mwaka 392-423/429 BK) ananukuru Mak 10:2-9 kama, "kutoka kwa Bwana kwenye injili" (Commentary on Malachi sura ya 2, uk.412).

Mwasi mwenye mlengo wa Kipelagia Theodore wa Mopsuestia (mwaka 392-423/429 BK) anadokezea ya Luk 11:42 kama "katika injili" (Commentary on Hosea sura ya 5, uk.63).