Maswali ya Biblia kutoka Waraka wa Wakolosai

 

Swali (S): Kwenye waraka wa Wakolosai, ujumbe mkuu wa kitabu hiki ni nini?

Jibu (J): Kwa kanisa la kiungu lililoingiliwa na theolojia “ya ajabu sana” iliyopelekea kuwafanya watu wajikite kwenye kuabudu malaika, falsafa, nk. badala ya Mungu, ujumbe wa Paulo ulikuwa rahisi sana wenye wazo kuu moja, ingawa lenye matokeo mengi: Kristo pekee ndiye unayemhitaji; kama unaishi ndani ya Kristo, unatakiwa kuwa mfu kwenye mambo mengine. Mambo mengine ya kidini yanaweza kuwa mazuri au yenye kufurahisha, lakini kama yanachukua nafasi ya mapenzi yako kwa Mungu, basi yatakuwa mabaya kwako.

   Kwa kweli ni vigumu kuupata mstari unaotoa muhtasari mzuri zaidi wa kitabu cha Wakolosai, kwa kuwa kuna mihtasari mingi na miziri sana. Baadhi ya mihtasari hii ni Wakolosai 1:17-18; 2:3; 2:6; 2:8-10; 3:1-3; 3:11; 3:17. Binafsi, mihtasari miwili ninayoipenda zaidi ni Wakolosai 2:8-10 na 3:1-3.

 

S: Kwenye waraka wa Wakolosai, muhtasari wa kitabu ukoje?

J: Ufuatao ni muhtasari wenye maelezo mengi kiasi.

Kwa kuwa mmempokea Kristo, endeleeni kwenye injili ya Kristo

I. Utangulizi

…A. Salamu Kol 1:1-2

……1. Kitoka kwa Paulo na Timotheo Kol 1:1

……2. Salamu kwa watakatifu waaminifu walioko Kolosai Kol 1:2

…B. Kumshukuru Mungu kwa ajili yao Kol 1:3-8

……1. Imani na upendo vyao vinatoka kwenye tumaini Kol 1:3-6a

……2. Injili inazaa matunda ndani yao Kol 1:6b-8

…C. Kuwaombea kwa Mungu Kol 1:9-14

……1. Wajazwe ufahamu na kuishi kwa uaminifu na kwa kumpendeza Mungu katika nguvu zake Kol 1:9-11

……2. Wao nao wamshukuru Mungu Kol 1:12-14. (Mabadiliko: Kol 13:b-14)

II. Kuyafahamu mamlaka makubwa zaidi ya Kristo Kol 1:15-23

…A. Ni kwa vipi Kristo pekee ndiye unayemhitaji Kol 1:15-18

……1. Mfano wa Mungu na Bwana wa viumbe vyote Kol 1:15-17

……2. Kichwa cha kanisa na mzaliwa wa kwanza Kol 1:18

…B. Ni kwa nini Kristo pekee ndiye unayemhitaji Kol 1:19-23

……1. Ukamilifu wa Mungu umo ndani yake Kol 1:19

……2. Yesu alikupatanisha Kol 1:20-22

…C. Lakini endapo tu mnaendelea Kol 1:23 (Mabadiliko: Paulo ni mtumwa wa injili yake Kol 1:23b)

……1. Endeleeni katika imani na tumaini la injili Kol 1:23a

……2. Injili mliishaisikia na ikihubiriwa na Paulo Kol 1:23b

Endeleeni katika Kristo, hivyo msichukuliwe mateka

III. Juhudi na kazi ya Paulo kwa ajili yao Kol 1:24-2:7

…A. Mambo ambayo Paulo anafanya kwa ajili yao Kol 1:24-29

……1.Kufurahi katika mateso ya Paulo Kol 1:24

……2. Mtumishi akihibiri fumbo Kol 1:25-29

…B. Kwa nini Paulo alikuwa anasumbuka Kol 2:1-5

……1. Ni kitu gani kinachomsumbua Paulo Kol 2:1-3

……2. Paulo anapambana na kitu gani Kol 2:4-5

…C. Endeleeni kuwa na mizizi na kujengwa katika Kristo Kol 2:6-7

……1. Endeleeni kuishi ndani ya Kristo Kol 2:6

……2. Mkiwa na mizizi na kujengwa katika imani waliyofunzwa na shukrani Kol 2:7

IV Kusimama na Kristo dhidi ya makosa ya zamani Kol 2:8-3:4

…A. Hakuna kutumaimi vitu vya kibinadamu, bali Kristo

……1. Si falsafa ya kibinadamu bali ukamilifu wa Kristo Kol 2:8-10

……2. Si tohara ya kibinadamu bali ubatizo unaofanywa na Kristo Kol 2:11-12

…B. Si kudumu katika dhambi au taratibu, bali Kristo

……1. Si kufa katika dhambi, bali kuwa hai katika Kristo kwa ushindi wa msalaba Kol 2:13-15

……2. Si kivuli cha taratibu za zamani, bali uhalisi wa Kristo Kol 1:16-17

…C. Si kufurahia amri au malaika, bali Kristo

……1. Si unyenyekevu wa uongo na kuabudu malaika Kol 1:18-19

……2. Tunamhitaji Kristo, hivyo si sheria za kujinyima anasa za kimwili Kol 2::20-23

Kwa kuwa mmekufa na kufufuka na Kristo, ishini ndani ya Kristo

V. Maisha mapya ndani ya Kristo Kol 3:1-4:6

…A. Maisha ya ndani: mmekufa kwa nafsi zenu, mnaishi ndani ya Kristo Kol 3:1-3:17

……1. Yafisheni mambo ya dunia Kol 3:1-9

……2. Maisha yetu yamefichwa ndani ya Yesu Kol 3:10-17

…B. Mahusiano ya kifamilia na kikazi Kol 3:18-4:7

……1. Ndoa na familia Kol 3:18-21

……2. Watumwa na mabwana wao Kol 3:22-4:1

…C. Mawasiliano Kol 4:2-6

……1. Kujitoa kuomba Kol 4:2-4

……2. Kuongea na watu wengine kwa hekima Kol 2:5-6

VI. Salamu za mwisho Kol 4:7-18

…A. Salamu kutoka kwa Paulo na marafiki wake Kol 4:7-15

……1. Tikiko na Onesmo wanakuja Kol 4:4-9

……2. Paulo na watu wengine sita wanawasalimu Kol 4:10-15

…B. Maagizo ya Paulo na baraka Kol 4:16-18

……1. Badilishaneni nyaraka na Walaodikia Kol 4:16

……2. Arkipo fanya kazi yako Kol 4:17

…C. Maneno ya mwisho ya Paulo Kol 4:18

……1. Mwandiko wake Paulo mwenyewe akiwa gerezani Kol 4:18a

……2. Neema kwao Kol 4:18b

 

S: Kwenye waraka kwa Wakolosai, kuna uhusiano gani na kitabu cha Waefeso?

J: Kuna mambo mawili yanayofanana na tofauti kuu moja.

Kuhusu muda, “…kwa hakika hakuna muda mrefu unaozitenga nyaraka hizi mbili” kwa mujibu wa The Expositor’s Bible Commentary juzuu ya 11 uk.166.

Kuhusu mambo yanayoongelewa, karibu robo ya mambo yaliyomo kwenye waraka wa Wakolosai yanalingana na mambo yaliyomo kwenye waraka wa Waefeso.

Lakint, Paulo hawakemei Waefeso, bali kwenye Wakolosai anawapinga mkazo uliopitiliza wa sheria wa mchanganyiko wa Uyudaiza na Uebioni, Uastesizia (kujikana nafsi kuliko pitiliza kunakoenda pamoja na kujiepusha na aina zote za anasa zisizotakiwa wala kuruhusiwa kwa sababu za kidini), na kuabudu malaika. Kuna wanazuoni wanaosema kuwa waraka huu ulikuwa na maonyo dhidi ya Unostasia (harakati maarufu ya kizushi ya zama za kanisa la kikristo la karne ya pili BK iliyokazia kuwa mada ni ovu na kuwa uhuru unapatikana kwa ufahamu) uliyokuwa kwenye hatua za awali. Waandishi wa awali wa kikristo waliamini kuwa kwa sehemu Unostisia wa baadaye ulianzishwa na Simoni Msamaria kwenye Mdo 8:9-25. Unostasia wa awali unatofautiana na Unostasia wenyewe kwa kuwa Unostasia wa awali haukulikana Agano la Kale kuwa lilitokana na Mungu tofauti.

 

S: Kwenye waraka wa Wakolosai, je Paulo anapingana na Unostasia wa awali?

M: Hapana, lakini hebu tulielewe swali kwanza.

   Dini za Kinostisia zilikuwa sehemu ya kundi la mchanganyiko wa dini zaidi ya 30 za kipagani, kikristo wenye asili ya Kigiriki ambao ulikuwa unapingana na Agano la Kale. Madhehebu tofauti ya Unostasia yaliungana kwenye mambo haya: yaliamini kuwa Mungu wa Agano la Kale alikuwa na nia mbaya au mjinga, ulimwemgu uliumbwa muovu/wenye giza/chini kuliko ulimwengu wa kiroho ulio sirini, walikuwa na mkusanyiko wa miungu ya Kigiriki uliofafanuliwa vizuri sana na miungu mingine iliyovumbuliwa karibuni, na wao tu walikuwa na ufahamu wa siri unaohitajika ili kujiunga na miungu na kuuepuka ulimwengu huu wa kimwili. Baadhi yao walikuwa Waasetizia na wengine walikuwa waasherati. Wanostasia wa awali walitofautiana na Wanostasia wenyewe kwa kuwa Unostasia wa awali haukulikana Agano la Kale kuwa limetoka kwa Mungu tofauti. Waandishi wa awali wa kikristo waliamini kuwa kwa sehemu Unostisia wa baadaye ulianzishwa na Simoni Msamaria kwenye Mdo 8:9-25.

   Baadhi ya wanazuoni wanadai kuwa waraka wa Wakolosai unaweza kuwa unaupinga Unostasia wa awali kwa sababu unaongea dhidi ya 1) kuabudu malaika, 2) Kupunguza ukuu wa Kristo unaozidi wengine wote, 3) Kristo ndiye mpatanishi pekee, 4) taratibu za kidini, 5) Uastesizia, na 6) ufahamu uliofichika (wa siri). Pia, Marcion, mwanzolishi wa Unostasia, alikuwa Mfrigia kutoka Ponto, kaskazini mwa Kolosai. Angalia The Expositor’s Bible Commentary juzuu ya 11 uk.166, The NIV Study Bible uk.1811, Believer’s Bible Commentary uk.1986-1987.

   Hata hivyo, siafiki kwa sababu mambo haya sita yaliyotolewa tahadhari kwenye waraka wa Wakolosai yalikuwemo kwenye madhehebu ya Kiyahudi na/au Wajudaiza/Waebioni pia. Sababu ya pili na ambayo ni muhimu pia, ingawa Marcion alivikataa vitabu vingi vya Agano Jipya, alikubali kuwa Paulo ndiye mwandishi wa waraka kwa Wakolosai, hivyo Marcion anaashiria kuwa hakuna mafundisho bayana yaliyolenga kuupinga Unostasia.

 

 

 

S: Tunafanamu kitu gani kuhusu mji wa Kolosai?

J: Kolosai ulikuwa mji mkubwa uliokuwa maili 100 mashariki ya Efeso kwenye Mto Lycus. Upo kiasi cha maili 12 tu kutoka Hierapoli na Laodikia. Miji hii mitatu ilikuwa na madini na maeneo mazuri ya kulishia mifugo, lakini ilikuwa inapitiwa na tetemeko la ardhi mara kwa mara. Kwa kadri ushawishi wa Kigiriki ulivyokuwa unaenea kuelekea mashariki baada ya ushindi wa Alexander wa Makedonia, Kolosai uliendelea kuwa mahali wanapolinda askari mbali na kundi kuu la jeshi pa Wafrigia na Walidia, ingawa Wagiriki nao pia walioshi hapo. Kwenye karne ya 2 KK mfalme wa Seleusidi  Antiochus III aliwalazimisha Wayanudi kuishi Kolosai.

 

J: Kwenye Kol 1:3, kwa kuwa kuna Mungu na Baba wa Yesu, kwa hiyo Yesu anawezaje kuwa Mungu?

S: Hapa kwa kweli kuna maswali mawili yaliyowasilishwa kama moja. Kwanza, Yesu anawezaje kuwa Mungu, na la pili kuwa chini ya Baba. Hebu tuangalie sehemu ya kwanza hapa; sehemu inayofuata itajibiwa kwen sanamu ye swali linalofuata.

   Kwenye Biblia, neno “Mungu/mungu” linaweza kumaanisha ya uongo, au Mungu Mmoja wa Kweli. Lakini linapomaanisha Mungu Mmoja wa Kweli, linawezakuwa na maana nne. Linawezakuwa linamungelea Mungu Baba tu, Yesu tu, Mungu Mwana, na Kwenye Matendo ya Mitume, Roho Mtakatifu tu. Maana ya nne ni kuwa inawezakuwa linawaongelea wote watu kwenye. Hivyo kwa hiyo, kwenye Yohana 1:1, wakati Yesu (Neno), alipokuwa “na Mungu”, neno Mungu hapo linamuongelea Mungu Baba, lakini baadaye kwenye mstari huo huo unaposema neno “alikuwa Mungu”, ni Mungu Mmoja katika Utatu.

   Waebrania 1:9 pia inaonyesha maana tofauti tofauti za neno “Mungu” inaposema “Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta.” Fundisho la Utatu Mtakatifu linazitaja nafsi tatu tofauti, Mungu Baba, Mungu Mwana, Mungu Roho Mtakatifu, na Mungu Mmoja wa Pekee katika Utatu.

   Kwa hiyo kwenye Wakolosai 1:3 tunafahamu kuwa neno “Mungu” hapa linamuongelea Mungu Baba tu.  

 

S: Kwenye Kol 1:3, ni kwa vipi Baba sasa ni Baba wa Yesu?

J: Kwanza nitasema jambo lisilo kuwa jibu, kisha jibu.

Duniani, Yesu alipofanyika mwili kama mwanadamu, Yesu kwa hiari “alijifanya kuwa hana utukufu” aliokuwa nao kabla ya kuja duniani, kama ambavyo Wafilipi 2:7 na Yohana 17:5 zinavyotuambia. Wakati Yesu yupo duniani, alikuwa mtiifu kwa Baba kwenye jukumu lake kama Mungu wake. Lakini, kwenye Yohana17:5, Yesu alipomwomba Baba ampe utukufu aliokuwa nao kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Inasadikiwa kuwa Baba alijibu ombi lake hilo kama alivyomwomba, hivyo Yesu alijifanyaje kuwa hana utukufu, wakati alipokuwa duniani, ni swali lisilokuwa na maana hapa.

   Kwenye 1 Wakorintho 15:23-28 Biblia inasema kuwa kwenye siku za mwisho, baada ya Milenia (miaka elfu moja ya utawala wa Yesu hapa duniani), Mwana“atatiishwa” chini ya Baba, ambaye ameweka vitu vyote chini ya miguu yake. Hivyo, hata sasa Mwana analo jukumu chini ya Baba.

   Je jambo hili linamaanisha kuwa Mwana ni “mdogo” – hapana. Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wako sawa ki asili (tabia za msingi), utukufu, na heshima. Lakini ni dhahiri kuwa wana majukumu tofauti: kwa mfano, Mwana ndiye aliyemuomba Mungu kwenye bustani ya Getsemani, siyo kinyume cha hivyo. Si Roho Mtakatifu, Bali Mwana, aliyesema pale msalabani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” kwenye Mathayo 27:46 na Marko 15:35. Haiwezekani kuwa ni Baba ndiye aliyesema “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui walitendalo”, kwenye Luka 23:34.

  Lakini kama ambavyo wanatofautiana kwenye makukumu, ndivyo wanavyotofautiana kwenye mamlaka. Baba ndiye aliyemtuma Mwana, si kinyume na hivyo. Baba na Mwana ndio waliomtuma Roho Mtakatifu, siyo kinyume cha hivyo.

   Hakuna kitu duniani kinachofanana kabisa na Utatu Mtakatifu. Lakini kitu kimoja ambacho tunaweza kukifananisha kwa kiasi fulani ni uhusiano wa baba na mwanae wa kiume. Mtoto wa kiume “analingana na baba yake kwa asili, mbele ya sheria. Kama baba angekuwa mkuu kuliko mwanae wa kiume, na babaye angekuwa mkuu kuliko mwanae wa kiume, na kadhalika na kadhalika, basi babu wa babu wa babu wa babu yake alikuwa mtu mwenye uwezo kupita kiasi! Hapana, sisi sote tu sawa kiasili. Hata hivyo, kwenye uhusiano wa baba na mwanae wa kiume kuna utofauti wa majukumu, na kuna utofauti wa mamlaka.

   Jambo la kuzingatia kihistoria ni kuwa mtheolojia mmoja mkristo wa zamani aliyeona jambo hili wazi alikuwa Tertullian (aliyeandika mwaka 200-240 BK). Mtheolojia mwimgine mkristo wa zamani, ambaye hakukubaliana na wazo kuwa kuna utofauti wowote wa mamlaka ni Ambrose wa Milani (aliyeishi mwaka 370-390 BK). Hawa wote waliamini Utatu Mtakatifu, na maoni yao wote yanaendana na Imani ya Mitume na Imani ya Nikea. Lakini katika imani ya pamoja ya Utatu Mtakatifu, kuna tofauti hii ya pili.

 

S: Kwenye  Kol 1:3, ni kwa vipi Mtume Paulo alikuwa anawaombea watu ambao hakuwahi kukutana nao?

J: Mtume Paulo aliwaombea kila siku alipowakumbuka. Kama ambavyo The Tony Evans Bible Commentary uk.1252 inavyosema kwa kupendeza, “huhitaji kupikwa kwa haraka na kwa kutumia muda mfupi na Mungu; unahitaji kupikwa polepole na kwa kutumia muda mrefu na Mungu. Jipashe moto polepole kwenye uwepo wake, na yaguse maisha ya watu wengine kwa mguso ambao Mungu amekugusa nao.”

 

S: Mkosoaji wa Biblia Bart Ehrman anasema, “Wakolosai 1:3-8 ni sentensi moja kwenye Kigiriki; ni uongo ulio wazi, na ni aina ya sentensi ambayo haifanani kabisa na sentensi ambazo Mtume Paulo alikuwa na desturi ya kuandika.” (Jesus, Interrupted uk.126).

J: Waraka wa Wakolosai hautofautiani sana na vitabu vingine vya Mtume Paulo. Kihistoria, hakuna mtu aliyetia shaka kuwa Paulo ndiye maandishi wa waraka huu hadi Meyerhoff alipotia shaka mwaka 1838, kwa mujibu wa The Expositor’s Greek Testament juzuu ya.3 uk.488. Nimeshtushwa kuona kuwa Ehrman hatoi sababu ya kulinganisha. Nimetoa sababu moja hapa chini. Kwa kuwa watu wachache wanafikiri kuwa Waraka kwa Waebrania unawezakuwa uliandikwa na Mtume Paulo, nimeuweka pia. Injili ya Luka na Kitabu cha Matendo ya Mitume vinakubalika kuwa viliandikwa na mwandishi mmoja, kwa hiyo hivyo navyo vimewekwa kwa lengo la kulinganisha.

Sentensi

Maneno kwenye sentensi ndefu zaidi

Wastani kwenye sentensi ndefu zaidi 3

Jumla ya maneno ya Kigiriki kwenye kitabu

Maandiko. Haya yanatoka kwenye toleo la nne la Aland na wenzake (Aland et al. 4th edition)

2 Wathesalonike

158,  57,  54

90

823

2 The 1:3-10; 2:8-10; 2:1-3a

Wakolosai

157, 123, 102

127

1,582

Kol 1:11b-20; 1:24-29; 1:3-8

Warumi

139, 123, 113

125

7,111

Rum 9:19-26; 4:16-21; 2:2-8

Waebrania

135,  72,  65

91

4,953

Ebr 8:8-12; 1:1-4, 2:2-5

Waefeso

124, 124, 104

117

2,422

Efe 2:1-7; 4:11-16; 3:1-7

2 Wakorintho

118, 102,  94

105

4,477

2 Kor 6:2b-10; 9:10-14; 8:1-6

2 Timotheo

105,  61,  52

73

1,238

2 Tim 1:8-12; 1:3-5; 2:23-26

1 Wathesalonike

104,  81,  70

85

1,481

1 The 3:9-13; 1:2-5; 4:15-17

1 Wakorintho

  95,  84,  82

87

6,830

1 Kor 1:20-25; 9:4-9a; 14:6-9

Filemoni

  94,  47,  41

62

335

Flm 8-14; 4-6; 1-3

Wagalatia

  94,  77,  75

90

2,230

Gal 2:6-10; 2:14-16; 1:1-5

Wafilipi

  88,  82,  79

127

1,629

Flp 1:3-7; 1:27-30; 3:8-11

1 Timotheo

  71,  57,  56

61

1,591

1 Tim 6:13-16; 3:2-6; 1:8-11

Tito

  65,  64,  57

62

659

Tit 1:1-4; 2:1-14; 3:4-7

Luka 1-7

165,  95,  77

109

5,960

Lk 3:23-28; 1:67-75; 3:15-17

Matendo 1-6

108,  89,  87

95

3,582

Mdo 4:5-10; 3:12-15; 1:1-5

Matendo 7-11

  72,  65,  64

67

3,971

Mdo 7:38-40; 10:36-38; 7:44-46

Ehrman anakubali kuwa vitabu vyenye maandishi ya italiki vina uwezekano mkubwa wa kuwa viliandikwa na Mtume Paulo. “Uongo” wenye maneno 102 kwenye Wakolosai 1:3-8 si mfupi kuliko mistari mingine ya kwenye Waraka wa Wakolosai, lakini mfupi kuliko mistari mingine mingi kwenye vitabu ambavyo Ehrman anakubali kuwa viliandikwa na Mtume Paulo. Sentensi ndefu zaidi kwenye kila kitabu na vitabu vipi anakubali kuwa viliandikwa na Mtume Paulo linaonekana kuwa jambo la kubahatisha.

   Kwa hiyo unaweza kusema nini kuhusu mwandishi wa kitabu kwa kuangalia urefu wa hizi sentensi? Ukiangalia kitabu kimoja au viwili tu, kimsingi unaweza kusema kitu chochote unachotaka kusema. Lakini ukiangalia vitabu vyote, kundi hili halisemi kitu chochote kuhusu mwandishi wa vitabu hivi.

   Ehrman hapingi kama mtu asiyekuwa na ufahamu kuhusu jambo hili; Waislamu wawili tofauti wameniambia kuwa Ehrman mtaalamu mkubwa zaidi wa Agano Jipya kwa sasa. Sielewi ni vipi mtu anayedai kuwa mtaalamu wa Agano Jipya atoe hoja hii ya urefu wa sentensi ndefu zaidi, labda kama hakuwa anaangalia muda kitabu kilipoandikwa kama mwanazuoni makini.


 

S: Kwenye Kol 1:7 na Flm 23, Epafra ni nani?

J: Hili ni ufupisho wa jina  Epaphroditus. Hata hivyo, Epaphroditus lilikuwa jina lililokuwa linatumiwa  sana na watu, kwa hiyo, huyu anaweza kuwa ni mtu yuleyule kwenye Flp  2:25-30 na 4:18, au mtu mwingine.

   Epafra alihubiri kwa Wakolosai ujumbe wa injili kwa uaminifu kama alivyojifunza kwa Paulo. Mtume Paulo anamsifia yeye pamoja na Wakolosai waaminifu. Lakini baadhi ya sehemu zilizofuata za Waraka huu zinaonyesha kuwa kuna baadhi ya Wakolosai ambao hawakuwa na uhakika kama Epafra aliwapa “maelezo yote” au kulikuwa na mambo ya msingi ambayo walitakiwa kujifunza, kama ambavyo waalimu wa uongo wanawezakuwa waliwaambia.

   Mwisho, Paulo aliwezaje kujua baadhi ya matatizo yaliyoko kwenye kanisa ambalo hajawahi kulitembelea? Huenda Epafra alimtembelea Paulo na kumwambia.

 

S: Kwenye Kol 1:9-20, sentensi hii inatakiwa iishie wapi?

J:Maandiko ya mwanzo ya Kigiriki hayakuwa yanatumia alama zozote zile, hivyo inakuwa vigumu kutambua. Lakini, kwa mujibu wa Greek New Testament by Aland et al. toleo la 4, na Nestle-Aland UBS toleo la 28th, Wakolosai 1:9-11a ni sentensi moja, na 11b-20 ni sentensi ya pili. Lakini, kwa mujibu wa toleo la 3, Wakolosai 1:9-17 ni sentensi moja na 1:18-20 ni sentensi ya pili. Toleo la 5 lina 1:9-20 kama sentensi moja. Msomaji mmoja mwenye msaada alisema Wakolosai 1:9-20 inaweza ikachukuliwa kuwa sentensi moja kwa sababu ya mambo haya mawili yanayoishuhudia:

a) Hakuna kitenzi kwenye mistari ya  11b-20, na

b) Michoro ya Agano Jipya ya Leedy kwenye program ya kompyuta ya Bibleworks pia inaonyesha kuwa Wakolosai 1:9-20 ni sentensi moja.

Hoja inayochanganya mjadala huu ni ile ya watheolojia wachache inayosema kuwa Mtume Paulo anaweza kuwa alichukua sehemu ya mistari hii kutoka kwenye wimbo uliokuwepo wakati ule uliyokuwa unafahamika na Wakristo wa kwanza, ambao The Message of Colossians and Philemon Revised Edition & Philemon Revised Edition uk.28 ya Dick Lucas inauelezea kwa ufupi.

 

S: Kwenye Kol 1:10, tunawezaje kuenenda kama ulivyo wajibu wetu kwa Bwana kwa kuwa tunaokolewa kwa neema?

J: Kuokolewa sio mwisho wa uhusiano wetu na Mungu; ni mwanzo tu. Kama waumini, hatuhimizwi tu bali tunaamriwa kuishi maisha matakatifu (1 Petro 1:15-16). Hatujaamriwa kupata wokovu katika uhusiano wetu na Mungu, bali tumeamriwa na kupewa nguvu kufanya hivyo kutokana na kuzaliwa kwetu upya katika uhusiano wetu na Mungu.

 

S: Kwenye Kol 1:11, je anaonekanaje mkristo ambaye hajatiwa nguvu na uweza wote wa Kristo??

J: Mtu huyo anaweza kuamini,kuomba, na kufanya mambo mengine ya kiungu, lakini nguvu, uvumilivu, ustahimilivu, na furaha havimo ndani yake. Huenda akawa anajaribu kuishi maisha ya kikristo kwa nguvu zake mwenyewe, badala ya nguvu ya Kristo. Unatakiwa uweze “Kuachia mambo unayofanya na kumuachia Mungu afanye.”

 

S: Kwenye Kol 1:12, tumewezaje kustahilishwa kupokea sehemu ya urithi wa mbinguni?

J: Kama waumini sote tunafahamu kuwa hatustahili kwa nafsi zetu wenyewe kwenda mbinguni. Dhambi moja tu, wakati wowote wa maisha yetu itatutenga na neema ya Mungu. Lakini jambo ambalo Tunaweza tushindwe kulitambua ni kuwa si tu kwamba hatustahili kwenda mbinguni kwa nafsi zetu wenyewe, lakini hatujakidhi vigezo vya kwenda mbinguni kwa nafsi zetu wenyewe.

   The Believer’s Bible Commentary uk.1993 inaongea vizuri sana: “Kwa kweli, kama watu ambao hawajakombolewa wangepelekwa mbinguni, wasingekufurahia sana, lakini wangependelea kuwa kwenye mateso makubwa zaidi. Ili mtu apapende mbinguni anahitaji kukidhi vigezo vya kwenda huko. Hata waumini wa Bwana Yesu, hatujakidhi vigezo vya kwenda mbinguni kwa namna yeyote ile kwa nafsi zetu wenyewe …. Mungu anapomuokoa mtu, humuwezesha mara hiyo kukidhi vigezo vya kwenda mbinguni. Kukidhi huko kwa vigezo ni Kristo. Hakuna kitu chochote chenye kuweza kuboresha jambo hilo. Kwa hiyo, hata mtu aliyempokea Yesu, na akauawa muda mfupi baadaye, bado atakuwa amekidhi vigezo vya kwenda mbinguni.

 

S: Kwenye Kol 1:15-18 na Ebr 1:6, kama Yesu hakuumbwa na si kiumbe, ni kwa vipi basi Yesu ni “mzaliwa wa kwanza wa viumbe wote”? (Mashahidi wa Yehova wanaleta hoja hii)

J: Neno la Kigiriki hapa, prototokos, linamaanisha mwenye kushinda wengine wote/vingine vyote. Sisi ni kaka na dada wa Kristo, lakini Kristo ni mzaliwa wa kwanza anayewashinda wote.

   Kwenye nyakati za Biblia, neno mzaliwa wa kwanza halikumaanisha mtu wa kwanza kuzaliwa tu, bali urithi na haki ya kuzaliwa vya mzaliwa wa kwanza. Jehovah’s Witnesses Answered Verse by Verse uk.97-98 inasema kuwa kama mfano wa “mzaliwa wa kwanza” haumanaishi mtoto wa kwanza kuzaliwa, Zaburi 89:27 inasema Daudi atateuliwa kuwa mzaliwa wake wa kwanza, ingawa Daudi alikuwa mtoto wa mwisho kuzaliwa kwa Yese.

   Kama ambavyo When Critics Ask uk.485 kinasema, Kristo si mzaliwa wa kwanza kwa kuumbwa, bali mzaliwa wa kwanza kwa viumbe. Kristo si wa kwanza kuzaliwa duniani (watu wa Agano la Kale walimtangulia) lakini Kristo ni mzaliwa wa kwanza kwa kufufuka na kwa kuwa mrithi wa vitu vyote.

   Swali hili pia lilijibiwa na Athanasius wa Alexandria huko nyuma karibu mwaka 330 BK. Alisema kwamba kwa kuwa Kristo ni Mwana pekee na mzaliwa wa kwanza, mambo haya mawili yanaongelea maana mbili za Kristo. Baada ya kutofautisha kati ya “kuumbwa” na “kuzaliwa”, Athanasius wa Alexandria anaonyesha kuwa Mwana pekee inamaanisha kuwa Yesu alitoka kwa Baba, wakati mzaliwa wa kwanza inamaanisha ukuu wake unaowashinda wanadamu wote na ukuu wake juu ya watu wote waliozaliwa upya. Ili kupata andiko lote lenye maelezo ya kina ya hoja ya Athanasius, tazama Four Discourses Against the Arians Discourse II sura ya 21 kifungu 57-60.

   Lakini, kabla ya Athanasius, Hippolytus wa Rumi (aliyeandika mwaka 222-235/6 BK) alijibu hoja hii kwenye ufafanuzi wake wa Luka 2:7. Alisema, “Na kama itakupendeza, tunasema kwamba Neno alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Mungu, aliyetoka mbinguni na kuja kwa Mariamu mbarikiwa, na alifanywa kuwa mzaliwa wa kwanza mwanadamu kwenye tumbo la Mariamu, ili kwamba mzaliwa wa kwanza wa Mungu adhihirishwe kwa pamoja na mzaliwa wa kwanza mwanadamu.”

 

S: Kwenye Kol 1:15, 18 ni vyanzo vipi vinavyoonyesha kuwa neno la Kigiriki prototokos lina maana zaidi ya mzaliwa wa kwanza kimwili au wa kwanza kuumbwa?

J: Nimemuuliza mhadhiri wa Dallas Seminary, na nimeona kamusi za Kigiriki za kisasa zikisema kuwa neno prototokos (Strong’s Concordance 4416) linaweza kumaanisha wa kwanza kwa cheo au kitu kingine mbali ya kuzaliwa kimwili au wa kwanza kuumbwa kwa mujibu wa Baur-Arndt-Gingrich-Danker na Lyddell-Scott-Jones.

Kwenye Agano la Kale, kwenye Yeremia 31:9 Mungu anaita “Efraimu mzaliwa wangu wa kwanza.” Lakini, kwenye Mwanzo 48:17-19 Manase alizaliwa kabla ya Efraimu, lakini Efraimu alipokea baraka za mzaliwa wa kwanza kutoka kwa Yakobo. Zaburi 89:27 inasema Daudi atachaguliwa kuwa mzaliwa wake wa kwanza, ingawa Daudi alikuwa mzaliwa wa mwisho wa Yese.

  Kwenye baadhi ya sehemu, wakristo wa mwanzo hawakutumia neno prototokos kumaanisha mzaliwa wa kwanza kimwili. Epistle of Barnabas (karibu mwaka 70-130 BK) sura ya 13 uk.145 inawaongelea Manase na Efraimu, na 1 Clement (mwaka 96-98 BK) sura ya 4 juzuu ya 1 uk.6 inamuongelea mzaliwa wa kwanza wa kondoo wa Habili.

   Neno hasa la Kigiriki HALIMAANISHI bayana mzaliwa wa kwanza wa kimwili au wa kwanza kuumbwa kwenye Epistle of Polycarp to the Philippians (mwaka 100-155 BK) sura ya 7 uk.35. “‘Kwa kuwa mtu yeyote asiyekiri kuwa Yesu Kristo amekuja katika mwili, ni mpinga Kristo’ na yeyote asiyekiri ushuhuda wa msalaba, ni wa ibilisi; na yeyote anayepotosha maneno ya Bwana kwa ajili ya tamaa zake mwenyewe, na anasema kuwa hakuna ufufuko wala hukumu, huyu ni mzaliwa wa kwanza wa shetani.”

   Pia, Irenaeus wa Lyons (mwaka 182-188 BK) aliandika, “Na Polycarp mwenyewe alimjibu Marcion, aliyekutana naye siku moja, na alisema, ‘Je hunijui mimi?’ ‘Sikujui, mzaliwa wa kwanza wa shetani’ Hili ndilo tishio ambalo mitume na wanafunzi wao walilokuwa nalo dhidi ya kuzuia hata mawasiliano ya mdomo kwa mdomo na watu wenye” (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 3.4 uk. 416).

Adamantius (karibu mwaka 300 BK) anasema, “Inasema, ‘Hakuna aliyepanda kwenda mbinguni, isipokuwa yule aliyeshuka kutoka mbinguni’. Yeye ‘aliyeshuka’ inaonyesha wakati uliopita. Haisemi kuwa hakuna mtu atakayepanda, lakini ‘hakuna aliyepanda.’ Hivyo, inadhihirisha wazi kuwa kabla ya Kristo hakuna aliyepanda. Hivi ni kama Mtume Paulo anavyosema, ‘mzaliwa wa kwanza’; na tena, ‘malimbuko yao waliolala.’ Lakini anaendelea kusema, ‘mazao ya kwanza, Kristo; kisha wale walio wa Kristo’ (Dialogue on the True Faith fifth sehemu za 855b uk.157).

Athanasius wa Alexandria (aliyeishi mwaka 326-373 BK) “kama ambavyo Paulo mahali pengine anavyomuita’mzaliwa wa kwanza wa viumbe wote’’ (Kol 1:15). Lakini kwa kumuita yeye Mzaliwa wa kwanza, anaonyesha kuwa si Kiumbe, bali mzaliwa wa Baba. Kwa sababu itakuwa kinyume na uungu wake kwa Yeye kuitwa kiumbe. Kwa sababu vitu vyote viliumbwa na Baba kupitia kwa Mwana, lakini Mwana peke yake milele amefanywa kuwepo na Baba, kutoka kwa Mungu Neno ni ‘mzaliwa wa kwanza wa viumbe wote,’ yeye asiyebadilika kutoka kwake asiyebadilika. Lakini, mwili aliouvaa kwa ajili yetu ni kiumbe” (Statement of Faith sura ya 3 uk.85).

John Chrysostom (alikufa mwaka 407 BK) anajadili kirefu kuhusu Yesu kuwa mzaliwa wa kwanza. Baada ya kutofautisha kati ya Kristo kuitwa “mzaliwa wa kwanza” lakini sio “wa kwanza kuumbwa”, anasema maana moja ni “mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu” (Kol 1:18; Rum 8:29) inaongelea ufufuko wa kwanza. “Pia neno ‘mzaliwa wa kwanza,’ kwa maana ya msingi. Lakini jambo hili halionyeshi kuwa viumbe wana asili moja na Yeye; lakini kuwa vitu vyote vimekuja kupitia kwake, na kuwa vinashikiliwa ndani yake.” (Homilies on Colossians Homily 3 uk.270-271).

 

S: Kwenye Kol 1:15-20, je maneno haya yenye theolojia ya juu sana na iliyo endelea [kwa kiasi fulani] yanaonyesha kuwa Mtume Paulo hakuwa mwandishi wa Waraka wa Wakolosai? (Bart Ehrman anadai hivi kwenye uk.127).

J: Hapana. Ehrman anadai kuwa baadhi ya nyaraka ziliandikwa na Mtume Paulo na nyingine hazikuandikwa naye. Wakati Kol 1:15-20 ni kifungu muhimu sana, nyingi ya dhana na misemo 18 hapa inafanana na mambo mengine ambayo Paulo aliyaandika, au yanafanana angalau na mistari mingine ya kwenye Biblia.

“Yesu ni mfano wa”

Kol 1:15a

-

“Mungu asiyeonekana”

Kol 1:15a

1 Tim 1:17b; Heb 11:27

“Mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.”

Kol 1:15b

Rum 8:29; Ebr1:6

Katika Yeye vitu vyote viliumbwa

Kol 1:16a

1 Kor 8:6b

Vinavyoonekana na visivyoonekana [hapa haongelewi Mungu]

Kol 1:16b

Ebr 11:3

Enzi, usultani, watawala, mamlaka

Kol 1:16c

Efe 1:21

“Naye amekuwako kabla ya vitu vyote”

Kol 1:17a

Flp2:9

“Na vitu vyote hushikana katika Yeye”

Col 1:17b

Ebr 1:3b

“Naye ndiye kichwa cha mwili”

Kol 1:18a

1 Kor 12:12-13,27

“Kanisa”

Kol 1:18a

Efe 5:23

“Naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu”

Kol 1:18b

-

Kristo ana mamlaka kuu zaidi juu ya wote

Kol 1:18c

1 Kor 1:27a; 27f

“Kwa kuwa katika Yeye ilipendeza” [Ilimpendeza Mungu]

Kol 1:19a

1 Kor 1:21b

“Utimilifu wote ukae (kwake)” [Kristo]

Kol 1:19b

Efe 1:23; ~Yoh 1:16

Na kwa Yeye kuvipatanisha vitu vyote

Kol 1:20a

Rum 5:10; 2 Kor 5:19; Efe 2:16

“Akiisha kufanya amani”

Kol 1:20b

Rum 5:1; Efe 2:14

“Kwa damu”

Kol 1:20b

Rum 3:25; 5:9; Efe 1:7; 2:13

“Ya msalaba wake”

Kol 1:20c

Ebr 9:22

 

 

 

Sehemu nyingine kwenye Wakolosai kuna dhana zinazofanana na hizi.

 

Fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu

 

Kol 3:17

1 Kor 10:31

Dumuni sana katika kuomba

Kol 3:2; 4:2

1 The 5:17

Hapo hapana Myunani wala Myahudi . . . mtumwa wala muungwana

Kol 3:11

Gal 3:28

Kutahiriwa wala kutokutahiriwa

Kol 3:11

Gal 5:6

Zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni

Kol 3:16

Efe 5:19

Wake watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana

Kol 3:18

Efe 5:22

Waume wapendeni wake zenu

Kol 3:19

Efe 5:25

Watoto watiini wazazi wenu katka mambo yote

Kol 3:20

Efe 6:1

Akına baba msiwachokoze watoto wenu

Kol 3:21

Efe 6:4

Ninyi watumwa watiini bwana zenu, si kwa kujipendekeza kwa wanadamu, bali kwa kumcha Mungu

Kol 3:22

Efe 6:5-6

Akina Bwana wapeni watumwa wenu yaliyo haki

Kol 4:1

Efe 6:9

Tuinene siri ya Kristo

Kol 4:3

 

Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje.

Kol 4:5

 

Onesimo

Kol 4:9

Filemoni 10

Yako na mambo mengine pia.

 

S: Kwenye Kol 1:16, je kila mtu anapokufa anabadilika na kuwa malaika?

J: Hapana. Watu wanaoenda mbinguni hawatakuwa malaika, bali tutakuwa tukiwahukumu malaika kwa mujibu wa 1 Wakorintho 6:3. Tutaketi pamoja na Kristo kwenye kiti chake cha enzi kwenye Efeso 2:6.

   Wako watu ambao wangependa endapo wangezaliwa malaika badala ya kuwa wanadamu. Kama malaika, wangekuwa na furaha ya kumtumikia Mungu na kuishi mbinguni na kutokupitia hali ya dhambi, mateso, na kifo. Hata hivyo, tofauti na malaika, tunashiriki kimwili kwenye mapambano kupitia maneno yetu, maisha yetu, na maombi yetu katika kuitangaza injili. Tunaweza kuzaa watoto, na kwenye 1 Wakorintho 6:2-3 tunaona kuwa watu wanaomwamini Yesu watakuwa juu ya malaika.

 

S: Kwenye Kol 1:16, je Mungu alihitaji malaika kuumba ulimwengu?

J:  Hapana. Kwamba aliwatumia haimaanishi kuwa aliwajitaji.

 

S: Kwenye Kol  1:16, je kuna madaraja tofauti ya malaika?

A: Ndyo, ingawa Biblia haielezi kwa undani kuhusu madaraja na majukumu ya malaika. Tunajua kuhusu maserafi/makerubi kwenye Isaya 6:2,3, makerubi kwenye Ezekiel 1:5-21; 10:1-22; na wenye uhai wanne kwenye Ufunuo 4:6-9. Hawa wote yaelekea ni wale wale. Pia tunajua kuhusu Mikaeli malaika mkuu kwenye Yuda 9, Ufunuo  12:7; na Daniel 12:1. Gabrieli alikuwa mjumbe kwenye Daniel 9:21 na Luka 1:26.

 

S: Kwenye Kol 1:17-22, ni kitu gani kinachofurahisha kuhusu Kigiriki cha kwenye kifungu hiki?

J:  Kristo ni (wakati uliopo) mzaliwa wa kwanza wa viumbe wote. Kwa kufufuka kwake Kristo amekuwa (wakati uliopita) mzaliwa wa kwanza wa kanisa. Neno la Kigiriki lililotafsiriwa“ukae” hapa, ketoikesai, kwa usahihi zaidi linamaanisha “kukaa wakati wote”, tofauti na maoni kuwa Mungu alikaa kwa muda mfupi tu ndani ya Kristo. Kwenye Wakolosai 1:22 neno la Kigiriki hapa halina mtindo mzuri sana wa uandishi kwenye Kigiriki – huenda ni kwa makusudi hivyo kwa msistizo zaidi na zaidi. Linaweza kutafsiriwa kuwa mwili wa nyama wa Kristo, msistizo usiohitajika wa mwili wenyewe wa Kristo.

 

S: Kwenye Ko 1:20, Efe 1:10, na 2 Kor 5:1, je mapepo nayo yanapatanishwa?

J: Hapana. Kwenye Wafilipi 2:10, Mungu anatofautisha kati ya “mbinguni”, “duniani”, na “chini ya nchi.” Kama mapepo ni sehemu ya ulimwengu unaoitwa “chini ya nchi”, Waraka wa Wakolosai hausemi kitu kuhusu kuwapatanisha walio “chini ya nchi.” Kama mapepo ni sehemu ya ulimwengu ulioitwa “chini ya nchi” tayari wameishafanya uamuzi wao, wakiwa wanajua kabisa, wakati walipokuwa wanaasi. Waebrania 2:16 inaonyesha kuwa Yesu alilipia dhambi za wanadamu na hakuwasaidia malaika au malaika walioasi.

 

S: Kwenye Ko1:20, Efe 1:10, na 2 Kor 5:19, kwa kuwa Mungu amevipatanisha vitu vyote mbinguni na duniani, je watu wote wataokolewa, kama wapotoshaji wa Universalism wanavyofundisha?

J: Hapana. Mungu alivipatanisha vitu vyote na yeye, lakini si vitu vyote vilivyojipatanisha na Mungu. Watu wote “wanaweza kuokolewa” lakini si watu wote wanaounganisha mambo wanayoyasikia na imani, kama Waebrania 4:2 inavyoonyesha. Warumi 4:2-5,16 na Waefeso 2:8-9 zinaonyesha kuwa tunahesabiwa haki kwa imani.

   Wokovu si kusamehewa au hata kuhesabiwa haki. Wokovu ni maisha, na Yohana 5:39, 40 inaonyesha ulimwengu hautakuja kwa Kristo kupata uzima.

   Jehanamu ni hukumu ya milele kwenye Mathayo 25:41,4 6.  Mwovu na watu wengine watateswa milele kwenye Ufunuo 20:10. Jehanamu ni mahali pa mauti ya milele kwenye 2 Wathesolanike 1:9.

 

S: Kwenye Kol 1:20, ni kitu gani hasa kinachopatanishwa hapa?

J: Kwanza kitu gani kisichokuwa jibu la swali hili kisha jibu la swali hili.

Hili si jibu la swali: Mstari huu hausemi, “chini ya dunia”, au “Kuzimu”, bali mbinguni na duniani tu. Ingawa ulimwengu ulio chini ya dunia utasujudu na kuwekwa chini ya Kristo (Wafilipi 2:10-11), na ingawa jambo hilo linaweza kuchukuliwa kuwa kupatanishwa kwa hiari, si hiari kwa walio kwenye “chini ya dunia.” Waebrania 2:16 inasema kwamba Yesu alilipa deni la binadamu, wala si malaika anaowasaidia. Hukumu ni ya milele kwa mujibu wa Mathayo 25:41, 46, na shetani na viumbe wengine watateswa huko milele kwenye Ufunuo  20:10. Jehanamu ni mahali pa mateso ya milele kwenye 2 Wathesolanike 1:9.

Jibu la swali hili lina sehemu mbili: jibu la jumla na jibu bayana.

Jibu la jumla, mwisho wa siku, vitu vyote ulimwenguni vitapatanishwa na Mungu kwa hiari. Lakini wote walio kwenye ziwa la moto hawamo ulimwenguni. Hata wale ambao hawakuasi au kuvunja sheria nao watawekwa chini ya Kristo, ambaye atakuwa juu yao wote. Lakini maneno “vitu vyote” yanamaanisha aina zaidi ya moja ya vitu/viumbe. Kwa hiyo hebu na tuangalie nini hasa kinahitaji kuwekwa sawa.

Jibu bayana, Maandiko yanadokeza vitu kadhaa.

Watu waliookoka walikuwa wamepotea na kutengwa na Mungu, lakini sasa wamepatanishwa naye.

Viumbe vyote viliwekwa chini ya utumwa mwanadamu alipoanguka dhambini. Ni kwa nini binadamu aliyeanguka dhambini aishi kwenye ulimwengu ulio mkamilifu? Lakini viumbe vyote, hata kama vimevunjwa sasa, vitarejeshwa kwa mujibu wa Warumi 8:19-21. Ardhi ililaaniwa na Mungu baada ya Adamu na Hawa kufanya dhambi kwenye Mwanzo 3:17.

Hata nyota machoni pa Mungu, kwa mujibu wa Bildadi kwenye Ayubu 25:5.

Mbinguni vitu vyote vitatakiwa kutakaswa, kwa mujibu wa Waebrania 9:23. Jambo hili linawezakuwa ni kwa sababu shetani alikuwa anaruhusiwa kuingia mbinguni, kama ambavyo Ayubu 1:6,7 na Ufunuo 12:10 zinavyoonyesha.

Tutawahukumu malaika kwa mujibu wa 1 Wakorintho 6:3. Lakini, jambo hili haliko wazi kabisa, endapo tutahukumu tu ni jinsi gani mambo waliyoyafanya yalikuwa mazuri.

 

S: Kwenye Kol 1:21-23, nini ni muhtasari wa jambo ambalo Mtume Paulo analiongelea hapa?

J: Kuna sehemu tatu: ulikuwa vipi zamani, ukoje sasa, na unapaswa kuendelea vipi.

 

S: Kwenye Kol 1:22, kama sehemu ya fidia, je Yesu alitoa mwili wake milele, kama Mashahidi wa Yehova, Mchungaji Moon, na wazushi wengine wanavyofundisha?

J: Hapana. Kutupatanisha sisi kupitia kifo cha mwili wa Kristo hakumaanishi kuwa Kristo hakuupata mwili wake tena katika kufufuka kwake. Kama unamwamini Yesu, basi unapaswa kukubali kuwa mwili wa Yesu ulifufuliwa kwa sababu ya aya hizi.

1. Kwenye Yohana 2:19-22, “Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.’ … Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.”

2. Kwenye Yohana 20:25-29, wakati Yesu alipomwambia Tomaso aweke kidole chake na mkono wake kwake, ama

2a) Yesu alikuwa anamfanyia ujanja Tomaso, kwa maneno mengine alikuwa anamdangnya Tomaso, au

2b) Huu ulikuwa mwili halisi wa Yesu.

3. Kwenye Luka 24:37 Yesu alisema, “Tazameni mikono yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa, kama mnavyoniona mimi kuwa navyo.”

   Mitume walifundisha kuhusu mambo wanayoyapitia wao wenyewe, kuhusu mambo waliyoyaona na hata kuyagusa wao wenyewe (1 Yohana 1:1-4). Kama unashiriki dini inayokana mambo ambayo Yesu na mitume walisema kuhusiana na jambo hili, unahitaji kuchagua ama kumfuata mungu wa dini yako, ama kumfuata Mungu wa Yesu na mitume. Nataraji utafanya uchaguzi mzuri.

 

S: Je Kol 1:23 inasema kuwa watu ambao hawaendelei na imani watapoteza wokovu wao?

J: Kuna mambo matano ya kuyazingatia katika kujibu swali hili.

Mungu anawajua watu aliowachagua: Hapa duniani, watu wengi wanaweza kuonekana kuwa kama wakristo, lakini kabla ya kuuumba ulimwengu, Mungu alijua nani watakwenda mbinguni, na hakuna mtu atakayekwenda bila ya Mungu kujua. Kusema kuwa Mungu alijua kwa hakika kuwa mtu fulani atakwenda mbinguni, kisha mtu huyo asiende mbinguni ni jambo lenye kujipinga.

Kuongoka kwa uongo: Mtu anaweza kuwadanganya watu wengine wafikiri kuwa amempokea Yesu moyoni mwake. Mbaya zaidi, watu wanaweza kujidanganya wao wenyewe, kama Mathayo 7:21-23 inavyoonyesha.

Haja ya kujichungza sisi wenyewe: Hakika ya wokovu haingekuwa na maana endapo uongofu wa uongo usingeweza kutambuliwa kabisa. Lakini unaweza kutambuliwa. Mtume Paulo anatusihi tujichunguze sisi wenyewe kuona kuwa tumo kwenye imani kwenye 2 Wakorintho 13:5-6.

Kukengeuka: Wakati mwingine watu huwa wanaiacha imani ya kikristo, - na hawarudi tena. Lakini 1 Yohana 2:19 inasema kuwa walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Pia Waebrania 3:10 na kuendelea inasema kuwa wakengeufu wa Agano la Kale “hawakuzijua” njia za Mungu.

Zaidi ya hili, wakristo wa kweli hawakubaliani kwenye suala la kuwa mtu aliyeokoka hawezi kupoteza wokovu. Ama

a) watu ambao hawaendelei katika imani wanakuwa wameipoteza, ama

b) watu ambao hawaendelei katika imani hawakuwahi kuamini.

   Tazama majadiliano kwenye Efe 1:14  na Waebrania 6:4-10 kwa habari zaidi.

 

S: Kwenye Kol 1:24, Mtume Paulo angewezaje “kuyatimiliza” mambo yaliyokuwa yamepungua katika mateso ya Kristo”?

A: Maneno mawili ya kukumbuka: kulinganisha maneno na matendo, na kutumia lugha inayokaribiana na maneno aliyoyasema Yesu.

Kulinganisha maneno na matendo: Njia pekee ya kutafsiri vibaya maneno yake ni kupuuzia mambo aliyoyasema sehemu nyingine. Kwa ujumla, hakuna mtu, wakati ule au sasa, ambaye angeweza kufikiri kuwa Paulo hakuwa anajaribu kuchukua nafasi ya msalaba aliokuwa anauhubiri au aliwahi kufikiri kuwa yeye ni masihi wa pili. Lakini, kwenye Wakolosai 2, baadhi ya Wakolosai walikuwa wanajaribu kuyatimiliza mambo ambayo waliyaona kuwa yamepungua kwa Kristo kwa kutumia sheria, kuabudu malaika, na taratibu za kidini. Kwenye Wakolosai 1, Paulo alitimiliza mambo yaliyokuwa yanapungua kwenye ufahamu wao wa ukamilifu wa mateso ya Kristo. Paulo alifanya hivi si tu kwa maneno yake kwenye Wakolosai 1:15-23, bali kwa maisha yake na uvumilivu wake wa mateso, ambayo yalithibitisha kuwa maneno yake yalidhihirisha utoshelezi wa Yesu.

Lugha inayokaribiana na maneno ya Yesu: Paulo aliongea kwa ufasaha wa kuwatosha watu wote waliotaka kumuelewa. Paulo hakufikiria kuchukua nafasi ya Kristo alipojaribu “kuwaokoa watu” kwenye 1 Wakorintho 9:22, na Paulo alisema kuwa Timotheo atawaokoa watu aliokuwa anaongea nao kwenye 1 Timotheo 4:16, na Yakobo alisema kuwa tutaweza kuwaokoa watu wengine kwenye Yakobo 5:20.

 

S: Kwenye Kol 1:28 na 1 Kor 2:2, Mtume Paulo alihubiri kuhusu kitu gani hasa?

J: Tunahitajika  kukua katika ufahamu (Wakolosai 1:10), lakini ufahamu pekee usiwe mwisho. Kimsingi, Paulo hakufundisha falsafa nyingine au mafundisho yaliyokuwa tofauti na waalimu wazushi, ingawa Paulo alifanya hivyo pia. Lakini tofauti na wao, kimsingi Paulo alimhubiri mtu mmoja. Je tunapohubiri injili kimsingi tunahubiri kweli, falsafa, au mtu?

 

S: Kwenye Kol 1:28, inakuwaje Paulo anamfundisha kila mwanaume, na si mwanamke?

J: Kama maneno ya Kiingereza na Kiebrania yenye kumaanisha “mwanaume”, neno la Kigiriki lenye kumaanisha “mwanaume”, anthropos, linawawakilisha wanawake pia. Wagalatia 3:28 inasema bayana kuwa kwa Kristo hakuna mwanaume au mwanamke.

 

S: Kwenye Kol 1:29, tunwezaje “kujitaabisha” kwa nguvu ya Mungu itendayo kazi kwa jinsi alivyofanya Paulo?

J: Tunakaa ndani yake, tukitafuta kuwa na muda na Yeye kwa njia ya maombi, kumtafakari, na kusoma Biblia. Tunapumzika kwa Mungu, na tunatafuta kumtumikia kwa bidii. Hatuondolewi kwenye lengo letu kwa kutafuta vitu vingine. Hatujaribu kumtumikia kwa nguvu zetu wenyewe. Hatushikwi na mambo mengi sana, hata kwa nguvu ya Mungu, kiasi cha kufikiri kuwa shughuli nyingi zinachukua nafasi ya uhusiano binafsi na Mungu.

 

S: Kwenye Kol 2:4, neno “kudanganya” linamaanisha nini?

J: Kwenye Kigiriki kuna maneno tofauti yanayotumika kwa aina tofauti za njia za kudanganya. Neno bayana la Kigiriki lililotumiwa hapa kwa kudanganya hapa ni paralogizetai. Linamaanisha kukosea hesabu au sababu ya jambo fulani. Mwishoni mwa Wakolosai 2:4, Paulo anasema bayana hamaanishi kutokuwepo kwa sababu yeyote au mabishano, lakini mantiki isiyokuwa nzuri. Neno moja la Kigiriki ambalo limetafsiriwa kuwa “hoja zenye nguvu”, linamaanisha “uongeaji wenye ushshawishi” au kwa kutumia lugha ya mtaani ya Kiingereza cha leo “kuongea kwa haraka.” Kunaweza kuwa na dhambi za mawazo na dhambi za moyo. Wuest’s Expanded Translation inalitafsiri neno hili kuwa “kupotosha kwa kutumia mantiki isiyokuwa sahihi.”

   Wakolosai 2:8 inatuagiza kuyachunguza mafundisho tunayoyasikia au kuyasoma. Kama Dick Lucas kwenye The Message of Colossians & Philemon Revised Edition anavyosema, “tunahitaji kuyachunguza mafundisho yote ili kuona ukweli wake katika mambo yanayoyaongelea siyo uzuri wa namna yalivyowasilishwa.” Wakati mwingine kama mtu amedanganywa, shida inawezakuwa ni mafundisho yenyewe kwa kiasi fulani.

 

S: Kwenye Kol2:5 na 1 Kor 5:3, ni kwa namna gani Paulo yupo na watu wengine kiroho, kwa kuwa Paulo hakuwepo mahali pote?

J: Paulo angeweza kujua kwa sababu Mungu ana uwezo wa kumfundisha rohoni. Wakristo wameunganishwa na kifungo maalumu cha roho kwa mujibu wa Waefeso 4:3.

 

S: Kwenye Kol 2:7, nyakati za maneno haya zina umuhimu gani?

J: Vitenzi vikubwa vya kwanza vitatu “kuwa na shina”, “kujengwa”, ”, na “kufanywa imara” vyote hivi vimo kwenye kauli ya kutendewa. Kwa maneno mengine, haya ni mambo ambayo Mungu anayafanya kwetu. Kuwa na shina ni wakati mtimilifu uliopita, ikimaanisha tukio lililokwisha kufanyika wakati uliopita na matokeo yake yanaendelea hata wakati uliopo. Maneno “mkizidi kutoa shukrani” ni kauli ya kutenda, na inaonyesha itikio letu kwa mambo ambayo Mungu ameyatenda. Watu wengi wanahamasishwa kwa kiasi kikubwa na uroho, tamaa, hofu, au haja ya kutaka kufikiriwa vizuri zaidi kwenye macho ya watu wengine. Lakini, wakristo wanatakiwa wahamasishwe zaidi na kumshukuru Mungu. Tunatakiwa tuwe na moyo wa shukrani kwa Mungu.

   Pia neno “mkiwa na shina” kwenye Kigiriki lina maana mbili. Kama Kiingereza, linaweza kumaanisha kuwa mimea ina shina. Lakini maana ya pili ni kuwa jengo lina shina, kwa maana ya kuwa jengo lina msingi mzuri. Unawezaje kutambua endapo mti, au jengo una shina? Huwezi kutambua wakati jua linaangaza. Lakini wakati mawimbi au dhoruba vinakuja, kitu chenye shina; na kitu ambacho hakina shina kitapeperushwa.

 

S: Kwenye Kol 2:8, ni falsafa gani ya kishetani inayotegemea mapokeo ya kibinadamu ya ulimwengu wa uovu?

J: Kwanza kabisa, falsafa ni nini hasa? Falsafa inamaanisha kupenda hekima, na inawezakuwa upendo hasa, au tamaa isiyozuilika ya sanamu. Falsafa si rasmi na za magharibi tu au falsafa zenye asili ya Asia, bali ni kwa jinsi gani watu wanafikiri kuhusu vitu mbalimbali, ama kwa njia rasmi ama kwa njia isiyokuwa rasmi. Jina linaloweza kuwafaa zaidi ni mitazamo, ambayo ni mifano au mitindo ya kifikra ya maisha ya watu, ulimwengu, watu, na/au maadili. Lakini mfano ni mfano, si maisha yenyewe. Kwenye mitindo ya kihesabu, mtindo mzuri wa tabia tuli ya kiwanda cha kikemikali au mifumo mingine mara nyingi si mtindo mzuri wa tabia inayobadilika badilika, na kinyume ya hapo. Kwa ajili hiyo, mfano wa maisha, kama ni mzuri kiasi cha kufaa kwa malengo kadhaa, hauhakikishi kuwa utafaa kila mahali na kwa malengo yote. Kama falsafa yako inachukua nafasi ya maisha,falsafa inawezakuwa sanamu, na uchaguzi usiokuwa mzuri wa mwenye kuufanya. Vivyo hivyo, hata theolojia inawezakuwa sanamu, kama inakuwa muhimu kuliko neno la Mungu. Tunapaswa kuwasaidia watu wengine kuwekwa huru na utumwa wa kifikra wa sanamu zenye ukatili, bali tuhakikishe kuwa hatuna sanamu kwenye mawazo yetu sisi wenyewe pia.

   Lakini, wana falsafa wengi, hata wana falsafa wasiomwamini Mungu, hawaabudu falsafa yao. Hata hivyo, falafa yeyote ya “ulimwengu huu” yenye kudai kujua namna ya kuyamudu maisha bila kumhitaji Mungu ni falsafa yenye uovu. Kuna uongo kwako na kwa watu wengine pia. Kuna dhambi za mawazo na dhambi za ulimi. Kama mfano, muangalie Jean Paul Sartre (linatamkwa sart), aliyesema “Maisha ni kama puto tupu kwenye bahari ya utupu. Sasa, hoja ya Sartre ingewezakuwa na mshiko kama Mungu asingekuwepo. Lakini Mungu ndiye maana ya maisha yetu, na kwa hiyo Sartre anaelekea upande usiokuwa sahihi.

   Utani, mantiki ya kifalsafa inaweza ikawa inavutia sana. Kama mfano, mwangalie mwana falsafa, David Hume. Aliandika, “Kama tunajichukulia mikononi mwetu kiasi chochote kile cha metafizikia ya uungu au shule, kwa mfano; hebu natujiulize, je ina mantiki yeyote ya kinadharia kuhusiana na kiasi au namba? Hapana. Je ina sababu zozote za majaribio kuhusiana na mada na uwepo. Iweke basi motoni: kwani haina kitu chochote isipokuwa maneno ya hila na ndoto.” Wana falsafa wachache wasioamini uwepo wa Mungu wamekuwa wazi na waaminifu kuwaambia watu kuwa maandishi yao wenyewe hayakuwa na maana na yanatakiwa kuchomwa moto isipokuwa David Hume huenda hakutambua kuwa alikuwa anazihukumu kazi zake mwenyewe. Kwa sababu, ninafikiri, kuwa kazi za Hume si mantiki ya kihesabu au sayansi ya majaribio (angalau kwa mijibu wa ufafanuzi wangu mwenyewe), naweza kuhitimisha kwa kusema Hume anaongelea kuchoma moto vitabu vyake mwenyewe.

   Mfano mwingine, Immanuel Kant alijaribu kufafanua wema bila kumhusisha Mungu. Kant alisema kuwa wema ni jambo linalofanywa kwa kutimiza wajibu. Kwa kifananishi hicho, maaskari wa Kinazi wa Ujerumani waliowatesa na kuwaua Wayahudi kama kutimiza wajibu wao, na Wakomunisti walioua hata wanawake na watoto, wote hawa walikuwa wanatenda mema. Kama nikijisikia kuwa ninatimiza wajibu wangu kwa kuharibu kazi zote za Kant, basi nadhani Kant atakubali kuwa nilikuwa nafanya jambo jema.

   Wana falsafa wasioamini uwepo wa Mungu na mimi tunaweza kukubaliana kwenye jambo hili moja: niendelee kufanya kazi yangu ya mchana, kwa kuwa hakuna faida kwangu kutoa maisha yangu kufanya falsafa!

   Jambo moja la mwisho. Wakolosai 2:8 inaweza kumaanisha kuwa hatupaswi kufundisha falsafa tupu na isiyo ya kweli, lakini hivyo sivyo mstari huu unavyosema. Badala yake, tunatakiwa kuhakikisha hakuna mtu yeyote anayetuteka mateka (neno la Kigiriki hapa linamaanisha kutekwa vitani) na falsafa tupu na za uongo. Wakolosai 2:8 inasema kuwa kuna hatari hapa, na tunao wajibu wa kuiepuka hatari hiyo. Sijasoma kitabu cha Hume (kama alivyokuwa amenishauri), au kazi za Kant. Kwa nini niutafute ukweli mahali ambapo Mungu anasema pana hatari? Kwa nini nijiunge na kanisa ambalo watumishi ndani yake wanafundisha mambo ambayo yanapingana na injili?

 

S: Kwenye Kol 2:8-9, ni jambo gani linalokinzana hapa, na mkristo anawezaje kuchukuliwa mateka?

J: Paulo anatofautisha utupu wa falsafa ya kibinadamu na ukamilifu wa Kristo. Falsafa tupu ya kibinadamu inaweza kuingia kanisani kwa kujifanya kuwa inakubaliana na imani ya kikristo.

   Kama wakristo tunaweza kupenda kufikiri kuwa tuko huru sasa dhidi ya kudanganywa kwenda kwenye uelekeo usiokuwa sahihi, lakini angalizo la Mtume Paulo linamaanisha kuwa kwa bahati mbaya hivi sivyo mambo yalivyo. Na kama mkristo ana majivuno kwenye maisha yake ya kiroho au ufahamu wake inaweza kuwa rahisi zaidi kudanganyika. Mkristo anaweza kuchukuliwa mateka kiroho, kwanza kwa kufuata falsafa tupu kama kitu cha “ziada” badala ya kumfuata Kristo. Lakini hatutakiwi “kwenda nje” ya imani kupata kweli zaidi kwenye dini za uongo na falsafa zenye kumkana Mungu. Badala yake mkristo anayefanya hivyo, ndipo falsafa tupu inapoweza kuwa muhimu kwake kama kumfuata Kristo. Baada ya hapo, falsafa tupu itakuwa ya muhimu kuliko kumfuata Kristo. Swali rahisi kujiuliza wewe mwenyewe, kama Mungu anataka uache mambo yote unayoyafanya, na mambo yote unayoamini, isipokuwa Mungu mwenyewe na mambo aliyoyasema kwenye neno lake, ni kwa jinsi gani utasita kufanya hivi?

 

S: Kwenye Kol 2:9-10, ni kwa njia ya nani sisi waumini tunapata ukamilifu ndani ya Kristo?

J: Kristo kama kichwa inamaanisha kuwa Yeye ni mtawala na kanisa ni kiumbe chenye uhai. Hatuhitaji kitu kingine chochote. Sehemu kubwa ya Waraka wa Wakolosai haizungumzii mambo ya kuanza kufanya, bali mambo ya kuacha kufanya. Kama Peter Drucker alivyosema, “Tunatumia muda mrefu sana kufundisha viongozi mambo ya kufanya. Hatutumii muda wa kutosha kuwafundisha viongozi mambo ya kuacha kufanya. Nusu ya viongozi ambao nimekutana nao hawahitaji kujifunza mambo ya kufanya. Wanahitaji kujifunza mambo ya kuacha kufanya.” Imenukuliwa kutoka Marshall Goldsmith What Got You Here Won’t Get you There uk.36.

 

S: Kol 2:10 inaonyesha kuwa Mungu ana mfano wa kimwili kama sisi?

J: Hapana. Wakolosai 1:15,17 inasema mfano wa Mungu asiyeonekana. Lakini Mungu hana mfano wa mwili unaoonekana; kwa kuwa Yesu ana mwili, mwili wa utukufu, kama Yohana 20:25-29; 2:19-22; na Luka 24:37 inavyoonyesha. Waebrania 13:8 inasema kuwa Yesu ni yule yule jana, leo, na hata milele..

 

S: Kwenye Kol 2:11-12, ni kwa jinsi gani sisi waumimi tunakuwa na ushirika mkamilifu na Kristo?

J: Hatuna ushirika wa sehemu tu, bali uhusiano kamili. Tunaweza kumwendea si tu kwa muda fulani, wakati mambo yanatuendea vibaya, bali wakati wote, mzuri au mbaya.

 

S: Kwenye Kol 2:11-12, kwa kuwa ubatizo ni aina ya tohara, je watoto wadogo wanahitaji kubatizwa?

J: Ubatizo ni ishara ya nje ya “kutahiriwa nanKristo”, iliyofanywa tulipokuwa tumekufa katika dhambi zetu tukiwa na asili yetu ya dhambi. Wakristo wa kweli wana maoni yanayotofautiana kuhusu ubatizo wa watoto wadogo..

Wakristo wanaounga mkono ubatizo wa watoto wadogo: Kama tohara kwa watoto wa kiume wa Wayahudi ilivyokuwa ishara ya kushiriki kwao katika kielelezi kinachoonekana cha watu wa Mungu duniani, ubatizo unafanya vivyo hivyo. Neno “watoto wadogo” linamaanisha kuwa utashi wao haukutakiwa, neno “watoto wa kiume” linamaanisha kuwa haikuwa kwa ajili ya manufaa binafsi bali kuwa kielelezi cha pamoja cha imani. Kuanzia nyakati za Ambrose wa Milani (karibu mwaka 378 BK) na  Augustino wa Hippo (aliyeishi mwaka 388-430 BK) na kuendelea, kanisa limekuwa likibatiza watoto wadogo kama kama desturi.

   R.C. Sproul kwenye Now That’s a Good Question uk.341-342, kwenye muktadha wa ubatizo wa mtu mzima ambaye alikuwa amebatizwa alipokuwa mtoto anasema, “Ningeweza kusema kuwa kurudia kubatizwa kunaweza kuwa ni fedheha iliyofunikwa kwa kiasi ya uaminifu wa Mungu, ingawa natambua kabisa kuwa hakuna mtu mmoja miongoni mwa milioni ambaye anabatizwa mara ya pili kwa kwa lengo la kumfedhehesha Mungu.”

Watu wanaounga mkono ubatizo wa waumini watu wazima: Wakolosai 2:12 na Warumi 6:3-7 zinaonyesha kuwa ubatizo ni kielezi kinachoonekana cha utambulisho wetu katika kuzikwa na kufufuka kwa Yesu. Ingawa watoto wanaokufa bado wanaweza kuokolewa kwa neema ya Mungu, ubatizo ni ishara ya dhamana yetu kwa Mungu (1 Petro 3:21) na kumpokea Roho Mtakatifu. Kama ambavyo wanaume wa Kiyahudi walitahiriwa mara baada ya kujiunga na taifa la Uyahudi (kwa kuzaliwa kimwili), wakristo wanatakiwa kubatizwa mara baada ya kujiunga na jumuiya ya watu wa Mungu, yaani kanisa, kwa kuzaliwa mara ya pili. Justin Martyr (karibu mwaka 138-165 BK First Apology sura ya 61) anasema kuwa kwenye kanisa la mwanzo, ubatizo ulifanywa kwa “watu waliokuwa wameelezwa na kuamini” na mara baada ya kuongea kuhusu watoto anasema si kwamba watoto wanabatizwa, bali kwamba ubatizo ni kwa “mtu anayechagua kuzaliwa upya, na ametubu dhambi zake.” Justin anawaita waumini “watoto wa uchaguzi na ufahamu.”

   Mzushi wa Kiebioni kwenye Clementine homily 17 sura ya 7 anasema, “Alitutuma kwa watu wa mataifa wasio na ufahamu ili tuwabatize kwa ajili ya msamaha wa dhambi, na alituamuru kuwafunza kwanza” (Mwandishi ambaye hajulikani wa karne ya 1-4 BK).

Kwa watu wote: Kama sababu ya kuu ya ubatizo ni kumtii Yesu, wakristo wa kweli hawatakiwi kujitenga na wakristo wengine ambao wanafanya bidii kumtii Yesu.

   Kwa maelezo zaidi kuhusu ubatizo wa watoto wadogo, angalia mjadala luhusu 1 Wakorintho 1:16; 7:14 na Christian Theology kitabu kilichoandikwa na Millard Erickson (Baker 1985) uk.1089-1105.

 

S: Kwenye Kol 2:13 na Efe 2:1,5, je watu waliokufa dhambini wana uhuru wowote wa kuchagua kitu cha kufanya zaidi ya wanyama waliokufa?

J: Bila ya neema ya Mungu, hakuna mtu anayemtafuta Mungu, kwa mujibu wa Zaburi 14:1-3; 53:1-3 na Warumi 3:10-12. Lakini watu wengi wamemtafuta Mungu kwa neema yake kwa mujibu wa Zaburi 9:10; 22:26; 24:6; 27:4,8; 40:16; 105:3,4; 119:2,30,45,94,173. Mungu si tu kwamba anafanya kazi kwenye maisha ya watu baada ya kuwa wamezaliwa upya, lakini pia inatakiwa kuwa Mungu afanye kazi kwenye maisha ya watu kabla hawajaja kwake kuzaliwa upya, kama Yohana 6:44; 15:5 inavyoonyesha.

   Ulimwengu wote ni “wafungwa” wa dhambi kwenye Wagalatia 3:22. Pamoja na kufa kiroho, tumekufa kisheria na tuna hukumu ya mauti ya milele. Charles Spurgeon alitoa kifananishi hiki cha wahalifu waliohukumiwa kwenye kipeperushi kiitwacho Free Will - a Slave (uk.3), “Ingawa mwezi unaweza kupita kabla hajaletwa kwenye jukwaa kupata hukumu ya sheria, lakini sheria inamuona kama mtu aliyekufa.”

 

S: Kwenye Kol 2:13-15, ni kwa namna gani waumini wana uhuru ndani ya Kristo?

J: Hatuko huru kufanya dhambi; badala yake tunao uhuru dhidi ya dhambi. Tuna uhuru dhidi ya dunia, uhuru dhidi ya sheria, na uhuru dhidi ya mwili. Tunaishi ili kumtukuza Mungu, jambo ambalo linahusisha kufanya mambo ambayo yanampendeza na kutokufanya mambo ambayo hayampendezi.

 

S: Kwenye Kol 2:14, Paulo alimaanisha nini hasa aliposema “hati iliyoandikwa/iliyoandikwa kwa mkono dhidi yetu?

J: Neno la Kigiriki lenye kumaanisha “kuondoa” linamaanisha “kufuta”, kama kupangusa au kuchana maandishi. Wanazuoni wakristo wana maoni mawili kuhusu maana halisi ya neno hili.

Sheria ya Mungu, iliyoandikwa na Musa. Hii inafutwa tunapokuwa ndani ya Kristo. Tunatumika kwenye njia mpya ya Roho Mtakatifu, tukiitii sheria ya Kristo, siyo njia ya zamani ya hati iliyoandikwa (Warumi 7:6; Waebrania 7:18-198:6-8,13). The Believer’s Bible Commentary uk.2004 ina maoni haya.

Ukiri wetu wenyewe wa deni letu. Hata kwa watu ambao hawajawahi kuwa na Sheria ya Musa, dhamiri zao wenyewe zinashuhudia kuwa wamefanya mambo maovu, na hawastahili kwenda kwenye ulimwengu mkamilifu usiokuwa na dhambi.

   Jawabu linaweza kupatikana kwa kusoma maelezo ya kina ya Mtume Paulo ya mahali petu mbele ya Mungu bila ya Kristo, kwenye Warumi 2:1-3:20. Jambo hili linamaanisha kuwa jibu ni yote hayo mawili.

 

S: Kwenye Kol 2:16, ni kitu gani kinachowafanya watu kujikita kwenye mambo madogo na kutoa uzito mdogo kwenye mambo makubwa?

J: Sheria ya Musa haizuii kunywa, hivyo Mtume Paulo anaongelea uasetia (kujinyima anasa za kimwili) hapa, si tu kushika Sheria ya Musa. Watu wengi wanakuwa na “faraja” wanapoweza kuwaonyesha watu wengine kuwa wao ni washika dini sana au watu wa kiroho sana kwa sababu ya chakula na vinywaji. Kuna ambao hawali nyama ya nguruwe, nyama ya ng’ombe,  nyama na samaki, au nyama nyingine yeyote nyekundu siku ya ijumaa, kwa sababu jambo hili linawafanya wajisikie kuwa watu wa kiroho sanal.

   Ungefikiri nini kama ningekuambia kuwa sili koli flawa (aina ya kabichi), kwa lengo pekee la kuonyesha watu wengine jinsi nilivyokuwa mtu wa kiriho? Lakini kama kutokula koli flawa, ambayo haijatajwa kwenye Biblia, ni dhihaka kuonyesha hali ya kiroho, basi kwa nini kula nyama au samaki kuomuonyeshe mtu kuwa wa kiroho zaidi, ikiwa hakujatajwa kwenye maandiko ya Kihindu (Vedas), Upanishad (maandiko madogo ya dini ya kihindu yenye kufafanua Vedas), Kuran, Biblia, au kitabu kingine chochote kinachochukuliwa na mtu yeyote kuwa maandiko matakatifu. Kama unataka kumfuata Mungu vizuri zaidi, na kumfurahisha zaidi, tumia muda wako na nguvu kufanya mambo ambayo Mungu amesema kuwa anapenda tuyafanye, na acha kufanya mambo ambayo ametuzuia tusiyafanye. Usianze kutengeneza mambo yako mwenyewe, yasiyojulikana yalikotoka, ukidai kuwa unamfuata Mungu kiroho zaidi.

 

S: Kwenye Kol 2:16, ni kwa jinsi gani watu wanajikita kwenye chakula na vinywaji siku hizi?

J: Wamomoni hawatakiwi kunywa vinywaji vya kuburudisha kama vile kahawa, chai, au vinywaji baridi (soda). Wakatoliki mara nyingi huwa hawali nyama (isipokuwa ya samaki) siku za ijumaa. Wakatoliki pia wanaacha kufanya vitu kadhaa kwenye majira ya Kwaresma, na wanaadhimisha Mardi Gras (jumanne inayoitangulia jumatano ya majivu) na mambo yake yote yanayovuka mpaka, kabla ya kipindi cha Kwaresma kuanza. Wabaptist wengi wanafikiri kuwa si sahihi kunywa pombe ya aina yeyote ile. Ni kweli hakuna jambo lolote lile kati ya haya lililoandikwa moja kwa moja kwenye Biblia. Agano la Kale linasema kuwa watu wa Mungu wa wakati ule hawakuruhusiwa kula nyama ya nguruwe, uduvi (ushimba), samakigamba, ngamia, au damu. Waislamu hawali nyama ya nguruwe au damu. Wahindu wengi hawali nyama ya ng’ombe. Dini ya Jain inafundisha kuwa ni jambo la kiroho zaidi kujiepusha kula kitu chochote, kwa kadri inavyowezekana. Kwa ajili hiyo, baadhi ya Wajain “wa haki” wanajinyima kula chakula hadi wanakufa.

 

S: Kol 2:18, je inamaanisha nini kutokuabudu malaika?

J: Ndani ya mioyo ya watu wengi kumewekwa ujuzi kuwa wanapaswa kuabudu kitu fulani au mtu fulani. Huko Kolosai, kulikuwa na watu waliokuwa wanaabudu malaika. Kwa kuwa malaika wanafahamika kuwa viumbe wa Mungu, huenda watu hawa walikuwa wanataka kuwaabudu malaika pamoja na Mungu. Ingawa wanawezakuwa walikuwa na sababu zao wenyewe (haikuwa upendo wao au ibada, tukuzo, nk), Paulo alisema kuwa jambo hili siyo sahihi kwa ujumla wake.

   Kwenye maandiko ya Kiyahudi ya Apokrifa (vitabu vya kubuniwa vya dini ya kiyahudi), kulikuwa na msistizo mkubwa wa kukutana na malaika mbinguni kama ulivyokuwa kwa Mungu. Vitabu vya Kiyahudi vya Apokrifa, kama Jubilees 2:2, 1 Enoch 43:1-2; 80:6; 2 Enoch 4:1-2 vinasema kuwa kila kitu hapa duniani kina malaika wake juu yake. Kwenye vitabu vya Unostasia (Gnostic literature), mengi ya maandiko yake yanaongelea miungu midogo/nusu-mungu na jinsi inavyohusiana yenyewe kwa yenyewe na kiumbe mkuu, ambaye alipingana na mpango wa kuumba ulimwengu unaoonekana. Kwenye Ubudha wa Mahayana, kuna mkazo mkubwa sana kuhusu odhisattva, ambaye anaacha au anachelewa kwenda kwa Nirvana ili awasaidie wengine wanaoomba kwao. Katika sehemu kadhaa za Uislamu wa madhehebu ya Shia kuna mkazo katika “watakatifu” wa Kiislamu na matendo mema ya kutembelea neema zao. Pia Mashariki ya Kati kuna dini ya Yezidi ambayo inadai kumfuata kiumbe ambaye ni mwovu na amemuasi mungu, lakini alitubu na sasa anamfuata mungu, angalau hivi ndivyo alivyowaambia na walimwamini. Kwa hiyo wanamfuata kiumbe huyu “Tausi” badala ya Mungu. Kwenye Ukatoliki na Uothodoksi wa Mashariki, wao hawaabudu malaika, lakini wanamuomba Mariamu na ”watakatifu” wengine kama viumbe vya kupitia kuifikia neema yao kutoka kwenye “maghala ya matendo mema” badala ya kumuomba Mungu tu.

   Neno la Kigiriki lenye kumaanisha “kufutwa”, katabrabeueto linaweza pia kumaanisha “hukumu” au “kuamua dhidi ya” kwa mujibu wa New International Bible Commentary uk.1457. Kama linamuongelea mwamuzi akimfuta mtu kwenye mashindano ya mchezo. Neno kama hili linaweza pia kutafsiriwa kama “usimruhusu mtu yeyote awe mwamuzi wako” kwa mujibu wa The Expositor’s Bible Commentary juzuu ya 11 uk.205.

   Mtu anaweza kuhitimisha kuwa kwa wanadamu walioanguka dhambini duniani kote, kuna nia kubwa ya kuabudu viumbe vingine vilivyo kati yetu na Mungu.

 

S: Kwenye Kol 2:18-23, mambo gani yanaweza kuwa mifano ya majivuno kujifanya unyenyekevu?

J: Waothodoksi wa Mashariki na Wakatoliki wanamuomba Mariamu na watakatifu waliokufa, kwa sababu wanajiona kuwa wadogo sana kumuomba Yesu au Mungu Baba.

 

S: Kwenye Kol 2:20; 3:3, ni kwa namna gani wakristo wamekufa ndani ya Kristo?

J: Tunapaswa kuwa wafu katika kuishi kwa ajili yetu. Kama Kristo alivyokufa kwenye ulimwengu huu, ubatizo unawasilisha kufa kwa habari ya kuishi kwa ajili yetu sisi wenyewe, kwa njia yetu wenyewe, hekima yetu wenyewe, malengo yetu wenyewe, na matakwa yetu wenyewe.

 

S: Kwenye Kol 2:21, kwa nini baadhi ya washika dini wana mazoea ya kuongeza vitu vingine kwenye neno la Mungu?

J: Mithali 30:6 inatuonya tusiongeze kitu kwenye maneno ya Mungu, usije ukaonekana mwong.gcfy Kwenye 1 Wakorintho  4:6 tunaonywa kutokupita yale yaliyoandikwa. Lakini, washika dini wengi wanapenda kufafanua kupita mambo yaliyoandikwa. Hoja ya kuongeza neno “msiguse,  kwenye amri ya Mungu ilianzia kwa nyoka alipomjaribu Hawa kwenye Mwanzo 3:3.

   Njia moja Wakatoliki na Waothodoksi wa Mashariki wanaongeza mambo mengine kwenye neno la Mungu ni kile watheolojia wa Kikatoliki wamekipa jina la utani “stuli ya miguu mitatu” ya Maandiko, Papa, na mitaguso. Wanaithamini muguu hii miwili sawa na Maandiko. Waothodoksi wa Mashariki wanasema kuwa maneno ya watakatifu wachamungu ni ya kweli kama Maandiko. Kwa makundi yote haya mawili, kuwa na Maandiko peke yake hakutoshi, machoni pao. Kuna baadhi ya Waprotestant ambao nao wanaweza kufanya makosa kama haya kwenye mapokeo yao. Njia ya pili ni ile inayoitwa “kutengeneza mafundisho.” Hoja ni kwamba Maandiko yametupa mafundisho tunayoyahitaji katika hali isiyokamilika. Ni jukumu jema la watheolojia wa miaka yote kuyaboresha, kuyafafanua, na kuyaendeleza mafundisho tunayohitaji kuyajua.

Wamebadilisha jukumu lao kutoka kuyaeleza Maandiko na kuwa kujenga vikorombwezo vyao wenyewe juu ya Maandiko. Tofauti na hii, ni hoja ambayo ninaiita “ubiblisti.” Mafundisho yeyote ambayo hayajaongelewa kwenye Biblia yanaweza kuwa sahihi au siyo sahihi. Lakini, hata kama yakiwa sahihi, hayakuwa na umuhimu wa kutosha hata kumfanya Mungu ayaweke kwenye Maandiko, hivyo hayana ulazima sana. Kama mafundisho yako hayakubaliani na Maandiko, basi usichelewe kutupa “makapi.”

   Msomaji mmoja Mkatoliki aliniuliza kwa upole kuhusiana na jambo hili. Kuna ushahidi gani kuwa baada ya Agano Jipya kuandikwa, wakristo wa mwanzo waliyafikiria Maandiko kuwa na mamlaka kwenye maisha (si tu kwenye uzuri wa kuyasoma)? Ilinichukua muda kupata ushahidi wote, na nililigawa swali sehemu mbili: Agano la Kale, na Agano Jipya. Baada ya kufanya utafiti, niliwakuta waandishi wa kikristo 41 walioandika kabla ya mkutao wa Nikea ambao waliyaelezea Maandiko kuwa ndiyo mamlaka yetu. Waandishi wa kikristo 38 walioandika kabla ya mkutano wa Nikea walilielezea Agano la Kale kuwa ni neno la Mungu, 28 walisema kuwa Agano Jipya ni neno la Mungu, na 35 walisema kuwa maneno ya Paulo yana mamlaka. Kwa kweli, maneno haya matatu “Agano la Kale” yametumiwa na waandishi 18 walioandika kabla ya mkutano wa Nikea. Maneno haya mawili “Agano Jipya” yametumiwa na waandishi 16 walioandika kabla ya mkutano wa Nikea. Hawa walikuwa na upendo, utiifu, mzigo, na waliyajali Maandiko kama wainjili (evangelicals) wanavyoyajali sasa. Unaweza kuangalia maelezo ya kina ya tafiti hizo zote hapa: www.biblquery.org/history/churchhistory/WhatEarlyChristiansTaughtOnDoctrine.html (and .docx) yenye vichwa Sc1, Sc2, Sc3, Otc26, Ntc19.

 

S: Kwenye Kol 3:1, kwa nini moyo/kupenda ni jambo la msingi hapa?

J: Kupenda ndicho kitu tunachokihitaji, au tunachopenda kukiepuka. Tunapaswa kuondoa kwenye mawazo yetu kupenda vitu vibaya na mazoea mabaya. Vivyo hivyo, Kol 3:1 inaagiza kuyatafuta yaliyo juu, kwa sababu upendo wetu utafuata. Kama Mithali 23:7 inasema,”Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.” Kama hakuna mabadiliko katika mambo tunayoyapenda, hakutakuwa na mabadiliko ya mwenendo wetu.

   Kama Paulo anavyofundisha, tunahitaji kukumbuka kuwa tulikufa, maisha yetu yamefichwa ndani ya Kristo, na tumefufuliwa pamoja na Yesu.

 

S: Kol 3:5 inaonekana kama ni wajibu wetu. Kwa kuwa tu wadhaifu na wenye dhambi, tunawezaje kufanya mambo ambayo tumeamriwa kuyafanya?

J: Kuwa dhaifu na wenye dhambi ni kisingizio tu kwa mtu ambaye amejazwa Roho Mtakatifu.

 

S: Kwenye Kol 3:8, kama tunaweza kufanya mojawapo ya dhambi hizi, unawezaje “kuyafisha” mambo ambayo yanaweza kuonekana kuwa ni ya kawaida kwako?

J: Neno “kufisha” linamaanisha kitu kama kuvua nguo, kwa hiyo kifananishi kinaweza kusaidia hapa. Ni “kawaida” tu kwa nguo zetu kuchafuka zaidi na zaidi,na kuwa zenye kutoa harufu zaidi, tunavyozivaa kwa miezi bila kuzibadilisha au kuzifua. “Unawezaje kupingana na kitu cha asli.” Unaweza kubadilisha nguo, na kuoga wewe mwenyewe. Tunaweza kuja kwa Kristo, kwa njia ya maombi, kusoma Biblia, na kutafakari. Tunapodumu kwa Kristo, tunaweza kupata nguvu za kiroho kubadilisha nguo zetu, na kumruhusu Roho Mtakatifu kututakasa. Tunaweza kuhiari, au kutarajia Roho Mtakatifu kutakasa zaidi mioyo yetu ili tupende zaidi mambo yanayompendeza Mungu na kuchukia kufanya mambo yanayomchukiza Mungu.

   Neno lenye kumaanisha “uroho” hapa, pleonexion, lina wazo la kutaka kitu au vitu zaidi, na linadokeza imani kuwa kila kitu na kila mtu kipo kwa manufaa yake yenyewe.

   Mambo kadhaa yanayoweza kusaidia ni kutunza rekodi ya jinsi unavyoenenda, kama kitu cha kukukumbusha. Pia, unaweza kuangalia uwezekano wa kuwa na rafiki mkristo ambaye kwa pamoja mtakuwa wazi kila mmoja kwa mwenzake na a) anakujali kama ulivyo, na b) anakujali kiasi cha kutokukuacha uwe kama ulivyo, wakati unatakiwa kutenda zaidi ya hayo na kuwa kama Yesu zaidi na zaidi.

   Je unaweza kuutawala mdomo wako, tumbo lako, na mwenendo wako, au vitu hivi vinakutawala wewe?

 

S: Kwenye Kol 3:12, je “tunabadilisha makabati yetu ya nguo” na kuongeza mambo haya?

J: Unapaswa kukusudia kufanikiwa kwenye maisha ya kikristo. Hakuna mbadala wa kufanya mazoezi mara kwa mara; unapofanya mambo ambayo Mungu anataka ufanye, itakuja kuwa rahisi. Tambua kuwa baadhi ya sehemu za maisha yako zitajiweka sawa kadri unavyoendelea na unataka sehemu hizo kuondoka.

 

S: Kwenye Kol 3:13, kwa nini ni muhimu kwetu kusamehe watu wengine?

J: Vinyongo havina nafasi kwenye moyo wa mkristo. Kama Tony Evans anavyosema, kukataa kusamehe ni kuchoma daraja unalotakiwa kulivuka, na ni gumu sana kuogelea hata kulivuka, wakati ungeweza kutembea na kulivuka, daraja ambalo umelichoma.

   Kusamehe kunamaamisha kuachilia mambo waliyotenda. Inamaanisha kuachilia deni unalowadai, au unafikiri unawadai, kwa mambo waliyofanya.

 

S: Kwenye Kol 3:15, kwenye mazingira yenye shughuli nyingi na msongo wa mawazo, tunawezaje kudumisha amani mioyoni mwetu?

J: Kwanza, hebu tuwe wazi. Wakolosai 3:15 haisemi kuwa hapatakuwa na mazingira yenye shughuli nyingi na msongo wa mawazo, Wakolosai 3:15 haisemi kuwa unatakiwa kuwa na amani wakati hakuna shughuli nyingi na msongo wa mawazo. Tunatakiwa kuwa na amani wakati wote, hata nyakati zenye shughuli nyingi na msongo wa mawazo. Kama kijitabu kiitwacho My Heart Christ’s Home kinavyofundisha kuwa tunapaswa kumruhusu Kristo atawale kila chumba cha nyumba yetu, yaani mioyo yetu. Mpe Yeye kila kitu, na matokeo ya kufanya hivyo ni wajibu wake.

 

S: Je Kol 3:16 inasema kuwa hatutakiwi kutumia vyombo vya muziki?

J: Kwa ukweli inasema kinyume cha hivyo. Watu kwenye Kanisa la Kristo wanaonyesha kuwa maneno ya kwenye mstari huu yanaongelea kuimba, na kuwa kuimba hakuhitaji vyombo vya muziki.

   Watu wa kwenye Kanisa la Kristo mara nyingi huwawanafikiri kuwa kama kitu hakina mfano kwenye Agano Jipya basi hakipaswi kufanywa. Hata hivyo, kama hakuna mfano wa watu wanaoosha mikono yao kabla ya kula, na Yesu hakuosha mikono yake kabla ya kula kwenye Luka 11:38-41. Kwa hiyo wakristo leo hii wamezuiliwa kuosha mikono yao kabla ya kula? – ukweli ni kuwa si hivyo.

   Lakini tukirudi kwenye hoja kuu, Wakolosai 3:16 inasema ikitumia zaburi. Maagizo kwenye zaburi nyingi yalihusisha kutumia vyombo vya muziki. Baadhi ya hizi ni Zaburi 4, 5, 6, 54, 55, 61, 67, na 76. Zaburi nyingine nazo pia zinaweza kuwa zinaagiza hivyo, lakini hatuna uhakika wa maneno ya kimuziki. Wakolosai 3:16 inaagiza kutumia zaburi wakati wa kuimba. Jaribu kutumia zaburi hii, “…Nitaimba, nitaimba zaburi, Naam, kwa utukufu wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri” (Zaburi 108:1-2). Nadhani watu wa Kanisa la Kristo hawatakiwi kusikiliza nyimbo wanazoimba, ni kweli?

   Zaburi hızı zinataja hapa 33:2; 43:4; 49:4; 57:8; 71:22; 81:2; 92:3; 98:5; 108:12; 147:7; 149:3; 150:3.

Hapa ni ushahidi zaidi kuwa vyombo vya muziki vimeruhusiwa.

 

Habakuki 3 ulikuwa ni wimbo ulioimbwa na kucheza kwa kutumia vyombo vya nyuzi, kwa mujibu wa Habakuki 3:19.

Manabii wa Mungu kwenye Agano la Kale walitoa utabiri kwa kutumia vinubi, matari, na filimbi kwenye  1 Samuel 10:5.

Nabii Miriam alimsifu Mungu kwa matari kwenye Kutoka 15:20.

Daudi alipiga kinubi na kumwabudu Mungu kwa mujibu wa 1 Samuel 18:10, pia  Zaburi 4 -6.

Chini ya uongozi wa Daudi, watu wengi walipiga matarumbeta, matuazi, na vyombo vingine kwenye 1 Nyakati 16:5,6,42.

Kwenye hekalu la Suleiman wako waliotumia vinubi kumsifu na kumtukuza Bwana kwenye 1 Nyakati 24:3.

Kwenye hekalu la Nehemia, waliliweka wakfu pamoja na matuazi, na vinubi kwenye Nehemia 12:27.

Kwenye Ufunuo14:2; 15:2, 5:8, wanaomwabudu Mungu walitumia vinubi.

Muhtasari: Mambo ambayo Daudi na manabii wengine waliyafanya kumfurahisha Mungu nyakati za Agano la Kale, mambo ambayo wenye uhai wanne na watu wa Mungu watafanya kwenye ibada ya mbinguni, halitakuwa jambo lisilompendeza Mungu sasa. Mungu mwenyewe anawapa watu wake vinubi ili wamsifu Yeye kwenye Ufunuo 15:2. Kama wewe ni muumini wa kweli, jizoeze kufanya hivyo.

   Lakini, tazama pia swali linalofuata kupata majibu mawili ambayo watu wa Kanisa la Kristo wanaweza kutoa.

 

S: Kwenye Kol 3:16, kwa kuwa kuna ushahidi wa kutumika kwa vyombo kwenye swali lililotangulia, mtu wa kwenye Kanisa la Kristo anaweza kuitikia vipi?

J: Kuna maitikio mawili yanayoweza kutolewa..

Ibada ya kanisani tu: Watu wengi (huenda wakawa wote) kwenye Kanisa la Kristo hawapingi vyombo vya muziki katika katika mazingira yote, wala hawapingi vyombo vya muziki kutumika kumwabudu Mungu. Wao wanapinga tu vyombo vya muziki kutumika kwenye majengo ya kanisa na/au kwenye ibada kanisani. Nilimsikia mmoja wa watumishi kwenye Kanisa la Kristo aliyewahi kumpinga mkristo mwingine kuhusiana na matumizi ya vyombo vinavyoendeshwa na mashine kwenye muziki, na baadaye alionekana akifurahia kusikiliza kituo cha redio cha kikristo kwenye gari lake. Hakuwa mnafiki, kama wakati alipokuwa kanisani. Nilisikia kuwa alivipinga vyombo vya muziki kanisani tu.

   Lakini, hakuna kifungu chochote cha Maandiko chenye kutofautisha kati ya ibada ya kanisa na ibada ya kuabudu. Kwa kweli, hakuna kifungu kinachosema kuwa kuimba kunaruhusiwa lakini kutumia vyombo vya muziki hakuruhusiwi kwenye ibada yeyote ile ya kuabudu.

Nyakati za Agano Jipya: Kuna watu wanaoweza kusema kuwa vyombo vya muziki viliruhusiwa kwenye Agano la Kale tu, kwani Agano Jipya halitoi mfano wowote wa kutumia vyombo vya muziki katika kuabudu hapa duniani.

   Lakini, Agano Jipya halisemi kuwa jambo hili lilibatilishwa, na kwa kweli halijabatilishwa, kama ambavyo watu watakuwa wanaendelea kutumia vinubi mbinguni wakati ujao.

Wote wanakubaliana kwenye mambo matatu.

1. Kumsifu Mungu na kuimba bila vyombo vya muziki kunaruhusiwa.

2. Wakati malaika saba walikuwa na matarumbeta kwenye Ufunuo, matarumbeta saba hayakuwa kwa ajili ya kuimba.

3.  Kama mkazo wa watu kwenye ibada kanisani upo kwenye kitu kingine mbali ya Mungu, kama vile kusikiliza ama vyombo vya muziki nyimbo, basi wanapaswa kubadilisha mkazo wao ili uwe kwa Mungu.

 

S: Kwenye Kol 3:16, unafikiria nini kuhusu Kanisa la Kristo: ni kwa kiasi gani linaendana na Biblia?

J: Kanisa la Kristo ni la tofauti sana. Nimewahi kutumika kwenye umoja wa madhehebu mbalmbali wa wanafunzi wakristo kwenye chuo kikuu nilichokuwa nasoma tulikuwa na wanafunzi wazuri sana toka Kanisa la Kristo. Kwa bahati mbaya wanaenda mbali na mafundisho ya Biblia kwenye mambo kadhaa: vyombo vya muziki, ubatizo wa maji, nk. Lakini wanafunzi hawa toka Kanisa la Biblia na wanafunzi wengine wasiotoka Kanisa la Biblia waliweza kukubaliana kuwa aliyetuunganisha ni mkubwa kuliko mambo yanayotutenganisha. Hata hivyo, hakuna tofauti iloyohusu mambo ya msingi. Jambo la msingi hapa lipo kwenye kundi la pili la watu, ambalo pia linaitwa Kanisa la Kristo.

   Kundi la kwanza linasema (kwa sehemu kubwa) vyombo vya muziki vyenye kuendeshwa na mashine haviruhusiwi kanisani. Kundi la pili pia linasema kuwa vyombo vya muziki vinavyoendeshwawatu kwa mashine ni ishara ya mpinga Kristo na vitawapeleka watu jehanamu. Kundi la kwanza linaamini kuwa Mungu hufanya kazi ya kuwazaa upya watu wakati wanabatizwa kwa maji. Kundi la pili pia linaamini kuwa mtu yeyote anayetofautiana na tafsiri yao atakwenda jehanamu.

   Kundi la kwanza linafanana sana na waumini kwa mwonekano wao na hawaamini kuwa kuna hakika ya wokovu. Kundi la pili, nimewasikia mimi mwenyewe wakisema vizuri sana kuhusu Wapelagia, na wanapinga kuwa watu walizaliwa na dhambi. Mafundisho kuwa Mungu amekwishaamua watu watakaoenda mbinguni na watakaoenda motoni ni neno chafu kwao.

   Watu wa kwenye kundi la kwanza ni wakristo ambao wana mafundisho yenye makosa kadhaa. Watu wa kwenye kundi la pili wanaonekana wakiweka kwa karibu sana mafundisho yao mahali pa damu ya Yesu inayookoa.

   Mbali ya makundi haya mawili ya Kanisa la Kristo, kuna kundi la tatu, lenye majina mawili: Boston Church of Christ (= Church of Christ International). Watu hawa wanafikiri kuwa Kanisa la Kristo lote (pamoja na madhehebu yote) hayako sahihi na ni makundi ya uongo ambayo hayamtukuzi Mungu. Tofauti na makundi mawili hapo juu, Boston Church of Christ nao pia wanafanya mambo kadhaa ambayo yanafanana na madhehebu ya kikristo ya uongo, kama vile waumini kutakiwa kuumgama dhambi zote kwa wazee wa kanisa, ambao huyaweka maungamo hayo kwenye kumbukumbu na wanaweza kuyatumia kuwatisha waumini hawa endapo wanataka kuondoka..

 

S: Kwenye Kol 3:17, ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya jambo lolote, hata mambo yasiyokuwa ya kiroho, kwa jina la Bwana Yesu?

J: Mambo yote tunayoyafanya, tuyafanye kama tunamfanyia Mungu. Jambo hili linawezakuhusisha njia nne: mtegemee Mungu, tambua mamlaka ya Yesu, fanya kazi kwa bidii kama mtu anayemfanyia Mungu, na fanya kazi kana kwamba Mungu atakufanya uwe shahidi. Unapokuwa kazini na hakuna mtu anayekuangalia, bado unafanya kazi kwa bidii, kwa manufaa ya mwajiri wako?

   Mkristo mmoja alikuwa na alama kwenye sinki la jikoni kwake, ambapo walikuwa wanaoshea vyombo. Alama hiyo iliandikwa hivi, “Ibada ya kiungu inafanyika hapa mara tatu kwa siku.”

 

S: Kwenye Kol 3:18, katika ndoa sahihi na ya kiungu, wake wanatakiwa kuwatii vipi waume zao kwa namna ambayo waume hawatakiwi kuwatii wake zao, kwa sababu Efe 5:21 inasema kila mmoja amtii mwenzake?

J: Tambua kuwa waume na wake wako sawa machoni pa Mungu. Lakini kama ambavyo Baba na Mwana walivyo sawa, ingawa pia Mwana anamtii Baba, mume na mke wako sawa, lakini mke humtii mume.

  Kama hakubali, basi liongeleeni jambo hilo. Lakini kama bado hakuna makubaliano, basi mume anatakiwa kufanya uamuzi.

Itakuwaje endapo mke hatatii? Biblia haijawahi kuagiza kuwa mume amlazimishe mke au amfanye mke kutii. Mume alipeleke jambo hilo kwa Mungu. Kama u mwangalifu katika kufanya mambo yako mwenyewe kuliko kuomba, basi hilo ndilo tatizo la kwenye mazingira yote.

   Wake wanapaswa kuwatii waume zao kama vile Sara alivyomtii Abraham kwenye 1 Petro 3:5. Kwa Bwana tu. Waume si madikteta, na wake si mali zao. Kiukweli, wake wanaonyeshwa kuwa na jukumu kubwa kwenye kununua mali zisizohamishika, na maamuzi yao yanayohusu fedha kwenye Mithali 31:10-31.

  Tofauti na mafundisho haya, kwenye uislamu, wake na mabinti na watumwa ni kama mali mbele ya mume.

Mtu anapopewa mke, mtumwa, au ng’ombe, alitakiwa kushika paji lake la uso na kumwomba Allah (Ibn-i-Majah juzuu ya 3 namba 1918 uk.157).

Kuhusu wanawake kwa ujumla, hivi ndivyo alivyosema Mtume Muhammad, “Mtumwa ni mchungaji wa mali za bwana wake, na mke ni mchungaji wa nyumba na watoto wa mume wake” (Abu Dawud juzuu ya 2 namba 2922 uk.827). Kumbuka kuwa nyumba na watoto ni mali ya mume hapa.

Yahya aliniambia kutoka kwa Malik kutoka kwa Zayd ibn Aslam kuwa Mjumbe wa Allah, Allah ambariki na kumpa amani, alisema, ‘Ukioa mwanamke au kununua mtumwa msichana, mshike kishungi na umwombe Baraka. Ukinunua ngamia, ondoa sehemu ya juu ya nundu, na kimbilia kwa Allah (Shaytan.” Muwatta’ Malik 28.22.52).

 

S: Kwenye Kol 3:18-22, ni kwa namna gani mistari yote hii inafanana?

J: Hizi ni jozi zenye kukubaliana. Mtume Paulo hamuongelei mke bila mume, mtoto bila wazazi, mtumwa bila bwana wake. Unapofikiri kuwa watu wengine wana majukumu kwako, lakini wewe huna majukumu yeyote kwao, mawazo yako yako mbali kabisa na jinsi Paulo alivyokuwa anawaza.

 

S: Kwenye Kol 3:18-22, njia zipi ni sahihi na zipi si sahihi za kuridhia kwa kuonyesha heshima kwa mtu mwingine?

J: Hata kama mtu hana mamlaka juu yako, kama atakuagiza au kukuomba kitu, na kitu hicho si kinyume cha sheria, si kiovu, wala hakipingani na Mungu, basi kwa nini usifanye kitu hicho wanachokutaka ufanye? Ni kweli kwamba kama wanakuagiza au wanataka kitu ambacho hakimpendezi Mungu, basi kama mtoto mtiifu wa Mungu huwezi kufanya. Mungu mara nyingi (si mara zote) huwa anawatumia watu wenye mamlaka juu yetu kutuelekeza, na mara nyingi tunapaswa kufuata maelekezo yao.

   Hebu tuangalie mfano mmoja, na tuone ni jinsi gani jibu la swali hili mara nyingine haliwi rahisi. Natuseme, kwa mfano, mume au mzazi amekuagiza usiende au usisikilize ibada za kanisani. Kwa kuwa Mungu ametuagiza kuwa tusiache kukutanika pamoja kwenye Waebrania 10:25, unao wajibu wa kuitii Waebrania 10:25. Unatakiwa kusema kwa upole, lakini kwa wazi kuwa haupaswi kulitii agizo hilo na kuwa utaendelea kukutanika pamoja na waumini wengine, au ufanye hivyo kwa siri? Bila shaka kama maisha yako yako hatarini basi utafanya hivyo kwa siri. Vipi kama wamekuzuia kwenda kwenye kanisa fulani, lakini unaweza kwenda kwenye kanisa lingine. Hapo utatakiwa uangalie mambo machache. Kwanza kabisa, kama kanisa lingine wanalotaka uende haliko makini katika kufuata neno la Mungu, basi unatakiwa kutokulitii agizo hilo. Unatakiwa pia kuuliza sababu ya wao kukuzuia kwenda kwenye kanisa husika. Huenda, kwa mfano, ikawa ni kwa sababu nzuri, kama kanisa hilo linajihusisha na kutokumtii Mungu kwa kiasi kikubwa. Lakini kama ni kwa sababu hawakubaliani na mafundisho yasiyokuwa ya msingi, au kwa sababu ya jambo dogo, au dharau ambayo haijasamehewa, basi ombi lao halitoki kwa Mungu. Lakini kama unashindwa kutii amri ya mtu mwingine kwako kwa sababu unatakiwa kumtii Mungu, unaweza ukapata madhara au mapambano ya aina au kiasi fulani. Lakini furahi, kwa kuwa Mungu anaona jinsi unavyoteseka kwa ajili yake.

   Kama mfano wa pili, chukulia kuwa mkubwa wako kazini ama anawafaanyia dhihaka au anawakosea heshima rafiki zako, ikiwa wapo au hawapo. Usiuchukulie kirahisi utani wao wenye dharau, bali usimame pamoja na rafiki zako, hata kama itamanisha kuingia kwenye hatari ya kumkasirisha au kumchukiza mwenye mamlaka juu yako? Utafanyaje hapa?

 

S: Kwenye Kol 3:18-22, kinyume cha mstari huu, ni njia zipi zisizokuwa sahihi ambazo mtu anaweza kuzitumia kujitwalia madaraka ya mtu mwingine?

J: Dhalilisha mamlaka yao wakiwa hawapo, au vinginevyo mbele zao. Wakati mwingine ni vizuri kuhoji mambo, lakini kuendelea kuhoji hasa mbele ya watu wengine. Unapaswa kuwashauri kuhusu kufanya maamuzi, lakini kama wao ndio wenye jukumu la kufanya maamuzi, na wameyafanya, basi usiendelee kuhoji au kuyadhalilisha..

 

S: Kwenye Kol 3:20; Mat 10:37, je watoto wanatakiwa kuwatii wazazi wao?

J: Watoto wanatakiwa kuwaheshimu (Kutoka 20:12; Kumbukumbu 5:16), na kuwatii wazazi wao (Wakolosai 3:20; Kutoka 21:17; Walawi 20:9), katika Bwana (Waefeso 6:1), lakini hawatakiwi kuwapenda wazazi wao zaidi ya jinsi wanavyompenda Mungu (Mathayo 10:37). Kama kifananishi, unatakiwa kutii sheria za jimbo lako, isipokuwa pale zinapopingana na sheria za nchi yako Vivyo hivyo, unatakiwa kuwatii wazazi wako, isipokuwa wakati wanapingana na maneno ya Mungu.

   Kwa mfano mkamilifu, unaweza kumuangalia Yesu na mama yake. Wazazi wa Yesu waliporudi hekaluni na kumkuta humo, Yesu aliwaambia kwa utulivu kabisa jambo alilolifanya kwenye Luka 2:41-50. Yesu alisikia ombi la Mariamu la kubadili maji yawe divai, ingawa muda wake ulikuwa bado Yohana 2:1-11. Lakini wakati mama na kaka wa Yesu walipokwenda kumchukua alikataa kwenda nao kwenye Marko 3:31-35.

 

S: Kwenye Kol 3:20, je tunatakiwa kuwalea vipi watoto wetu?

J: Mfano wetu unaweza kuwa wa maana sawa na maneno yetu. Wazazi wanatakiwa kuwa na sauti moja katika kuwalea watoto wao. Inakuwa vigumu kwa mtoto wakati mzazi mmoja anaposema kitu fülanı si kizuri, lakini mzazi mwingine anampinga.

   Hatutakiwi kuwaadhibu watoto wakati tunapokuwa tumekasirika, bila haki, au bila kuwaeleza sababu. Ni jambo zuri kabisa kumwambia mtoto “Ninakwenda kukuadhibu kwa koşa hili, lakini siyo sasa. Nataka nitulie kwanza.” Usifanye jambo ambalo litamletea mtoto madhara ya kudumu, kama kupiga masikio, kumpiga kichwani, au kumtikisa kwa nguvu.

   Usiwachokoze au kuwakatisha tamaa watoto.

 

S: Kwenye Kol 3:20, je wazazi wana jukumu gani kwa watoto wao watu wazima?

J: Amri kwa watoto zinakuwa miongozo na mapendekezo kwa watoto watu wazima. Wazazi wanatakiwa kutambua kuwa kwenye eneo moja au zaidi, mtoto atakuwa anafahamu kuliko mzazi, na mzazi anatakiwa kufurahiia jambo hilo. Lakini watu wazima bado wanaweza kufanya makosa ya kijinga pia. Tunategemea kuwa kwa maneno ya hekima na imani uliyoijenga kwa miaka mingi, wataendelea kukusikiliza.

 

S: Kwenye Kol 3:20, je wazazi wana jukumu gani kwa watoto wao watu wazima?

J: Amri kwa watoto zinakuwa miongozo na mapendekezo kwa watoto watu wazima. Wazazi wanatakiwa kutambua kuwa kwenye eneo moja au zaidi, mtoto atakuwa anafahamu kuliko mzazi, na mzazi anatakiwa kufurahiia jambo hilo. Lakini watu wazima bado wanaweza kufanya makosa ya kijinga pia. Tunategemea kuwa kwa maneno ya hekima na imani uliyoijenga kwa miaka mingi, wataendelea kukusikiliza.

 

S: Kwenye Kol 3:20, ni kwa namna gani watoto watu wazima wanapaswa kuwaheshimu wazazi wao?

J: Fikiria wakati uliopita, uliopo, na ujao.

Wakati uliopita: Kuna kipindi ambacho utatambua kuwa unafahamu mambo mengi sasa kuliko wazazi wako walivyokuwa wanafahamu kwenye maeneo fulani. Kwa sasa unaweza kuwa unawalinda wao na hata nyinyi wenyewe. Hata hivyo, unapaswa kuwashukuru kwa kuwekeza maisha yao kwako, kukujali na kukulinda, kukupatia mahitaji yako, na kukupa hekima zao, kama walıyo nayo. Bila shaka utakuwa umetambua kuwa wazazi wako hawakuwa wakamilifu, na wewe pia hautakuwa mkamilifu. Lakini waheshimu kwa kujaribu kuwa wakamilifu, kwa kadri walivyoweza kufanya.

Wakati uliopo: Toa shukrani mkiwa peke yenu na wao pia mbele za watu kwa kazi waliyoifanya, na waheshimu. Jambo moja wazazi walitaka zaidi kutoka kwa wanao watu wazima ni kupata muda wa kuongea nao. Unaweza ukawa na mambo mengi sana ya kufanya, lakini itakuwa vema kama utatoa kipaumbele kwa muda wa kuwatembelea na kuongea nao.

Wakati ujao Kipindi fulani kikifika, wazazi watahitaji zaidi msaada, hekima, na hata fedha kuliko ambavyo wangependa kufanya hivyo. Kama walivyokutunza wewe ulipokuwa mdogo, unaweza kurudisha fadhili kwao wakati huu ambapo wamekuwa wazee. Pia, unaweza kukumbuka kuwa watoto wako mwenyewe wanakuangalia, na wanajifunza, kutoka kwa mfano wako wa jinsi unavyowatunza wazazi wako.

 

S: Kwenye Kol 3:22, ni kwa nini watumwa wanatakiwa kuwatii mabwana zao?

J: Agano Jipya halikuunga mkomo utumwa, lakini halikuupinga pia. Hata wakati mazingira yalipokoşa kuwa mazuri, kama wakati ambapo mkristo alikuwa na bwana asiyetenda haki na anapitia mateso yasiyokuwa ya haki kwenye 1 Petro 2:18-19, wakristo bado walitakiwa kuvumilia hali hizi mbaya. Mambo yatakuwa mazuri zaidi kwa wakristo kwenye maisha haya, na utakuwa ni ushahidi kwa watu wengine wa Kristo anayeishi ndani yao.

 

S: Kwenye Kol 3:22, je tunatakiwa kuwatendea vipi watu wanaokuwa chini yako kimadaraka?

J: Watendee watu walio chini ya mamlaka yako utu a heshima. Walipe kwa haraka sana kwa kila kazi wanayofanya, na tunza ahadi zako kwao. Kanuni ya msingi, kama mnavyotaka watu wawatendee nyinyi, watendeeni vivyo hivyo, itawafikisheni mbali. Ni şifa gani njema ulizoziona kwa wakubwa wako wa kazi wa zamani? Ulitendewaje, au ulipaswa kutendewa vipi na wakubwa wako wa kazi wa zamani. Watendee watu walio chini ya mamlaka yako namna hiyo hiyo. Kiri makosa yako. Usishangazwe kuwa watu walio chini ya mamlaka yako wanafanya makosa, labda kama kampuni yako inaajiri watu wakamilifu tu. Unaweza kuwaonyesha makosa yao, na kujadiliana nao namna ya kujifunza kujiepusha kufanya makosa kama hayo siku zijazo. Lakini hutakiwi kutoa ujumbe kuwa hautayasahau makosa yao, kama unapenda waendelee kufanya kazi kwako. Jiepushe kuonekana kuwa unapenda kufahamu mambo mabaya tu ili uyatumie dhidi yao wakati wa kutathmini utendaji wao wa kazi, lakini unayasahau mambo yote mazuri wanayofanya.

Usiwacheke watu walio chini ya madaraka yako, wakiwepo au hata kama hawapo.

   Mwisho, watu walio chini ya madaraka yako ambao unafanya nao kazi kila siku; wachukulie kuwa wanawezakuwa na kitu muhimu cha kukufundisha. Panaweza kuwa na jambo ambalo unashindwa kulielewa, njia ambazo unatakiwa kuzibadilisha na kuziboresha, kuwa unaweza usifahamu. Waombe wakupe mrejesho wa jinsi unavyoweza kufanya vizuri zaidi katika kazi unayoifanya.

 

S: Kwenye Kol 3:22, tunawezaje kuwaheshimu watu walio na mamlaka juu yetu?

J: Waonyeshe kuwa unawaheshimu, angalau mafasi zao. Lakini usiwe mtu anayetaka kuwapendeza watu wengine. Ni jambo jema kuwasifia na kuwatia moyo, lakini usiseme mambo ambayo si kweli au huyasemi kwa kumaanisha. Unaposhindwa kukubaliana na njia yao ya kufikia malengo ya taasisi yenu, una wajibu wa kupendekeza njia ambayo unadhani ni nzuri zaidi ya kufanya, angalau mara moja. Lakini kama hawatapenda kuifuata hapatakuwa na haja ya kulalamika. Wamekwishafanya uamuzi wao na wanatakiwa kuutekeleza. Ni vema kutumia barua pepe na kuweka kumbukumbu ya mambo haya ili kujikinga na mambo yeyote utakayoyafanya siku zijazo. Mkubwa wako kazini anayo mamlaka ya kukuambia mambo ya kufanya, lakini hana mamlaka ya kukufanya wewe kuwa mbuzi wa kafara. Kama ambavyo meneja mmoja hivi alivyoandika kwenye kijichumba chake (kwa utani) kuwa “Sisemi kuwa ni kosa lako. Ninasema kuwa nakulaumu wewe.” Lakini kwa upande mwingine, tunatakiwa kuwajibika na kukiri makosa yetu yaliyosababishwa na sisi au maamuzi yetu yasiyokuwa mazuri.

   Wakubwa wetu kazini ni binadamu, na wanaweza kuvunjika moyo nao wanahitaji kutiwa moyo. Wanaweza kubadilisha mawazo yao kwa sababu ya mabadiliko ya hali itokayo nje ambayo haiwezi kutarajiwa. Wakubwa wetu kazini wanaweza pia kubadilisha mawazo yao wakati hakuna kitu kilichobadilika, isipokuwa kuna jambo wamelitambua. Kama ambavyo msanifu mmoja wa programu za kompyuta anavyosema mara kwa mara, “Nitaendelea kuwa na haki ya kuwa na maarifa zaidi.” Hapana shida kumweleza mkubwa wako kazini jambo hilo mara moja ili kuhakikisha kuwa wazo jipya linafahamika, wazo lenye kukinzana na wazo zamani linawekwa wazi, lakini usiendelee kuzungumza kwa kurudia rudia. Sisi sote siyo wakamilifu.

 

S: Kwenye Kol 4:1, ni kwa namna gani unamtendea kwa haki mtu ambaye yuko chini yako kimadaraka kazini, kanisani, jeshini, au kwenye ofisi ya kisiasa?

J: Kuna mambo angalau matatu yanayohusika na jinsi ya kuwatendea “kwa haki” watu walio chini ya mamlaka yako.

Kuwa mwamimifu kwa maneno yako: Kama mtu alikubali kufanya kazi chini yako katika masharti na malipo fulani, mara baada ya kuacha nafasi yingine za kazi ambazo angeweza kuzichukua, je utafanya kwa uaminifu mambo yaliyokubaliwa? Au, sasa kwa kuwa hawapo kwenye nafasi nzuri ya kwenda sehemu nyingine, je utabadilisha masharti na malipo ili zikupendelee? Kama unatarajia kuajiriwa, na umekubali kwa mdomo au kwa maandishi kufanya kazi kwa kiasi fulani cha fedha, kama fursa nyingine inatokea, je utavunja ahadi yako, urudi na kutishia kuvunja makubaliano yako isipokuwa ama watakulipa hela zaidi, au uwe mwanaume au mwanamke anayesimamia maneno yake?

Kanuni muhimu zaidi: Kwenye Mathayo 7:12  inaagiza kufanya kwa watu wengine kama ambavyo ungetaka watu wengine wakufanyie wewe. Kama ungekuwa mahala pa mwajiriwa wako, na una mkubwa wako wa kazi ambaye ni mzuri, ni kwa namna gani mkubwa wako huyu wa kazi atatenda kwako? Kuwa mkubwa huyu wa kazi kwa watu walio chini yako!

Usiwe na upendeleo: Je wewe unawasamehe baadhi ya watu walio chini ya mamlaka yako wanapofanya makosa kuliko watu wengine, tu kwa sababu ya majina yao? Je unathamini juhudi ya kazi na michango ya baadhi ya wafanyakazi kuliko  wengine? Unaweza kugawa kazi tofauti kwa wafanyakazi tofauti kutegemea na ujuzi na uzoefu wao, lakini je una desturi ya kuwapa baadhi ya wafanyakazi kazi zenye mshahara zaidi na zenye kuwahakikishia kuwa watakua kitaaluma, na kuwafanya waonekana wazuri, wakati wafanyakazi wengine wanapewa kazi ambazo hata kama wakizifanya vizuri sana mchango wao utasahaulika? Au je unawatengenezea baadhi ya wafanyakazi mazingira ya kushindwa bila hata ya wewe mwenyewe kujua? Mungu ametuagiza kwenye Yakobo 2:1 tusipendelee watu. Muktadha wa kwenye waraka wa Yakobo ni mtu anayekuja kanisani, lakini amri hii inatakiwa kufanyiwa kazi na waumini wote popote pale walipo. Walawi 19:15 inaagiza tusipendelee matajiri wala maskini, na ingawa hatupo tena chini ya Sheria ya Musa, amri hii inaendelea kuwa na nguvu.

   Je ungependa watu walio chini ya mamlaka yako wahamasike kufanya kazi kwa bidii? Usipuuzie kufanya mambo haya matatu.

 

S: Kwenye Kol 4:2-18, je sura ya 4 inahusiana vipi na Kol 3:18-25?

J: Wakolosai 3:1-17 inatuambia namna ya kuishi maisha binafsi na yaliyo ya kweli ndani ya Kristo yanayoonyesha ukomavu, na yenye kupendeza. Wakolosai 3:18-4:1 inatuagiza jinsi ya kuweka mahusiano yetu mikononi mwa Mungu. Lakini Wakolosai 4:2-18 si salamu za haraka tu na hitimisho, bali Mtume Paulo anatupa mifano ya namna mahusiano yalivyoitia nguvu huduma yake kupitia ushirika wa injili wa waumini wengine.

 

S: Kwenye Kol 4:2, nini maana ya “kuwa macho” katika maombi?

J: Waefeso 6:11-17 inatuagiza kuvaa silaha zote za Mungu, na kisha Waefeso 6:18 inatuagiza kuomba. Je umewahi kusikia kuwa askari makini ambaye alivaa silaha vizuri, lakini alikwenda kwenye uwanja wa mapambano wakati ule tu aliojisikia kwenda? Mimi pia sijawahi kusikia.

   Kukesha katika maombi kunamaanisha kuwa macho dhidi ya uchovu unaoongezeka kwenye maombi na kuanguka kwenye “usngizi wa kiroho.” Pambana kuwa na nidhamu ya kudumu katika maombi kwa ajili ya ufalme wa Mungu, mahitaji ya watu wengine, na mahitaji yetu. Kwenye mfano wa hakimu asiyetenda haki kwenye Luka 18:1-8, Yesu anatoa mfano wa kung’ang’ana tunakotakiwa kuwa nako. Kama kung’ang’ana kulisaidia mbele ya hakimu asiyetenda haki, je kutasaidia kwa kiasi kikubwa namna gani kwa Baba yetu mwema? Lakini mwishoni mwa mfano, Yesu hayatilii mashaka mapenzi ya Mungu, bali imani yetu ili iweze kuendelea kuwepo. Je Mungu anapokuona anaangalia ukiomba anakuona ukiendelea kufanya hivyo mara kwa mara? Epafra alikuwa anajibidisha kwenye maombi kwa ajili yao kwenye Wakolosai 4:12, hivyo basi ni kwa nini wao nao wasiungane naye kwenye kazi hii? Wakolosai 4:2-3 inaonyesha kuwa Mtume Paulo hakuweza kupumzika hadi hapo anapokuwa ametumia kila fursa iliyopo kwa neno, tendo, au maombi kueneza injili, na wao pia wanatakiwa kutumia fursa zao.

 

S: Kwenye Kol 4:3, Paulo alikuwa wa kiroho sana, mwenye hekima sana, na mwenye kufanya kazi kwa bidii sana. Ni kwa nini mtu kama yeye awe na haja ya kuomba maombi kwa Wakolosai?

J: Hapa Paulo anaomba bayana kuwa milango ifunguliwe kwa ajili ya injili. Paulo aliona wazi kabisa maisha yake mwenyewe ya uaminifu ya kiroho, kujitoa kwake, busara, imani, na kufanya kwake kazi kwa bidii haviwezi kufungua fursa za injili ambazo Paulo alikuwa anazitafuta. Mungu tu ndiye anayeweza kufanya hivyo. Mungu atafanya hivyo kupitia maombi yetu. Wala haikuwa kupitia kujiona kwake kuwa hajitoshelezi, bali kutambua kwake umuhimu wa kumuomba Mungu, vinginevyo kazi yake isingekuwa na mafanikio. Kitu cha kushangaza zaidi ni kuwa hatumuoni Paulo akiomba kuwa atolewe gerezani, isipokuwa kwenye maneno machache na yasiyokuwa wazi “Kumbukeni kufungwa kwangu” kwenye Wakolosai 4:18. Mtume Paulo ni kama alikuwa na mawazo kuwa “Kwangu mimi kutupwa gerezani si jambo kubwa kwa ufanisi wa huduma yangu, lakini kushindwa kwenu kuniombea hilo ndilo jambo kubwa.” Kama maombi, yake mwenyewe na ya watu wengine, yalikuwa muhimu sana kwa ajili ya kazi ya Paulo, ni kwa namna gani unayathamini maombi kwenye huduma yako?”

 

S: Kwenye Kol 4:5, ni kwa njia zipi, ama za makusudi ama za kutokukusudia, tunaweza kushindwa kuenenda kwa hekima mbele ya watu wasiokuwa waumini?

J: Tunaweza kujificha tusitambulike kuwa tu wakristo, tunaweza kuutia matatani ushuhuda wetu, na tunaweza kukwaza watu wengine bila sababu.

Kujificha: Kuhusu kujificha tusitambulike kuwa wakristo, kipindi fulani, nilipokuwa nasoma chuo kikuu, nilikuwa nimekaa kwenye bwalo la kulia chakula na mtu mmoja ambaye sikuwanamfahamu, nikiwa nafanya kazi wakati wa likizo ya majira ya joto, na tulianza kuongea. Nilimfahamisha ndoto zangu za muda mrefu na haja yangu ya kuwa mmishenari. Bila kuchelewa akasema, “Aha! Nilifikiri wewe ni mmomoni.” Kwa haraka nikamrekebisha lakini sikumweleza habari za Yesu na jinsi anavyonifaa mimi.

   Niliwahi kusoma habari ya mtu mmoja aliyekwenda kazini kwake siku moja na kuwaambia watu kuwa amempokea Yesu maishani mwake. Mtu mmoja ambaye naye alikuwa amempokea Yesu maishani mwake alimpongeza, na muumini mpya alimwangalia muumini wa muda mrefu kwa mshangao. Akamwambia, unajua wewe ndiwe sababu ya mimi kuchelewa kumpokea Yesu maishani mwangu kwa miaka kadhaa? Muumini wa muda mrefu alishangazwa na akauliza ni kwa sababu gani? Muumini mpya akasema, ulikuwa unaonekana kuwa umetosheka na maisha yako yalikuwa na utaratibu. Sikujua kuwa wewe ulikuwa umempokea Yesu, na nilifikiri kuwa kama umeweza kuwa na maisha yenye utaratibu, basi sihitaji kumpokea Yesu.

Kuutia ushuhuda matatani  ushuhuda wetu unaweza kuhusisha kutokumtii Mungu kiuwazi kabisa au kuchelewa kumtii Mungu, kwa manufaa ya kazi, marafiki, au familia zetu.

   Kwa kutokuongea kwa kumaanisha kuhusu ukristo, kujitoa kwetu, na kwenda kwetu kanisani.

   Je unatumia muda wako wote kwenye maongezi yasiyokuwa na maana na mizaha, wakati rafiki zetu hawaoni kuwa tunayamaanisha maneno tunayoyasema? Kuna nyakati ambazo tunatakiwa kuongea mambo ya maana na watu tunaokuwa karibu nao tukiwashirikisha injil.

Kukwaza watu wengine: Injili haikosi kukwaza baadhi ya watu, na hatupaswi kuogopa kuhusiana na jambo hilo. Lakini tunawiwa kuepuka kukwaza watu ambako hakuna ulazima au kuwaudhi jirani zetu wasiokuwa waumini.

 

S: Kwenye Kol 4:6, ni kwa namna gani maneno yetu yanatakiwa kuwa na neema yakiwa yamekolea munyu, na tuweze kumjibu kila mtu jinsi itupasavyo?

J: Maneno yetu yanatakiwa yawe na upole, yasiyokuwa matusi, yasiyokwaza, wala kuwa na machungu. Lakini tunatakiwa pia kutafuta namna ya kuwashirikisha watu wengine neema ya Mungu. Chumvi huhifadhi, huleta radha, na huwafanya watu wajisikie kiu. Tunatakiwa tuwe na maneno mazuri tu, yasiyokuwa machafu, matusi, masengenyo, na magomvi. Natuongee kutoka katika maisha yetu tukiwaonyesha watu wengine furaha ya kuokolewa na Yesu. Mwisho, tunatakiwa kuongea ili tuwatengenezee watu wengine kiu ya kumjua Yesu, Maji yetu ya Uzima. Je maneno yako yanaustahili mwenendo wa mtu aliyeokolewa na Yesu? Je maneno unayotarajia kusema yanafaa kusemwa, na je yanastahili kusemwa?

   Tunahitaji kuweka uwiano mzuri wa kushirikisha injili kwa ujasiri na mikakati na busara. Uwiano mzuri unategemea na mazingira na aina ya watu unaokwenda kuongea nao? Wakati mwingine, hasa kwenye mazingira ya kazi, kuna ukomo wa kiasi cha uinjilisti wa moja kwa moja utakaoweza kuufanya hasa kama malipo ya kazi yako yanategemea urefu wa muda (masaa) ulioifanya. Lakini unaweza kuwa na maneno ya kiungu na kujibu maswali kwa kadri yatakavyoulizwa kuhusu tumani ulilonalo.

 

S: Kwenye Kol 4:7, je waraka wa Wakolosai uliandikwa wakati mmoja na nyaraka za Waefeso, 2 Timotheo, na Tito?

J: Waefeso  6:21 na Wakolosai 4:7 zinasema kuwa Tikito atawaambia atakapokutana nanyi. Kwenye 2 Timotheo 4:12, Paulo anasema kuwa alimtuma Tikito aende Efeso. Kwenye Tito 3:12, Paulo anasema kuwa atamtuma Artema au Tikito aende kwa Tito. Tikito ndiye aliyezibeba nyaraka hizi, na Tikito huenda hakujua kuwa watu watamfahamu kwa zaidi ya miaka 2,000 kwa sababu ya vipande vya ngozi alivyokuwa anabeba.

   Hata hivyo, kwenye Tito 3:12, Paulo alikuwa huru, na marejeo mengine yalikuwa wakati Paulo akiwa gerezani, hivyo zilikuwa angalau safari mbili. Kwa kuwa kulikuwa na safari zisizopungua mbili, kuna uwezekano kuwa palikuwa na safari nyingine tatu au zaidi. Hata hivyo, namna yeyote ilivyokuwa, haiathiri imani ya kikristo au mamlaka ya Maandiko (vitabu vya Biblia vinavyotambuliwa na Kanisa) ya nyaraka hizi.

 

S: Kwenye Kol 4:9, kwa nini Paulo hakujijenga mwenyewe hapa kwa kuwaambia watu aliowaandikia kuwa Onesmo alikimbia, na kuwa Paulo alimshawishi arudi?

J: Paulo alilitaja tu jina lake na kuwa Onesmo alikuwa mwamimifu. Wakristo wa Kolosai watakuwa walimfahamu Onesmo, aliyekuwa mmoja wao. Paulo hakuwa na haja ya kuwaeleza Onesmo alikuwa ni nani, alijijenga mwenyewe, au kuwa Onesmo alikimbia. Paulo hakuona haja ya kuelezea kitu chochote kilichokuwa hasi kuhusu Onesmo, kama ambavyo na sisi hatutakiwi kueleza jambo lolote hasi kuhusu watu wengine isipokuwa tu kuna sababu nzuri ya kufanya hivyo. Kama The Expositor’s Greek Testament juzuu ya 3 uk.545 inavyosema, “ukimya wa aina hii ni kawaida ya uangalifu aliokuwa nao Paulo.” Na kwa taarifa, mtu anapoeleza jambo kwa urefu sana ili kujijenga, inakuwa dhahiri kwa watu wote au angalau kila mmoja kasoro yeye mwenyewe, kuwa anatafuta kujijenga.

 

S: Kwenye Kol 4:10, ni nani ambaye Paulo anawaambia Wakolosai wampokee Marko, kwa kuwa Paulo hakuwaambia wampokee mtu mwingine yeyote?

J: Ni dhahiri kuwa Wakolosai walitakiwa kumpokea mtu yeyote yule anayemtumikia Bwana, lakini inawezekana walikuwa na maswali kwenye mawazo yao kuhusiana na Marko. Watu wengi wangeweza kuwa wanafahamu kuwa Marko alimwacha Paulo na wamishenari wenzake hapo awali. Badala ya kueleza kwa undani kuhusu Marko kwa watu ambao hawakufahamu kosa hilo la Marko, Paulo anaongea kwa namna isiyokuwa ya moja kwa moja, ili kwamba watu waliokuwa wanafahamu wajue kuwa Marko amerudi, amepatana na Paulo, na uhusiano na ushirika wao kwenye injili umerejeshwa.

 

S: Kwenye Kol 4:11 “Yusto” ni nani ambaye Paulo anamtaja? Na kuna uhusiano gani kati ya jina lake na jina la Yesu (Mat 1:21)?

J: Yusto ni jina la muumini ambaye aliitwa pia Yesu. Kama hii leo kuna watu wanaoitwa Yoshua kwa Kiswahili, na “Yesu” (linatamkwa he sus) kwa Kihispania/Kispanishi. Watu wengine wakati ule waliitwa Yeshua (Yesu kwa Kiebrania) pia.

 

S: Kwenye Kol 4:11, ni jambo gani la kusikitisha ambalo Paulo analiongea hapa?

J: Paulo alikuwa na sera ya kwenda kwenye sinagogi la Wayahudi na kuhubiri kwa Wayahudi kwanza, kisha kwa watu wa mataifa. Lakini licha ya mkazo wake mkubwa kwa Wayahudi, hawa walikuwa ni Wayahudi pekee waliokuwa wanafanya naye kazi. Wakati mwingine tunapofikiri kuwa tumeielewa kabisa huduma au tunadhani hivyo, mambo tuliyofikiri kuwa ni ya muhimu yanakuwa na matunda kidogo, na mambo ambayo hatukuyatilia maanani yanazaa matunda zaidi.

 

S: Kwenye Kol 4:13-14, je waraka kwa Walaodikia ni kitabu cha Biblia kilichopotea?

J: Hapana, kwa sababu mbil.

1) Kwanza, si lazima kuwa waraka huu ulikuwa sehemu ya Biblia, kwa sababu hata kama palikuwa na kitabu ambacho kilipotea kweli, Mungu “halazimishwi” kuhifadhi kitabu chochote ambacho hakutaka kukihifadhi. Kama jambo la ziada, kulikuwa na waraka wa kughushi wa Walaodikia, lakini uliandikwa kwenye karne ya nne na ulitambuliwa kuwa ni wa kughushi wakati huo.

2) Pili, je palikuwa na kitabu kilichopotea au huu ulikuwa ni waraka uliofahamika Waraka kwa Waefeso.

2a)  Huu unadhaniwa kuwa ni waraka ambao haukuhifadhiwa.

2b) Paulo hasemi kwenye Wakolosai kuwa aliandika waraka kwa Walaodikia, bali moja ya nyaraka za Paulo zilizosambazwa ulikuwa unakuja kutoka Laodikia. Mji wa Efeso ulikuwa karibu maili 100 (Km 160) kutoka mji wa Kolosai, na mji wa Laodikia ulikuwa kati ya miji hii miwili, maili 10-12  (Km 16-19) magharibi na kusini kiasi mwa Kolosai. Kwa hiyo waraka huu ulikuwa wa mzunguko, ambao tunautambua kuwa ni Waraka wa Waefeso.

 

J: Kwenye Kol 4:17, ni kwa jinsi gani, kama mkubwa mahali pa kazi aliye muumini, au msimamizi, unamwambia mtu aliye chini ya madaraka yako kuwa aweke mkazo katika kufanya kazi yake?

J: Kuna uwezekano kuwa Arkipo, kwenye Filemoni 1-2, alikuwa mtoto wa Filemoni na Afia. Maneno haya yanawezakuwa yanawaongelea watu hawa watatu waliokuwa wanampokea Onesmo, mtumwa aliyekuwa ametoroka. Kwa upande mwingine, maneno haya yanawezakuwa yanaongelea majukumu mengine ya kihuduma, zaidi ya kumpokea Onesmo.

   Katika kuwaeleza watu kuwa wanahitaji kufanya kazi zao vizuri zaidi, ama kwenye huduma ya injili ama kwenye kazi isiyokuwa huduma ya injili, panaweza kuwa na hatua zisizopungua tatu.

1) Jambo la kwanza ni kuangalia namna bora zaidi ya kuwaendea, kutegemeana na ukubwa wa tatizo.

2) Jambo la pili linawezakuwa kuwathibitishia kuwa unawaheshimu, unatambua kazi yao na mambo mazuri ambayo wameyafanya.

3) Jambo la tatu ni kupata usikivu wao wa jambo ambalo linatakiwa kubadilika. Hili linaweza kuhusisha madhara ya kutokubadilika kwao kwa taasisi, au kurudia tena kitu wanachokifanya, pia madhara yake kwao.

4) Jambo la nne ni kudumisha uhusiano, kwamba bado unawajali na kuwaheshimu, na unapenda kuwa kosa hili litakaporekebishwa litabaki kuwa historia.

5) Mwisho, utahitaji kuiandika tarehe, maneno uliyosema, maneno waliyosema, mambo mliyokubaliana, mambo ya kufanya, na muda ambao mambo ya kufanya yatatakiwa kukamilika.

 

S: Kwenye Kol, kwa nini kitabu hiki kimo kwenye Biblia?

J: Kuna sababu zisizopungua tatu.

1. Paulo alikiandika, na alikuwa mtume. Petro anathibitisha kuwa maneno ya Paulo yalikuwa Maandiko kwenye 2 Petro 3:15-16.

2. Paulo mwenyewe alisema kuwa yeye ni mtume kwenye 1 Timotheo 1:1; 2:7, Warumi 1:1; 1 Wakorintho 1:1; 9:1, 2 Wakorintho 1:1, 11:5; Wagalatia 1:1, Waefeso 1:1; Wakolosai 1:1; 1 Timotheo 1:1; 2 Timotheo 1:1; Tito 1:1.

3. Ushahidi wa kanisa la awali. Tazama swali linalofuata kujua waandishi walionukuu aya za Wakolosai.

 

S: Kwenye Kol, tunawezaje kujua kuwa maandiko tuliyonayo leo hii yametunza kwa usahihi maandiko yaliyoandikwa kwa mara ya kwanza?

J: Kuna sababu zisizopungua tatu.

1. Mungu ameahidi kutunza neno lake kwenye Isaya 55:10-11; Isaya 59:21; Isaya 40:6-8; 1 Petro 1:24-25; Mathayo 24:35.

2. Ushahidi wa kanisa la awali. Waandishi wa kwenye kanisa la awali hadi wakati wa Baraza la kwanza la Nikea (mwaka 325 BK) waliunukuu waraka wa Wakolosai karibu mara 105,:bila kuhesabu sehemu walizodokeza. Walinukuu 65% ya kitabu cha Wakolosai, ukiziondoa aya ambazo zimenukuliwa kwa sehemu. Kwa ajili hiyo ni aya 61.7 kati ya aya zote 95.

 

   Wafuatao ni waandishi 17 walioandika kabla ya Baraza la Nikea ambao walizitumia aya za Wakolosai

Clement wa Rumi (aliyeandika mwaka 96-98 BK) alidokezea Wakolosai 1:18 1 Clement sura ya .24 juzuu ya 1 uk.11; juzuu ya 9 uk.236

Waraka wa Barnaba sura ya 12 uk.145 unadokezea Wakolosai 1:16.

Irenaeus wa Lyons (aliyeandika mwaka 182-188 BK) alinukuu Wakolosai 3:5 kama kazi ya mtume kwenye waraka wa Wakolosai (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 5 sura ya 2.3 uk.538),

 Muratorian Canon (mwaka 190-217 BK) inautaja waraka wa Paulo kwa Wakolosai, na nyaraka nyingine 12 za Paulo.

Clement wa Alexandria anasema, “na mahali pengine [mtume] anasema, “ili wazielewe siri zote za Mumgu katika Kristo, ambaye ndani mwake mmefichwa hazina zote za hekima na ufahamu’” (Wakolosai 2:2b-3) [Stromata (mwaka 293-202 BK) kitabu cha 5 sura ya 12 uk.463].

Tertullian (mwaka 198-220 BK) anaifafanua Wakolosai 1:21 kama “mtume … waraka wake kwa Wakolosai” kwenye On the Resurrection of the Flesh sura ya 23 uk.561.

Hippolytus (mwaka 222-235/6 BK) ananukuu Wakolosai 1:19 (maneno machache kwa mfuatano tofauti) kwenye The Refutation of All Heresies kitabu cha 8 sura ya 6.

Origen (mwaka 225-253/254 BK) ananukuu Wakolosai 1:15 kama kazi ya Paulo  (de Principiis kitabu cha 1 sura ya.5 uk.247)

Novatian (mwaka 250-257 BK) ananukuu Wakolosai 1:16 kama kazi ya “mtume” (Treatise Concerning the Trinity sura ya 13 uk.622).

Novatian (mwaka 250-257 BK)  ananukuu Wakolosai 1:15 kama kazi ya  “mtume huyo huyo” (Treatise Concerning the Trinity sura ya .21 uk.632)

Cyprian alikuwa askofu wa Carthage kutoka mwaka 248 BK hadi kufa kwake mwaka 258 BK. Ananukuu “Wakolosai” kwenye Treatises of Cyprian makala ya 12 kitabu cha 11.

Adamantius (karibu mwaka 300 BK) anaiongelea Wakolosai 1:21-22 kama kazi ya Paulo (Dialogue on the True Faith sehemu ya tano uk.151).

Theonas wa Alexandria (karibu mwaka 300 BK) ananukuu kwa mbali nusu ya Wakolosai 4:6 (Letter to Lucianus the Chief Chamberlain sura ya 8 uk.161).

Methodius (mwaka 270-311/312 BK) anadokezea Wakolosai 1:15 kama kazi ya Paulo (The Banquet of the Ten Virgins Mhadhara wa 3 sura 3 uk.317). Paulo ametajwa mwisho kabisa wa sura ya 2 na mwanzo kabisa mwa sura ya 4.

Methodius (mwaka 270-311/312 BK) inaongelea Wakolosai 3:4 kwa mujibu wa The Greek New Testament 4th revised edition by Aland et al. Hata hivyo, sijaweza kuthibitisha hili kwenye kazi za Methodius ambazo ninazo.

Adamantius (karibu mwaka 300 BK) ananukuu Wakolosai 4:10-11  “Waraka wa Paulo kwa Wakolosai.”

Victorinus askofu wa Petau Austria (aliyeuawa mwaka 304 BK), anayataja Agano la Kale na Agano Jipya kwenye kazi yake, Commentary on the Apocalypse of the Blessed John uk.345. Ameziorodhesha nyaraka za Paulo: Warumi, Wakorintho, Wagalatia, Waefeso, Wathesolanike, Wafilipi, Wakolosai, Timotheo na anainukuu 1 Timotheo 3:15 kwenye sura ya 16 uk.345. Anaendelea kunukuu 1 Wakorintho 15:53 kwenye uk.346.

Methodius (mwaka 270-311/312 BK) anadokezea Wakolosai 1:15 “Kwa kuwa atafikiriwaje kuwa ‘mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote’” (The Banquet of the Ten Virgins kitabu cha 3 sura ya 3 uk.317).

Athanasius wa Alexandria (mwaka 318 BK) ananukuu Wakolosai 1:15-18 kwenye Against the Heathen sura ya 41 uk.26).

Alexander wa Alexandria (mwaka 313-326 BK) ananukuu 1 Wakorintho 2:9 kama kazi ya Mtume Paulo na Wakolosai 1:16,17 kama kazi ya Paulo kwenye Epistles on the Arian Heresy Epistle 1 sura ya 5 uk.293.

Baada ya Baraza la Nikea

Eusebius wa Kaisaria (mwaka 318-339/340 BK)

Hegemonius (karne ya 4) ananukuu Wakolosai 1:23 na 2:6-9 na anadokezea Wakolosai 1:24 kwenye Disputation with Manes sura ya 35 uk.209.

Athanasius wa Alexandria (mwaka 367 BK) anaorodhesha vitabu vya Agano Jipya kwenye Festal Letter 39 uk.552.

Victorinus wa Rumi (baada ya mwaka 363 BK) anaongelea Wakolosai 1:14.

Hilary wa Poitiers (mwaka 355-367/368 BK) anaongelea Wakolosai 2:2-3 kama kazi ya Paulo (On the Trinity kitabu cha 9 sura ya 62 uk.177).

Synopsis Scripturae Sacrae (mwaka 350-370 BK au karne ya 5) inautaja waraka wa Paulo kwa Wakolosai kwa mujibu wa Agano Jipya. Pia inanukuu Wakolosai 1:1-2a.

Ephraim/Ephem mwandishi wa nyimbo wa Shamu (mwaka 350-378 BK)

Basil wa Cappadocia (mwaka 357-378/379 BK) ananukuu Wakolosai 2:19 kama “Wakolosai” (On the Spirit sura ya 5.9 uk.9).

Synod ya Laodikia (Phrygia, mwaka 343-381 BK) canon 60 uk.159 inaorodhesha vitabu vya Agano la Kale na Agano Jipya. Canon 59 uk.158 inasema vitabu tu vya Agano la Kale na Agano Jipya vilivyokubaliwa na Kanisa vinaruhusiwa kusomwa kanisani.

Ambrosiaster (baada ya mwaka 384 BK) anaongelea Wakolosai 1:2-3,7,12,14,20,22 2:7,8,13,18,23; 3:4,6,13,16,17,21; 3:3,8,12

Cyril wa Yerusalemu (karibu mwaka 349-386 BK) ananukuu Wakolosai Kwenye uk.9.

Ambrose wa Milani (mwaka 370-390 BK)

Mdonastia aliyechochea mpasuko Tyconius (baada ya mwaka 390 BK) anaongelea Wakolosai 3:6.

Mdonastia Tyconius (baada ya mwaka 390 BK)

Pacian wa Barcelona (mwaka 342-379/392 BK)

John Chrysostom mwaka 396 BK aliandika mahubiri 12 ya Wakolosai, ambayo tunayo hata leo. Alisema kuwa waraka huu uliandikwa na Paulo.

Gregory wa Nyssa (karibu mwaka 356-397 BK) ananukuu Wakolosai 1:16 kama kazi ya Paulo kwenye Against Eunomius kitabu cha 1 sura ya 22 uk.63-64. Pia anaongelea Wakolosai 1:14.

Didymus (mwaka 398 BK) anaongelea Wakolosai 1:12

Mchochea mpasuko Lucifer wa Cagliari, Sardinia (mwaka 361-c.399 BK).

Gaudentius (baada ya mwaka 406 BK).

John Chrysostom (mwaka 392-407 BK).

Chromatius (mwaka 407 BK).

Severian (baada ya mwaka 408 BK).

Jerome (mwaka 373-420 BK).

Augustine wa Hippo (mwaka 388-430 BK) anasema Paulo (On the Forgiveness of Sin, and Baptism kitabu cha 1 sura ya 43 uk.31 juzuu ya 5) aliandika nyaraka za Warumi, 1 Wakorintho, 2 Wakorintho (sura ya 44 uk.32), Wagalatia (sura ya 45 uk.32), Waefeso (sura ya 46 uk.33), Wakolosai (sura ya 47 uk.33), 1 Timotheo na 2 Timotheo (sura ya 48 uk.33), Tito (sura ya 49 uk.33), Waraka wa Waebrania (unaotiliwa mashaka na baadhi ya wanazuoni, kwenye sura ya 50 uk.34).

Mpelagia nusu John Cassian (mwaka 419-430 BK) ananukuu Wakolosai 1:16 kama kazi ya Paulo kwenye Seven Books kitabu cha 6.21 uk.601.

Nilus (karibu mwaka 430 ) inaongelea Wakolosai 3:13.

Paulinus wa Nola (mwaka 431 BK) anaongelea Wakolosai  1:12.

Speculum (karne ya 5 BK) inaongelea Wakolosai 1:12.

Nilus (karibu mwaka 430 BK) inaongelea Wakolosai  3:13.

Cyril wa Alexandria (mwaka 444 BK).

Quodvultdeus (karibu mwaka 453 BK).

Varimadum (mwaka 445/480 BK) anaongelea Wakolosai  1:12

Theodoret wa Cyrus (askofu na mwana historia mwaka 423-458 BK).

Miongoni mwa vitabu vya wazushi na vyenye mafundisho ya uongo

Mzushi Priscillian (mwaka 385 BK) anaongelea Wakolosai 2:13.

Mzushi Marcion  kwa mujibu wa Tertullian.

Mzushi Elagius (mwaka 416-418 BK) anaongelea Wakolosai 3:4.

Mzushi wa Pelagia Theodore wa Mopsuestia (mwaka 428 BK).

3.Maandiko ya awali tuliyonayo ya Wakolosai yanaonyesha kuna tofauti kidogo za jinsi yanavyosomeka. Hata hivyo,, tofauti hizi hazina umuhimu wowote kitheolojia.

p46 Chester Beatty (karne ya 2 mwaka II 100-150 BK) ina aya 79 za Wakolosai. Kwa kueleza bayana, ina Wakolosai 1:1-2,5-13,16-24; 1:27-2:19; 2:23-3:11; 3:13-24; 4:3-12,16-18 na sehemu nyingine za nyaraka za Paulo na Waebrania. The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts kina picha ya sehemu ya p46 kwenye uk.192. Pia inasema kwenye uk.197 kuwa ubora na alama zenye kuonyesha kuwa waraka huu umeandikwa na mwandishi mweledi.

Nusu ya kwanza ya karne ya 3 - 1936 - Frederic G. Kenyon kwa mujibu wa  The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts.

Karne ya 2, mwaka 200 BK - 1935 - Ulrich Wilken  kwa mujibu wa The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts.

Mwaka 200 BK - 1968 - The Text of the New Testament.

Mwaka 81-96 BK - 1988 - Young Kyu Kim kwa mujibu wa The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts.

Karibu mwaka 200 BK - 1975 - Aland et al. roleo la tatu..

Karibu mwaka 200 BK - 1998 - Aland et al. toleo la nne.

Mwanzoni hadi katikati ya karne ya 2 - 1999 - The Complete Text of the Earliest New Testament Manuscripts. Kitabu hiki kimetokana kwa sehemu na kazi iliyoandikwa kwa mkono ambayo inafanana sana na Papyrus Oxyrhynchus 8 (mwishoni mwa karne ya kwanza au mwanzoni mwa karne ya pili) na Papyrus Oxyrhynchus 2337 (mwishoni mwa karne ya kwanza).

p61 Warumi 16:23,25-27; 1 Wakorintho 1:1-2, 2-6; 5:1-3, 5-6, 9-13; Wafilipi 3:5-9, 12-16, Wakolosai 1:3-7, 9-13, 1 Wathesalonike 1:2-3; Tito 3:1-5, 8-11, 14-15 Filemoni 4-7 (karibu mwaka 700 BK).

Karibu mwaka 700 BK - 1968 - The Text of the New Testament.

Karibu mwaka 700 BK - 1975 - Aland et al. toleo la tatu.

Karibu mwaka 700 BK - 1998 - Aland et al. toleo la nne.

Vaticanus [B] mwaka 325-350 BK.

Sinaiticus [Si] mwaka 340-350 BK.

Bohairic Coptic [Boh] karne ya 3 au 4 BK.

Sahidic Coptic [Sah] karme ya 3 au 4 BK.

Gothic mwaka 493-555 BK

 

Angalia www.BibleQuery.org/Colossians Manuscripts.html kuona maandiko zaidi ya mwanzo ya waraka wa Wakolosai.